Bingwaman
JF-Expert Member
- Oct 22, 2010
- 548
- 288
Muungano wa Nchi za Kishoshalisti za Kisovieti (USSR) ulikuwa ni mahiri katika uundaji wa ndege. Moja ya aina nyingi za ndege nyingi zilizotengenezwa na USSR kabla ya kuvunjika kwake mwanzoni mwa miaka ya 1990 ni Tupolev Tu-114 iliyotumika kusafirisha abiria. Ndege hii iliyoruka mara ya kwanza 1955 na kustaafishwa 1976 bado inashikilia rekodi ya dunia ya kuwa ndege inayoendeshwa na mapangaboi (propellers) yenye kasi zaidi duniani. Muundo wake na injini za turboprop zenye nguvu kubwa ziliiwezesha Tu-114 kuruka kwa kasi ya kilomita 880 kwa saa, sawa na ndege za abiria za jet za wakati huu (modern jetliners). Iliporuka mara ya kwanza, Tu-114 ilikuwa ni ndege kubwa zaidi ya abiria duniani na yenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu zaidi bila kutua (kilomita 10,000). Ndege hiyo iliweza kubeba hadi abiria 220 na ilikuwa na injini nne aina ya Kuznetsov NK-12 ambazo kila moja ina nguvu ya horsepower 14,000. Kuznetsov NK-12 ni injini za turboprop zenye nguvu zaidi kuwahi kutengenezwa duniani. Kila moja ya injini za Tu-114 iliendesha mapangaboi mawili yaliyozunguka pande tofauti (contra-rotating propellers). Mapangaboi hayo yalikuwa na kipenyo (diameter) cha zaidi ya mita tatu. Tu-114 ilitumika kumsafirisha kiongozi wa zamani wa USSR Nikita Khrushchev kutoka Moscow mpaka New York na kurudi bila kutua (non-stop) mwaka 1959 kabla ya kuanza kusafirisha abiria mwaka uliofuata. Wamarekani walikubali wamepigwa bao kabla ya kujibu mapigo na Boeing 707. Sehemu pekee unapoweza kuiona Tu-114 ni katika makumbusho kadhaa za usafiri wa anga nchini Russia.
Watoto wakiwa wamepozi pembeni ya mapangaboi ya Tu/114
Watoto wakiwa wamepozi pembeni ya mapangaboi ya Tu/114