Design simple za Nyumba vyumba 2

Mkuu nikuombe kitu kimoja, kama haita athiri malengo na mtazamo wako kwenye hili bandiko, niombe ukiweka picha ya nyumba tuwekee na plan yake bila vipimo , itatushawishi zaidi kuona mpangilio wa vyumba, sebure nk,asante

Asante kwa wazo zuri.
 
gharama zote ni milioni 10 kwa ujenzi wa kawaida kisha unahamia nyumba yako. Kwa anayetaka complicated finishing na installations ya vitu vya pesa ndefu basi ni 25-30 milioni.

kwa uzoefu wangu mdogo naona kama unawadanganya wananchi wa kawaida.....kwamba 10m ujenzi wa kawaida nyumba imeisha unahamia kwako...duhh. Sio kweli aisee. Nimepiga hisabati zangu naona kama msingi au hiyo unayoita substructure ukijibana sana itagharimu kama 7.326 milion kwa mchanganua huu hapa chini

1- tofali 1206 @ 1000/= = tshs 1,206,000/=
2- cement 30bags @13,000/= =tshs 390,000/=
3- mchanga 5 lories @ 150,000/= =tshs 750,000/=
4- chuma 30pcs y12 @ 16,000/= = tshs 480,000/=
5- zege 13.2 cubic metre @ 225,000/= =tshs 2,970,000/=
6- labour charges =tshs 1,000,000/=
7- gharama nyinginezo =tshs 500,000/=
hapo nimejaribu kuchanganua gharama za ujenzi wa msingi...na ikizingatiwa nyumba ni msingi ndugu yangu...sasa tunafikia milion 7...hatujanunua bati, hatujanunua mbao, hatujanunua milango na madirisha, bado wiring, bado plumbing installations, bado plastering nje na ndani, bado ceiling brandering, bado ceiling boards, bado skimming, bado painting, bado magrill ya milango na madirisha.

Kaka unawadanganya watu...waambie ukweli wakiingia waingie kiume au wawe wamejipanga kujenga.

Kwa uzoefu wangu hicho kijumba cha vyumba viwili kwa hizo sq metre 88 hakuna jinsi utakimaliza kukijenga kwa standard ya kawaida kikawa chini ya mill 44. Na ukizingatia muonekano wake kwenye 3d au perspectives...kinaweza kuzidi gharama iwapo anasa zitazidi kwenye finishing.

Ni hayo tuu....
 
Uko sahihi whoCares?

BOQ ni 47Milioni, imefanyika.
 
Last edited by a moderator:
sasa hapo ndio patamu!!

Mbona naamini mungu?

Lbd kuna imani ya ziada?

Mbona najitahidi kuisaka sh??

Mbona ctoki kama wenzangu??

Mbona cfanikiwi???

Kila kukicha heri ya jana...

Lbd kuna ninapokosea ila cjajua ni wapi!!!


ahahahahaa...nisamehe nahisi kama nitakuwa nimekukwaza.....kuna sehemu kubwa tuu umeikosea...wealth can be aqcuired through 2 main ways
1- self made
2- inheritance
njia ngumu kuliko zote kuwa tajiri ni ya kwanza ingawa pia ni njia ambayo kila aliyeupata utajiri kwa njia hiyo aliheshimiwa sana.

Njia ya pili ni rahisi ila wengi hawaijui wamejazana kwenye njia ya kwanza.......utajiri kwa kurithi. Ndio, mungu alivyotuumba alitupatia kila mtu kipawa au uwezo wa ziada wa kuzaliwa nao unaoweza kumfanya akabiliane na changamoto zozote zinazojitokeza mbele yake.

Dada sahivi tumia kile alichokupa mungu kitakufaa na utafanikiwa...tumia urithi wako uwe tajiri ufanikiwe.
 
Chumba, sebule, master, na public toilet, hii poa kwa servant quoter
 
Mkuu nikuombe kitu kimoja, kama haita athiri malengo na mtazamo wako kwenye hili bandiko, niombe ukiweka picha ya nyumba tuwekee na plan yake bila vipimo , itatushawishi zaidi kuona mpangilio wa vyumba, sebure nk,asante

Vema rejea ukurasa wa kwanza, floor plan imewekwa pale.
 
Chumba, sebule, master, na public toilet, hii poa kwa servant quoter

Mm ushari wangu naona sio mbaya ukaweka na ukubwa (urefu*upana) wa eneo itakapo fiti hiyo ramani husika ili tujipime na ukubwa wa viwanja vyetu hivi vya hatua.
 
Mm ushari wangu naona sio mbaya ukaweka na ukubwa (urefu*upana) wa eneo itakapo fiti hiyo ramani husika ili tujipime na ukubwa wa viwanja vyetu hivi vya hatua.

Ni rahisi sana plot yako ni kiasi gani!? Bofya namba hiyo tukusaidie
 

Vyumba viwili milion 47?? khaaa
 
Three bedroom self contained
 
Mkuu jenga tabia ya kuamini kile wanachofanya watz wenzako, mpaka ramani huamini kama mtanzania anaweza kuchora? wewe mpe specifications unazotaka uone kama hatokupa kitu roho inataka (kwenye sector hii tuna vijana wanaweza)

Ofcoz jamaa katudhalilisha sana, ina maana hajui kama Architects na Cartographers tupo hapa hapa Tanzania? Tatizo tumezoea kila kitu ni mpaka mzungu tu.

Kazi nzuri mtoa mada japo nakushauri utoe sample tu ila usiweke Ground floor plan na "measurements" zake kama lengo ni matangazo tu, nadhani umenisoma hapa namaanisha nini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…