Diane Shima wa Rwanda ni nani na ametokea wapi?

Diane Shima wa Rwanda ni nani na ametokea wapi?

manchoso

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
1,605
Reaction score
2,058
22-28.jpg
4608.jpg


Diane Shima ni mtutsi alizaliwa Kigali 1981, ni mjasiriamali mwanaharakati wa haki za wanawake na kitaaluma ni mhasibu,bado hajaolewa.

Ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabiashara tajiri nchini Rwanda, Assinapol Rwigara ambae alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya jeshi, siasa na biashara za nchi hiyo.

Baba yake alikuwa mfadhili mkuu wa chama cha Rwandan Patriotic Front ambae alikufa katika ajali ya kutatanisha 4.2.2015 katika mji wa Kigali, na kwa mujibu ya familia yake wanasema aliuawa kutokana na sababu za kisiasa.

Diane anakiri kifo hicho cha kutatanisha cha baba yake ni miongoni mwa mambo yaliomsukuma kuingia katika siasa. anasema nchini Rwanda kila mtu anaogopa utawala wa Rais Kagame na watu hawakao huru katika kueleza hisia zao na yeye anasema yupo tayari kupapambana kuondoa ukandamizaji huo na hatoogopa lolote.

Tarehe 3.5.2017, Diane alitangaza nia yake ya kugombea uraisi nchini humo na masaa matatu baade zikasambaa picha zake za utupu ili kumdhalilisha na kumtisha ila pia baadae tume ya uchaguzi nchini humo ilimuondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu kwa madai kuwa aliwasilisha majina ya watu waliokufa kama wadhamini wake wa kugombea kiti cha urais na hatimaye Paul Kagame aliibuka na ushindi wa asilimia 98.8

Rwanda ni nchi inayoonekana inaendelea kiuchumi lakini kuna changamoto katika demokrasia, haki za binadamu na utawala bora. Rais Paul Kagame ametawala kwa muda wa miaka 23, miaka 17 katika hiyo akiwa rais na amesifika kwa kuiltea nchi maendeleo lakini kuna lawama juu yake juu ya kuendesha nchi kiimla na kukandamiza wapinzani.

Hivi karibuni, Mamlaka za Rwanda zilimtia nguvuni Diane Shima akituhumiwa kuhatarisha usalama na kughushi nyaraka.

Kabla ya hapo aliwahi kukamatwa kwa makosa mengine. Mama yake na dada yake pia walikamatwa

Hayo ni machache ninayoyajua kuhusu huyu binti mdogo mwenye ndoto kubwa, aliyethubutu na anaamini ni wakati sasa wa Kagame kuondoka madarakani.
 
Hivi kuna rais aliyeweza kutawala nchi bila jeshi bali akitegemea popularity? Patrice Lumumba aliyetegemea popularity yuko wapi? Kuweni realistic kwenye kauli zenu!
Ndo umeandika nini kiongozi!?
Kuna rais hapa duniani anaeongoza nchi bila jeshi!???
Costa rica na Andora hawana jeshi na wanaishi kwa amani
chukueni hiyo kama mlikuwa hamuijui
 
Sorry, that is U S surrogate.
mshauri na kagame aweke surrogate!!!
point hapo ni suala la kujiamini kwa kiongozi kutokana na utawala wake unaofata sheria na demokrasia, kwa nchi nyingi za africa ambazo viongozi wake ni wachumia tumbo, kufanya hivyo ni ndoto sababu hakuna wanaemuamini sababu ya dhulma na mikono inayonuka damu za watu wasio na hatia hivyo hutumia jeshi kama kinga yao
 
mshauri na kagame aweke surrogate!!!
point hapo ni suala la kujiamini kwa kiongozi kutokana na utawala wake unaofata sheria na demokrasia, kwa nchi nyingi za africa ambazo viongozi wake ni wachumia tumbo, kufanya hivyo ni ndoto sababu hakuna wanaemuamini sababu ya dhulma na mikono inayonuka damu za watu wasio na hatia hivyo hutumia jeshi kama kinga yao
Jielekeze zaidi kwenye dhana ya dola, peace and security na diplomasia utaelewa umuhimu na jukumu la jeshi. Uongozi wa dola siyo mchezo wa ridhaa.
 
Back
Top Bottom