Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Kazi kazi i magu kopa hadi ifike kikomo then ukiondoka mwezako achukue maamuzi magumu kama ya Zairw Kuitwa DR CONGO na ndo utakua mwisho a muungano na azaznjbari atakua wanekonbolewa kutoka utumwani... inchi halisi iliyopata uhuru naina inarudi Karibu Tanganyika..
 
Aksante kwa kutujuza kila harua ya deni letu linavyoongeka je mikopo haitumiki katika matumizi sahihi yaliyokusudiwa na deni lote ni la awamu ya tano tu au tangu nyerere!
Kwa miradi inavyo pishana huko mikoani wacha deni liongezeke maana kuna miradi ikikamilika itarudisha hilo deni mapema sana
 
Kwa mujibu wa taarifa toka ITV, Deni la taifa laongezeka hadi kufikia shilingi trilioni sitini na moja nukta nane. Mwaka 2015 deni la taifa lilifikia Shilingi Trilioni 40

========


Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imebaini kuwa deni la taifa limekua kukua kutoka shilingi trilioni hamsini na tatu nukta tatu mwaka 2017 hadi shilingi trilioni sitini na moja nukta nane mwaka 2018 kutokana na mahitaji ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa majukumu kamati hiyo kwa kipindi cha Januari 2018/19 Mwenyekiti wa kamati Mhe. George Simbachawene amesema deni hilo linajumuisha fedha zilizokopwa na serikali kutoka vyanzo vya ndani na nje pamoja na sekta binafsi kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo.

Akizungumza na ITV kuhusu taarifa ya uwekezaji wa mitaji ya umma ya Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma, Mwenyekiti wa kamati hiyo Mheshimiwa Raphael Chegeni amesema baadhi ya tasisi na mashirika mengi ya umma yanayowekeza kibiashara hayana mpango mkakati, mpango wa kibiashara na sera ya uwekezaji na kusababisha kushindwa kujiendesha kwa tija.

Wakichangia taarifa ya Kamati za Bunge ya Bajeti na Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Umma, baadhi ya wabunge wamesema hakuna nchi iliyoendelea kwa kutegemea wafadhili, hivyo wameitaka serikali kuongeza kodi kwa bidhaa zinazoingia nchni, ambazo zinaweza kutengenezwa hapa nchni,ili kuinua bidhaa za ndani.

Chanzo: ITV
Ukiona unakopwa ujue unaaminika kuwa unalipa.
Pia Ukopaji huu is direct proportional to the investment/development we see in the land, so it's OK.
 
Kila mara napenda kufahamu hivi vyanzo vya ndani vya mikopo ya serikali ni vipi? Kati ya hizo wanazosema T61, deni la ndani ni kiasi gani?
Vile vile hii miradi wanayosema bado inajengwa ni hipi na inagharimu kiasi gani? Kwa awamu zilizopita tumeona barabara na miundo mbInu mingi sana ilijengwa au ilikuwa ipo katika hatua za mwisho mwisho kumalizika, hivyo basi tulitegemea kwa awamu hii matumizi ama gharama zipungue na hivyo deni kubaki liwe chini na si kupanda kiasi hicho
 
Kwa hiyo ndani ya miaka mitatu ya utawala wake katuingiza kwenye deni la trillion 21 {61-40 (deni alilolikuta)}.
Na jk katika miaka yake kumi alituacha na deni la 40 trillion tu.
Kwa rate hii kama kila baada ya miaka mitatu tuna ingia deni la trillion 21 huyu jamaa miaka 10 atayo kaa deni litafikia {61+45}=106 trillion.
Outrageous!!!!!
 
ala kumbe bado tunaendelea kukopa kwa hawa mabeberu.
 
Hii ndo maana halisi ya kuuza nchi yetu mana nadhani tulivyonavyo nchin itafika mda vitakua avina thamani kabs zidi ya deni na wengi wetu tushakua vipifu tunashabikia sawa na mtt wa mwanasiasa mwenye nyumba marekani account uswiss ipo siku watatushangaa kama tunavyowashangaa wakina mabutu seseko na wengine wengi starehe wanazofanya kwa pesa za wananchi tatizo alijaisha ila limebadilishwa maana tulipiga kelele kama taifa escrow account cjui na nn leo wizi ule ule tunautetea ngoja tuone itakuaje


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kwa hiyo ndani ya miaka mitatu ya utawala wake katuingiza kwenye deni la trillion 21 {61-40 (deni alilolikuta)}.
Na jk katika miaka yake kumi alituacha na deni la 40 trillion tu.
Kwa rate hii kama kila baada ya miaka mitatu tuna ingia deni la trillion 21 huyu jamaa miaka 10 atayo kaa deni litafikia {61+45}=106 trillion.
Outrageous!!!!!
Je jk aliachiwa kiasi gani na Benja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania tutembee kifua mbele! Tupo kwenye right track! Miradi tunaijenga kwa fedha zetu kwani serikali hii ya awamu ya 5 tunakusanya kodi toka 800Bil hadi 1.3Tr.......Serikali ya wapenda vitu bila mipango baada ya miaka 5 itajikuta imeacha deni lisilolipika uku baadhi ya miradi ikiishia njiani na ajira hakuna! Nadhan msemaji wa Ikulu atakuja kupinga ata hili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aksante kwa kutujuza kila harua ya deni letu linavyoongeka je mikopo haitumiki katika matumizi sahihi yaliyokusudiwa na deni lote ni la awamu ya tano tu au tangu nyerere!
Mbona kama ameeleza ongezeko la tn 28 ktk kipindi cha miaka 3, sasa tangu Nyerere inakuwa na Mantiki gani?
 
Back
Top Bottom