Dereva anaposhambulia mtu asiyemjua kutetea uvunjaji wa sheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dereva anaposhambulia mtu asiyemjua kutetea uvunjaji wa sheria

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Jan 15, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  MWENYEKITI WENU NIMEVAMIWA NA KUSHAMBULIWA PORINI MADIBIRA

  Hizi si habari njema. Juzi alhamisi kunako saa kumi na mbili na nusu asubuhi nilipatwa na balaa la barabarani.
  Ilikuwaje? Niliondoka Iringa Jumatano jioni kuelekea kijijini kwetu Nyeregete. Nilifika Madibira, Mbeya jioni ya saa kumi na mbili na nusu. Kwa vile giza lilikaribia, nikaamua kulala kijijini Mahango, nyumbani kwa ndugu yangu aitwaye Salim Raphael Mjengwa.

  Alfajiri tukaondoka pamoja maana naye alitamani kufika kijijini Nyeregete kumsalimu baba yake mzazi. Tukiwa katikati ya pori eneo la Ikoga kuelekea mji wa Rujewa nikabaini gari iliyokuwa ikija nyuma yetu kwa mwendo wa kasi.

  Nikamwambia ndugu yangu Salim juu ya uwepo wa gari nyuma yetu. Akaniambia kuwa ni basi dogo la abiria. Kupitia sight mirror nikamwona dereva wa nyuma yangu akijaribu kunipita mahali pasipostahili na kwa mwendo wa kasi. Kwa vile barabara ilikuwa ni nyembamba sana , basi, akalazimika kukatisha jaribio la kunipita.

  Baada ya mwendo wa nusu kilomita hivi nikapaona mahali muafaka pa kuegesha gari yangu pembeni kumruhusu apite. Nikawasha indiketa, nikaweka gari yangu pembeni. Dereva yule akapita na kusimamisha gari yake katikati ya barabara. Akatoka kunifuata. Nami nikaanza kujiandaa kufungua mlango na mkanda wangu ili nitoke tuongee. Kabla hata sijafungua mlango, yeye akauvuta mlango wangu na kunishambilia kwa ngumi usoni. Nikainamisha uso wangu kwenye usukani. Nikasikia pia ndugu yangu Salim akitamka; " Seme unafanya nini?" Salim alimfahamu kwa jina dereva huyo, anaitwa Seme.

  Mara, dereva mwenzangu akaacha kunishambulia na kunitukana. Nikainua kichwa. Nikamwona akiondoka huku kundi la vijana waliokuwa abiria wake nao wakirudi kwenye gari lao. Walikuja kushiriki shambulizi dhidi yangu. Walikuwa na dhamira mbaya sana. Kama si uwepo wa ndugu yangu Salim ambaye wote walimtambua hadithi ingekuwa nyingine.

  Tulipofika Rujewa nikaripoti tukio hilo kituo cha Polisi Mbarali. Dereva mwenzangu naye akafika kituoni. Afande Mwamakula, ambaye ni mkuu wa kituo aliweka wazi kuwa alichofanya dereva yule ilikuwa ni jinai.

  Kwa vile nilihitajika kufika kijijini kumwona mgonjwa aliye taabani. Na kwa vile nilihitajika kurudi Iringa kupokea ugeni kutoka Ubalozi wa Sweden. Na kwa vile dereva yule alikiri kosa lake na kuniomba radhi. Na kwa vile dereva yule aliweka wazi kuwa ni msomaji wa makala zangu, basi, nikaamua kutoendelea na shauri lile. Nilimsamehe kwa kumwambia; hupaswi kufanya tendo kama lile kwa mtu yeyote yule. Ule haukuwa uungwana.
  Wenu, Maggid Mjengwa, Iringa.
   
 2. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,678
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Pole kaka, pole saaana kwa yaliyokukuta. Endelea kutoa elimu mbadala kwa tulio wajinga bado, tuko wengi tunaohitaji msamaha na kuelimishwa hasa huku vijijini.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Inaelekea huko vijijini ni kujichukulia sheria mkononi.
   
 4. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,975
  Likes Received: 6,612
  Trophy Points: 280
  pole kwa yaliyo kukuta mkuu. Mia
   
 5. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Iliwahi kutokea mwanza, kuna dereva wa daldala na utukutu wao, aliamua kupakia abiria katikati ya barabara, nyuma yake alikuwapo OCD na gari ya kiraia. Alipoaanza kuingiza abiria, yeye akampigia honi, jamaa akatoa vidole nje na kumuoneshea ishara yakuwa kama ana haraka, basi apae hewani ili alipite gari lake. OCD kuona vile akapaki gar pembeni na kutoka nje ya gari lake full manyota, jamaa alichukuliwa mpaka central, kutoka huko sijui ilikuwaje
   
 6. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  pole hawa watu hata katiba hawaijui,
  wamenyimwa elimu hata hiyo leseni ni mjomba wake yupo dar ndo alimletea,tusubiri aende nit li kuibadilisha labda atatoka na uelewa.
   
 7. S

  Sting007 JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Pole sana ndugu, huyo si dereva ni mzoefu wa kuendesha magari sisi tunawaita NYOKA, dereva ni yule anayesoma mazingira na kuyatambua yanayomzunguka wakati anaendesha gari, kwa huyu aliyekupiga hawa ndio wale wanaosababisha ajali zinazogharimu maisha ya watu, wapo wengi sana hasa maeneo ya vijijini.
   
 8. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hakustahili msamaha.Ungeacha tu sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwake.
   
 9. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  wanatakiwa wapitiea nit wakapewe elimu kwanza,si kujifunzia gari gereji
   
 10. ATUGLORY

  ATUGLORY Senior Member

  #10
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We mwenyekiti wa nani????????????!!!!!!!!!????????????
   
 11. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  mWENYEKITI WA MTANDAO WAKE, akiwa kama mmiliki wa Mjengwa blog wadau wake ni members yeye akiwa ndiye mwenye kigoda.
   
 12. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Gari zingine si za kupiga nazo picha.........bora uazime

  [​IMG]
   
 13. Chris_Mambo

  Chris_Mambo JF-Expert Member

  #13
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 597
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mi nisingekubali! Ile ngumi a a, lazima ningerudisha. Tena kama vipi mbili. Baada ya hapo ndipo msamaa ungefuata!:hatari::hatari::hatari:
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Marehemu Dr. Remmy alikuwa na kigari amekiandika "BABA YAKO ANAYO?"

  Tofauti yako wewe na yeye ni kuwa, Mwenzako alinunua Sweden ukweni kwenye Model ya SUZUKI iliyotengenezwa kwa ajili ya matumizi ndani ya EUROPEAN UNION na ilikuwa MPYA. Wewe unanunua used kutoka FUKUSHIMA na unaanza kujiona bora.

  Mjengwa, pole sana kwa hili tukio. Ulifanya makosa kumuachia hivihivi. Alitakiwa walau alipe faini fulani kwa ajili ya watoto yatima.
   
 15. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #15
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Samahani........ni mtizamo wangu tuu na silazimishi wengine waufuate.....ila nashukuru umesema amenunua wapi na amenunua vipi.....mimi langu sikununua FUKUSHIMA bali CROYDON area London.......ni hili hapa

  [​IMG]
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Jan 16, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  CAMARADERIE,

  Hivi unajua kuwa Warren Buffet hadi leo anaishi kwenye nyumba yake aliyonunua miaka ya 60's?

  Hivi unajua gari gani anatumia Boss wa Toyota kwenda kazini? Kama ulikuwa hujui, jamaa anaenda kwa MGUU.

  Mfuatilie mama mmoja Mgeruman aitwaye Izabella Bosch ambaye ni CEO na owner wa BOSCH uone maisha yake yalivyo SIMPLE.

  Michael Jordan, moja ya magari yake aliyokuwa akionekana nayo Chicago ilikuwa SUZUKI.

  Kuna watu duniani hawapendi kujionyesha utajiri wao. Ila masikini wakipata, akina MARIO BALOTELLI.
   
 17. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #17
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  kumbe ni mwana jf?
   
 18. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #18
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu,

  Utajiri huja kwa namna nne
  1. Ubahili(kama wa huyo Buffet na hao wengine)
  2. Bidii(kama yangu)
  3. Bahati
  4. Dhulma
  Sera yangu ninapopata faida ni kununua kile nikipendacho kama hiyo Q7....na kusaidia wasio na bahati na kipato
   
 19. Ndi.Wa.Nkaka

  Ndi.Wa.Nkaka Member

  #19
  Jan 16, 2012
  Joined: Oct 24, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CAMARADERIE:

  Hiyo GX100 (Nyeusi) unayoendesha ina tofauti gani na SUZUKI Escudo?
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  Jan 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ndio kitu gani tena hicho?
   
Loading...