Wamasai wenye rasta walitulizwa na Masai rapa, mwenda pole hajikwai, alijikwaa baada ya kutegwa na jiwe kubwa, hakunyanyuka tena!

Wamasai wenye rasta walitulizwa na Masai rapa, mwenda pole hajikwai, alijikwaa baada ya kutegwa na jiwe kubwa, hakunyanyuka tena!

britanicca

Platinum Member
Joined
May 20, 2015
Posts
18,178
Reaction score
48,087
Mwenda pole wahenga waliotuambia hajikwai, alijikwaa, aliwekewa jiwe kubwa, akaliona lakini akasema kwa mwendo wake atavuka salama, akajipa moyo na kujiamini. Ahhh akaingia kingi, akajikwaa kweli kweli safari hii kujikwaa ikawa kuanguka, hakuamka tena! Hawana hata habari, sababu hakupita kwenye njia rasmi alipoanza safari yake, alitumia njia za panya. Ndo maana kila siku wanasema hawajui chochote kuhusu jiwe walilomwekea kumtega. Taarifa ni kwamba, methali ilishabadilika maana kitambo sana, wote waliojikwaa baada ya kuwekewa jiwe hawanyanyuki tena, ndio imetoka hiyo, hawatarudi!

Ukiachana na huyo kuna kichomi, huyu nae ilikuwa asindikizwe kenani sababu kawavuruga kwelikweli, na besti yake ndio alikuwa akamalishe hilo, sema kichomi mjanja, akawapiga na uno reverse, kuja kushutuka ameshavaa zake koti😂

Kwa upande mwingine kuna wamasai wenye rasta halafu kuna hawa wa mchongo, ambao hata kimasai hawajui wapo zao kupiga hela tu kwa watalii, wametengeza kichaka chao katika mgodi wa dhahabu, wana nguvu, hakuna wa kuzuia kufanya chochote hapo mgodini, wakizinguliwa tu wanaenda kuripoti kwa Msimamizi Mkuu wapuuzi wote wanatulizwa, jamaa wana mizizi hasa baada ya kuzidi kupewa nguvu na kampuni mama, walianza ubabe toka 80's huko chini ya mwenyekiti fulani.

Sasa, wafanyakazi wa mgodi walichoka kupelekwa kama punda, wakagoma kupiga kazi na kushusha mizigo! Wamasai rapa wakasema usintanie, baada ya kupeleka taarifa kwa Msimamizi Mkuu, wakarudi na kimemo kwa wamasai wenye rasta, hapo wakiwa wamefungiwa ofisini, wakaambiwa ole wenu wafanyakazi waache kupiga mzigo, tutadeal na nyie. Kusikia hivyo wakasema ya nini, hata wale morani walio chini yao wakaminywa, upinzani ulikuwa mkali lakini mwishoni wakamanage kutuliza moto uliosababisha karibu ya nusu ya vitalu kuharibiwa.

Sasa, Msimamizi Mkuu wa mgodi na watu wake wanajitathimini na kuangalia namna na kustopisha kuchukua morani wapya ili kutathimini namna ya kupata wataokuwa waaminifu kwao, maana wangecheza kidogo tu baadhi ya morani huenda wangechukua mgodi na kuungana na wafanyakazi, sababu nao wamechoka.

Sasa Msimamizi Mkuu ana mpinzani mkubwa anayetaka kumtoa hapo kwenye mgodi - yule anayempa kichomi, ili kuhakikisha hawezi kufanya kitu, kuna mijusi imewekwa kuangalia kila kinachofanyika kwake na kwa wapambe wake na kutoa ripoti, japokuwa kuna baadhi ya mijusi ina kazi ya kuhakikisha mgodi unafanya kazi vizuri kwa maslahi ya wote, hivyo hata kama aliaminiwa na kichomi haendi kutoa ripoti kwa Msimamizi Mkuu, mmoja wapo aliwahi kuwa karibu na rafiki wa Msimamizi.

Japokuwa kichomi katulizwa na hawezi kufurukuta kwa kiasi kikubwa, bado anawapa joto, maana hapo alipo hawawezi kumfanya kitu na yeye anatumia upenyo huo kuwachachafya zaidi na kuwakera mpaka wateme bungo wenyewe.

Nashuka sasa baada ya kuachia dukuduku.

Britanicca
 
Tobaaaah sasa km hali ndio hiyo, mbona tumekwisha sisi? Jamaniii kumbe mambo yako hivyooo??
Halafu mbona kuhusu Mwanakwetu hujazungumzia? Au nimesahau kunasa code? Nimetafuta sijaona,
Uwiiiiiii!! 😢😢😭😭
 
Back
Top Bottom