Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,955
- 828,658
Ni neno la kawaida la kiimani kwa wale waamini na waaminio. Lakini awamu hii ya tano linaelekea kupata umaarufu
Nimejikuta napitia makabrasha mbalimbali ya kidini kuona ni nani wanaopaswa kuombewa na kwanini
.wagonjwa
.yatima
.Wajane
.wenye shida za kiroho
.wenye shida za kimwili
Hawa ndio tmefundishwa kuwaombea kwa imani ya kikristo
Lakini vile vile tuna maombi na sala maalum za kuombea Taifa na viongozi wake wote ...tuna maombi na sala rasmi kila siku ikianza na kila siku ikiisha
Napatwa na ukakasi mkubwa kuendelea kuombwa nimuombee mtu mwenye kila aina ya ulinzi kuanzia wa mitambo mpaka wa majeshi na usalama
Napatwa na mshangao kuendelea kuombwa nimuombee mtu ambaye hajui bajeti yake ya mahitaji ya kila siku kuanzia chakula usafiri ada za watoto shule , mahitaji ya ndugu na jamaa nk nk..vyote hivi anavipata bure na ziada
Hii ni aina fulani ya uchoyo na ubinafsi uliopitiliza...! Hivi yule mgonjwa pale Hospitali ataombewa na nani? Je yule mjane aliyedhulumiwa nyumba na mirathi yake yeye ataombewa na nani?
Nchi imezungukwa na matatizo na shida kila mahali ni vilio na maumivu...maisha magumu hela hakuna kazi hakuna....hawa ndio waombe? Wamuombee asiye na dhiki wala changamoto za maisha yetu haya???jamani mbona mnatuonea na kututia majaribu ni tumkufuru Muumba wetu
Yani kweli kabisa nitoke Muhimbili kumuangalia mgonjwa wangu ninayetakiwa kutafuta pesa ili aweze kutibiwa huku nadaiwa kodi ya nyumba na ada za watoto na mengine mengi...na uchovu wote na changamoto zote hizi halafu niombwe kumuombea mtu ambaye hata nilitaka kuonana naye siwezi? Kweli dunia ina mengi
Uongozi wa nchi ni uongozi wa kisiasa...michezo ya kisiasa inajulikana pote duniani ni michafu tena huku Africa ndio kabisa...kumhusisha Mungu kwenye mambo ya kisiasa ni kumdhihaki
Mtu Hapaswi kuwa na wasiwasi...kama una imani kwa Mungu wako na utendalo ni sahihi hata Mungu anajua , hupaswi kuwa na wasiwasi kwakuwa yeye hachagui wala habagui...na ukitenda kwa haki mkono wake utakuepusha na mabaya yote na malaika mlinzi atakuwa nawe bila hata maombi ya mzinifu, muongo, mtenda dhambi zote....