Diamond Platnumz adai kuwa ni sahihi kuchukua mapato ya wasanii wake kwa 60%

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
images (1) (4).jpeg

Baada ya sakata linaloendelea mitandaoni kuwa lebo ya WCB inakandamiza wasanii, mkurugenzi wa lebo hiyo, Diamond Platnumz amesema, haoni tatizo kuchukua asilimia 60 ya mapato ya msanii wake.

Amesema anafanya hivyo kwani mziki ni biashara inayohitaji uwekezaji mkubwa na mpaka msanii awe mkubwa inatumika kati ya Sh 400-500 milioni zinakuwa zimetumika kuwekeza kwa wasanii.

Mziki ni biashara, unaona sisi tunavyochukua vijana walikuwepo katika malebo flani ila hawakuwa wakubwa.

“Ila wanapokuja kwetu sisi wanajua kuimba tunachukua kile anachofanya kuwa biashara kiweze kuingiza hela, ndio maana wasanii wa Wasafi wanakuwa wakubwa na matajiri,” amesema Diamond katika mahojiano yake na Kituo cha Kimataifa cha DW

“Biashara inapokuwa kubwa wengi wa vijana wanataka ile biashara aichukue yeye peke yake wakati ni uwekezaji nilifanya haya kwa kuwekeza mamilioni ya pesa zangu ndani yake,”
amesema

Diamond amesema lakini sasa msanii anaposema wanataka kuondoka na biashara nzima siwezi kuruhusu hilo, napaswa kurejeshewa pesa zangu na faida pia.

Sakata hilo limeibuka kufuatia kuondoka kwa msanii Rayvanny wiki mbili zilizopita, ambaye Mwananchi inafahamu kuwa alilipa Sh 1 bilioni kama fidia ya sehemu iliyobaki katika mkataba wake wa miaka 10.

Mtayarishaji nguli wa muziki nchini, P Funk Majani ambaye alifanya vizuri kwa kipindi cha miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000 na lebo yake ya Bongo Records naye alitoa maoni yake kuhusu mikataba ya wasanii wanayosaini na WCB.

Unajua kitu kimoja nachopenda uwe fair, usifanye biashara kuangamiza wenzio, ndio maana hujawahi kuona imetokea kwetu kwamba sisi tuna maelewano yetu na tunakula sambamba, wale wanamdidimiza msanii wanachukua asilimia kubwa halafu yeye anabaki na ndogo, akienda kuimba au kutumbuiza anakatwa hela kubwa, akiuza kwenye albam anakatwa hela kubwa” alisema P Funk na kuongeza.

“Mimi naona tujifunze fair play kwenye industry yetu zote ziwe za filamu, mziki, uchongaji, uchoraji, mitindo kila sekta tuwe na fair play tuelewe pia hizi haki tofauti au atleast kuwe na vyombo ambavyo vinaundika kulinda hizo haki,” alisema

Akijibu tuhuma za P Funk mmoja wa mameneja wa WCB, Hamis Tale Tale “Babu Tale” hakutaka kuliongelea kiundani ila alisema P Funk ni mkongwe na anamheshimu na akasema ishu za mikataba ni ishu za ndani.

Mheshimu mkongwe kasema tuachane nalo, namuheshimu sana P Funk, tumuache na mkataba haupo kwenye mic wala camera tumuache majani, ushawahi kumuona mtu amebandika mkataba kwenye mic au kwenye camera? Heshima ya Majani kwenye hii Industry ni kubwa tumuache,” alisema Tale na kuongeza.

Rayvanny anakuwa msanii wa pili kuondoka kwenye lebo hiyo ya WCB akitanguliwa na Harmonize aliyeondoka mwaka 2019.

Harmonize alikuwa msanii wa kwanza kusainiwa na WCB na alikuwa kwenye lebo hiyo kwa miaka minne.

Alipolazimika kuondoka, kuliibuka mjadala mitandaoni huku yeye mwenyewe akisema amediriki kutoa fedha nyingi ili kuachana na WCB.

Taarifa zinadai alitoa Sh 500 milioni kuvunja mkataba wake uliokuwa umebaki kati ya miaka 10 aliyokuwa amesaini.
 
View attachment 2309683

Baada ya sakata linaloendelea mitandaoni kuwa lebo ya WCB inakandamiza wasanii, mkurugenzi wa lebo hiyo, Diamond
Endeleeni kumponda mwana ila kumkuza msanii ,from zero to hero sio swala dogo na kuna mtu kishaanza kuwachoka wasanii wake mwenyewe ,sasa sijui mzigo wa promo hana au naye anaogopa lawama na maneno ya walimwengu.
Screenshot_20220731-145802_Chrome.jpg
 
Tatizo la sadala alizidi kuwabana maana hata akipata deal la ubalozi analazimisha na wasanii wake watangaze dili hilo wakati yeye pekee ndo kasain na mshiko anapokea wote. Na pia deal nyingi za ubalozi alizidaka yeye kuliko wasanii wake
 
Tatizo la sadala alizidi kuwabana maana hata akipata deal la ubalozi analazimisha na wasanii wake watangaze dili hilo wakati yeye pekee ndo kasain na mshiko anapokea wote. Na pia deal nyingi za ubalozi alizidaka yeye kuliko wasanii wake
Sasa mbona Mbosso, Zuchu wanamadili ya ubalozi hivi nje ya Wasafi msanii gani anadili nyingi kuliko mondi?
 
Mtu kukutoa hatua moja kwenda nyingine mheshimu tu bila kujali madhila uliyokutana nayo. Kinachofanyika kwa wakina harmonize na Rayvann ni sawasawa na yaleyale ya baba mdogo au mjomba kamtoa mtu kijijini kumleta mjini,, sawa ulikuwa hauli ukashiba, sawa ilikubidi kuwapeleka na kuwafuata watoto wake shule, ilkubidi uamke mapema kumfungulia geti asubuhi lakini kama ulifanikiwa kuiona njia kutokea kwake, mheshimu .

Hata sisi wengine tulipitia hayo maisha na sasa hivi tuna maendeleo makubwa hata kuliko watoto wa hao waliotuleta mjini. Tusahau madhila na kuwashukuru kwa kutuonyesha njia.
 
Lavalava je,queen darleen wapo miaka nenda rudi wana ubalozi upi?Zuchu dili nyingi ni za boss wake huwa najiuliza ile wasafi bet nae ni balozi ama kawekwa kama pambo kunogesha biashara ya watu. Nje ya wasafi tuanze na Nandy haya swali jingine?
Sasa mbona mbosso, Zuchu wanamadili ya ubalozi hivi nje ya Wasafi msanii gani anadili nyingi kuliko mondi?
 
Mtu kukutoa hatua moja kwenda nyingine mheshimu tu bila kujali madhila uliyokutana nayo. Kinachofanyika kwa wakina harmonize na Rayvann ni sawasawa na yaleyale ya baba mdogo au mjomba kamtoa mtu kijijini kumleta mjini,, sawa ulikuwa hauli ukashiba, sawa ilikubidi kuwapeleka na kuwafuata watoto wake shule, ilkubidi uamke mapema kumfungulia geti asubuhi lakini kama ulifanikiwa kuiona njia kutokea kwake, mheshimu . Hata sisi wengine tulipitia hayo maisha na sasa hivi tuna maendeleo makubwa hata kuliko watoto wa hao waliotuleta mjini. Tusahau madhila na kuwashukuru kwa kutuonyesha njia.
Kuna wengine Mwanzo walikuwa bodaboda,leo mtu kakutoa kakutengeneza umejulikana,unapata senti kadhaa unaona hapana
Kwenye maisha ya kibiashara hakuna hyo

Ova
 
Lavalava je,queen darleen wapo miaka nenda rudi wana ubalozi upi?Zuchu dili nyingi ni za boss wake huwa najiuliza ile wasafi bet nae ni balozi ama kawekwa kama pambo kunogesha biashara ya watu. Nje ya wasafi tuanze na Nandy haya swali jingine?
Lavalava ana dili la uber, Zuchu ni balozi wa infinix pamoja na kampuni ya nywele na vipodozi za ngozi, sasa best queen darling nae ni msanii au yupo pale kwasababu ni ndugu wa diamond? Nimekuuliza nitajie msanii aliyemzidi diamond kwa ubalozi unasema Nandy upo serious kweli? au ujaelewa swali langu
 
Back
Top Bottom