Civilian Coin
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 2,305
- 4,379
Ndugu Watanzania wenzangu na binadam mnaopenda maendeleo, nilikamatwa siku ya Alhamis tarehe 24 February 2017 kazini kwangu Mkolani sekondari mbele ya Makamu Mkuu wa shule na baadhi ya waalimu na kupelekwa kituo cha Polisi Central cha Jijini Mwanza kwa mahojiano na pia siku hiyohiyo niliwekwa lupango/sello na nimekaa Sello tangu tarehe 24 February 2017 na nimeachiwa leo kwa dhamana tarehe 2 marchi 2017 jioni hii kwa msaada wa ndugu zangu.
Mungu awabariki sana kwani nimekaa Lupango kwa siku 8, huku watu wakiogopa kuniwekea mdhamana kwa vitisho kutoka kwa watu mbalimbali. Kosa langu nimetuhumiwa "KUTUMIA VIBAYA MITANDAO YA KIJAMII HASA FACEBOOK" mengi sitayazungumza leo mpaka kesi itakapoanza lakini kiuhalisia hakuna kesi zaidi ya uonevu.
Aidha simu zangu zote mbili hazitakuwa hewani(Vodacom na Tigo) zimeshikiliwa kwa uchunguzi zaidi, poleni mtakaonitafuta bila mafanikio, pia ni njia ya kunifanya NITAFAKARI UPYA na kuanza upya. Maana naweza kurudishwa tena muda wowote kwa kesi nyingine ambayo sijajua.
Aidha nimejifunza mambo mengi sana nilipokuwa Lupango na pia nilipata ushirikiano mzuri sana na mahabusu wenzangu na kujua mengi sana, ambayo yatakuja kwenye kitabu changu "MAISHA YA MAHABUSU" ambacho nitakuwa naishauri Serikali kubadili mazingira ya mfumo wa selo na kufanya maboresho, yote haya yatafanyika kwa nia njema ili kuijenga Serikali yetu ya awamu ya tano. Ni lazima tuikosoe Serikali kwenye mambo mhimu ili iweze kujirekebisha na kufanya upya.
Deogratius Nalimi Kisandu
Mtemi Kiongozi wa chama tarajiwa cha ACA.
2 march 2017