Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Ahsante kwa ripoti...

Naona sasa tushajua tatizo la mambo mengi kusimama kwa sababu za fedha kukosekana...

Na si ni tunatumia pesa zetu wenyewe, pesa tunazo na uwezo tunao, sasa deni linaongezeka vipi tena?


Cc: mahondaw
 
Kwa mwenendo huo hakuna mradi hata mmoja utakaokamilika miradi itakosa fedha, na wananchi watakuwa maskini wa kutupwa, tangu lini manunuzi ya umma yakapangwa na mtu asiye na elimu yoyote ya uchumi? Mtanunua midege mtakosa sifa ya kuendesha biashara hiyo, mtajenga reli kwa mikopo mtakosa bidhaa za kusafirisha, mtaacha bomba la gas, mtaanzisha stiegler's hamtakopesheka hamtaumaliza mradi huo, mtatumbukia kwa wachina, mtawafidia bandari, airports, reli, ikulu, n.k.
 
Wakati Rais wa wamu ya nne,Rais Jakaya Mrisho Kikwete anakabidhi nchi mwaka 2015, deni la Taifa lilikuwa Tril 43.

Baadae akaingia Rais Magufuli,hata hivyo taarifa zinaonesha kuwa deni la taifa limepanda mpaka Tril 62 ndani ya miaka mitatu tu ya utawala wa awamu ya tano.

Maswali ya mjadala.
1.Ni miradi hani iliyokwisha gharimu tril 19 zilizokopwa mpaka sasa?

2.Fedha tunazoambiwa ni makusanyo ya ndani zinatekeleza miradi gani?

3.Muradi gani inatekelezwa kwa fedha za mkopo na ipi inatekelezwa kwa fedha zitokanazo na makusanyo yetu wenyewe?

4.Kasi hii ya ukuaji wa deni,inaendana na ukuaji wa uchumi wetu?

5.Serikali ipongezwe kwa kasi hii ya ukopaji au idhibitiwe ili tutekeleze miradi kwa fedha zetu wenyewe?

Mjadala upo wazi,ushabiki wa vyama vyenu hauna tija,tutangulize maslahi ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hilo deni limeongezeka vp wakati tunatumia fedha zetu kuendesha nchi?
 
kwenye zile pesa tunazowadai(matrilion tunayowadai ACACIA) tutachomoa huto tusent twa deni la taifa alafu tunalipa,.....nani anateseka? jifanye unajikuna tu
 
Ninasubiria litakapofikia trilion 500. Maana ni muda mfupi tu ujao.
 
hivi hili deni na sawa na madeni tunayo daiwa sisi mtaani au benk maana mpaka umri unakwenda na sikia tuna deni la taifa
haya madeni ya mtaa ni nouma sana,unaweza ukajifungia ndani na usitoke njee hata kwenda kucheki game ya simba na ahly au vita club ukaisikia kwa wachambuzi (shafih dauda na edga kibwana tu)
 
Natumai taarifa hii ya deni itakuja kukanushwa au kufafanuliwa. Na aliyeisoma atasema walimnukuu vibaya.
 
Niliwahi sema huyu bwana atatuachia structures lakini tutabaki masikini wa kutupwa.

Kwa mujibu wa Zitto,ripoti ya Benki ya Dunia teyari imeonyesha ongezeko la watu masikini wapatao milioni 2 tangu huyu bwana achukue madaraka.

Tafsiri ya haya madeni ni serikali kutumia makusanyo ya ndani kuhudumia deni la Taifa na matokeo yake ni serikali kupunguza uwezo wa kuajiri,kununua madawa,kugharamia elimu,kutoa mikopo ya elimu ya juu,kupambana na umasikini,miradi ya maendeleo kuathirika kwa kukosa fedha za kutosha,serilali kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi,kulipa madeni ya ndani,n.k.

Kwa kifupi, haya madeni ni janga kubwa sana kwa Taifa na yanachangia umasikini wa mtu mmoja mmoja kwa njia mbalimbali.

Na bahati mbaya sana,baadhi ya miradi tunayokopea fedha kuitekeleza inaweza kuja kugeuka kuwa ni white elephant projects na hivyo ikawa ni hasara juu ya hasara.
Kwamba tutabaki masikini wa kutupwa ni ndoto za alinacha, USA Ndo anaongoza kwa madeni lakini pia ndo anaongoza kwa uchumi mkubwa. Mo ni tajiri lakini kuna mwaka alienda south Africa kukopa, hapa bongo benki hazikua na pesa anayotaka. Ishu ni unautumiaje mkopo

Unapojenga SGR unapanua wigo wa transportation, kama wafanya biashara walikua wanatumia wiki kusafirisha mzigo now wanaweza kua faster zaidi, hapo utavutia nchi nying majirani ku opt kutumia bandari yetu. Huo ni umasikini?
Unakopa kijenga STIGLERS dam, unazalisha umeme zaidi ya matarajio. Umeme utashuka bei, utavutia uwekezaji wa viwanda tofauti na sasa tunabahatisha.
Ila tungekua tunakopa kununua vx, kulipa posho za viongozi kusafiri nk. Hapo tungeshtuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio orodha kamili ya mataifa ambayo yako na madeni makubwa Barani Afrika

1. Angola = KSh 4.28 trilioni

2. Ethiopia = KSh 1.37 trilioni

3. Kenya = KSh 980 bilioni

4. Republic of Congo = KSh 742 bilioni

5. Sudan = KSh 649 bilioni

6. Zambia = KSh 637 bilioni

7. Cameroon = KSh 556 bilioni

8. Nigeria = KSh 483 bilioni

9. Ghana = KSh 349 bilioni

10. Democratic Republic of Congo = KSh 342 bilioni




Tanzania bado tupo pazuri na hasa ukizingatia miradi mingi mikubwa inakwenda kwa kasi.
 
hizi ni habari njema sana kwa wazalendo😊 wasio na vyama!hawafunhaman na upande wowote ule..auawe Lissu sawa..achomwe kisu cha makalio Makonda sawa tu😏
 
Bila kuiona tanzania hapo siwezi kukubaliana na post yako

juzi hapo tumeletewa bili kua tunadaiwa tilion 68+ halafu leo kwenye list hatupo kweli? Au yamelipwa tayali jana?, au wanaotudai wametusamehe?

Sent using unknown device
 
yamekuwa cleared juzi mkuu
Tuko namba saba boss, sijajua hiyo update ni yalini labda atupe link
Screenshot_2019-02-04-00-34-35.jpeg


Sent using unknown device
 
Hii ndio orodha kamili ya mataifa ambayo yako na madeni makubwa Barani Afrika

1. Angola = KSh 4.28 trilioni

2. Ethiopia = KSh 1.37 trilioni

3. Kenya = KSh 980 bilioni

4. Republic of Congo = KSh 742 bilioni

5. Sudan = KSh 649 bilioni

6. Zambia = KSh 637 bilioni

7. Cameroon = KSh 556 bilioni

8. Nigeria = KSh 483 bilioni

9. Ghana = KSh 349 bilioni

10. Democratic Republic of Congo = KSh 342 bilioni



Tanzania bado tupo pazuri na hasa ukizingatia miradi mingi mikubwa inakwenda kwa kasi.
Sijui umeanzisha uzi huu kwa sababu ipi zaidi, ila naona kama lengo lako ni kuaminisha kwamba Tanzania iko safe.. tunajaribu kuangalia ni jinsi gani hili deni letu linakuwa kwa kasi na Athari kama taifa ikoje.. Rais amekuwa anatuaminisha kwamba tunafanya miradi ya maendeleo kwa pesa zetu wenyewe.. kwa nn mikopo inachukuliwa kimya kimya!? Hiyo List isiwe kigezo cha kutafuta comfort zone.. hii nchi kwa sasa haiendi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui umeanzisha uzi huu kwa sababu ipi zaidi, ila naona kama lengo lako ni kuaminisha kwamba Tanzania iko safe.. tunajaribu kuangalia ni jinsi gani hili deni letu linakuwa kwa kasi na Athari kama taifa ikoje.. Rais amekuwa anatuaminisha kwamba tunafanya miradi ya maendeleo kwa pesa zetu wenyewe.. kwa nn mikopo inachukuliwa kimya kimya!? Hiyo List isiwe kigezo cha kutafuta comfort zone.. hii nchi kwa sasa haiendi..

Sent using Jamii Forums mobile app


ww unatumika na mabeberu bila kujijua..wewe nachelea kusema sio mzalendo wa kweli..tupishe wazalendo wakweli
 
Tanzania inafuatia hapo kwa Angola maana kama inadaiwa TZS 61 trillion ni sawa na Kshs. 3.05 trillion
 
Bila kuiona tanzania hapo siwezi kukubaliana na post yako

juzi hapo tumeletewa bili kua tunadaiwa tilion 68+ halafu leo kwenye list hatupo kweli? Au yamelipwa tayali jana?, au wanaotudai wametusamehe?

Sent using unknown device

Na wala hataki kuonyesha hiyo listi kaitoa wapi! Ujinga ni hatari sana!

Na sijui kwa nini kaweka madeni hayo yawe katika Ks. Naona yeye anaamini hiyo ndio sarafu muhimu sana katika dunia yake.

Tanzania ina deni la zaidi ya $26 Billioni; Kenya zaidi ya $56 Billioni anaweka $9.8 Billioni tu; hata hawezi kuwaza tu kwamba deni la SGR pekee ni zaidi ya nusu ya hiyo $9 aliyoweka hapo.
Shule hizi zinaleta wahitimu wa ajabu sana!
 
Back
Top Bottom