Diaspora wa Kenya wafanya makubwa Marekani. Sisi Diaspora Wetu wanafanya nini cha kuonekana huko walipo?

Uraia pacha sio sababu pekee...!

Una taka uraia pacha wakati tanzania huna ata shamba la mkonge...

Huo uraia pacha ni kwa ajili ya nini? Kusoma? Kutibiwa? Kupata posho? Kuishi kifahari?

Kama ni hivyo una ukana tu na kuendelea na mishe zako ughaibuni... wapo wengi wamekana uraia wa Tz na watoto wa vigogo ndio wengi zaidi kuliko mnavyo fikiria...
 
Pascal Mayalla, hao vijana wachache wanaojihusisha na uhalifu hapo S. Africa wasikupofushe kiasi cha kudharau diaspora wote.

Pamoja na serikali ya ccm kutokuwapa mazingira mazuri lakini wapo wengi wanaofanya vizuri huko ughaibuni.
Ukiachilia wanaofanya kazi katika taasisi za kiserikali, kuna ambao wanafanya biashara pia.
Mfano kuna dada mmoja wa kitanzania huko Marekani aliripotiwa na Maulid Kitenge, amefungua restaurant yake ya vyakula vya kibongo.

Ni kweli wenzetu wametuacha kiasi (na hii ni kutokana na mfumo wa elimu pia 'sapoti' ya serikali yao), hilo lisikufanye udharau kabisa kila mtz aliyeko nje.
 

Hao unawaita wakenya kwa sababu wana uraia pacha. Kwani kwetu ccm wanasema je kuhusu uraia pacha?
 
Matatizo ni
Ccm
Katiba
Elimu
Kama watanzania mtaamka kudeal na aya mambo mtakuwa mmesolve kila kitu
Maisha ni rahisi sana
Lakini kuna watu huyafanya magumu kwa maslahi yao
Maisha yanapokuwa magumu kwetu kuna watu wanafaidika
 
ukiwafanyia kazi mossad umekuwa mtumwa wa mossad, zama za ujinga huo zilishapita.
Kwani wanaoifanyia kazi serikali yetu wamekua watumwa wa serikali????Mwisho wa siku wote tunahitaji mshahara!!!Huo mfano nilikua nampa mayala kua watanzania wapo wengi huko nje wanafanya makubwa ila wapo low profile kutokana na aina za kazi
 
Ni kama waandishi wa habari wa Tanzania, wapo vizuri kwenye kuandika habari za udaku na majungu na kuisifia serikali ya mafisadi ya ccm, ila wakihitajika kuandika habari zenye tija na mantiki kwenye jamii wote wanapotea. Sijui tatizo ni nini kwenye hili taifa.
 
Kwani wanaoifanyia kazi serikali yetu wamekua watumwa wa serikali????Mwisho wa siku wote tunahitaji mshahara!!!Huo mfano nilikua nampa mayala kua watanzania wapo wengi huko nje wanafanya makubwa ila wapo low profile kutokana na aina za kazi
ndiyo ni watumwa wa serikali. Wanatumia karibia kutwa yao kuitumikia serikali badala ya kufanya mambo yao. Ukiajiriwa wewe ni mtumwa wa aliyekuajiri ndiyo sababu huwezi ukakosa kuwepo kwenye ofisi yake bila yeye kukuruhusu...........kwa wewe unayeabudu kuajiriwa, huwezi ukanielewa. Ajira ni utumwa. Mwenye akili timamu atanielewa
 
Naona hujanielewa Mkuu
 
Nilikua nampa mfano kaka Mayala!!!Watanzania sio kama wakenya hatupendi kujianika anika!!!!Low key's ndio motto wetu sababu kazi zingine ukiwa Diaspora huwezi kuziweka adharani!!!Lakini watanzania wanafanya mengi makubwa tu ila hawajitangazi kama wakenya sababu hawaoni sababu ya kufanya hivyo
 
Acha ufara hapo kuna nchi inayojielewa
 
Na hili nalo la kupost hapa? Hujui kuwa hao wana dual citizenship wanapata mikopo ya SBA ambayo wabongo hawawezi kuigusa labda wale waliokwisha ukana ubtanzania ambao wengi watakauw wanafanya kazi kwenyer taasisi za kiserikali?
Kwani ili ufanye hio biashara lazima uwe na Dual Citzen ship? Ndio matumanini unajipa? Tunapenda sana kujipa matumaini aisee
 
Tanzania itowe raia pacha kwa Diaspora ili nao wakate kiu kwanza. Akili ya kufanya makubwa kama haya nchi yako ikujali uraia wa kuzali sio kukukataa.
Wakenya wako Tanzania wanafanya makubwa na hawana urai Pacha, hebu acheni kujipa matumaini aisee, wakenya wamewekeza sana Tanzania vipi wana Uraia pacha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…