Dhana potofu kuhusu bima ya afya, nashauri ipigwe vita ni wakati wa watanzania wapewe elimu zaidi kuhusu umuhimu wa bima ya afya kwa wote

Doctor MD

Senior Member
Jan 10, 2020
129
147
Katika chanzo kikuu Cha kuendesha mfumo wa maisha basi afya ni kitu Cha msingi zaidi katika kuendesha uchumi hata siasa.
Nadhani wengi au baadhi yetu tushawahi pitia maswaibu ya kuuguza au wenyewe kuugua lakini Kama mjuavyo gharama za matibabu zimekuwa ghali hii huchangiwa zaidi na gharam za uendeshaji wa hizo hudum za afya.
Na gharama hizo huja ghafla kutokana na magonjwa mengi huja ghafla hivyo hupelekea mtu kutumia nguvu nyingi Sana katika matibabu hayo
Sasa ni wakati wa watanzania kutambua kwamba magonjwa yasioambukiza nayo Yana athiri Sana uchumi
Hebu tuhamasishane zaidi kujiunga kuokoa gharama ambazo ni kubwa wakati wa matibabu
 
Kwa miaka ya hivi karibuni bima imekua kitu muhimu sana kwa kila mtu na inaweza kuokoa mtu pale usipotarajia, lakini hapo nyuma kidogo ilikua ni uozo.

Kuna mzee wangu mmoja aliwahi fariki miaka ya 2013 kwa kucheleweshewa huduma kisa anatumia bima, toka miaka hiyo sikuwahi amini bima tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yeah usemalo upo sahihi Mana kipindi Cha nyuma bima ilionekana kama kitu Cha kawaida Sana lakin kwa Sasa mambo yamebadilika Sana hospital zimekuwa zikifaidika na zenyewe kupitia hizo bima kwa kiwango kikubwa

Ikiwemo:-
1. Madaktari kutoa huduma haraka kwa mgonjwa kutokana na uwepo wa dawa na vipimo kupitia hizo bima
2. Na bima imekuwa nguzo katika kulipa pesa kwa hospital ili ziendeshwe
 
Mfano mzuri
CT scan ya kichwa Ina range Tsh 200K-300K hizo ni bei ya kawaida kabisa chukulia ndugu yako anahitajika afanyiwe hiyo CT scan kwa haraka haraka na hiyo hela huna lakini ungekuwa na bima inakuwa rahisi kufanyika
 
Back
Top Bottom