Demu wa facebook

msani

JF-Expert Member
Jun 13, 2011
1,801
1,191
Ndugu zanguni,nimekuwa kwenye facebook takribani miaka 2 sasa na imekuwa nzuri kwangu kwani imenifanya kukutana na baadhi marafiki zangu ambao tulipotezana kwa muda wa miaka mingi hasa wa shule ya msingi. Pia nimebahatika kufahamiana na watu wengi sana na kuwa nao karibu utadhani tulifahamiana hapo awali kabla ya facebook. Nilitokea kukutana na dada mmoja ambaye tulikuwa karibu sana naye,tulishirkiana katika mambo mengi na kiasi kwamba marafiki zangu walijua kila kitu baina yetu,ilifika hatua tukaamua kwamba tunaweza kufunga ndoa,lakini takribani mwezi haji kunitembelea kama ilivyokuwa awali na pia tulipenda sana kuchat kwenye facebook hasa usiku,baadaye alianza kubadilika hadi ikafikia tuko hewani lakini akatumia saa 1 kujibu meseji yangu,suala hilo likanichanganya nikaamua kufungua akaunti nyingine nikatuma friend request naye akakubali tukawa tunawasiliana naye vizuri sana,hapa nyumbani kuna compyuta 2,nikaonganisha zote na internet,tukawa tukiwasiliana kwa akaunti zote 2 ila hii yangu anayoijua yeye mawasiliano yakawa sio mazuri kama hii mpya,nikamuuliza kwenye akaunti mpya iwapo kama ana mtu akajibu hana,na hapo awali tuliamua kubadilisha status zetu wote na kuandika 'in relatioship' ingawa hakutaka tuandike tuko na nani kwenye hiyo relationship.
siku ya trh 2/08/2011 usiku alikuwa hewani ila hakuwasiliana na mimi kwenye akaunti yangu ya awali ila alikuwa ananijibu iwapo nitatumia akaunti mpya ambayo hajui anawasiliana na nani maana sikuweka picha! ila ilipofika asubuhi akanitumia meseji kwamba anashida na vocha kwamba anataka kuwasiliana na ndg yake aliyeko A town ambaye ni mimi bila ya yeye kujua
KAZI KWENU WANA JF KWA NASAHA ZENU
 
so unataka tukuambie nini?

face book siyo mtakutana na majin uko shauri zenu....
 
Pole! achana naye huyo hayuko na wewe tena. Ila chunguza uone ni wapi 'ulipoanguka' ikiwezekana urekebishe.
 
mbona jibu tayari unalo.huyo atakuwa anawapanga,mpo wengi. inauma kama wewe ulimpenda kumbe mwenzako ana ku use tu.ila kuna rafiki yangu mmoja alipata mchumba face book,na ameshaolewa,mimi kwa upande wangu ,mambo ya face book huwa siyaamini.
 
Ndugu zanguni,nimekuwa kwenye facebook takribani miaka 2 sasa na imekuwa nzuri kwangu kwani imenifanya kukutana na baadhi marafiki zangu ambao tulipotezana kwa muda wa miaka mingi hasa wa shule ya msingi. Pia nimebahatika kufahamiana na watu wengi sana na kuwa nao karibu utadhani tulifahamiana hapo awali kabla ya facebook. Nilitokea kukutana na dada mmoja ambaye tulikuwa karibu sana naye,tulishirkiana katika mambo mengi na kiasi kwamba marafiki zangu walijua kila kitu baina yetu,ilifika hatua tukaamua kwamba tunaweza kufunga ndoa,lakini takribani mwezi haji kunitembelea kama ilivyokuwa awali na pia tulipenda sana kuchat kwenye facebook hasa usiku,baadaye alianza kubadilika hadi ikafikia tuko hewani lakini akatumia saa 1 kujibu meseji yangu,suala hilo likanichanganya nikaamua kufungua akaunti nyingine nikatuma friend request naye akakubali tukawa tunawasiliana naye vizuri sana,hapa nyumbani kuna compyuta 2,nikaonganisha zote na internet,tukawa tukiwasiliana kwa akaunti zote 2 ila hii yangu anayoijua yeye mawasiliano yakawa sio mazuri kama hii mpya,nikamuuliza kwenye akaunti mpya iwapo kama ana mtu akajibu hana,na hapo awali tuliamua kubadilisha status zetu wote na kuandika 'in relatioship' ingawa hakutaka tuandike tuko na nani kwenye hiyo relationship.
siku ya trh 2/08/2011 usiku alikuwa hewani ila hakuwasiliana na mimi kwenye akaunti yangu ya awali ila alikuwa ananijibu iwapo nitatumia akaunti mpya ambayo hajui anawasiliana na nani maana sikuweka picha! ila ilipofika asubuhi akanitumia meseji kwamba anashida na vocha kwamba anataka kuwasiliana na ndg yake aliyeko A town ambaye ni mimi bila ya yeye kujua
KAZI KWENU WANA JF KWA NASAHA ZENU
dah!!!, huku uliko wewe leo ni tarehe ngapi mkuu?
 
Du. usiku wa tarehe mbili august 2011?sawa. Hivi huko facebook ndo pakutongozea? Kwakweli nilikuwa na account ya facebook ikabidi niifunge kwakuwa sikuona chochote cha maana zaidi ya kuuza sura tu, huwezi kupata mchango wa mawazo wala ideal mpya zaidi ya usharobaro tu, unakuwa na friends 100 unajuana na 5 tu, utakuta wanaume kazi kuadd ladies tu kuwa friends, wengine wala hawaweki picha zao halisi.

huo ni ujinga tu wacha facebook love story
 
Mkuu the same happens to me. Unajikuta kwa siku kuna friends 100 wako on line ila unaowez akuchat nao issue za maana ni wawili na wengine either hata ukituma msg hawajibu au wakichat na wewe hawana issue ya maana
Niliifunga account mapema sana
Issue nyingi ni za kutongozana na kuombana vocha za simu hata kama hawakujui
 
sasa hivi ni saa 11 jioni bado ucku trh 02-08-11 haujafika au uko far east
ila si mbaya just dating
 
Kumbe unatoa taarifa!Bora mimi sijawahi hata kuifungua hiyo facebook,i don't knw anything about facebook!
 
U gotta be kidding me!!!ivi kuna watu bado wako serious kabisa na hizi relationship za kwenye social networks? kwanza sijui unataka uambiwe nini???
 
Kwa kweli FB ni mtandao wa kuuza sura tu. Mimi naitumia kutunza picha zangu ninazopiga na washkaji zangu wakiniTAG basi nazikusanya poa.Lakini kwa habari ya Mahusiano huko ni kuzinguana tu. Kwanza angalia Profile za wadada kisha angalia za watoto wa kiume yaan sanaa tupu.Anyway mmekutana wote sanaa mtindo1. Vipi uklijiunga na Dating Club?
 
Kumbe unatoa taarifa!Bora mimi sijawahi hata kuifungua hiyo facebook,i don't knw anything about facebook!
<br />
<br />
halafu wewe, hebu nenda ukaaccept friendship request yangu kule.
 
Bongo dalisalam alijisemea Prof jay cheni ya bandia kwa fedha bandia basi ngoma drooo
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom