Diamond na Harmonize wanatuzuga hawajatengana, show zao zina utata

DissDotCom

JF-Expert Member
Mar 31, 2014
395
268
HABARI ZA KAZI WAKUU,

Napenda kutumia muda huu kujadili kuhusu muziki wetu kwa sasa, mahali ulipotoka na unapoelekea... Awli ya yote tuwapongeze wasanii wetu baadhi wanaopeperusha bendera kimataifa.

Wengi najua tunajua habari kubwa zilizotikisa kiburudani katika kufunga mwaka ni kuhusu tamasha la miaka 10 ya Diamond ambapo lilifanyika Mkoani Kigoma na lingine siku hiyohiyo lilikua la Harmonize ambalo lilifanyika Mtwara, hakika burudani ilikua yakufana kotekote kulingana na picha zinazozagaa mitandaoni.

Kwanza tuanze kuzungumuzia nani aliyekuwepo nyuma ya matamasha haya....Tukianza tamasha la DIAMOND nilipata wasiwasi sana baada ya kusikia yeye binafsi amelipia mabehewa 9 ya treni ili watu wasafiri bure, vilevile amelipia hoteli kwaajili ya wote waliokuwepo kwenye hizo behewa, vilevile amelipia chakula kwa wote walikuwepo kwa siku zote watakazokuwepo huko kigoma na kama haitoshi tamasha hilo lilifanyika bureee bila kiingilio, Je gharama hizo alizozitumia hazikuhitajika kurejea au ndio sadaka?

Lakini cha ajabu katikati ya show bila kutarajiwa alipanda Mh. Polepole na kuanza kuongea machache hususani kumpongeza Rais na Chama cha CCM ambapo haikujulikana imekuaje na kuwaacha watu kupigwa na butwaa lakini mwisho wa siku watu wakapata jibu kuwa nyuma ya pazia ni nani aliyeandaa hiyo event...tukirudi kule kwa Harmonize yeye aliweka kiingilio na watu walijaa kuliko kawaida, vilevile kama ilivyo kwa Diamond na kwa Harmonize maswali yakazuka ni nani aliyenyuma ya hizi show, mwishoni ikaonekana wote ni watoto wa baba mmoja kulingana na maudhui ya show zao. Kuna watu wanaweza kuamini moja kwa moja kuwa Harmonize na Diamond haziivi lakini kiukweli kwa jicho la tatu inatazamika ni kama mbinu ya kibiashara ambayo wameibuni ili kuteka soko la mziki nyanja zote...

By the way Big Up kwa Ally Kiba wakati wenzake wanapiga show kubwa yeye alikua anaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa ya mama yake mzazi.
 
Sema ni mbinu yakibiashara ili wateke soko la siasa,na kuwazuga WANYONGE,ambao kuwaona wanamziki ni kwa msimu.
 
Kipimo cha upu.mbavu wa watanzania ni idadi ya wafuasi wa diamond.Sina shaka na ninachoamini kwani sioni anachofanya hadi kuwachanganya madaktari,mainijinia,wanasheria,walimu na wakufunzi wa vyuo bila kuwaacha wasomi katika level zote ambao akili zao zimelingana kabisa na wahuni wa Temeke .

Mtu mwenye akili,ni lazima apitie mule mule..maana kama mtego wa kukamata tai ni kuweka mzoga,unaitafuta ilipo na unaitumia.

Heko ccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba unateseka ulipogundua kwamba hawajatengana, furaha yako kuona chuki kati ya binadamu wenzako.... kongole kwa Kiba mfalme kapumzika kushindanishwa.
 
Back
Top Bottom