Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,597
- 46,230
Bila kuuondoa umaskini ni vigumu sana kusimika demokrasia.
Nchi zote zenye demokrasia iliyoshamiri zimefika hapo baada ya kupiga hatua kubwa kuuondoa umaskini.
Mambo matano ya yanayofanya umaskini kwa sumu kwa demokrasia ni;
1. Umaskini unadumuza kwa kiasi kikubwa uwezo wa raia kufikiri na kudadavua mambo. Mitazamo ya maskini na matajiri katika maisha ni tofauti sana. Maskini mara zote huwa anawaza mlo unaofuta utatoka wapi, matajiri huwa wanawaza miaka 2, 3, 5 wawekeze kwenye katika kitu gani kukuza zaidi utajiri wao. Kwa maana hiyo ata maamuzi ya kisiasa yanayofanywa na maskini ni kwa mtazamo wa muda mfupi wakati matajiri ni kwa muda mrefu.
2. Ukiwa maskini unakosa msimamo, mara nyingi inakubidi kukubaliana na misimamo ya wenye pesa au mamlaka ukifikiri maisha yako yatafanywa rahisi na wao lakini mara zote sio kweli kwamba maisha yanaboreka kwa kuwa
3. Maskini mara nyingi ni rahisi kupandikizwa chuki na kufanya mambo kwa hasira ambayo wakati mwingine hayana faida kwao. Hiyo ndio njia aliyoitumia Hitler kuingia madarakani. matajiri wao wanafanya mambo yao kwa kuangalia maslahi yao ya kibiashara, haijalishi mmetofautiana kiasi gani wao wanatanguliza biashara zao mbele zaidi kuliko hisia.
4. Maskini hawana umoja, ushirikiani na muunganiko wenye nguvu sana tofauti na wenzao matajiri. Masikini wanakosa "cooperation" kwa kiasi kikubwa tofauti na matajiri ambao mara nyingi ni rahisi sana kuungana dhidi ya mambo yanayotishia maslahi yao na ndio maana unaona wengi wanaokali viti vya mamlaka ni wenye hali nzuri kiuchumi.
5. Maskini hata akiwa "smart" sana sio rahisi kuchaguliwa kiongozi kupitia uchaguzi huru. Hii inasababishwa na ukweli kwamba matajiri wana connection, nyenzo na njia nyingi za kupenya na kuwa viongozi.
Umaskini ni mwiba mkali wa demokrasia, tupambane nao kwa nguvu zaidi.