Dini Pro - Kurani app ya Kiswahili

robbyl

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Posts
493
Reaction score
501
Nimetengeneza app ya Kurani ya Kiswahili inaitwa Dini Pro

Unaweza kufanya yafuatayo kwenye app yangu

Kurani Tukufu (Soma na Usikilize):
Soma Surah zote kwa urahisi na usikilize sauti popote ulipo.

Mwelekeo Sahihi wa Qibla:
Pata mwelekeo wa Qibla kwa haraka na usahihi mkubwa haijalishi uko wapi duniani.

Nyakati za Swala na Arifa:
Pata ratiba sahihi za swala na ukumbusho wa Adhana ili usipitwe na ibada hata ukiwa na majukumu mengi.

Tasbih ya Kidijitali na Dhikr:
Kaa karibu na Mwenyezi Mungu ukitumia Tasbih yetu ya kidijitali na orodha nzuri ya Dhikr mbalimbali.

Dua za Kila Siku:
Jifunze na usome dua mbalimbali, na upokee ukumbusho wa "Dua ya Siku" (Today's Dua) kila siku.

Misikiti Iliyo Karibu:
Tafuta misikiti iliyo karibu nawe kwa urahisi kupitia ramani unapokuwa safarini au eneo geni.

Matukio ya Kiislamu:
Fuatilia matukio na sikukuu muhimu za Kiislamu kwa mwaka mzima.

Pakua sasa Play store itafute kwa jina Dini Pro na ufanye ibada zako kuwa rahisi zaidi!
 
Safi , ila jina la hiyo app badilisha.
 
Nimeipakua iko safi,ila kwa ufafanuzi zaidi kwa atakaye ifungua ataikuta kwenye tafsir ya kiingereza,hapo nenda kwenye kubadilisha lugha ya tafsir,chagua Tanzania Albaruwan tafsir ,imekaa vyema
 
Naomba uniwekee kwenye sura ya wale Mabikira 72 tutakaoenda kukabidhiwa niisikilize na mimi initially moyo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…