Dhana ya Kumuinua Mtoto wa Kike ni bomu kwa Vizazi vijavyo

Abrianna

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
4,697
15,383
Note: Andiko hili lilitolewa May 16, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kiume Duniani.

Kuanzia mwaka 2018, Dr Jerome wa Trinidad and Tobago alifanikiwa kuitambulisha tarehe 16 May ya kila mwaka kama siku maalum ya kutambua mchango wa mtoto wa kiume katika jamii. Tangu mwaka 2012 UN ilipotambulisha tarehe 10 October ya kila mwaka kama siku ya mtoto wa kike Duniani, swali liliibuka kwa nini tunatenga watoto? Kwanini tuna siku ya mtoto wa kike na hatuna siku ya mtoto wa kiume?

Ndugu zangu mtakubaliana na mimi kwamba katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia matabaka makubwa katika makuzi na malezi ya watoto wetu wa kike na wa kiume na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya WATOTO WA KIUME. Jitihada za lazima zisipofanywa na wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kumrudisha mtoto wa kiume katika nafasi yake madhara yanaweza kuwa makubwa sana. Naomba leo tukiwa tunaadhimisha siku ya mtoto wa kiume duniani niwakumbushe madhara machache tu kati ya hayo ili tuweze kujua na kutambua wajibu wetu;

1. Kwa sasa zaidi ya 20% ya watoto wa kiume wanaacha shule kati ya umri wa miaka 15 - 24. Wengi wao wanaenda kuwa madereva boda boda au watumishi kwenye migodi na mashambani. Wengi wa vijana hawa wanaishia kupata vilema vya maisha kama sio kufa kabisa kutokana na ajali nyingi za bodaboda na hivyo kupokonywa haki yao ya kuishi maisha kamilifu.

2. Watoto wetu hawa wa kiume hawakuwahi kushiriki katika mila wala desturi zozote kandamizi dhidi ya wanawake, hivyo hawaelewi kwa nini mtoto wa kike anapendelewa. Wakiendelea kuishi hivi watajenga chuki dhidi ya wanawake, na kwa kuwa bado 70% ya viongozi wataendelea kuwa wanaume, tutarudi tulikotoka kuwa na wanaume wasiothamini uwezo wa wanawake kwa kuwa wao hawakuthaminiwa katika makuzi yao walishuhudia wanawake wakipendelewa na hivyo wataona ni fursa ya kurudisha kisasi.

3. Watoto wetu wa kiume tusipowaandaa kujua namna ya kuishi na hawa watoto wa kike tunaowajenga kwa sasa tutashuhudia ndoa nyingi kuvunjika, watoto wengi kulelewa na single parent, wanaume kutokujua majukumu yao kwenye familia. Mwisho wa siku hawa watoto wa kike tunaowajengwa kwa nguvu zote watakosa support kutoka kwa watoto wetu wa kiume.

4. Kuongezeka kwa ukatili wa kijinsia, watoto wetu wa kiume watakaposhindwa kushindana kwa hoja na watoto wa kike tutashuhudia na tayari tumeshashuhudia kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa watoto wetu wa kike kwa kuwa wako empowered na watoto wetu wa kiume hawajui namna ya kuishi nao. Hivyo watoto wa kiume wataendelea kutumia UBABE ili tu uwanaume wao uweze kuonekana.

5. Kuongezeka kwa vitendo vya ujambazi na matumizi ya madawa ya kulevya. Waathirika wakubwa wa madawa ya kulevya ni watoto wetu wa kiume na pia wao ni rahisi mara 20 zaidi ya watoto wa kike kufungwa jela. Mtoto aliyekosa makuzi sahihi ukua akiwa hatari kubwa kwa jamii iliyomzunguka. Tukiendelea kuwatenga watoto wa kiume vitendo vya ujambazi, unyang'anyi, ubakaji, utapeli n.k. vitaongezeka na hivyo kuendelea kumpoteza mtoto wa kiume na kuhatarisha maisha ya jamii inayomzunguka.

6. Kwa sasa kuna nia madhubuti kabisa ya kumwinua mtoto wa kike kielimu na kumpatia fursa mbalimbali za kumkwamua kiuchumi. Fursa hizi watoto wa kiume hawapati na hivyo wengi wakikosa kazi utawakuta VIJIWENI hata ukitoka nyumbani kwako leo angalia njia nzima unayopita utaona makundi ya watoto wa kiume wenye nguvu na hari lakini hawana kazi za kufanya. Hii inasababisha wakose vipato na hivyo kutegemea kuishi kwa kubangaiza au kutegemea watoto wa kike.

Watoto wetu wa kiume wamekuwa wavivu, hawajiongezi, hawajui majukumu yao, wengi wanapenda kulelewa, hawafanyi vizuri kwenye mitihani yao mashuleni n.k. lakini je NANI WA KULAUMIWA?

Leo ni siku nzuri sana tunaposherehekea hii siku ya mtoto wa kiume duniani wanajamii wenzangu tujiulize, nini mchango wetu katika kumpoteza mtoto wa kiume ? Na je nini kifanyike ili tuanze kurekebisha haya makosa?

Naomba nimalize kwa kunukuu msemo wa Frederic Douglas usemao " It is easier to build strong children than to repair broken men ". Watoto wa kiume wana haki sawa na watoto wa kike kupata Elimu bora, Fursa za kujikwamua kiuchumi na Kuendelezwa vipaji vyao.

Imeandikwa na
Mercy Mchechu - Mkurugenzi Rightway Schools
 
Note: Andiko hili lilitolewa May 16, Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kiume Duniani.

Kuanzia mwaka 2018, Dr Jerome wa Trinidad and Tobago alifanikiwa kuitambulisha tarehe 16 May ya kila mwaka kama siku maalum ya kutambua mchango wa mtoto wa kiume katika jamii. Tangu mwaka 2012 UN ilipotambulisha tarehe 10 October ya kila mwaka kama siku ya mtoto wa kike Duniani, swali liliibuka kwa nini tunatenga watoto? Kwanini tuna siku ya mtoto wa kike na hatuna siku ya mtoto wa kiume?
Naomba nimalize kwa kunukuu msemo wa Frederic Douglas usemao " It is easier to build strong children than to repair broken men ". Watoto wa kiume wana haki sawa na watoto wa kike kupata Elimu bora, Fursa za kujikwamua kiuchumi na Kuendelezwa vipaji vyao.
 
Jumuiya na asasi za kijamii pamoja na mm mwenyewe tusipokuwa makini tutaanza kampeni ya kumuinua mtoto wa kiume

Kwa miaka hii ya karibun kumeibuka haki sawa za kijinsia na hapo ndpo mtoto wa kike anapopewa kpaumbele Sana kuliko wa kiume

Usasa na wanawake wanaojiita wanaharakat wametufanya tuucheze huu wimbo wao nakumsahau mtoto wa kiume

Ongezeko la mashoga n kubwa Sana mitaani na wanaharakat wanasema n haki yao

Nje ya mada hivi Bibi @hellenkijobisimba kaolewa?
 
Ni kweli, mimi naona hili jambo la kuwainua watoto wa kike litakuja kuwapa shida haohao watoto wa kike kwa sababu watakosa waume bora wa kuwao, taifa litakosa respobsible men in future na kutakua na gap kubwa sana kati ya wanaume na wanawake maana hawa wa kiume watakua wamesahaulika

Watakosa ujasiri mbele ta watoto wa kike, kwa namna hiyo tutakua na kizazi ambacho hakina balance kati ya mwanaume na mwanamke

Mwisho kabisa, mwanaume ni kichwa ndani ya familia, na familia ni component ya taiafa, hii familia ikikosa mwongozo mzuri basi taifa litakua halina mwongozo mzuri pia, tutakua na taifa lenye wananchi wa hovyo kabisa

Ni wakati wa serikali kuingilia kati, kuweka mchakato wa usawa kati ya watoto wa kiume na wa kike
 
Ngoja feminist waje
Naskia harufu ya Vita hapa
Kama una watoto you can well understand this, binafsi nadhani watoto wote wanatakiwa kupewa usawa bila kuathiri jinsia na uasili wa jinsia, ni lazima tuwafundishe watoto asili ya jinsia zao ili tuwe na vizazi bora ambavyo mwanamke atakua anatambua majukumu yake kama mwanamke na mipaka yake kama mwanamke, na mwanaume atakua anatambua majukumu yake kama mwanaume na mipaka yake kama mwanaume
 
Jumuiya na asasi za kijamii pamoja na mm mwenyewe tusipokuwa makini tutaanza kampeni ya kumuinua mtoto wa kiume

Kwa miaka hii ya karibun kumeibuka haki sawa za kijinsia na hapo ndpo mtoto wa kike anapopewa kpaumbele Sana kuliko wa kiume

Usasa na wanawake wanaojiita wanaharakat wametufanya tuucheze huu wimbo wao nakumsahau mtoto wa kiume

Ongezeko la mashoga n kubwa Sana mitaani na wanaharakat wanasema n haki yao

Nje ya mada hivi Bibi @hellenkijobisimba kaolewa?
Na pia kwa miaka hii ya karibuni limeibuka wimbi la watoto wa kiume ambao ni tegemezi au wanapenda kulelewa, hii ni moja ya impact ya hii kampeni ya kumwinua mtoto wa kike ambayo ilianza miaka mingi nyuma

Tusipoangalia hili jambo kwa jicho la tatu tutapoteza kizazi cha watoto wa kiume
 
Kama una watoto you can well understand this, binafsi nadhani watoto wote wanatakiwa kupewa usawa bila kuathiri jinsia na uasili wa jinsia, ni lazima tuwafundishe watoto asili ya jinsia zao ili tuwe na vizazi bora ambavyo mwanamke atakua anatambua majukumu yake kama mwanamke na mipaka yake kama mwanamke, na mwanaume atakua anatambua majukumu yake kama mwanaume na mipaka yake kama mwanaume
Well said
Hicho ndicho kinachotakiwa
Mwanaume afanye majukumu yake, na mwanamke/msjchana pia. Pasipo jinsia moja kupewa favour zaidi ya nyingine.
 
Kama una watoto you can well understand this, binafsi nadhani watoto wote wanatakiwa kupewa usawa bila kuathiri jinsia na uasili wa jinsia, ni lazima tuwafundishe watoto asili ya jinsia zao ili tuwe na vizazi bora ambavyo mwanamke atakua anatambua majukumu yake kama mwanamke na mipaka yake kama mwanamke, na mwanaume atakua anatambua majukumu yake kama mwanaume na mipaka yake kama mwanaume
Siku hizi wanawake wako bize kutaka kujionesha kuwa wanaweza fanya kila kitu ambacho mwanaume anaweza fanya wakati kiasili kila mtu ana majukumu yake

Haya mambo ya haki sawa naona kabisa maana asili ya harakati hizi zimepotoshwa na baadhi ya watu kuwa kufanya iwe mashindano Kati ya mwanamke vs mwanaume
 
Na pia kwa miaka hii ya karibuni limeibuka wimbi la watoto wa kiume ambao ni tegemezi au wanapenda kulelewa, hii ni moja ya impact ya hii kampeni ya kumwinua mtoto wa kike ambayo ilianza miaka mingi nyuma

Tusipoangalia hili jambo kwa jicho la tatu tutapoteza kizazi cha watoto wa kiume
Unaonaje hii reply tuingenezee bango likae pale posta?
 
Siku hizi wanawake wako bize kutaka kujionesha kuwa wanaweza fanya kila kitu ambacho mwanaume anaweza fanya wakati kiasili kila mtu ana majukumu yake

Haya mambo ya haki sawa naona kabisa maana asili ya harakati hizi zimepotoshwa na baadhi ya watu kuwa kufanya iwe mashindano Kati ya mwanamke vs mwanaume
Hii imesababishwa na hizi kampeni za kumwinua mtoto wa kike, na sijui nini kifabyike ili turudi kwenye msitari la sivyo madhara yatakua makubwa baadaye
 
Back
Top Bottom