Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 2,286
- 3,018
Habari wanamichezo, ikiwa siku kadhaa zimesalia kuelekea ufunguzi wa pazia jipya la ligi kuu Tanzania bara. Ikiwa ni mechi ya vigogo wanne waliobora kwa Tanzania hapa nazungumzia Yanga, Simba, Singida na Azam. Hawa ndio waliong'ara katika ligi na katika Azam Federation cup kwa wao kuwa top 4 kote kote.
Kwasasa kwa Tanzania, kwa maoni yangu hakuna mechi tamu yenye burudani kama Azam wakikutana na Yanga, ni wazi ukiachana na matokeo ya uwanjani watazamaji kwanzia uwanjani hadi kwenye luninga huwa wanarifhika ela zao walizotoa kwa kushuhudia kandanda safi, ufundi na mbinu safi inayopelekea kuwe na soka tamu kabisa uwanjani.
Wiki ijao bila shaka tunaenda kuonana radha zaidi ya tuliyoiona hapo kabla, kwasababu kila upande una watu haswa na benchi ni jipya kwa kila upande. Hivyo kama kawaida tutashuhudia mpira usiokuwa wa papatu papatu wala kukamiana bali tunaenda kuona mpira wa kitabuni, mpira wa kasi na ufundi na ni mechi inayoongeza hisia zaidi hasa baada ya Feisal na Bangala kuongeza kitu kwa upande wa Azam wakitokea Yanga.
Weka utabiri wako hapa kutokana na vikosi vya timu zote mbili je ni timu ipi itavuka kucheza fainali ya ngao ya jamii?