Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Deni la Taifa lafikia Tzs trilioni 61.8

Tafsiri ya hii ni kwamba, hali ya uchumi ni mbaya, serikali inaendeshwa kwa mikopo.
Jiwe ni janga la taifa.
 
Watanganyika wanaoishadadia Kenya kwa kila kitu na kuiona Kenya Kama USA watakuja kuisifia Kenya kwa kudaiwa zaidi kuliko TZ.
 
Aksante kwa kutujuza kila harua ya deni letu linavyoongeka je mikopo haitumiki katika matumizi sahihi yaliyokusudiwa na deni lote ni la awamu ya tano tu au tangu nyerere!
Hata zile donor(mabeberu) walikuwa wakitoa kupeleka wagonjwa india siku hizi zinaitwa ni mapato ya ndani, Lakini hata wewe unashangaa limekuwaje kwa kasi kubwa hivyo? Juzi juzi hapa kabla hawajafungia Takwimu zao, Zito aliposema limekuwa kufikia Trilioni 60. walikataa wakasema deni linahimilika na wakashauriana waendelee kukopa kwasababu wankopesheka.
Wakaonjeshwa mikopo ya kichina ya muda mrefu kwa liba kubwa wakafurahi, Wakatutangazia kwamba marafiki wa kweli ni wachina, mikopo ambayo yeye aliita misaada yao haina masharti. waliposikia ya Malysia na Zambia wakapunguza speed.
Makusanyo ni makubwa na tunatumia pesa za ndani, kumbe uongo.
 
Pombe anatuambia makusanyo yameongezeka, anadai miradi mingi mfano mradi wa reli, umeme, ndege, elimu bure nk yanafanyika kwa kutumia mapato yetu ya ndani, ukiangalia hakuna ongezeko la mishahara au watumishi wapya, je hilo deni limeongezeka kwa sababu zipi??? Niliwahi kusema, awamu ya tano ndiyo awamu iliyojaa ufisadi kuliko awamu zilizopita.
 
Niliwahi sema huyu bwana atatuachia structures lakini tutabaki masikini wa kutupwa.

Kwa mujibu wa Zitto,ripoti ya Benki ya Dunia teyari imeonyesha ongezeko la watu masikini wapatao milioni 2 tangu huyu bwana achukue madaraka.

Tafsiri ya haya madeni ni serikali kutumia makusanyo ya ndani kuhudumia deni la Taifa na matokeo yake ni serikali kupunguza uwezo wa kuajiri,kununua madawa,kugharamia elimu,kutoa mikopo ya elimu ya juu,kupambana na umasikini,miradi ya maendeleo kuathirika kwa kukosa fedha za kutosha,serilali kushindwa kuongeza mishahara ya watumishi,kulipa madeni ya ndani,n.k.

Kwa kifupi, haya madeni ni janga kubwa sana kwa Taifa na yanachangia umasikini wa mtu mmoja mmoja kwa njia mbalimbali.

Na bahati mbaya sana,baadhi ya miradi tunayokopea fedha kuitekeleza inaweza kuja kugeuka kuwa ni white elephant projects na hivyo ikawa ni hasara juu ya hasara.
Siyo hiyo tuu atajenga treni na kununua madege na tutshindwa kukidhi mahitaji ya kuyatunza, preventive maintenance, na baada ya kuwa na TAZARA moja tutakuwa nazo zaidi ya tatu
 
Hii inamaana kuwa kwa wastani kila mtanzania anadaiwa Tsh 1,123,636.36. Hii ni kwa idadi ya Watanzania Millioni 55. Hivi kuna analysis yoyote iliyofanyika kuwa hii miradi inayoanzishwa inauwezo wa kulipa hili deni ndani ya muda husika? Isije ikatukuta ya Zambia rasilimali za Taifa kutaifishwa na Wachina.
Katengeneza mazingira ya hakuna anaweza kumuuliza labda mkewe
 
Serikali kukopa kwenye mabenki ya ndani inazinyima fursa sekata binafsi kukopa kwenye mabenki serikali hukopa kwa riba kubwa zaidi kuliko sekta binafsi mabenki hufurahia kuikopesha serikali
Very true, government bonds za miaka 15 unapata annual interest ya zaidi ya 15% wakati fixed deposit kwenye mabenki interest ni less than 8% , kwa hiyo anakomba hela za mabenki, hela zalizofichwa ndani , hela za mashirika na anaucha uchumi ukiwa mpweke, hili ni janga kubwa hailjawahi kutokea toka uhuru, we will pay mpaka na vitukuuu
 
Kwa mujibu wa taarifa toka ITV, Deni la taifa laongezeka hadi kufikia shilingi trilioni sitini na moja nukta nane. Mwaka 2015 deni la taifa lilifikia Shilingi Trilioni 40



========

Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imebaini kuwa deni la taifa limekua kukua kutoka shilingi trilioni hamsini na tatu nukta tatu mwaka 2017 hadi shilingi trilioni sitini na moja nukta nane mwaka 2018 kutokana na mahitaji ya uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

Akizungumza bungeni jana wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika kipindi cha nusu ya mwaka 2018/19, mwenyekiti wake, George Simbachawene alisema, “Kwa sasa Serikali imelazimika kujielekeza kukopa mikopo yenye masharti ya kibisahara (non concessional loans) kuliko yenye masharti nafuu (concessional) kama ilivyokuwa awali.

“Kamati inaona mikopo hiyo ina riba kubwa na hivyo kuwepo kwa mzigo mkubwa wa ugharamiaji wa mikopo kupitia mapato ya ndani.”

Simbachawene alisema hadi Novemba mwaka jana, Deni la Taifa lilikuwa Sh61.8 trilioni ambazo zimetokana na ukuaji wa deni hilo kwa taratibu kutokana na uwekezaji kwenye miradi ya maendeleo na kijamii nchini kwa ajili ya kukuza uchumi.

Alisema deni la Serikali linaendelea kukua likijumlisha fedha zilizokopwa kutoka vyanzo vya ndani na nje na sekta binafsi kwa ajili ya kugharamia miradi.

“Kamati inatambua kuwa Serikali hukopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kupata fedha za kigeni na kukopesha taasisi za ndani za umma kwa ajili ya kutekeleza miradi ya kimkakati,” alisema.

Mbunge huyo wa Kibakwe alisema kutokana na sababu nzuri za ukopaji ikiwamo uhimilivu wa deni, bado kamati yao inashauri Serikali iangalie uwiano uliopo kati ya mwenendo wa upatikanaji wa mapato ya ndani pamoja na ulipaji wa deni la Serikali na athari zake katika bajeti a uchumi.

Kamati hiyo ilishauri kuwa, umefika wakati Serikali ipange bajeti yake ya maendeleo kwa kutegemea mapato yake ya ndani na mikopo ya ndani ambayo upatikanaji wake ni wa uhakika.
Aliitaka Serikali kuhakikisha kuwa ukopaji wake katika vyanzo vya ndani hauathiri upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi huku akiipongeza kwa kuendelea kufanyia kazi mapendekezo mbalimbali yanayotolewa na kamati hiyo.

Simbachawene alisema hadi Desemba mwaka jana, Serikali ilikuwa imekusanya Sh12.8 trilioni sawa na asilimia 80.4 ya lengo la kukusanya Sh15.974 trilioni na asilimia 32.5 ya lengo la mwaka ambapo zinatakiwa kukusanywa Sh32.475trilioni.

Alisema kodi ya ushuru wa forodha inaongoza kwa kukusanya Sh3.143 trilioni ikifuatiwa na walipa kodi wakubwa waliokusanya Sh2.980 trilioni wakifuatiwa na kodi za ndani Sh 1.594trilioni.

Alitaja sababu ya kutofikiwa kwa lengo la nusu mwaka kuwa ni kutokana na kutopokewa kwa misaada kwa wakati ambapo hadi kufikia Desemba mwaka jana, kiasi kilichokuwa kimepokewa na Serikali kutoka nchi wahisani ilikuwa ni Sh878.8 bilioni kati ya Sh 2.676 trilioni zilizoahidiwa.

Alisema kati ya Sh12.839 trilioni zilizokusanywa, Sh4.77trilioni sawa na asilimia 37.1 zilitumika kugharamia Deni la Taifa pamoja na riba ya madeni yaliyoiva ambapo Sh3.311 trilioni zilitumika kulipa mishahara na Sh4.749 trilioni ndizo zilizotumika kwa shughuli za maendeleo.

Alisema kwa mwendo huo, huenda Serikali ikashindwa kufikia malengo yake ya makusanyo kwani inaonyesha inaweza kufikia asilimia 80 hadi 95 na kupendekeza iongeze wigo wa ukusanyaji mapato ya ndani na kutafuta vyanzo vipya vya mapato.


Mh Mwenyekiti bila shaka vyama vya upinzani ndiyo vimesababisha pia kukua kwa deni la Taifa kiasi hiki. Shukuru Mungu uwaziri ulikuwa unakucover ujinga wako vinginevyo tungeujua uzumbukuku wako long time.
 
Pombe anatuambia makusanyo yameongezeka, anadai miradi mingi mfano mradi wa reli, umeme, ndege, elimu bure nk yanafanyika kwa kutumia mapato yetu ya ndani, ukiangalia hakuna ongezeko la mishahara au watumishi wapya, je hilo deni limeongezeka kwa sababu zipi??? Niliwahi kusema, awamu ya tano ndiyo awamu iliyojaa ufisadi kuliko awamu zilizopita.
Hata zipite karne tano zijazo,hakutatokea serikali fisadi kama hii.
Miaka ya 70 na 80 huko Latin America, kulikuwa na serikali za watu kupotea kama ilivyo Tanzania ya leo. Angalau hizo zilikuwa serikali za kijeshi.
 
Usichokijua wewe kukopa lazima uwe na sifa za kukopesheka. Jiulize hizo sifa za kukopesheka kazipata vipi?

Kitu kimoja hujaelewa, jiulize kwanini tumeacha kukopa kwa riba nafuu tukaenda kwenye commercial rates!? hapa kuna tatizo ambalo halisemwi na huyo Mh. Simbachawene hajalisema. Kujiingiza kwenye commercial rates in hatari maana deni litakua haraka sana na masharti yake ni tight.
Naomba aliye karibu na Mh. Simbachawene amwambie aelleze kwanini tumeenda comercial rates!? ni kwasababu kwenye riba nafuu hatuqualify tena? ni kwasababu commercial rates ni haraka kupita kuliko riba nafuu? nini hasa tradeoff iliyopo hapa?

Hii quote inaashiria kitu fulani
......“Kwa sasa Serikali imelazimika kujielekeza kukopa mikopo yenye masharti ya kibisahara (non concessional loans) kuliko yenye masharti nafuu (concessional) kama ilivyokuwa awali"
 
Kusema kulalamika kuwa Deni linaongexeka haisaidii kitu Kama hsmuuzi bidhaa nje na hamna hzo bidhaa mnategemea kununua tokea kwa wenzenu mnategemea nini?

Njia pekee ya kubadilisha Hilo Deni na kulipunguza n kila mtanzania achukue Nia ya dhati ya kupunguza Deni la taifa kupitia mikono, ujuzi na nguvu zake ahahakikishe analeta ubunifu katika kile anachofanya anaongeza juhudi na nguvu ili aweze kutimiza na kuzalisha kitu chenye ubora na aweke +ve mark kwake yeye binafsi hvyo kila mtu akifanya hvyo tutachangia pato kwa serikali hvyo litakuwa kubwa kwa wakati husika na kuifanya serikali kutokutafuta fedha nje ya mifuko yako hvyo kufanya Deni Hilo kupungua Hadi kuisha.

Ndomana hasa vijana yatupasa kujikita kwenye shughuli za uzalishaji uliobora zenye kukidhi haja ya soko la kimataifa hvyo tutauza bidhaa zetu nnje ya nchi sababu ndani tutakuwa tumejitoshelexa.

Kuhusu swala la mitaji kweli NI changamoto sababu tulichelewa kuelemika na kujitengenezea miundombinu ya kukopa na kukopesheka kwako wote sio mabenki Kama mkopeshaji japo nayo yanakopa pia na mtu mmoja mmoja au taasisi kwa maana ya mkopeshwaji lakini sikuhz zipo fursa za kukopesheka hasa kwa vijana na kina mama jinsi ya kukidhi vigezo

1. Jitafuteni vijana wenye mawazo + uaminifu sawa ili mje na mradi wenye kufanikiwa

2. Jiridhisheni kuwa mtaweza kufanikiwa kwenye mradi wenu na mtakuwa mfano wa kuigwa ndani ya jamii na taifa

3. Nendeni ofisi za halmashauri ya wilaya ofisi ya maendeleo jamii mtakopesheka


AU


Nendeni ofisi za Vision fund na zingine kamahzo ambazo masharti yake n nafuu mtakopesheka


Tukianzia hapa tutalipunguza Deni letu tuladaiwa Kama taifa Mana hzo pesa serikali imezikopea kujenga barabara, kununua madawa, kutengeneza mazingira rafiki kwa kila mtanzania aweze kufanya shughuli zake kiurahisi.

Tuweke mitazamo mibaya ebu tulichukulie Hilo den positive na tujifunge mkanda Kama hatutaushangaza ulimwengu.
 
Wakati Rais wa wamu ya nne,Rais Jakaya Mrisho Kikwete anakabidhi nchi mwaka 2015, deni la Taifa lilikuwa Tril 43.

Baadae akaingia Rais Magufuli,hata hivyo taarifa zinaonesha kuwa deni la taifa limepanda mpaka Tril 62 ndani ya miaka mitatu tu ya utawala wa awamu ya tano.

Maswali ya mjadala.
1.Ni miradi hani iliyokwisha gharimu tril 19 zilizokopwa mpaka sasa?

2.Fedha tunazoambiwa ni makusanyo ya ndani zinatekeleza miradi gani?

3.Muradi gani inatekelezwa kwa fedha za mkopo na ipi inatekelezwa kwa fedha zitokanazo na makusanyo yetu wenyewe?

4.Kasi hii ya ukuaji wa deni,inaendana na ukuaji wa uchumi wetu?

5.Serikali ipongezwe kwa kasi hii ya ukopaji au idhibitiwe ili tutekeleze miradi kwa fedha zetu wenyewe?

Mjadala upo wazi,ushabiki wa vyama vyenu hauna tija,tutangulize maslahi ya taifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwaiyo tokea aingie miaka mitatu huoni kinachofanyika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom