Demokrasia inavyodumaza Maendeleo Afrika

Waafrika tumekaa kama mizigo tu kila kitu demokrasia, ujerumani ya leo walifanya kazi kwa bidii kufikia pale. Sio kukosoa tu bali ni kufanya kazi kwa weledi na bidii kubwa.
Mwaka gani huo mkuu kama vile umeandika tu
 
Afrika tunahitaji mijeledi ili tukae sawa. Demokrasia imefeli Afrika (ikiwemo Tanzania)
acha kupotosha africa hakujawahi kuwepo demokrasia ya kweli. siku tukifikia hata 50% ya demokrasia tutapiga hatua
 
Hapana demokrasia tunahitaji tena sana. Ambacho hatuhitaji ni haya maisha ya kuendekeza too much politics tena muda wote.
Mtu anaamka asubui hata kabla hajajua leo ataingiza nini anatafuta Rais kaongea nini ili amponde au apongeze. Hiyo ni kila siku. Inatija gani kwako?
Mwingine hata ujasiri wa kujichomoa home kwa wazazi au nyumbani kwa shemeji hana anashinda humu anapambana na Magu. It's a crazy!

Hata zilikotoka hizi demokrasia wana balance mambo yao vizuri sana. Sasa huku unamkuta mtu yuko kwenye mkutano wa hadhara Mchana katikati ya wiki na hamna hata uchaguzi. Anatoa wapi huo muda!

Kingine, sijaona popote duniani vijana wengi wanamaliza vyuo wanaota kuingia kwenye siasa kama ajira yao ya kwanza, ni hapa kwetu tu.

Halafu aliyetupa hili jina la wabongo, atafutwe please aje alichukue aende nalo. Wabongo inaashiria watu wanaotegemea ujanja-ujanja kuishi. Kwangu hiyo imekaa fyongo sana ndio maana tunapenda saaana siasa kwani nayo ni ujanja-ujanja pia.
 
Wengi wamekupinga na watakupinga ila huo ndio ukweli,Haka ka dubwana Demokrasia ndio kamesababisha nchi nyingi zimepoteza rasilimali na kuingiliwa baadhi ya mabo yao,kuna mwandishi mmoja Wa kitabu cha ASA=OLD AS EMPIRE anaeleza vizuri jinsi nchi za kimagharibi zinavyotupumbaza kupitia demokrasia,anasema kwanza nchi nyingi hata hiyo demokrasia yenyewe haipo,kuna vyama vimekata tamaa hata ya kuja kushika madaraka,na si kwamba havina vigezo ila vitapewa ushindi vile vinavyoonekana kutetea matakwa ya western countries,wanaojifanya wanakuja kutetea demokrasia wana kazi nyingine kabisa ya kuhakikisha nchi zao zinakomba resources za nchi husika,ila ukiwauliza watakujibu kuwa wamekuja kusimamia Demokrasia safi kwenye nchi husika,after all hata hivyo vyama vikiingia hakuna kinachobadilika zaidi ya kukaa na kujiliwaza kuwa siku akiingia fulani aaaah tutakula bata kwa mrija,kama watoto wa kuku kila siku wanamfuata mama yao wakiamini kesho watanyonya,Ndio maana hakuna nchi zenye aendeleo makubwa na amani kama nchi tunazoziita za 'kidikteta' nyingi zina maisha bora kabisa,zina ustawi mzuri wa kiuchumi na kijamii,zile za kidemokrasis zimechoka taabani,zinapumulia gesi,mfano Tanzania eti miaka 50 mtu anajivunia kuwapa wananchi wake maji na kujenga barabara,yaani hayo ni sawa na mtu ana miaka 50 anajisifia kula na kuvaa wakati hayo ni mambo ya lazima,yaani leo hii tungekuwa tunaongelea fly overs za kwenda mikoani,treni za umeme nk,nenda nchi za kifalme kama Saudia,Brunei,Qatar,Rwanda,Libya kabla hizo fikra za demokrasia hazijavamia
 
Yaani umri huo bado unajikojolea ndani ya chupi, hahahaaaa. Bashite yako itakuwa nyang'anyang'a wewe.
Eti demokrasia, my foot! Futa chaguzi na uhuru wa ajabu ajabu. Hupeleki mtoto shule kisa huna pesa lakini hela ya kwenda kumpa Nabii akanunulie helikopta au kupanda ndege kwenda kuhiji ipo. Hatuwez kuendelea kwa style hii. Lazima mabadiliko makubwa yafanyike.
NB: mijeledi iongeze kurudisha heshima ta kazi.
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
3. Tuombe tuendelee kutawaliwa wao wakoloni wana vipaumbele vizuri vya kulete maendeleo, wanajua ni watu gani wanapaswa kusoma, labour force, wajeshi n.k ili nchi iweze kusonga mbele.
 
Daaaaaah mpaka chuki za kidini????umeichambua ibada ya hija kichuki sana
 
Eti demokrasia, my foot! Futa chaguzi na uhuru wa ajabu ajabu. Hupeleki mtoto shule kisa huna pesa lakini hela ya kwenda kumpa Nabii akanunulie helikopta au kupanda ndege kwenda kuhiji ipo. Hatuwez kuendelea kwa style hii. Lazima mabadiliko makubwa yafanyike.
NB: mijeledi iongeze kurudisha heshima ta kazi.
Kwani uliambiwa huku walikoendelea Marekani, Europe Japan nk hakuna makanisa au misikiti au nyumba nyingine za ibada? Au wenzetu walipotaka kuendelea walibomoa nyumba zote za ibada na kuwa wapagani?
 
Wengi wamekupinga na watakupinga ila huo ndio ukweli,Haka ka dubwana Demokrasia ndio kamesababisha nchi nyingi zimepoteza rasilimali na kuingiliwa baadhi ya mabo yao,kuna mwandishi mmoja Wa kitabu cha ASA=OLD AS EMPIRE anaeleza vizuri jinsi nchi za kimagharibi zinavyotupumbaza kupitia demokrasia,anasema kwanza nchi nyingi hata hiyo demokrasia yenyewe haipo,kuna vyama vimekata tamaa hata ya kuja kushika madaraka,na si kwamba havina vigezo ila vitapewa ushindi vile vinavyoonekana kutetea matakwa ya western countries,wanaojifanya wanakuja kutetea demokrasia wana kazi nyingine kabisa ya kuhakikisha nchi zao zinakomba resources za nchi husika,ila ukiwauliza watakujibu kuwa wamekuja kusimamia Demokrasia safi kwenye nchi husika,after all hata hivyo vyama vikiingia hakuna kinachobadilika zaidi ya kukaa na kujiliwaza kuwa siku akiingia fulani aaaah tutakula bata kwa mrija,kama watoto wa kuku kila siku wanamfuata mama yao wakiamini kesho watanyonya,Ndio maana hakuna nchi zenye aendeleo makubwa na amani kama nchi tunazoziita za 'kidikteta' nyingi zina maisha bora kabisa,zina ustawi mzuri wa kiuchumi na kijamii,zile za kidemokrasis zimechoka taabani,zinapumulia gesi,mfano Tanzania eti miaka 50 mtu anajivunia kuwapa wananchi wake maji na kujenga barabara,yaani hayo ni sawa na mtu ana miaka 50 anajisifia kula na kuvaa wakati hayo ni mambo ya lazima,yaani leo hii tungekuwa tunaongelea fly overs za kwenda mikoani,treni za umeme nk,nenda nchi za kifalme kama Saudia,Brunei,Qatar,Rwanda,Libya kabla hizo fikra za demokrasia hazijavamia
Karudie kukisoma tena hicho kitabu "A game as old as Empire: The Secret World of Economic Hitmen..." kama ndio unachomaanisha.
 
kwani hicho hicho mkuu,sasa nikarudie nini tena wakati uhalisia hata kwenye maisha ya kawaida unaonekana,kwani nimeongea nini ambacho hakipo kwenye nchi zetu hizi za kidemokrasia?
 
Kukandamiza uhuru wa kujieleza ni kudumaza fikra za watu na hatimaye kudumaa maendeleo. tunakosea sana.
 
Daaaaaah mpaka chuki za kidini????umeichambua ibada ya hija kichuki sana
Huo ndo mfano halisi wa demokrasia (uhuru wa kuabudu) unavyoleta umaskini katika familia/taifa. Pesa hiyo ya hijja ikitumika kuboresha elimu kwa watoto wako ni kiasi gani wataneemeka? Afrika tuchague maendeleo badala ya demokrasia teketeke
 
Kama taifa/bara tukubali tumeteleza turudi kwenye misingi ya maendeleo. Tushikamane, tufanye kazi pamoja tena kwa bidii
 
Fikiria kinchi kimepata uhuru miaka 50 iliyopita leo hii bado ni tegemezi kwa zaidi ya 50% ya bajeti yake na bado watu wake wanataka demokrasia, ipi? Napendekeza yafuatayo;
1. Kufuta Uchaguzi ili kutumia pesa zinazotengwa uchaguzi kujenga miundo mbinu, vituo vya afya na mashule.
2. Futa vyama pinzani maana hivyo ndivyo vinapummbaza watu (miluzi mingi....)
Afrika bado kufikia mambo ya demokrasia, wananchi wetu ni maskini sana hivyo kwa sasa wanahitaji maji, elimu, afya, barabara na si eti inayoitwa DEMOKRASIA, hivi mtu wa huko Lindi vijijini demokrasia yeye ya nn?
** USA imepata uhuru 4 july 1776 na bado demokrasia ya kweli (true democracy) hawajaifikia, wewe na SACCOS yako unadai eti unataka Demokrasia. Piga chini.
NB: Pia hizi imani zinaleta umaskini zaidi, watu wanadanganywa kuwa kuna muujiza katika kufanikiwa (maendeleo) wakati wengine wanakamuliwa pesa ya Hijja na wanabebeshwa mawe toka Afrika kwenda kumtwanga shetani huko umangani (ukihoji eti uhuru wa kuabudu).
Ingekuwa hivyo hata wew usingetoa maoni yako humu!
 
Unaonaje Tuichague Chadema ikishika dola tufute vyama vyote ili sasa tubaki na maendeleo tu.
 
Waafrika ukiwapa demokrasia, atakun.nya barabaranni halafu adai eti nipo huru (demokrasia inamruhusu). Waafrika tunafaa kwenda kwa mjeledi mpaka tukae sawa baada ya miaka 100. (2117).
** Wacha tunyooshwe vizuri kwanza
Line ya mwisho sijakuelewa!Unaongea kana kwamba hayo uliyosema mistari ya juu yashafanikiwa;
 
Afrika tunahitaji mijeledi ili tukae sawa. Demokrasia imefeli Afrika (ikiwemo Tanzania)
Usiwasemee afrika jizungumzie Tanzania na ndugu zako wa Burundi. Africa kuna mataifa ya prosper kwa mwendo wa rocket na demokrasia imenawiri. Nakupa mifano michache South Africa, Botswana, Ethiopia, Ghana , Kenya n.k
 
Sources have confirmed that security officer who pulled gun on Nnauye Nape is from the Presidential Security Unit (PSU), not police
 
Afrika wacha tuendelee hivi hivi tulivyo, demokrasia hatuihitaji kwa sasa. Mahitaji kama chakula, dawa (afya), na elimu ndo muhimu kuliko uppuuzz wa demokrasia
Kwani Tanzania hakuna demokrasia???
 
Back
Top Bottom