Dereva wa Basi la Mwendokasi adaiwa kuwapitiliza Vituo Abiria baada ya kukasirishwa

Dereva katoka Gerezani akiwa na hasira gari limejaa milango hadi inataka kupasuka, Akasimama Faya watu wakawa wanamwambia kwa jinsi Gari ilivyojaa sana unatuumiza funga fungua fuata utaratibu sababu gari ni express kama ilivyoandikwa simama manzese kama ilivyo taratibu

Dereva akasimama na Magomeni kwa hasira, hapo gari imejaa vibaya sana na ni express, watu wakaanza kelele tena unatuumiza huku mlangoni na hakuna wakushuka na wala wakupakia, wakwamwabia wapo wakushuka manzese

Dereva akasimama anaanza kuzozana na abiria Kwa hasira

Dereva akawasha Gari kutoka Magomeni hakusimama hata kituo kimoja kwa hasira akaenda kuwashusha Abiria wote Kimara Mwisho hapo Kuna walemavu kibao, akashuka akapotea kusikojulikana, likatokea bonge la fujo pale, watu warudishwe walipotokea fujo kubwa sana, ikabidi Gari achukue Dereva mwingine awarudishe watu waliopitilizwa vituo

View attachment 2938988

Huu mradi unauliwa na wafanyKazi wenyewe ni shida
Safi sana dereva.Nchi imejaa wajinga hawajui kuiwajibisha serikali iliyokosa mwelekeo, wanapinga mambo ya kijinga ''eti mchele umewekwa vimelea vya ushoga''
 
Dereva katoka Gerezani akiwa na hasira gari limejaa milango hadi inataka kupasuka, Akasimama Faya watu wakawa wanamwambia kwa jinsi Gari ilivyojaa sana unatuumiza funga fungua fuata utaratibu sababu gari ni express kama ilivyoandikwa simama manzese kama ilivyo taratibu

Dereva akasimama na Magomeni kwa hasira, hapo gari imejaa vibaya sana na ni express, watu wakaanza kelele tena unatuumiza huku mlangoni na hakuna wakushuka na wala wakupakia, wakwamwabia wapo wakushuka manzese

Dereva akasimama anaanza kuzozana na abiria Kwa hasira

Dereva akawasha Gari kutoka Magomeni hakusimama hata kituo kimoja kwa hasira akaenda kuwashusha Abiria wote Kimara Mwisho hapo Kuna walemavu kibao, akashuka akapotea kusikojulikana, likatokea bonge la fujo pale, watu warudishwe walipotokea fujo kubwa sana, ikabidi Gari achukue Dereva mwingine awarudishe watu waliopitilizwa vituo

View attachment 2938988

Huu mradi unauliwa na wafanyKazi wenyewe ni shida
Mbona gari lenyewe halijajaa ila abiria ndo hawataki kusogea mbele?
 
Sitasahau siku moja asubuhi kabisa nawahi kwenda kariakoo pale usalama Nampa Hela mkata ticket ananiamba Hana chenchi nikatafute mim nimleteee ikiwa kamili ,muda huo Ni asubuhi hata maduka ya kununua vocha ili nipate Hela ya kumpa Hakuna .....aiseeee siku ile nilitoa tusi ambalo sikuwahi mtukana MTU yeyote toka nazaliwa .....Kwa hasira nikapanda pikipiki Kwa hasira ,nikala hasara maana nilitoa 6000 kwenye pikipiki
Kata tiketi online achana na mambo ya Chenji
 
Wana stress hai za malipo.
Na sikunhiiz wana kautaratibu kabaya sana. Ukienda kukaka ticket wanakuambia auwape 250 maana hawataki kusumbuka kutafuta chenji.

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba, zile kazi za kukata tiket na ku scani kwakwel inabid wapewe viwete na walemavu wengine ambao wanamudu kufanya.
Na wanaua Sana waendesha boda boda na bajaji hasa njia ya Kimara to kibaha
 
Abiria nao wa hovyo, unakuta mtu kasimama kashikilia mlango ukifunguka anaruka nao kama kambale kanaswa na ndoano, anaona kabisa pameandikwa usisimame hapa yeye ndio anasimika milonjo yake, wengine wanasimama kwenye kisahani cha maungio anakuwa anazunguka kama dracula, halafu watu wa dar sikuhizi wana mdomo sana
 
Tatizo abiria wa Daslam ni wajuaji sana...
Mpaka kutumia mwendokasi manake bado tunajitafuta hivyo tuvumiliane, tubanane kila mtu apate huduma.
Sasa ukileta ujuaji hata mimi nawasha Gari toka Gerezani mpaka Kimara bila kusimama wala kupunguza speed, si mnaharaka bwana ?
Kuna Dereva yeye huchochea speed ile ile akiulizwa anajibu hii ni mwendokasi sio Daladala.
 
Hata abiria wavuta bangi tu, aliyewaruhusu kusimama mlangoni ni nani?
Mtu kasimama mlangoni anamwamuru dereva asifungue mlango, haya dereva kanyooka hadi kimara bado wanamlaumu dereva kwa kutofungua mlango, gari limeandikwa express wanajua hilo likitoka faya kituo cha kwanza kimara bado mtu kapanda, inaonekana kuna shida mahali katika jamii yetu
 
Kwa mujibu wa mtoa habari, dereva alikuwa anasimama vituo anavyotakiwa kama kawaida ila abiria wakawa wanashout kwamba anyooshe!! Sioni kesi hapo....! Unless sijaelewa mnieleweshe
Kwamba watu walikuwa wengi hivyo akisimama wanaongezeka na wao wamepanda express yenye vituo vichache vya kushusha na kupanda na sio vituo vyote
 
Abiria nao wa hovyo, unakuta mtu kasimama kashikilia mlango ukifunguka anaruka nao kama kambale kanaswa na ndoano, anaona kabisa pameandikwa usisimame hapa yeye ndio anasimika milonjo yake, wengine wanasimama kwenye kisahani cha maungio anakuwa anazunguka kama dracula, halafu watu wa dar sikuhizi wana mdomo sana
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Aisee eti kama dracula.
 
Mmoja alipeleka gari la Kivukoni Gerezanii Abiri waliwasha motooo hatarii sijui waliishi wapi hao madereva wanahisi hayo magari ni yaoo
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜
Hizi jeuri dar huko huko
Arusha kwanza wanakuruhusuje utoke nje ya kituo na umewapitilizisha kituo
Ha ha ha watu wa Arusha achen vitisho kule yule Dogo Dangote alikuwa anawalaza saa 12 jion ha ha ha
 
Back
Top Bottom