Denial

gfsonwin

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
18,272
Reaction score
20,720
Ni kitu gani hutokea hadi mtu una deny jambo ambalo ni facts hasa mwenye mahusiano? what makes our eyes and ears closed?? kwa extent ya kuja kujuta baadae??
je mtu una deny jambo kwasababu gani??
je ni kwasababu uko sure of the ultimate results??
ama je hujui but unaamua tu out of empty slut??
ama unaamua kuwa risk taker and gambler??

sijui kama nimeeleweka but think of mtu anasema wewe gfsonwin huyu fulan hakufai kuwa mwenza wako, despite proof toka kwa watu wa karibu na hata wengine usiowajua lkn wewe unachukulia kama vile sijui ni utani ama haiwezi ama ni uzushi unasonga mbele na mtu wako. kisha inatokea tena huyu mtu anakuja kuwa kama ambavyo wengi walisema je nini husababisha haya?? why denying the truth at first sight?

Nimejikuta nawaza kwa sauti kwasababu ya novel moja nikuwa naisoma jana ya JAFFERY ARCHER inaitwa KANE & ABEL utamuona jinsi ambavyo mke wa tajiri Richard Kane aliyeitwa ANNE CABOTS alivyokuwa ana upinga ukweli wa tabia ya mwenzi wake mpya Henry Osborne hadi kumsababishia kupoteza kiasi kikubwa sana cha hela ambacho kilikuwa ni urithi wa mwanae WILLIAMS aliyeachiwa na marehem baba yake Richard Kane na hata yeye ANNE kupoteza maisha.
 
Upendo una nguvu kuliko mauti, so ikiwa mtu kampenda mwingine kwa moyo wote hata aambiwe nini mara nyingi inakuwa kama anapigiwa kelele kwa sababu Ubongo huwa haupewi nafasi yake ya msingi ya kufikiri, bali maamuzi mengi yanakuwa influenced na mihemko ya moyo. Hapa hata uimbe hutasikiwa hadi mwenyewe atakapofunguka na kujua au atakapoumizwa au atakapokuwa ameharibu sana upande mwingine ndio anaweza kuamka.

The shortest distance is from heart to Head but the longest one is from the head to te heart on issues of love''

NB ''Love is madness but in madness there is reasoning'' Albert Eistein
 
::
Hao wanatafuta unabii wa baadae utawasikia wanasema "nilijua tu,nilisema,"
Ila wanapogundua walikosea utawasikia "Wapendanao kuwatenganisha ni vigumu " n.k
::
Msimamo ktk maamuzi yako binafsi ndilo la kusikiliza.
=
 

hapo bold ina maana ukipenda huwezi kufanya maamuzi??
 
Kuna siku moja snowball aliongelea kuhusu loving eyes,na hilo haswa ndilo linalowaponza wengi wanaruhusu mapenzi yawapofushe hasa wanapoyaanza na huyo mtu iAl baada ya muda kusonga na mapenzi kuwa yamepungua kiasi fulani ndo hapo mtu anaanza kuona ukweli wa aliyokuwa akiambiwa when it's too late.In short it's only love feelings that blinds people and make people dumbs as it is said that LOVE IS BLIND.
 
Kwenye mapenzi, matumizi ya akili ni madogo sana,


Babu DC!
kwanini iwe hivyo??
je ni kwasababu moyo uko radhi?? na je kwann tusiangalie na udhaifu wa mwili pia??

manake nijuavyo mimi ni kwamba love accomplishes happiness, sasa hii furaha inatakiwa iwe ya kudumu na kama ndivyo inabidi tushirikishe akili zetu ili kuona possibilities za kupata furaha tunayoitaka. kwann sasa ni kinyume??
 
::
Hao wanatafuta unabii wa baadae utawasikia wanasema "nilijua tu,nilisema,"
Ila wanapogundua walikosea utawasikia "Wapendanao kuwatenganisha ni vigumu " n.k
::
Msimamo ktk maamuzi yako binafsi ndilo la kusikiliza.
=

msimamo hata pale inapooneka wazi kwamba mtu unapotea?? na watu tofauti tofauti wanasema?? tena wasiojuana??
 
gfsonwin kuna ulimbukeni fulani mtu anakuwa nao (samahani lakini) wakati anapenda so hata aambiwe kuwa fact ni hizi na hizi huwa ameziba masikio na akili yake inakuwa imesimama wakati huo moyo tuu ndo unaamua na at the end of the day likitokea ndo anajilaumu kwa nini hakusikia lile alilokuwa anaambiwa
Mapenzi sometime ni kama kichaa fulani hivi wakati unapenda unakuwa kama hujielewi hivyo kila anayekuambia jambo unamuona kama hapendi uhusiano wako na yule mtu
 
Last edited by a moderator:
for that case kwenye mapenzi sote tu wanafiki basi.
manake kama tuna assume wenzi wetu ni malaika na ni wema kiasi cha kupinga ubaya wao naona tunakuwa wanafiki.
 
hvi kwann tuseme haya mapenzi ni ukichaa ilihali vichaa ni sisi wenyewe ambao muda mwingine tunakataa yaliyo ya maana na ya kweli kwetu??
 
ukipenda kwa dhati lazma majuto yawepo. bora upende kwa kubip bip. ngoja nimwite sweetlady ajazie mapwents
 
Last edited by a moderator:
hvi kwann tuseme haya mapenzi ni ukichaa ilihali vichaa ni sisi wenyewe ambao muda mwingine tunakataa yaliyo ya maana na ya kweli kwetu??

Mwalimu gfsonwin vichaa ni sisi wenyewe na ndo maana nikasema ni kama ulimbukeni fulani yaani unakuwa blind ilhali macho unayo na masikio yapo na akili na utashi pia ila unakuwa umefungwa moyo wako hauelewi kitu zaidi ya kile wewe unachokiona na kukiamini
 
Last edited by a moderator:
Si sawa na unafiki dada gfsonwin ni kwamba hii kitu inakuja automatically na huyo mpendaji anakuwa hajitambui kama anakosea au anapuuzia mabaya,na hio ni kutokana na upendo alionao kwa mtu husika na ndio maana hata kwenye biblia tunaambiwa upendo hufunika makosa yote katika maana ya kwamba upendo unapokuwa kati ya watu si rahisi kuona makosa ya mwenzio na badala yake utaona mazuri na mabaya huenda usiyaone kabisa au ukayaona kuwa madogo yasiyo na madhara yoyote.
 
Last edited by a moderator:
Naungana na Tized kwamba ukipenda sawasawa inakuwa ngumu kumsikiliza mtu wa nje, hii huja pale ambapo mtu huyo atakuwa anaongelea mambo yanayomhusu mwenzi wako either akiwa anakuhadaa kwamba mwenzako anakucheat.
Utaona kama anakuharibia pozi tu na ni mnafiki au mchonganishi anayetaka kuyaharibu mapenzi yenu.

Hata snow ball aliliongelea hili kwenye mada yake ya mapenzi ni upofu.

Mtu huwa mgumu kuyaamini wasemayo watu haswaa manenio hayo yakiwa yanahusu mapenzi yao, ila yakishawakuta ndio majuto hutokea na ile dhana na "ningejua ningemsikiliza fulani" inapojitokeza.
 
Last edited by a moderator:
Mdogo wangu gfsonwin... Nachukulia kuwa unazungumzia Denial katika mahusiano. Mara nyingi ‘Denial' hutofautiana from one to another… Hiyo kufanya kuwe na Denial ya aina mbili.

Denial inayoshinikizwa na woga

Huu woga mara nyingi huwa woga wa madhara ambayo mhusika anahisi inaweza kuwa endapo asipokuwa na huyo mpenzi wake. Mara nyingi hudhani kuwa yupo better off hivyo hivyo na kuwa inaweza kuwa worse endapo hayupo na mtu wake huyo.

Denial ya namna hii mara nyingi huwa kwa wale ambao wanasifa ya hizi zifuatazo;

Ni mtu ambaye ni Tegemezi

Kwamba huyu mtu wake ndie anaye mtegemea kwa kila kitu na ndiye kamfanya awe hapo alipo (iwe ki hadhi – yaani high status ama kipesa). Unakuta mtu yupo katika mahusiano na mtu ambaye pengine ana uwezo sana huku yeye mwenyewe hana mbele wala nyuma kwa maana kuwa bila huyo mtu atashuka sana kiwango cha maisha ya kuishi, atapata taabu na kuhangaika sana or hata atakosa pa kwenda. Na hata kama ana chanzo ambacho kinamuingizia pesa ukute hicho kiwango ni thumni tu ya gharama za maisha yake ya kila siku.

Ni mtu asiyependa Mabadiliko (Change)

Kuna watu hawapendi kabisa change kabisa maisha yao… Kitendo cha kufikiria kuachana na mtu aliye naye ama kuanza kuchunguza na kutafakari ukweli kuwa yawezekana hamfai kunamchanganya kabisa. Na hivyo anaona ni kheri aishi in Denial kuliko kuanza kujipima nafasi yake kwa mpenzi wake huyo. Anaona ni kheri aishi in denial na aendelee kuwepo katika mahusiano kuliko kashi kasha zinazoweza fanya kuharibika kwa mahusiano hayo.

Denial inayoshinikizwa na Mapenzi

Hapa its simple… Yet so complicated. Unapompenda mtu… You love for the both of you. Unapo mpenda mtu unampenda kwa jinsi alivyo na mapungufu yake. Unaweza hata ukayaona mapungufu yake hayo ila in the name of love ukaona na ukamtetea kuwa yeye ni binadamu pia hivyo anaweza akakosea kama wanadamu wengine. Kupena huko mara nyingi kunaweza kudumu sana kama huyo ambaye anapendwa anapalilia na ku nurture hayo mapenzi anayopewa.

But sababu kila mwanadamu ana roho... Hata yule mwenye kupenda sana inapotokea kuwa anatendwa na kuchezewa katika mahusiano bila kikomo nae pia hufunguka macho - mara ngingi baada ya mapenzi kupungua taratibu na kubalance uwezo wa mahusiano hayo kutazamwa kwa moyo na ubongo. Mwisho wa siku mapenzi yanayeyuka na kumfanya hata yale madhaifu yaliyokuwa rahisi kuyapuuzia kuwa mazito mno kubeba.

Haya ndiyo mawazo yangu on the matter...
 
Last edited by a moderator:
msimamo hata pale inapooneka wazi kwamba mtu unapotea?? na watu tofauti tofauti wanasema?? tena wasiojuana??

::
Love in its natural settings itakufanya uwe na msimamo.
=
 
Hapana, Namaanisha katika ukicha huo kuna kufikiri, na bahati mbaya wengi hatufikiri, tunachuliwa tu na mihemuko tunaacha kufikiri pembeni. Ndo baadae mtu akisharudi kwenye senses zake anaanza kujuta na kujichukia, pengine pia kujiona mjinga kwa jela ya moyo aliokuwepo. You are very tough through!


hapo bold ina maana ukipenda huwezi kufanya maamuzi??
 
Tatizo ni moyo, Moyo ndio tatizo.... Endapo mtu atakuwa na maamuzi ya kuutumia ubongo wake japo kidogo katika mapenzi basi hatakuwa mpofu na hatofanya denial.. Huu moyo ndo unafumba uwezo wa ubongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…