Dini ni kwa ajili ya "Low minded people", Genius can't be trapped!

Uislam unakusaidia nini?
Uislam ni mfumo kamili wa Mzisha yangu ninayoishi kila siku. Chochote nikifanyacho Uislam umeshanielekeza nikifanye vipi kwa ubora. Na chochote kisichofaa kwenye maisha Uislam unanielekeza niwachane nacho vipi.
 
Sasa iweje utake wengine waishi kama uishivyo? Hujielewi,na wengine wafate mkumbo tuuuu?
 
Sasa iweje utake wengine waishi kama uishivyo? Hujielewi,na wengine wafate mkumbo tuuuu?
Uislam unanifundisha ukimuokowa mtu mmoja ni kama umeuokowa ulimwengu mzima, sasa nakuona kabisa mfumo wako unaoishi unaangamia, kwanini nisikutowe kizani nikakuleta kwenye nuru?
 
Kwanini kifo kiwe ending game? Do you believe that there is no chance of life after death?
𝐔𝐤𝐢𝐰𝐚𝐳𝐚 𝐤𝐢𝐟𝐨 𝐡𝐮𝐰𝐞𝐳𝐢 𝐟𝐚𝐧𝐲𝐚 𝐦𝐚𝐞𝐧𝐝𝐞𝐥𝐞𝐨 𝐧𝐚 𝐧𝐝𝐢𝐩𝐨 𝐬𝐞𝐡𝐞𝐦𝐮 𝐯𝐢𝐨𝐧𝐠𝐨𝐳𝐢 𝐰𝐚 𝐝𝐢𝐧𝐢 𝐡𝐮𝐭𝐮𝐦𝐢𝐚 𝐮𝐝𝐡𝐚𝐢𝐟𝐮 𝐡𝐢𝐢 𝐤𝐮𝐭𝐮𝐭𝐢𝐬𝐡𝐚. 𝐊𝐢𝐟𝐨 𝐤𝐢𝐩𝐨 𝐡𝐚𝐝𝐢 𝐤𝐰𝐚 𝐦𝐢𝐦𝐞𝐚.

𝐔𝐬𝐢𝐚𝐦𝐢𝐧𝐢 𝐤𝐚𝐭𝐢𝐤𝐚 𝐝𝐡𝐞𝐡𝐞𝐛𝐮 𝐟𝐮𝐥𝐚𝐧𝐢 𝐮𝐨𝐧𝐞 𝐧𝐝𝐢𝐥𝐨 𝐛𝐨𝐫𝐚 𝐤𝐮𝐥𝐢𝐤𝐨 𝐥𝐢𝐧𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐥𝐚𝐤𝐢𝐧𝐢 𝐚𝐦𝐢𝐧𝐢 𝐤𝐮𝐧𝐚 𝐍𝐆𝐔𝐕𝐔 𝐘𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈 𝐈𝐋𝐈𝐘𝐎𝐋𝐄𝐓𝐀 𝐕𝐈𝐔𝐌𝐁𝐄 𝐕𝐘𝐎𝐓𝐄 𝐔𝐋𝐈𝐌𝐖𝐄𝐍𝐆𝐔𝐍𝐈. 𝐓𝐇𝐄𝐑𝐄 𝐈𝐒 𝐒𝐔𝐏𝐄𝐑 𝐍𝐀𝐓𝐔𝐑𝐀𝐋(𝐒𝐔𝐏𝐑𝐄𝐌𝐄, 𝐄𝐗𝐀𝐋𝐓𝐄𝐃) 𝐏𝐎𝐖𝐄𝐑 𝐎𝐅 𝐀𝐋𝐋 𝐓𝐇𝐈𝐍𝐆𝐒 𝐈𝐍 𝐓𝐇𝐄 𝐔𝐍𝐈𝐕𝐄𝐑𝐒𝐄
 
Mimi ni Muislam, tuoneshe huo "mchanganyo" kwenye Qur'an, a,bacho ndicho muongozo kwa dini ya Kiislam, ukishindwa tuombe radhi.
Mchanganyo wa Quran unaanzia pale aliposhushiwa Muhammad ili aje atusambazie Dunia nzima! Harafu humohumo kwenye Quran imeandikwa Kwa kumsifia Mungu Ni mwenye haki na usawa asiye na ubaguzi right?sasa ilikuwaje ampe mtu mmoja habari muhimu kama hizi za kumjua yeye na Sheria zake ili aje atusambazie na sie !inashangaza Sana, hii Ni sawasawa uwe na watoto sita Kisha unaamua kumpenda na kumsomesha mtoto mmoja huku uwezo wa kuwasomesha wote unao huu ni ubaguzi ambao hata kibinadamu tu ni impossible! kitu kingine tutamuaminije Muhammad kama kweli alishushiwa na Mungu Hayo maandiko ya Quran pasi na Shaka?hii mikanganyiko ya kuhusu Dini aliyeileta Ni Mungu mwenyewe Kwa kuleta ubaguzi kwenye kufikisha taarifa utampaje mtu mmoja na duniani tuko billions of people?dini zote ni ujanja ujanja tu tupo kama tunapiga ramli Hakuna mwenye uhakika😁😁
 
Kila kitu Kina limit, inapoishia sayansi ndio miujiza inaanza.

Ni kweli sayansi na miujiza haviwezi kukaa pamoja, lakini hili halizuii vitu hivi kuwepo katika ulimwengu.

In short, miracles si business ya sayansi, lakini miracles zipo na sayansi ipo.
Miracles ni nini na unajuaje hii ni miracle na si kitu kisicho miracle ambacho wewe hukifahamu tu?

Nitakupa mfano, mababu zetu ambao hawakujua sayansi ya wazungu, walipoletewa vitu vya umeme kama redio, wakaona hiki kiboksi kinatoa sauti ya mtu, waliona miracle.

Walivyoona magari yanakwenda bila kusukumwa na wanyama, waliona miracle.

Walipoona watu wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua, waliona miracle.

Lakini, kiukweli, hakuna miracle hapo, ni sayansi tu inafanya kazi. Hakuna supernatural power, zote ni natural power.

Ni wao tu walikuwa hawajui hizo natural powers zinafanya kazi vipi.

Sasa, na wewe utakaposema hii ni miracle, hata kama hakuna mtu yeyote duniani anayejua hicho kitu kikoje, utajuaje hiyo ni miracle kweli, na si sayansi/natural power tu ambayo wewe bado hujaijua?

Yani unaweza kuona kitu ukafikiri ni miracle/supernatural power, kumbe ni natural science tu, ila wewe hujaijua.

Sasa, utajuaje kuwa, chochote unachokiita miracle ni miracle kweli, na si kitu kisicho na miracle ambacho wewe hujakijua tu?

Unaweza kuambiwa na mtu kuwa "mimi ni mchawi, ninaweza kumuua mtu bila kumgusa". Halafu huyo anayejiita mchawi akapita sehemu, akaua mtu kweli bila kumgusa.

Ukasema hiyo ni miracle, ni supernatural powers.

Kumbe huyo jamaa unayemuita mchawi ni mtu anayejua Chemistry tu, kaangalia upepo unaenda wapi, kanyunyuzia sumu ya hewani ya Cyanide, sumu ikampata mlengwa, mlengwa akafa bila kuguswa.

Wewe usiyejua Chemistry, ukiangalia unaona miracle. Unaona uchawi. Unaona supernatural power. Unaona this is beyond science, mtu kauawa bila kuguswa.

Kumbe hamna miracle yoyote, hakuna uchawi, hakuna supernatural power, ni Chemistry tu.

Sasa, wewe unaposema hii ni miracle, utajuaje ni miracle kweli na si natural power usiyoijua tu?
 
Yes, dini ni kwa ajili ya watu wasio na ufikiri sahihi. Dini ina vitu ambavyo ni vya watu wa akili za chini sana.

Vitabu vyote vya dini vina michanganyo isiyohitaji hata kutumia nguvu kujua kuwa "hapa tumepigwa na tunaendelea kupigwa"

Sayansi imejibu maswali mengi sana ambayo dini ilishindwa kuyajibu na kuishia kuwaambia wafuasi waamini tu bila kuona!

Sayansi imetibu magonjwa complex ambayo dini haijawahi hata kuyagusa, inaishia kujipenyeza kitapeli tu.

Mf katika mgogoro wa leo wa Gaza, dunia imegawanyika. Watu wasio na uelewa wanaishia kuchagua upande wa dini A na dini B. Wale wanaoiunga mkono Israel kwa kisa cha dini ya ukristo wajue kuwa % kubwa ya waisrael hawaamini ktk dini na Marekani 86% hawana dini. Pale kinachogombewa ni Maslahi tu!

Dini zetu tungeachana nazo tungekuwa na maendeleo makubwa. Mf China na Nchi za Ulimwengu wa kwanza, nyingi zimeachana na mambo ya dini na zinaendelea sana.

Watu wanavumbua issues za drones, AI na mirobotic machines kibao we unakesha kanisani eti uwe millionea, sijui upate mtoto real?

Unalala na vichupa vya maji sijui chumvi na mafuta ya upako upate gari, are u serious?

Nilikua namsikiliza Shehe/Maalim mmoja anasema wale kunguni wa Ufaransa ni jeshi la Allah limekuja kuwaangamiza kisa wana madhambi...are we real serious?

Dini zina mfumo ambao Unatufanya "tuwe limited" kwenye ufikiri na uvumbuzi.

Live your live, Death is the Ending game! Dini ni ulaji wao!

Atheists make sense than who are not
Mkuu umeongea ukweli tupu lskini subiri wafia dini akina FaizaFoxy waje kukumwagia mapovu yao ya OMO.
 
Miracles ni nini na unajuaje hii ni miracle na si kitu kisicho miracle ambacho wewe hukifahamu tu?

Nitakupa mfano, mababu zetu ambao hawakujua sayansi ya wazungu, walipoletewa vitu vya umeme kama redio, wakaona hiki kiboksi kinatoa sauti ya mtu, waliona miracle.

Walivyoona magari yanakwenda bila kusukumwa na wanyama, waliona miracle.

Walipoona watu wanaweza kutabiri kupatwa kwa jua, waliona miracle.

Lakini, kiukweli, hakuna miracle hapo, ni sayansi tu inafanya kazi. Hakuna supernatural power, zote ni natural power.

Ni wao tu walikuwa hawajui hizo natural powers zinafanya kazi vipi.

Sasa, na wewe utakaposema hii ni miracle, hata kama hakuna mtu yeyote duniani anayejua hicho kitu kikoje, utajuaje hiyo ni miracle kweli, na si sayansi/natural power tu ambayo wewe bado hujaijua?

Yani unaweza kuona kitu ukafikiri ni miracle/supernatural power, kumbe ni natural science tu, ila wewe hujaijua.

Sasa, utajuaje kuwa, chochote unachokiita miracle ni miracle kweli, na si kitu kisicho na miracle ambacho wewe hujakijua tu?

Unaweza kuambiwa na mtu kuwa "mimi ni mchawi, ninaweza kumuua mtu bila kumgusa". Halafu huyo anayejiita mchawi akapita sehemu, akaua mtu kweli bila kumgusa.

Ukasema hiyo ni miracle, ni supernatural powers.

Kumbe huyo jamaa unayemuita mchawi ni mtu anayejua Chemistry tu, kaangalia upepo unaenda wapi, kanyunyuzia sumu ya hewani ya Cyanide, sumu ikampata mlengwa, mlengwa akafa bila kuguswa.

Wewe usiyejua Chemistry, ukiangalia unaona miracle. Unaona uchawi. Unaona supernatural power. Unaona this is beyond science, mtu kauawa bila kuguswa.

Kumbe hamna miracle yoyote, hakuna uchawi, hakuna supernatural power, ni Chemistry tu.

Sasa, wewe unaposema hii ni miracle, utajuaje ni miracle kweli na si natural power usiyoijua tu?
Mkuu umenikumbusha jambo. Hapo zamani kulikuwa na wajanja wanajiita rain makers. Walichokuwa wakifanya ni ujanjaujanja tu. Waliweza kufahamu dalili zote za kunyesha mvua kama vile dew on grass in the morning, singing of some birds (kama vile dudumizi), frog croaking, and high temperature at night.

Sasa 'rain maker' akishaona ishara zote hizi anajitokeza mbele ya jamii kuomba alipwe ng'ombe awaletee mvua. Basi anachangiwa kundi kubwa la ng'ombe; baada ya siku 3 mvua inanyesha watu wanamtukuza kumbe mtu mwenyewe ni mwanamazingaombwe tu.

Kuwakamua watu ni akili. Tazama jinsi wachungaji feki wanavyofanya miujiza ya mchongo bila aibu. Siku hizi utume na unabii umekuwa upigaji. Eti akina Masanja nao wanajiita maaskofu wakati hawajasoma bible school hata kidogo bali ni ujanjaujanja tu. Ifike wakati serikali iingilie kati utapeli huu. Watu wanapigwa sana kule kwa akina Mwamposa, Geodavie, Mwingira, Lusekelo, etc.
 
Hakumfanyi awe na akili napigilia msumari,,,,sayansi imeshindwa kutuambia chanzo cha binaadam afu porojo kibao
Tangu lini sayansi ikashindwa kutuambia chanzo cha binadamu na ulimwengu mkuu? Sayansi ina maelelezo ya kutosha kuhusu hili. Kasome topic ya evolution katika biology ya kidato cha nne.....imeweka wazi kila kitu kuhusu origin of man and the world.
 
Mchanganyo wa Quran unaanzia pale aliposhushiwa Muhammad ili aje atusambazie Dunia nzima! Harafu humohumo kwenye Quran imeandikwa Kwa kumsifia Mungu Ni mwenye haki na usawa asiye na ubaguzi right?sasa ilikuwaje ampe mtu mmoja habari muhimu kama hizi za kumjua yeye na Sheria zake ili aje atusambazie na sie !inashangaza Sana, hii Ni sawasawa uwe na watoto sita Kisha unaamua kumpenda na kumsomesha mtoto mmoja huku uwezo wa kuwasomesha wote unao huu ni ubaguzi ambao hata kibinadamu tu ni impossible! kitu kingine tutamuaminije Muhammad kama kweli alishushiwa na Mungu Hayo maandiko ya Quran pasi na Shaka?hii mikanganyiko ya kuhusu Dini aliyeileta Ni Mungu mwenyewe Kwa kuleta ubaguzi kwenye kufikisha taarifa utampaje mtu mmoja na duniani tuko billions of people?dini zote ni ujanja ujanja tu tupo kama tunapiga ramli Hakuna mwenye uhakika😁😁
Hayo uliyoyaandika ndiyo "mchanganyo" wa Qur'an?
 
Mjue sana Mungu ili uwe na amani Ayubu 22:21.

Mimi binafsi nilikuja kumuamini Zaidi Mungu Baada ya kusoma Bible.

Nilianzia na kusoma vitabu viwili tu
1. Daniel kitabu kilichofanyiwa utafiti na Izac Newton zaidi ya miaka 10.

2 kitabu cha ufunuo wa Yohana.

Hivi vitabu vinaelezea
:Tawala nne za Dunia.

:Utabiri wa kuja kwa Yesu kristo tarehe mwezi hadi mwaka.

: Kuibuka kwa Roman catholic

:kuibuka kwa Dini ya kiislamu.

:Kuibuka kwa Taifa la Marekani tarehe hadi mwaka

: European Union.

Ila vimeandikwa kwa Codes kama.

1. Mnyama maana yake ni ufalme au utawala wa kisiasa (DANIELI 7:17)

2. Maji ni sehemu ya dunia inayokaliwa na watu (UFUNUO 17:15)

3. Nchi ni sehemu ya dunia isiyokaliwa na watu (kinyume cha maji ya UFUNUO 17:15)

4. Pembe yenye kilemba (crown) ni utawala mdogo au jimbo (Ufunuo 13:1)

5. Pembe isiyo na kilemba ni itikadi (Ideology)

6. Joka ni Shetani (Ufunuo 12:9)
Basi, Biblia ktk Ufunuo 13 imetaja wanyama wawili kwa maana ya tawala mbili. Ufunuo 13:1
 
FaizaFoxy

DADA FAIZA NAOMBA UNIJIBU HAYA MASWALI ILI NISLIM.

Nianze kusoma shahada.

Muhammad Alitumwa kwa Waarabu Pekee yao.

Ndugu zetu Waislamu wanapenda sana kudai kuwa Yesu alikuja kwa ajili ya Wayahudi peke yao na sio kwa ajili ya ulimwengu wote. Na andiko wanalolitumia tena na tena ni la Mathayo 15:24 pale Yesu alipozungumza na mwanamke Mkananayo: Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. Nitakwambia kwa niniYesu alisema hivyo.

Kwa sasa tuangalie sababu 10 ambazo Allah mwenyewe anazitoa kuthibitisha kwamba alimtuma Muhammad kwa Waarabu na si kwa wasio Waarab.

Kwa mujibu wa Quran, Muhammad ni mtume wa Waarabu Majahila peke yao kwa sababu zifuatazo:

SABABU YA KWANZA Surat Yunus 10:47 Na kila umma una Mtume. Alipowajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa uadilifu, wala hawakudhulumiwa.

Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “kila umma" si maana yake kila aina ya watu? Iwe ni Wazungu, Wahindi, Waafrika, nk?

2. Je, “Mtume wao” maana yake nini kama si wa kwao peke yao?
3. Je, Muhammad si ni Mwarabu ?

SABABU YA PILI

Surat Ibrahim 14:4 Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia.
Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “kwa ulimi” si maana yake kila mtume kwa lugha anayoongea?

2. Je, “wa kaumu yake” si maana yake ‘wa watu wake’; kama ni Mhindi kwa Wahindi?

3. Je, ulimi wa Muhammad si ni Kiarabu na kaumu yake ni Waarabu?

SABABU YA TATU

Suurat an Nah'l 16:36. Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.

Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “kila umma" si maana yake kila aina ya watu, mfano Wahindi na Waafrika?

2. Je, “tuliutumia Mtume” si maana yake mtume wa Wahindi si mtume wa Waafrika?

3. Je, Muhammad si ni Mwarabu?

SABABU YA NNE

Surat Al Maida 5:48 Na tumekuteremshia wewe, kwa haki, Kitabu hichi kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake katika Vitabu na kuyalinda. Basi hukumu baina yao kwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, wala usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.

Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja, lakini ni kukujaribuni kwa aliyo kupeni.

Tujiulize: 1. Kwa mujibu wa Allah, je, “Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake” si maana yake kila watu (Wazungu, Waafrika, nk) wamewekewa sharia zao wenyewe?

2. Je, Allah anaposema, “Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angelitaka angekufanyeni nyote umma mmoja” si anamaanisha kuwa angetaka tuwe na mtume mmoja na imani moja angetufanya taifa moja? Angalizo: “Kila mmoja katika nyinyi tumemwekea sharia yake na njia yake. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka ange kufanyeni nyote umma mmoja”, inasomeka hivi kwa Kiingereza katika Sahih International:

“To each of you We prescribed a law and a method. Had Allah willed, He would have made you one nation [united in religion]” Katika tafsiri ya Yusufu Ali, inasema hivi:

“To each among you have we prescribed a law and an open way. If Allah had so willed, He would have made you a single people”

SABABU YA TANO

Surat Assajdah 32:2-‐3 Huu ni mteremsho wa Kitabu kisichokuwa na shaka yoyote kinachotoka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Au wanasema: Amekizua? Bali hichi ni Kweli iliyotoka kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.

Tujiulize: 1. Kama kila umma Allah anadai aliupelekea mtume, je, “ili uwaonye watu wasiofikiwa na mwonyaji kabla yako” si maana yake anasema kuwa, ‘kwa vile Waarabu nilikuwa sijawaletea, wewe Muhammad ndio uende sasa’?

2. Je, kwa kuwa Muhammad si wa ule umma ambao tayari ulishaonywa, umma wake si unajulikana (Waarabu Majahila)? Maelezo tunayoyapata kwa Sayyid Abul Ala Maududi – Tafhim al-‐Qur'an -‐ The Meaning of the Qur'an (32. Surah As Sajdah (The Prostration) - Sayyid Abul Ala Maududi - Tafhim al-Qur'an - The Meaning of the Qur'an) wazi:

yanasema The main theme of the Surah is to remove the doubts of the people concerning Tauhid, the Hereafter and the Prophethood, and to invite them to all these three realities.

The disbelievers of Makkah, when they talked of the Holy Prophet in private, said to one another, "This person is forging strange things sometimes he gives news of what will happen after death. Yaani, kwa kifupi, watu wa Makkah ambao hawakumuamini Muhammad ndio walikuwa wakimwambia kuwa anatungatunga tu uongo na kuwaambia ni Mungu kasema.

SABABU YA SITA
Surat Ya-‐Sin 36:2-‐6 Kwa Haki ya Qur'ani yenye hikima! Hakika wewe ni miongoni mwa waliotumwa, Juu ya Njia Iliyonyooka. Uteremsho wa Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa , basi wao wamekuwa wenye kughafilika.

Tujiulize:
1. Allah anapomwambia Muhammad, “wewe ni miongoni mwa waliotumwa”, maana yake ni nini kama si ileile kwamba Allah alituma mitume mbalimbali – kila watu na mtume wao – na huyu Muhammad ni mmoja wa waliotumwa?

Je, “Ili uwaonye watu ambao baba zao hawakuonywa” maana yake si ni hao ambao ndio kaumu’ ya Muhammad? (Rejea sababu yatano hapo juu). SABABU YA SABA Surat Al -‐ An-‐A'am 6: 156-‐ 157 Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyokuwa wakiyasoma. Au mkasema: Lau kuwa tumeteremshiwa sisi Kitabu tungelikuwa waongofu zaidi kuliko wao. Basi imekufikieni bayana kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na uwongofu, na rehema. Basi nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayekanusha Ishara za Mwenyezi Mungu, na akajitenga nazo?

Tujiulize: 1. 2. 3. 4. Je, si kweli kwamba Allah anaongea na taifa Fulani hapa? Je, si kweli kwamba Allah anaonyesha kuwa kuna mataifa mawili (mengine) ambayo aliyateremshia vitabu vyao?
Je, si kweli kwamba Allah analiambia taifa hili analoongea nalo kuwa na wao amewaletea kitabu ili wasije kutoa visingizio kuwa hawakujua?

Je, Muhammad taifa lake si linajulikana?

SABABU YA NANE

Surat Ash-‐Shua'raa 26: 192-‐199 Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa walimwengu wote. Ameuteremsha Roho muaminifu, Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji, kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi. Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya kale.

Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya wanazuoni wa Wana wa Israili? Na lau kuwa tungeliiteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu, Na akawasomea, wasingelikuwa wenye kuamini.

Tujiulize:
1. Je, ulimi wa Kiarabu (lugha ya Kiarabu) iko wazi kwa mimi niliye Msukuma au Mnyakyusa au Mkikuyu?

2. Je, Allah anaposema, “Na lau kuwa tungeliiteremsha juu ya mmoja wa wasio kuwa Waarabu,” kuna asiyeelewa maana yake? -‐-‐-‐ kumbe unataka aseme wazi kiasi gani ndipo uelewe? – Basi maana yake ni kuwa kwa asiyekuwa Mwarabu Quran haimhusu!!

SABABU YA TISA

Surat Al -‐ An-‐A'am 6:92 Na hiki ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilichobarikiwa, chenye kuhakikisha yaliyo tangulia, na ili uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake. Tujiulize: 1. Je, Allah anaposema “Mama wa Miji” si maana yake Makkah?

2. Je, “uuwonye Mama wa Miji na walio pembezoni mwake” maana yake si ni kuwa Quran ni kwa ajili ya wakazi wa Makka na walio karibu na mji huo? Labda utasema kwamba “pembezoni” maana yake hata Marekani na Tanzania ni pembezoni. Basi soma sababu ya kumi ndio utajua ukomo wake.

SABABU YA KUMI
Surat Ash-‐Shuura 42:7 Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa Miji na walio pembezoni mwake.

Tujiulize:

1. Je, kwa kuwa tumeona kuwa “Mama wa Miji” ni Makkah, pembezoni mwake nako ni wapi?

2. Je, Allah anasema “tumekufunulia Qur'ani kwa Kiarabu”, je, maana yake si kuwa, ni hadi pale Kiarabu kilikokuwa kinazungumzwa?

3. Je, kama alimaanisha hadi mwisho wa ulimwengu, angetaja kigezo cha lugha?

Hitimisho
Kwa mujibu w Allah, ni wazi kabisa kuwa, Quran haikuletwa kwa ajili ya kila mwanadamu bali kwa ajili ya Waarab peke yao. Muhammad si mtume wa kila mwanadamu bali ni mtume wa Waarabu peke yao.
 
Back
Top Bottom