Dereva wa basi La Isamilo Afariki Dunia Akiwa Njiani

Dereva wa basi La Isamilo Afariki Dunia Akiwa Njiani

Chibudee

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2016
Posts
1,775
Reaction score
2,408
Shinyanga. Dereva wa Basi la Isamilo linalofanya safari zake kutoka Mwanza kwenda Mbeya nchini Tanzania Sebastian Mathias (43) mkazi wa Mwanza amefariki dunia wakati akiendelea na safari kutoka Mbeya kwenda Mwanza.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga, Deborah Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Ijumaa Machi 20,2020 saa nne asubuhi.

Kamanda Magiligimba amesema Sebastian wakati akitoka Mbeya kwenda Mwanza alikuwa akijisikia vibaya walipofika Singida ndipo hali yake ilibadilika wakawa wamebadilishana na dereva mwenzake.

“Katika basi hilo, madereva walikuwa wawili lakini baada ya kuona hali yake imebadilika alibadilishana na mwenzake yeye akaendelea kupumzika lakini walipofika saa nne asubuhi akawa amezidiwa sana, wakambeba na kumpeleka katika kituo cha afya Tinde," amesema Kamanda Magiligimba.

Magiligimba amesema baada ya kumfikisha hospitali daktari alibaini kuwa tayari Sebastian alikuwa ameshafariki dunia.

Amesema kwa kuwa gari lina madereva wawili, dereva mwingine ameendelea na safari kwenda Mwanza na maiti imehifadhiwa katika kituo cha afya cha Tinde.

20200320_154123.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
RIP sana kwa dereva. Pole nyingi kwa familia, ndugu jamaa na watanzania kwa ujumla akiwemo tajiri mwenye mabasi.

Ndugu mtoa habari na muwasilisha uzi, naomba wakati mwingine useme maiti amehifadhiwa na sio maiti imehifadhiwa............
 
Nadhani ni sahihi maana neno maiti lipo katika ngeli ya nomino ya I/ZI. Nisahihishwe kama nimekosea.
 
Nadhani ni sahihi maana neno maiti lipo katika ngeli ya nomino ya I/ZI. Nisahihishwe kama nimekosea.
... kwa binadamu maiti ana heshima zake tofauti na mnyama ndio yenye hizo ngeli zako ulizotaja.
 
RIP sana kwa dereva. Pole nyingi kwa familia, ndugu jamaa na watanzania kwa ujumla akiwemo tajiri mwenye mabasi.

Ndugu mtoa habari na muwasilisha uzi, naomba wakati mwingine useme maiti amehifadhiwa na sio maiti imehifadhiwa............
Maiti imehifadhiwa ni sahihi.
Mwili wa marehemu /merehemu amehifadhiwa ni sahihi.
Na sio maiti amehifadhiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa heshima ya ubinadam kuliwekwa spesho kesi kwa maiti ya mwanadamu mkuu

Heshima gani unataka, maiti ya mfalme tu walisema imehifadhiwa vipi ya dereva 😂😂😂

Tufanye yetu kadiri ya uwezavyo mbaba, tukishakufa yoyote/yeyote unakuwa 'chochote', heshima inaisha pale pumzi ya mwisho.inakata!
 
Imehifadhiwa Sioni Kama Inadhalilisha
Labda Kiswahili Kipana
Heshima gani unataka, maiti ya mfalme tu walisema imehifadhiwa vipi ya dereva [emoji23][emoji23][emoji23]

Tufanye yetu kadiri ya uwezavyo mbaba, tukishakufa yoyote/yeyote unakuwa 'chochote', heshima inaisha pale pumzi ya mwisho.inakata!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom