Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,888
- 831,218
Kuna jambo wana usalama wanafunzwa wanapokuwa mafunzoni ..uwezo wa kumwangalia mtu machoni...hii humfanya mtu anayeangaliwa kukosa ujasiri na kudondosha macho yake ama kuangalia pembeni.
Usifanye hilo kosa kabisa ukiruhusu kukwepesha macho yako umekwisha..hutapata ujasiri wa kimwangalia tena yule mnayeangaliana naye na hapo ndio atacheza na wewe atakavyo.
Macho huongea ukweli wa ndani..uhalisia wa vile ulivyo ama kile ulichokifanya...mara nyingi jambo jema hukupa ujasiri wa kuangalia bila kupepesa macho na jambo baya hukuondolea ujasiri wote na kuhisi unaonwa uovu wako wote.
Siku hizi kwenye makampuni makubwa kama ya simu nk kuna vyumba maalum vya mahojiano ya watuhumiwa wa makosa kazini...smart rooms..vyumba hivi ukituhumiwa unaingizwa hapo pekeyako na kufungiwa na kuanza kuhojiwa kupitia vipaza sauti na watu usiowaona lakini wao walikuona kupitia camera zilizofungwa kwenye hicho chumba. Daima watuhumiwa hufeli mahojiano kwakuwa chumba hurekodi movements na gesture zako zote kwa kila swali...
Kwenye mazingira ya kawaida kabisa mitaani mtu anapo win confidence yako umekwisha...atakuendesha atakavyo. Kuna swali watu wengi wanajiuliza juu ya ukimya mkuu vyombo vya usalama kwa wapinzani kipindi hiki...jamani hiki si ndio kilikuwa kilio chetu?
Sana sana ni ukimya wa CCM ..hawa wamepoteza ujasiri kabisa na kosa kubwaw la kwanza lilikuwa pale airport siku Lissu anatua akiwa na ujasiri wa ajabu mno.
Kwa miaka mitano nchi ilisimamiwa na sauti moja tu ..hakuna waziri wala mbunge aliyejaribu kusema kitu kuzidi sauti kuu ..mwisho wa siku wakawa kama wote wamepigwa ganzi.
Leo hii zinaposikika sauti za wapinzani wote wanaogopa kuzijibu kwa yale mazoea ya kusubiri ruhusa ama sauti kuu iseme..hata vile vitengo vya propaganda vipo kimya kabisa...wanashindwa kulianzisha...wanasubiri maagizo.
Kikubwa kwenye hili ni ile dhana ya ujasiri wa macho na kuhukumiwa na roho kwakuwa kila sauti ya wapinzani ikipaa inabeba ujumbe uliojaa ukweli na uhalisia..kitu kama hicho utaanzaje kukipinga kwa mfano.
Ganzi ya airport inazidi kushika kazi..tumetoka kwenye semi paralysis tunaelekea kwenye total paralysis..hata vyombo vya usalama vinauona uhalisia sasa...kwamba kumbe kile walichoaminishwa kuwa upinzani ni vurugu kumbe sio kweli kabisa.
Nina mashaka huko tuendako vyombo vinaweza kukengeuka maagizo na kufanya kinyume kama wajumbe walivyofanya. Macho huongea uhalisia wetu.
Macho husuta.
Macho hutuondolea ujasiri kama sisi ni watuhumiwa wa mambo mabaya...!!!
Na macho yakikuhukumu uso husawajika na sauti yako hupotea.
Ukimya wao umejaa maumivu mengi..!!!

, kuhusisha kutazamana macho na siasa za uchaguzi Tz kipindi hiki cha kampeni ndio upuuzi wenyewe.