Diamond Platnumz na International songs

Katkit

JF-Expert Member
Mar 12, 2023
1,891
4,588
Al Jumaa Mubarak wakuu...

Mwezi uliopita msanii mkubwa zaidi Tanzania Diamond Platnumz aka Chibu Dangote alijinasibu kwamba ataanza kuporomosha mangoma ya hatari kwa kuzingatia soko la ndani na la nje (local & International) na katika kuhakikisha anafanya alichokiahidi, akatoa ngoma mbili kali ambazo ni Shuu ft. Chley pamoja na My baby ft. Chike.

Kwa mara ya kwanza kuzisikiliza ngoma hizo nilipata doubt kidogo kwamba hizi ngoma nikweli kazingatia kulilisha soko la nje au ameanza na soko la ndani pekee? Baada ya mgagasiko huo nilipata kusikia kwamba ngoma aliyomshirikisha Chike (My baby) ndio ameitoa ili isumbue Kimataifa, binafsi niliona kama amechemka, ofcoz ni ngoma nzuri kibongobongo lakini kupenya kimataifa tusidanganyane aisee.

Sasa jana nilipata wasaa wa kusikiliza na kutazama ngoma mpya ya Burna Boy "Big 7" ambayo itakuwa ni miongoni mwa nyimbo zitakazokuwa kwenye album yake mpya inayotarajiwa kuachiwa baadae mwezi huu, kwa akili zangu fupi kama kimo cha Piere Likwidi nikajaribu kufanya comparison na ile ngoma ya kimataifa ya Chibu Dangote, majibu niliyoyapata ni kwamba, Diamond Platnumz aachane kabisa na kauli zake za "international song". You cant claim yourself as an International Musician halafu unatuimbia "My baby" We dont give a fucking https://jamii.app/JFUserGuide!!
Take your time, sikiliza Big 7 ya Burna then uje utoe ushuhuda hapa.

Waasalaam.
 
Ngoja wafuasi wake waje kwa kukupinga kwa kiki na makeke.
Kwa kifupi chibu ni msanii mkubwa Tanzania na Afrika na amejitahidi kutambulisha muziki wa Tanzania Afrika.
 
Back
Top Bottom