Demokrasia inavyodumaza Maendeleo Afrika

Demokrasia inavyodumaza Maendeleo Afrika

Sijawahi sikia mtu anakimbilia china, russia, north korea and the likes, katika incidence za ukimbizi au political asylums lakini ukiangalia kwa jicho la maendeleo ya vitu zimeendelea kweli kweli......sasa sijui ni kwa nini....??? Na kama sikosei hivi karibuni katibu wa chama cha jembe na nyundo alisema maendeleo ni watu na si vitu......
 
Tatizo kubwa la Africa ni mifumo tuliyorithi kwa wakoloni. Wakoloni walikuwa hawajamaliza kazi yao ya kutustaarabisha wakaondoka. Wakatuachia wakoloni weusi (serikali) ambao hawajui lengo la kuwa wakoloni ndani ya mataifa yao. Serikali kwa mfumo wake ina nguvu nyingi sana, serikali inaweza kufanya mazuri yoyote kwa watu au mabaya. Serikali ndio mkoloni mkuu mweusi ambaye akizingatia malengo ya mkoloni anaweza kutufikisha mbali. Kumbuka wananchi wote wanatii serikali. Wanaweza kufanya lolote serikali inataka liwe zuri au baya.
Serikali (Political institution) zetu za Afrika zikiamua kwa dhati shida zetu zote zitakwisha ukiwemo umaskini. Narudia tena Waafrika tupo tulipo kwa sababu serikali zetu zimetaka tuwe hivi, siku zikiamua zinaweza kutupeleka tunapotaka..
Matatizo tuliyo nayo yote ni kwa sababu ya mifumo mibovu ya kisiasa zikiwemo taasisi zake. Asilaumiwe mtu mmoja mmoja bali serikali/ siasa zetu. Wakubwa wanatamani utajiri uliokithiri, unadhani wadogo wataambulia nini? na hao ndio walioshikilia nguvu (wakoloni wetu)
 
Kwa waliosoma bila kuelimika demokrasia kwao ni:-
1.Wachache kuamua kwa niaba ya wengi.
2.Kusema na kudumisha uongo.
3.Kupuuza na kuzuia mawazo ya wengine.
4.Kudhulumu haki za wananchi.
5.Kukubali kila wazo la kiongozi.
Waafrika maana ya demokrasia kwao ni;
1. Kuzaa bila mpangilio;
2. Kulalamika bila kutimiza wajibu (Vyama pinzani)
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Fikiria nchi imepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;

1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.

2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)

Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?

** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.

NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa wanakosa mpaka ada ya kuwalipia watoto wao Chuo kikuu (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Ni vyema ujielimishe kidogo watu wanapozungumzia maendeleo na demokrasia wanamaanisha nini kwa kuanzia. Ni vizuri pia ukajua chanzo cha dhana ya demokrasia.
1. Maendeleo ni hatua kutoka kwenye hali duni kwenda kwenye iliyo bora: kijamii, kiuchumi, kiteknolojia, kisiasa, nk. Hatua zinaweza kuwa ndogo lakini hayasimami.
2. Demokrasia inajumuisha mambo kadhaa yakiwemo namna wananchi wanavyochaguana kujiongoza (serikali iliyochaguliwa na watu kuwatumikia), haki na uhuru wa wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo yao, haki na uhuru kusikilizwa,kuabudu bila kuvunja sheria, nk.
Dhana nyingi zinaboreshwa au zinakufa kutegemeana na uhitaji wa nyakati na maendeleo ya jamii husika. Dhana ya demokrasia naamini itaendelea kuboreka na kuimarika kwa sababu ulimwengu unaihitaji sana.
Kuna ustarabu zaidi duniani kwa sasa ikilinganishwa na zama za ushenzi ambako MTU mweusi aliuzwa mnadani kama mnyama na kusafirishwa kwenda utumwani. Aidha, kulikuwa na ukatili mkubwa enzi za tawala za ulaya na kwingineko zilizojengwa kwa nguvu za majeshi na vita. Tawala za kifalme hazikuchaguliwa; zilijisimika. Polepole ustarabu ukaja has a kutokana na mwamko na uthubutu wa watu kupinga uonevu na udhalimu wa watawala. Mifumo, mahusiano, na uwiano ya uchumi nayo ikabadilika. Hapo ndilo chimbuko la chaguzi na demokrasia.
Kuruhusiwa kwa mfumo wa siasa za ushindani katika nchi zinazoendelea ni moja ya masharti kutoka nchi "zilizostarabika". Ndiyo maana huu mfumo haujakulika barani Afrika.
Kwa bahati mbaya vikundi vya watu wachache vinaweza vikawa na mawazo hasi kama yako ya kufuta upinzani na chaguzi kwa muda na katika nchi chache tu. Gurudumu la mabadiliko halisimami wala halirudi nyuma. Ni suala la muda. Fikra na mitazamo inabadika. Wakati utafika Demokrasia kukubaliwa.
 
Ujinga unao wewe kung'ang'ania demokrasia huku shangazi yako hapati hata panadol akiumwa huko Hanang'-Bashnet. Wakati huku mjini unadai demokrasia na unaishi kwa kubahatisha.
Propoganda yako haina mashiko. Labda ni kutokana na kukosa uzoefu kwenye nyanja hii. Wengi tutashindwa kuelewa hoja yako. Hizo panadol zitapatikana tu kwa kuzuia chaguzi na mfumo wa vyama vingi vya siasa? Kwingineko duniani kunakopatikana huduma afya na maji, elimu bora, barabara, nk. hawachaguani?
 
Tungeendekeza demokrasia mpaka Leo mashirika ya ndege, simu/mawasiliano na zao la korosho yangekuwa mfu
 
Waafrika tumekaa kama mizigo tu kila kitu demokrasia, ujerumani ya leo walifanya kazi kwa bidii kufikia pale. Sio kukosoa tu bali ni kufanya kazi kwa weledi na bidii kubwa.[/QUOTE Mku shida ni kwamba sisi wa Tz hatujazoea mambo ya mitikasi.
 
Ndugu zangu tusiibeze Demokrasia wewe ukitoa mawazo yako na mwingine akatoa ya kwake halafu mukakaa mukayachambuwa mawazo yenu kwa pamoja mukapata muafaka hayo sio ndio maendeleo,'An Idea is a baby ,please treat it kindly' usimudharau mtu anaye kupa wazo jaribu kulichambua ukiona linafaa please adopt it.
 
Ethiopia ni choka mbaya tu!

Afadhali hata sisi!

Usiwasemee afrika jizungumzie Tanzania na ndugu zako wa Burundi. Africa kuna mataifa ya prosper kwa mwendo wa rocket na demokrasia imenawiri. Nakupa mifano michache South Africa, Botswana, Ethiopia, Ghana , Kenya n.k
 
Ethiopia ni choka mbaya tu!

Afadhali hata sisi!
Ethiopian Airline ingewekwa demokrasia pale nakuhakikishia mpaka Leo wangekuwa na ndege 2 tu.
Kwa taarifa tu Ethiopian Airline;
1. Hakuna vyama vya wafanyakazi (Trade Union) hivyo hakuna kelele/migomo za nyongeza ya Mshahara.
2. Hakuna Financial Audited Report (mapato & matumizi, hesabu za shirika ni siri kubwa).
 
Ukitaka usisumbuliwe kuhusu demokrasia na kupewa misaada ipende nchi yako hakikisha kila pesa inaenda kuinua uchumi wa taifa tatizo la viongozi wa africa hawazipendi nchi zao wao ni matumbo yao wanajali tu
China na urusi wamejikomboa kwa kuwa na viongozi wanataka kuona taifa likipiga hatua na sio ccm ikipiga hatua
 
Fikiria nchi imepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;

1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.

2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)

Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?

** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.

NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa wanakosa mpaka ada ya kuwalipia watoto wao Chuo kikuu (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Very true
 
2019 Mwaka wa Kufanikisha sekta kichocheo kwa maendeleo ya viwanda
 
...USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
Wewe USA unaijua? Kumbuka kuwa wanaoitwa Wamarekani ni wahamiaji waliozikimbia nchi zao kwa kuutafuta uhuru zaidi wa kidemokrasia. Ni Marekani wanakopatikana watu waliotoka mataifa yote duniani waliolazimika kuziacha nchi zao, asili zao, familia zao, rangi zao, imani zao, tamaduni zao na mali zao kuanzisha maisha mapya. Wengi ni wahanga wa tawala mbovu na za kidikteta wakiepuka ugumu wa maisha ulioambatana na mateso na utawala wa mabavu usiothamini uhuru na haki.
 
Wewe USA unaijua? Kumbuka kuwa wanaoitwa Wamarekani ni wahamiaji waliozikimbia nchi zao kwa kuutafuta uhuru zaidi wa kidemokrasia. Ni Marekani wanakopatikana watu waliotoka mataifa yote duniani waliolazimika kuziacha nchi zao, asili yao, familia zao, rangi zao, imani zao, tamaduni zao na mali zao kuanzisha maisha mapya. Wengi ni wahanga wa tawala mbovu na za kidikteta wakiepuka ugumu wa maisha ulioambatana na mateso na utawala wa mabavu usiothamini uhuru na haki.
1. Tulia, usome, uelewe punguza jazba na maneno ya kwenye kitchen party.
2. Naijua vizuri USA, nimesoma huko kwa miezi 18.
**Hoja yangu ni kuwa Demokrasia inayopigiwa kelele nchi nyingi za Afrika si sawa na USA ambao wamepata uhuru 1776. Demokrasia kwetu kwa sasa ni kuwezesha wananchi wafanye kazi zaidi na si kupiga domo na kubugia ruzuku tu
 
Back
Top Bottom