DID GIANTS EXIST? Historia ya Majitu ya Kale

KUNA WAKATI HUWA NAWAZA KUHUSU MIAKA YA SASA HIVI. NIKIWAZA BABANGU ALIYEZALIWA MWAKA 1927 NA JINSI ALIVYOKUWA BIG, HALAFU NAJIANGALIA MIMI, HUWA SIPATI PICHA. HUENDA MIAKA INAVYOENDA TUTAANZA KUZAA VIMTU (FUTI 3) NI KAMA KUNA KUPUNGUA SIZ YA WATU WITH TIME. MIAKA YA SASA HIVI WATU NI WADOGO WADOGO MPAKA BALAA.
 
Naksubiri mkuu kama kawa nategemea uje na ESSAY nzima kuhusu mada husika
nimewaho simuliwa pia majitu yaliexist interlacustrine region...walikuwa walikuwa abacwezi au wachwezi...babu alinieleza kuwa walikuwa ni watu wasio wa kawaida,wenye nguvu nyingi za kutenda miujiza alinieleza kuwa walipotea kimazingara badae...they had power to do telekinesis na telepathy
 
Hupajui? Nmetuma kavideo tazama mkuu hio ni sehemu tu ndogo ,ila kuna area kubwa sana ya hayo mawe yako kwenye safu ya vijimilima vidogo vidogo
Duuhh.. Nimeona mkuu.. bonge moja la mandhari

Haya mawe nahisi yamepangwa..
Aisee lzm nikatalii huko
 
hahaa nimependa hapo ulivyomalizia ktika ibara ya mwisho"" lakini kwa jibu lako hilo tu yaonyesha kuwa kuna mashaka mengi sana kutoka ktika hivyo vitabu...kwa sababu tunaambiwa kuwa qur'an nikitabu kisichokuwa na shaka na nimaneno ya mungu ..sasa inakuwaje tena Mungu asimulie kitu ambacho hana uhakika nacho kuwa huyu mtu anapatikana mahala fulani."" mbona kuna historia inayowahusu kina omary .kina aboubakari" kama zipo hizo ilikiwaje ishindikane kwa mtu kama huyu ambaye alikuwa na mchango mkubwa mnoo ktika ujenzi wa safina..huoni kuwa hapo palikuwa na ubaguzi ?yaani alishindwa hta kutoa mchanganuo wahilo.""
na sio kuhusu UJ tu juzi nilikuwa napitia article unayomuhusu bilqiss..daahh nasikitika kusema kuwa qur'an imeficha mnoo kuhusu ukweli wake kwa sababu wanazuoni wengi wanadai kuwa huyu mwanamama alikuwa anatokea Yemen wakati historia ya kweli inaonyesha kuwa ni alikuwa anatokea ethiopia"" na alikuwa akifahamika kama queen of sheba...kwa mantiki hiyo mpaka hapo tunaweza kuona kuwa waliotumika kuzisambaza hizi dini walifnya juu chini kuhakikisha kuwa wana fifiza historia ya mtu mweusi kwaajili ya maslahi yao""

anyway"" kwakuwa natoka nje ya mada "" nilikuwa naomba hili liishie hapa...ila kidogo nadhani utakuwa umeupata mustakabali wake
alibakariI

njoo huku"" alibakari
 
This is amazing.... However inashangaza sana jinsi gani sisi waafrika hatuwezi kutunza historia zetu za muhim kma hizo ambazo tulipaswa tuzitunze ili vizazi na vizazi viweze kujivunia uwepo wa watu wa maajabu kama hao
 
This is amazing.... However inashangaza sana jinsi gani sisi waafrika hatuwezi kutunza historia zetu za muhim kma hizo ambazo tulipaswa tuzitunze ili vizazi na vizazi viweze kujivunia uwepo wa watu wa maajabu kama hao
the stories are there....so they really existed...nilielezwa hawa wachwezi ndio walikuwa wafugaji wa Kwanzaa wa n'gombe mnazoziita za ankole....walikuwa na vtu ambavyo si vya kawaida
 
This is amazing.... However inashangaza sana jinsi gani sisi waafrika hatuwezi kutunza historia zetu za muhim kma hizo ambazo tulipaswa tuzitunze ili vizazi na vizazi viweze kujivunia uwepo wa watu wa maajabu kama hao
the stories are there....so they really existed...nilielezwa hawa wachwezi ndio walikuwa wafugaji wa Kwanzaa wa n'gombe mnazoziita za ankole....walikuwa na vtu ambavyo si vya kawaida
 
Mkuu Mhe.Professor... Kiukweli nimetumia biblia tu pamoja na mythology nyingine kwa kiasi kikubwa kwa sababu moja kuu kwamba makabila mengi duniani kila mmojawapo lina story ya uwepo wa mtu mwenye futi zaidi ya 40??
Ahsante

Kama ulitumia Biblia kama chanzo (Persuasive Source) basi hapa lazima umuweke mwanahistoria Flavius Josephus,
Huyu ndiye anayetumiwa mwanahistoria nguli wa Karne ya kwanza ambaye wanahistoria wengi na wasomi wengi wa taalimungu wanamtumia kama chanzo chao. Kwenye kitabu chake cha The Antiquities of the Jews amezingumzia uwepo wa majitu na jinsi yalivyopigana vita na Mfalme Daudi. Humu amewataja ndugu zake Goliati waliokuwa na vidole sita mikononi na miguuni, moja wapo ni Ishbibenob ambaye mkuki wake ulikuwa na kama kilo tatu na gramu kadhaa.

Kwanini umtuie Flavius Josephus ???
Huyu alikuwa ni msomi wa Kiyahudi ambaye alipewa Uraia wa Rumi na Kaisari Vespasian. Baada ya Jemedari Titus kuhusuru Israel mwaka 70 B.K huyu jamaa alichukuliwa mateka baada ya Masada kuanguka. Huko Rumi alionekana ni moja ya wasomi wenye akili sana basi mfalme akampa kazi ya kuandika kuhusu vita dhidi ya Wayahudi na Warumi ili kwamba huenda Wayahudi wengine wasifikirie kuleta uasi dhidi ya Rumi. Kitabu chake cha kwanza kiliitwa The Wars of the Jews. Hivyo kutokana na nafasi yake ya kitaifa aliyokuwa nayo mbele ya kaisari Vespasian na Titus wasomi wengi wa dini huwa wanamtumia huyu mwanahistoria kwasababu alikuwa msomi anayeaminika sana kwa kipindi hicho.

Kuhusu majitu ya kale,
Kweli yalikuwepo kwasababu ushahidi wa kihistoria bado tunao na kila siku unaendelea kupatikana.
Japo hapo katikati kuna mianya mingi sana ambayo sisi hutuwezi kuijaza kwa ushahidi mkubwa zaidi ya kutafuta nadharia mbali mbali (Theories). Wengine wanasema Majitu ni wana wa malaika (Bi'nai elohim), wengine wanasema wanadamu wa kale walikuwa majitu na kadiri siku ziendavyo tukapungua maumbile na wengine wanasema kabisa kulikuwa na kizazi cha majitu ambayo yalikuwa ni binadamu kama wengine lakini kikapotea tu. Hii ya mwisho inawezekan vizuri tu maana kuna viumbe kama dinosauri viliwahi kuwepo lakini leo vikapotea na kilichobaki kwetu ni mifupa ambayo wanasayansi wanaisoma.

Lakini kama umetumia Biblia kama chanzo chako mimi nakuachia maswali haya ya utafiti:
Kwanini Wahebrania walifanikiwa kupiga sehemu zote za Israeli kasoro Yerusalemu ??
Au kwanini Yerusalemu ulikuwa ndiyo mji wa mwisho kukamwatwa na Waisraeli baada ya Daudi kuwa mfalme ??
Kwanini mfalme Daudi aliwachukia sana wale vipofu na viwete waliokuwa wanakaa Yerusalemu ??
Kwanini Wakina Sauli hawakufikiria kuukamata Yerusalemu wakati ulikuwa ndani ya nchi yao ??

NB 1 : Kitu cha kukumbushana ni kwamba, kitu kuaminiwa au kutajwa na watu wengi haithibitishi uhalisia wake.
Hivyo kuwepo kwa hadithi nyingi na nadharia kunasiaidia tu kukuza uelewa wetu ili tuweze kuamua nini cha kuamini.
Hivyo kuna sehemu inasema Farao aliwahi kuwalaani kishirikina watu wa Kaanani (Majitu ) kwasababu walikuwa na ugomvi naye. Lakini pia usisahau kwamba haya majitu ya kwenye Biblia yalikuwa ni wana wa Kanani ambaye alikuwa ni mtoto wa Nuhu. Hivyo basi tuchambue taratibu na kusoma sana vitu vya kutosha halafu tuchague nini cha kuamini kuhusu asili ya haya majitu.

NB 2: Lakini muhimu kuliko yote, MAJITU YALIKUWEPO.
Ushahidi wa kihistoria unathibitisha uwepo wa majitu japo historia inashindwa kututhibitishia asili yao.
Mpaka sasa hatujui haya majitu yalikuwa ni Uzao wa binadamu (Adam) au Ilikuwa ni jamii nyingine tofauti kabisa na jamii ya Binadamu. Hivyo kwenye huu mjadala tungesema: GIANTS DID EXIST, BUT WHERE DID THEY COME FROM AND WHERE ARE THEY NOW ???? Hapa sasa ndipo tungeanza kuja na nadharia za kidini ambazo zinatoka kwenye Biblia, Kurani na hadithi za kidini (Mythologies) au Utafiti wa kisayansi ambao unazungumzua mabadiliko kutokana na muda na mzaingira (Evolution)
 
Ndi
Duh.. Huo unyayo upo juu ya jiwe au?
Yaani ukitaka kuuona ni mpaka upande juu ya jiwe?
Ndio na ukianzia hapo alipochukua hiyo video kwa nyuma yake ndo kuna hilo jiwe na kumepangwa vizuri sana unaeza hisi kuna mtu alikuwa anayakalia au alikuwa akitengeneza sanaa flani hivi
 
Mkuki kilo3 [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ila mm naamini kwamba duniani kulikuaga na "AT THE TIME OF MAGIC"
ambapo haya ya kusadikika yalitokea na yalikua ni mambo ya kawaida miongoni mwao
 
Queen of Sheba ni kweli nae historia yake inawekewa kigiza hivi lakini waethopia wanaijua vizur sana na huwadanganyi hapo

Lakini ndio maana nilikwambia hakuna kitabu cha dini kilicho straight katika mambo flanflan lakini kweli ni ipi kila mtu atakwambia kitabu chake cha dini kipo sawa lakini ukitizama vitabu vyote vinaeleza vizuri sana kuhusu watu weupe ila kunapokuwepo na kuonekana kwa mtu mweusi tu basi utaona historia yake inaisha bila kuelewa ilikuwaje

Ila tukiyaacha yote ni wakati wetu sasa kutafuta historia zetu wenyewe zile historia zilizopo zina jambo flani tata yaeza kuwa ni makusudi au walishindwa tu kupata ushirikiano kwa sababu walitoka mbali kuja kwetu au vinginevyo wanajua lakini wanataka tuwaamini zaidi wao yaani ni kama lile fumbo la ustarabu wa binadamu ulikoanzia kila siku hawataki kuamini ulianzia Afrika wanataka tuamini ulianzia kwao

Tuyaache yote na sisi ni wakati wetu kuweka historia zetu wenyewe na wao wasome kutuhusu lakini mtafanya wanagapi ili mganikiwe? Ikiwa hata serikali inaeza kushindwa kukupa ushirikiano pale inapohitajika.

Mfano.

Pale itigi wilayani Manyoni mkoa wa singida kuna njia ipo chini ya ardhi njia ndefu sana lakini njia hii inasemekana ilikuwa ni handaki la moja wa machifu alikuwa akijificha huko wakati wa vita na pia kunaaminika kuna sehemu alijenga kama madhabahu ya kufanya sala ya kimila huko chini lakini nilipoenda kuomba kibali cha kuingia huko nikakataliwa kwa nguvu zote lakini njia ya kuingilia ipo na inaonekana na watu kadhaa wamewahi kupita huko kiusalama ni popo tu waliopo huko na hata nilipoomba basi wanipe ulinzi walikataa ikabidi utafiti wangu uishie pale

Huo ni mfan mdogo sana kati ya mingieniliokutana nayo

Tukibadilika hata Mabomu tutatengeneza wenyewe
 
aiseee pole sana chief"" hao wameshindwa kukupa ruksa ..kwa sababu hawajui thamani yakile ulichotaka kukifanya "" bado hawajui historia ya kweli inayomuhusu mtu mweusi laiti kama wangekuwa wanamjua"" aiseee wangekuwa na hamasa na kujivunia kuhusu huo utafiti wako...maana elimu ambayo ungekuja kuitoa baada ya hapo ingekuwa kuwa sitiri mpka vilembwe vyao""" ila kwa kuwa wako brain washed wameshindwa kutambua thamani yakile ulichokuwa unakipigania....."""

but asante kwa huu mjadala"" kwasasa sina maswali mengine dhidi yko"""

alibakari
 
Pamoja
Sana kamanda
 
Malaika!! Alafu muasi mungu.??
 

Kaka hapo mbona Pagumu kidogo, maana kama hao ni magiant basi hata uume wao pia ni mkubwa kuendana na size ya miiki yao, waliwezaje kuwaingilia wanawake wa kawaida na kuwapa mimba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…