SoC01 Dhana ya Ndoa: Jinamizi hatari kwa Ustawi wa Wanawake na Hatma ya watoto

Stories of Change - 2021 Competition
Jul 16, 2021
25
25
Ondoka, nenda kwenu, mwanamke gani wewe, beba mizigo yako na watoto wako, sipendi ujinga!

Haya ni baadhi ya maneno ambayo yamekuwa ni kawaida kwa wanawakewngi kuyapokea kila uchwao,iwe mijini au vijijini hapa nchini. Tafsiri rahisi ya maneno hayo hayo huwa ni ndoa imevunjika, kidudu mtu kimevuruga mahusiano.

Mbaya zaidi kauli hizo hutolewa bila kujali wala kuwepo kwa majadiliano baina baina ya wanandoa waliotofautiana juu ya mustakabali wa namna malezi ya watoto waliopatikana kupitia ndoa hiyo na namna kila upande utakavyonufaika na matunda ya mali zilizopatikana katika kipindi chote walichoishi pamoja.

Ndoto za wanandoa wengi wanapooana huwa ni kuishi pamoja hadi kifo kinapowatenganisha. Vivyo hivyo, wazazi wao, ndugu na jamaa hupenda kushuhudia wanandoa hao wakifanikiwa katika safari ya maisha yao ikiwamo kuwa na familia imara yenye watoto wenye afya bora.

Hata hivyo, siyo wanandoa wote hutimiza ndoto hizo. Kasi ya wanandoa nchini kupeana talaka imeongezeka mara mbili ndani ya miaka sita ya hivi karibuni, jambo linalotishia mustakabali wa ‘taasisi’ hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu.

Ongezeko la Talaka nchini
Utafiti wa kufuatilia kaya Tanzania (National Panel Survey) wa mwaka 2014/15 uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) unaonyesha kuwa kiwango cha talaka kimeongezeka kutoka asilimia 1.1 mwaka 2008/09 hadi asilimia 2.1 mwaka 2014/15.

Hii ina maana kuwa kwa sasa kila watu 100 wenye umri wa kuoa au kuolewa waliopo nchini, wawili wametalakiwa kutoka mmoja mwaka 2008/09. Ikumbukwe kuwa utafiti huo unabainisha kuwa watu takriban 40 kwa kila 100 wanaopaswa kuoa au kuolewa bado hawajaingia kwenye ndoa.

Mbali na talaka, kuna wanandoa takriban wanne kwa kila 100 ambao wametengana, jambo linaloashiria huenda nao wakatalikiana siku zijazo iwapo hawatapata suluhu ya kudumu ya tofauti zao.

Kuvunjika kwa ndoa hizo kunawaweka watoto katika maisha magumu ya kukosa mapenzi ya wazazi wote wawili na hata baadhi yao kujikuta wakiingia mitaani kuwa ombaomba kutokana na kukosa huduma stahiki za malezi.

Lililo baya zaidi kuna kundi la watu wanaodhani wapo katika ndoa ilhali kiuhalisia aina ya kile wanachokitambua wao kuwa ni ndoa hakitambuliki kisheria.

Hawa ni wale wanaishi ndani ya mfumo unaotambulika kama dhana ya ndoa au ndoa dhahania pia maarufu kama sogea tukae.

Waliopo katika kundi hili hususani wanawake wamekuwa wahanga wakubwa pindi mahusiano yanapovunjika kwani wengi wao wamejikuta wakipoteza stahiki zao kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo kutotambulika kama ndoa rasmi.

Dhana ya Ndoa

Je ndoa ni nini? Kuna aina ngapi za ndoa na dhana ya ndoa ni nini?

Kifungu cha 9 cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinaeleza kuwa ndoa ni muungano wa hiyari kati ya pande mbili ambazo ni mwanamke na mwanaume.

Ndoa zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni ndoa ya mke mmoja na wake zaidi ya mmoja ilhali aina za ufungishaji wa ndoa zikiwa tatu ambazo ni ndoa ya dini,kimila na kiserikali.

Ukiangalia aina hizi za ndoa,dhana ya ndoa haiangukii katika kundi lolote hivyo kuinyima hadhi ya kutambulika kama ndoa.Kipindi cha nyuma wanawake wengi walikuwa wanapoteza haki zao mara baada ya dhana ya ndoa kukoma hatua iliyopelekea kuongezwa kwa kifungu cha 160 katika sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinachoitambua dhana ya ndoa ikiwa miongoni mwa wahusika hamna yeyote aliye na ndoa inayotambulika kisheria.

Kifungu hiki kinawatambua wahusika kuwa wako katika dhana ya ndoa endapo watakuwa wameishi pamoja kama mke na mume kwa kipindi kisichopungua miaka miwili na kuwapo kwa ushahidi wa kutosha katika jamii wanayoishi au waliyoishi.

Iwapo mmoja kati ya wahusika akifariki au dhana ya ndoa kuvunjika basi mwanamke au mwanaume anaweza kufungua kesi ya madai ya mali walizochuma kupitia dhana ya ndoa.

Msisitizo hapa ni kuwa inapaswa kufunguliwa kesi ya kudai mali na si kudai ndoa au kupinga ndoa ambayo huenda mwanaume au mwanamke aliyeachwa katika dhana ya ndoa kwasababu si aina ya ndoa inayotambulika kisheria.

Licha ya uwepo wa kifungu cha 160 katika sheria ya ndoa bado wanawake wanaendelea kuwa wahanga wa dhana ya ndoa, pindi mahusiano yanapovunjika mara nyingi wanaume hujiona wao ndio wenye stahiki za kufaidi mali zilizopatikana katika mahusiano yao.

Maumivu ya pili kwa wanawake ni yale yanayotokana na kutelekezewa watotona wanaume waliokuwa wakiishi nao bila ya msaada wowote hatua ambayo inawaweka wanawake katika wakati mgumu katika kutimiza mahitaji ya watoto wao.

Athari hizi haziishi ndani ya familia tu kwani hupelekea kuongezeka kwa watoto wa mitaani na hata mauaji yatokanayo na wivu wa kimapenzi.

Wakati umefika wa kuvunja ukimya na kutoa elimu juu ya uwepo wa dhana ya ndoa kwa wale ambao huamini kuwa wapo katika ndoa ilhali hakuna ukweli wowote,na wahanga wakubwa wakiwa ni wanawake pamoja na watoto.

Uelewa wa Sheria bado ni mdogo
Jamii inapaswa kujengewa uelewa juu ya uwepo wa kifungu cha 160 katika sheria ya ndoa ili wale ambao jasho lao limepotea baada ya mahusiano kuvunjika watumie kifungu hiki kupata haki zao.

Pia jamii inapswa kujengewa uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kufunga ndoa,kuwa na vyeti vya ndoa ambavyo vinaweza kutumika kama vyaraka muhimu pindi ndoa zinapovunjika hatua itakayowezesha kila upande kupata haki yake kwa mujibu wa sheria.

Hatua sahihi zikichukuliwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu hususani vijijini itasaidia kuondokana na dhuluma mpya inayonyonya jasho la wanawake ambao wamekuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha familia zinapata maendeleo na mwisho wa siku matunda ya kilichopatikana wanaume zao wanayafaidi na wanawake wengine ambao hawakuhusika hata chembe katika kuyahangaikia.
 
Nimeipenda taifa lolote linaanza na familia,familia imara inajenga taifa imara,kuvunjika kwa ndoa ndio maana inaleta watoto walio confused,wanaweza hata kuingia kwenye uhalifu sababu upendo ndani yao umepotea,,,,you have my vote
 
Shukrani Maximizer,jitahidi ufunge ndoa na shemeji ili usije kumdhulumu.
 
well said brother
 
Well said!! Mimi pia ni mhanga wa hiyo inayoitwa DHANA YA NDOA. Je, kama mlifanya hiyo SOGEA TUKAE kisha mkatengana kwa zaidi ya miaka mitatu na mmojawapo akafunga ndoa ya Kikristo, yule aliyebaki ana haki zipi kisheria?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom