Ni kweli tatizo liliopo isw ni la kiutawala na wala haliusiani na degree zinazotolewa hapo. Kwa ufahamisho tu chuo cha ustawi ni miongoni mwa vyuo vinavyotoa taaluma za kipekee hapa nchini. Mfn masomo ya hrm yalianza kutolewa hapo km profession inayojitegemea bila kumajor km baadhi ya vyuo vingine vilivyokuwa vinafanya hapo awali na wapo wanafunzi wengi 2 waliosoma hiyo kozi na wanafanya vzr kwenye soko la ajira. Pia kozi ya Industrial Relation ambayo inatolewa na chuo hicho pekee hapa nchini ambayo inahusiana na mambo ya uhusiano kazini wanafunzi waliomaliza wapo wengi tu kwenye soko la ajira kwa taarifa tu malabour offficers wengi waliopo wamesoma isw. Vilevile kozi ya ustawi wa jamii 'social work' ambayo imeanza kutolewa hapo tangu mwk 1974 pekee hapa TZ hadi sasa imezalisha wataalamu wengi wa fani hiyo ambapo wanafanya kazi kwenye int organazation mbalimbali duniani, na kwenye ngo's nyingi hapa nchini, na pia maafisa ustawi wote waliopo hapa tz wamesoma hapo chuo cha ustawi. Kwa mtazamo maslahi binafsi ya mngt team inapekea matatizo makubwa ktk chuo hicho kwa sasa.