Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,401
- Thread starter
- #81
Hahaaaaaaa karibu tena mahabusu
sitaki tena.
Hahaaaaaaa karibu tena mahabusu
Mkuu pole sana just hamia ktk uislam tutakufundisha kuishi vzr na kuheshimu mamlaka maana inaonyesha hueshimu mamlaka wewe
.....
.....Ngika pole sana Sebha akojiwe
Kama hutaki fuata taratibu zilizowekwa na watawala ili usije ukaingia tena mahabususitaki tena.
[emoji1] [emoji1] [emoji1]sitaki tena.
tatizo lake ,hata akisema ukweli ataonekana anatania tu.hahahahahahahahaha....Hahaa we jamaa bana!!!
Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.
Deo anasema kakamatwa tarehe 24/2/2017 na ametoka Leo tarehe 2/3/2017.
Anasema amelala rumande siku 8 wakati mwezi wa pili unasiku 28.
Deo acha uongo
tatizo lake ,hata akisema ukweli ataonekana anatania tu.hahahahahahahahaha....
Wale jamaa watakuwa wamemfanya kitu kibaya mpaka amesahau "siku zake" alizokaa huko.Ukiwa muongo uwe na kumbukumbu.
Deo anasema kakamatwa tarehe 24/2/2017 na ametoka Leo tarehe 2/3/2017.
Anasema amelala rumande siku 8 wakati mwezi wa pili unasiku 28.
Deo acha uongo
Pole sana Ndugu kwa maswaibu hayo yaliyokukuta. lakini badilika kulingana na hali halisi ilivyo nyakati hizi juu ya namna bora ya kutumia mitandao.
Hicho kitabu cha MAISHA YA MAHABUSU tafadhali sana usije kukanakiri(copy) hadithi/ riwaya ya The Bold (Vipepeo weusi ...mkakati number 0034). Kuna sehemu kazungumzia Mahabusu Morogoro!
Hakukuwa na Feb 29 mwaka huu.....unaaibikasikuya kwanza Alhamis 24 Feb 2017
siku ya pili Ijumaa 25 feb 2017
siku ya tatu Jumamosi 26 feb 2017
siku ya nne Jumapili 27 feb 2017
siku ya tano Jumatatu 28 feb 2017
siku ya sita Jumanne 29 feb 2017
siku ya saba Jumatano 1march 2017
siku ya sanane Alhamis 2march 2017
Yaani akili ya huyu mwalimu huwa siielewi, kwanza unafundisha masomo gani?
Hicho kituo cha Polisi ulichoenda umekuta wanatumia kalenda ya sayari ipi yenye siku 29 katika mwezi Feb.?sikuya kwanza Alhamis 24 Feb 2017
siku ya pili Ijumaa 25 feb 2017
siku ya tatu Jumamosi 26 feb 2017
siku ya nne Jumapili 27 feb 2017
siku ya tano Jumatatu 28 feb 2017
siku ya sita Jumanne 29 feb 2017
siku ya saba Jumatano 1march 2017
siku ya sanane Alhamis 2march 2017
Siku nane tu unakuja na kitabu watu tumekaa jera ma miaka...
Sasa umeanza kumchokoza bashiteUnaweza kukaa miaka kumi lakini usijifunze chochote. Unaweza kusoma miaka minne Form one mpaka four na ukapata zero lakini shemeji yako akasoma mwaka mmoja tu na akapat two.
Niliponea chupuchupu kuanzisha uzi humu, kuwa Deo yupo wapi?! !!Ndugu Watanzania wenzangu na binadam mnaopenda maendeleo, nilikamatwa siku ya Alhamis tarehe 24 February 2017 kazini kwangu Mkolani sekondari mbele ya Makamu Mkuu wa shule na baadhi ya waalimu na kupelekwa kituo cha Polisi Central cha Jijini Mwanza kwa mahojiano na pia siku hiyohiyo niliwekwa lupango/sello na nimekaa Sello tangu tarehe 24 February 2017 na nimeachiwa leo kwa dhamana tarehe 2 marchi 2017 jioni hii kwa msaada wa ndugu zangu.
Mungu awabariki sana kwani nimekaa Lupango kwa siku 8, huku watu wakiogopa kuniwekea mdhamana kwa vitisho kutoka kwa watu mbalimbali. Kosa langu nimetuhumiwa "KUTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII HASA FACEBOOK" mengi sitayazungumza leo mpaka kesi itakapoanza lakini kiuhalisia hakuna kesi zaidi ya uonevu.
Aidha simu zangu zote mbili hazitakuwa hewani(Vodacom na Tigo) zimeshikiliwa kwa uchunguzi zaidi, poleni mtakaonitafuta bila mafanikio, pia ni njia ya kunifanya NITAFAKARI UPYA na kuanza upya. Maana naweza kurudishwa tena muda wowote kwa kesi nyingine ambayo sijajua.
Aidha nimejifunza mambo mengi sana nilipokuwa Lupango na pia nilipata ushirikiano mzuri sana na mahabusu wenzangu na kujua mengi sana, ambayo yatakuja kwenye kitabu changu "MAISHA YA MAHABUSU" ambacho nitakuwa naishauri Serikali kubadili mazingira ya mfumo wa selo na kufanya maboresho, yote haya yatafanyika kwa nia njema ili kuijenga Serikali yetu ya awamu ya tano. Ni lazima tuikosoe Serikali kwenye mambo mhimu ili iweze kujirekebisha na kufanya upya.
Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa chama tarajiwa cha ACA.
2 march 2017