Niliwahi sema huyu bwana atatuachia structures lakini tutabaki masikini wa kutupwa.
Kwa mujibu wa Zitto,ripoti ya Benki ya Dunia teyari imeonyesha ongezeko la watu masikini wapatao milioni 2 tangu huyu bwana achukue madaraka.
Tafsiri ya haya madeni ni serikali kutumia makusanyo ya ndani kuhudumia deni la Taifa na matokeo yake ni serikali kupunguza uwezo wa kuajiri,kununua madawa,kugharamia elimu,kutoa mikopo ya elimu ya juu,kupambana na umasikini,miradi ya maendeleo kuathirika kwa kukosa fedha za kutosha,serilali kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi,kulipa madeni ya ndani,n.k.
Kwa kifupi, haya madeni ni janga kubwa sana kwa Taifa na yanachangia umasikini wa mtu mmoja mmoja kwa njia mbalimbali.
Na bahati mbaya sana,baadhi ya miradi tunayokopea fedha kuitekeleza ni white elephant projects kwahiyo ni hasara juu ya hasara.