Ni nini kilicho mnusuru Erdogan wa Turkey na mapinduzi?Hivi kuna rais aliyeweza kutawala nchi bila jeshi bali akitegemea popularity? Patrice Lumumba aliyetegemea popularity yuko wapi? Kuweni realistic kwenye kauli zenu!
Ni nini kilicho mnusuru Erdogan wa Turkey na mapinduzi?Hivi kuna rais aliyeweza kutawala nchi bila jeshi bali akitegemea popularity? Patrice Lumumba aliyetegemea popularity yuko wapi? Kuweni realistic kwenye kauli zenu!
Kweli kabisaBila jeshi la kikatiri Kagame ni mwepesi kuliko pamba .
Nakuongezea liechtensteinSorry, that is U S surrogate.
Kwa hiyo PK kutumia jeshi kumdhibiti huyo mama,wewe kwa mtizamo wako unaona siyo woga ila ndio kazi ya jeshi?.Is that what you mean/think?Jielekeze zaidi kwenye dhana ya dola, peace and security na diplomasia utaelewa umuhimu na jukumu la jeshi. Uongozi wa dola siyo mchezo wa ridhaa.
Wewe hebu futa hii comment yako.Nenda kule south china sea ukaone ma destroyer ya Kijapan.Japan wana jeshi tena siyo la kitoto.ongezea na japan
hivi Japan wanajesh? hata Vatican haina Jeshi. thinking aloud, Jeshi la SA linamsaada wowote kwa utawala wa zuma, Kenya je?Hivi kuna rais aliyeweza kutawala nchi bila jeshi bali akitegemea popularity? Patrice Lumumba aliyetegemea popularity yuko wapi? Kuweni realistic kwenye kauli zenu!
Kagame ni muoga sana ! Bila jeshi hawezi kuwa Rais wa Rwanda hata kwa wiki 1
usioneshe ujinga wako hadharani. kama hujui jambo husika kaa kimya au chukua muda kujifunza. jeshi ni chombo cha dola (dola siyo NGO).hivi Japan wanajesh? hata Vatican haina Jeshi. thinking aloud, Jeshi la SA linamsaada wowote kwa utawala wa zuma, Kenya je?
Kwa kweli wamuachie huyu dada. Kagame anamuogopea nini?
Inaamika alihisi baba yake alikuwa team Kateregiya.
msafara wa kima na ngedere wapoMrembo sana huyu dada
[HASHTAG]#freedianarwigara[/HASHTAG]
View attachment 605044 View attachment 604849
Diane Shima ni mtutsi alizaliwa Kigali 1981, ni mjasiriamali mwanaharakati wa haki za wanawake na kitaaluma ni mhasibu,bado hajaolewa.
Ni mtoto wa aliyekuwa mfanyabiashara tajiri nchini Rwanda, Assinapol Rwigara ambae alikuwa na ushawishi mkubwa ndani ya jeshi, siasa na biashara za nchi hiyo.
Baba yake alikuwa mfadhili mkuu wa chama cha Rwandan Patriotic Front ambae alikufa katika ajali ya kutatanisha 4.2.2015 katika mji wa Kigali, na kwa mujibu ya familia yake wanasema aliuawa kutokana na sababu za kisiasa.
Diane anakiri kifo hicho cha kutatanisha cha baba yake ni miongoni mwa mambo yaliomsukuma kuingia katika siasa. anasema nchini Rwanda kila mtu anaogopa utawala wa Rais Kagame na watu hawakao huru katika kueleza hisia zao na yeye anasema yupo tayari kupapambana kuondoa ukandamizaji huo na hatoogopa lolote.
Tarehe 3.5.2017, Diane alitangaza nia yake ya kugombea uraisi nchini humo na masaa matatu baade zikasambaa picha zake za utupu ili kumdhalilisha na kumtisha ila pia baadae tume ya uchaguzi nchini humo ilimuondoa katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu kwa madai kuwa aliwasilisha majina ya watu waliokufa kama wadhamini wake wa kugombea kiti cha urais na hatimaye Paul Kagame aliibuka na ushindi wa asilimia 98.8
Rwanda ni nchi inayoonekana inaendelea kiuchumi lakini kuna changamoto katika demokrasia, haki za binadamu na utawala bora. Rais Paul Kagame ametawala kwa muda wa miaka 23, miaka 17 katika hiyo akiwa rais na amesifika kwa kuiltea nchi maendeleo lakini kuna lawama juu yake juu ya kuendesha nchi kiimla na kukandamiza wapinzani.
Hivi karibuni, Mamlaka za Rwanda zilimtia nguvuni Diane Shima akituhumiwa kuhatarisha usalama na kughushi nyaraka.
Kabla ya hapo aliwahi kukamatwa kwa makosa mengine. Mama yake na dada yake pia walikamatwa
Hayo ni machache ninayoyajua kuhusu huyu binti mdogo mwenye ndoto kubwa, aliyethubutu na anaamini ni wakati sasa wa Kagame kuondoka madarakani.
....Kazi ya jeshi ni kulinda mipaka ya nchi. Popularity huja yenyewe pale unapoongoza (siyo kutawala) wananchi wako kwa uwazi, uhuru, usawa, bila ubaguzi na most of all kwa kufuata misingi ya haki na sheria za nchi. Utakuwa kipenzi cha kila mtu...hutakuwa na haja ya kuzunguka na lundo la maaskari. Siku hizi imebakia tuu mtendaji kata naye kuwa na body guard maana kila mtu sasa ana bodyguard.
hawezi kujiamini kwa sababu ya dhulma utesaji wapinzani na ukandamizaji diane shima alinukuliwa akisema ''Rwanda ni rahisi kumpata mbwa aliepotea kuliko binadamu!!''