Demokrasia inazidi kuyamaliza mataifa ya Ulaya

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,152
10,862
Kwa kutumia demokrasia watu wenye sifa mbaya kiutawala na ambao wamewahi kuzitiia nchi zao kwenye mizozo wamekuwa wakirudi madarakani kwa kasi.Mmojawapo ni Benjamin Netanyahu wa Israel.

Muda wote wa uongozi wake mbali na kuwaadhibu wapalestina alikuwa daima yuko mahakamani kwa shutuma mchanganyiko. Juzi imeelezwa ameshinda tena uchaguzi.

Mtu mwengine ambaye hana sifa za uongozi na kama mwenye kichaa ni Donald Trump.Tayari anafanya kampleni za kumrudisha madarakani na kwa kutumia demokrasia ana wafuasi wanaomuunga mkono.

Kwa mfumo huu wa utawala nchi za magharibi zitazidi kudidimia na sehemu yake kwa kuanzia kuchukuliwa na nchi kama vile China na Russia.
 
Hii ndiyo inatakiwa Afrika tufuate. Inakuza uchumi na inapunguza ugomvi. Hata zaidi ya miaka 20 ikiwa hajatukosea wacha atawale.
Ni Bora kutawaliwa na mtu mmoja hata miaka thelasini lakini maendeleo yaonekane kuliko kubadili wezi na wenye njaa Kila baada ya miaka kumi mtu anaingia madarakani akiwa maskini miaka yote kumi anaiba tu akifikia kiwango Cha kitajitika mda unakua umeisha anaingia mwingine Tena hivyohivyo Kwa kigezo Cha demokrasia ndio maana afrika inazidi kuwa maskini

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
 
Hujafikiria akipatikana kichaa mmoja akikaa madarakani kwa miaka 30 bila democracy itakuaje, kiongozi mbovu akiwa amechaguliwa na wananchi kwa majority vote hamna shida na hakuna atayelaumiwa.

Mi nasimama na democracy it's best option.
 
Katiba iwekwe vizuri.Mtu kichaa hatoweza kutawala kwa muda mrefu kwani mambo hayo yanatakiwa yapitie kwenye mabunge na mahakama bila uchaguzi. Muhimu Cha kukwepa ni uchaguzi ambao ni udanganyifu zaidi kuliko ukweli.Na ni kutajirisha nchi za Ulaya wanaotuuzia takataka za uchaguzi huku wenyewe tunahitaji hizo pesa.
 
Kwa kutumia demokrasia watu wenye sifa mbaya kiutawala na ambao wamewahi kuzitiia nchi zao kwenye mizozo wamekuwa wakirudi madarakani kwa kasi.Mmojawapo ni Benjamin Netanyahu wa Israel.

Muda wote wa uongozi wake mbali na kuwaadhibu wapalestina alikuwa daima yuko mahakamani kwa shutuma mchanganyiko. Juzi imeelezwa ameshinda tena uchaguzi.

Mtu mwengine ambaye hana sifa za uongozi na kama mwenye kichaa ni Donald Trump.Tayari anafanya kampleni za kumrudisha madarakani na kwa kutumia demokrasia ana wafuasi wanaomuunga mkono.

Kwa mfumo huu wa utawala nchi za magharibi zitazidi kudidimia na sehemu yake kwa kuanzia kuchukuliwa na nchi kama vile China na Russia.
unaona bora na wao wapate maji na umeme wa mgao huku ukishangilia Fisiem oyeee
 
Ni Bora kutawaliwa na mtu mmoja hata miaka thelasini lakini maendeleo yaonekane kuliko kubadili wezi na wenye njaa Kila baada ya miaka kumi mtu anaingia madarakani akiwa maskini miaka yote kumi anaiba tu akifikia kiwango Cha kitajitika mda unakua umeisha anaingia mwingine Tena hivyohivyo Kwa kigezo Cha demokrasia ndio maana afrika inazidi kuwa maskini

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
Hata hao madikteta wako hakuna anaefikia nchi za Ulaya , China yenyew ni mbuz tu , Ulaya hadi kijijini fulu kiyoyoz , China kuna sehem bora Afrika
 
Ni Bora kutawaliwa na mtu mmoja hata miaka thelasini lakini maendeleo yaonekane kuliko kubadili wezi na wenye njaa Kila baada ya miaka kumi mtu anaingia madarakani akiwa maskini miaka yote kumi anaiba tu akifikia kiwango Cha kitajitika mda unakua umeisha anaingia mwingine Tena hivyohivyo Kwa kigezo Cha demokrasia ndio maana afrika inazidi kuwa maskini

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
Huna tofauti na yule alikuwa anajiita Jiwe /Kichaa
 
Hata huelewei mwenyewe unachokizungumza.
Ni contradiction tupu.
Katiba iwekwe vizuri.Mtu kichaa hatoweza kutawala kwa muda mrefu kwani mambo hayo yanatakiwa yapitie kwenye mabunge na mahakama bila uchaguzi. Muhimu Cha kukwepa ni uchaguzi ambao ni udanganyifu zaidi kuliko ukweli.Na ni kutajirisha nchi za Ulaya wanaotuuzia takataka za uchaguzi huku wenyewe tunahitaji hizo pesa.
 
Demokrasia ulaya halafu mifano ni ya middle east na amerika? Au ramani ya dunia humu Jf ni tofauti na tuliyoizoea!
 
Hata huelewei mwenyewe unachokizungumza.
Ni contradiction tupu.
Unaposoma inaonekana huelewi halafu unaita contradiction.Onesha wapi ili upatiwe ufafanuzi.
 
Ni Bora kutawaliwa na mtu mmoja hata miaka thelasini lakini maendeleo yaonekane kuliko kubadili wezi na wenye njaa Kila baada ya miaka kumi mtu anaingia madarakani akiwa maskini miaka yote kumi anaiba tu akifikia kiwango Cha kitajitika mda unakua umeisha anaingia mwingine Tena hivyohivyo Kwa kigezo Cha demokrasia ndio maana afrika inazidi kuwa maskini

Sent from my RMX2189 using JamiiForums mobile app
Afrika hii hii tumetawaliwa na machifu kwa enzi na enzi lkn ni chifu tu na watu wake ndio waliokuwa wanaruhusiwa hata kuvaa nguo na kuishi vizuri huku raia wengine akiwafanya wapagazi wake na hata wake zao akiwanyang'anya.

Watawala wengi wa kiafrika ndio wameongoza kwa kukaa madarakani kwa muda mrefu lakini ndilo bara lililokubuhu kwa ufukara.

Wewe naona una akili kama za hao watawala wenu waliofanya leo muwe mabingwa wa kutembeza bakuli. Una akili za kitoto sana na inaonekana hauna exposure kabisa, wewe ni wa humu humu. Bure kabisa.
 
Usidharau tawala zetu kwa kufadhili za wazungu. Hizo tawala unazosema zikirudi zitakuwa za mifumo iliyoimarishwa.Tutamia teknolojia mpya na kufanya vyema zaidi pamoja na kuwa haitakuwa demokrasia ya magharibi. Ndio maana daima tukadharaulika na hata kujidharau wenyewe kama unavyofanya wewe kwa kudhani sisi hautwezi kufanya tofauti na wakoloni wetu.
 
Back
Top Bottom