Uchaguzi 2020 Watanzania wenzangu, Membe amekuja na leso ya kupangusa machozi yetu, tusifanye tena makosa tukajilaumu

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,506
51,111
Kwa kweli kama kuna siku nimefarijika ni jana tarehe 16 July 2020. Hii ni siku ya historia kubwa kwetu sisi wazalendo wa nchi yetu ya Tanzania.

Nimefurahi kuona kuwa katika usiku wa giza totoro la ukosefu wa matumaini ya watu wetu, na shimo refu la kuzikia haki za watu wetu kumbe bado Taifa lina watu wapambanaji, watu ambao wako tayari kusacrifice 'comfort zone' zao kwa ajili ya kulinusuru Taifa na watu wake wasiendelee kupotea katika giza hilo au kuangamia katika Shimo hilo.

Ipo haja ya kumpongeza sana na kumshukuru mheshimiwa Membe kwa kusimama kijasiri, na kujitolea kushiriki kikamilifu kwenye kuinusuru nchi yetu na watu wake wasiangamie!

1. Watanzania tusisahau kilio cha vyuma kukaza
Toka mwaka November 2015 utawala huu wa awamu ya tano ulipoingia madarakani, hali za kiuchumi za wananchi zimekuwa ni ngumu sana, Badala ya watawala kusaidia kuondoa hali hii wao waliona njia muafaka ni kupiga marufuku kutumia maneno vyuma kukaza, kwao maneno hayo yaliwakera zaidi kuliko hali halisi ya wananchi mifukoni mwao.

Pamoja na tambo za nchi kuingia kwenye uchumi wa kati, hebu jiulize wewe binafsi, jiangalie wewe binafsi je kipato mfukoni mwako kimeongezeka au haya ni maneno maneno tu? Jiulize, je hali yako mfukoni ni njema kabisakabisa sasa kuliko mwaka 2015? Kama wewe una kumbukumbu nzuri na unajitambua hali yako ilivyo, basi uamuzi ni wako, ama ukubali miaka mingine mitano ya maumivu, au utumie fursa hii tuliyopewa na katiba kufanya mabadiliko ya uongozi nchini.

2. Je, umesahau vilio vya waliobomolewa nyumba zao bila huruma, na wenye huzuni walivyoangaliwa kwa macho makavu?
Je, unakumbuka vunjavunja ya nyumba za watanzania wenzako huko Kimara - Mbezi? Unakumbuka zile picha na video za akina mama, wazee kwa watoto wakiwa pembeni ya mabaki ya mawe, matofali na kokoto vilivyovunjwavunjwa huku wanawake, wazee na watoto wakiwa pembeni ya nyumba zao zilizosagwasagwa na matingatinga, unakumbuka vilio, sononi na nyuso za kukata tamaa.

Wakati hayo yalipofanyika wananchi walikwenda mahakamani kutafuta zuio la mahakama na mahakama ikazuia zoezi hilo lakini bado tu wenye mamlaka ya dola wakaamua hilo zoezi liendelee bila kujali zuio la mahakama, Je wewe mwananchi umesahau haya? Je utawalipa waliofanya haya miaka mitano mingine au utawabadirisha ili watakaoingia waende wakafanye utu kwa wahanga wote waliotendewa yale? Je, una uhakika gani kuwa kama hawa walioko madarakani sasa kama wakipewa miaka mitano mingine hawatorudia tena kufanya kama waliyowatendea wananchi wale kwa wananchi wengine?

3. Wafanyakazi wa umma, je maslahi yenu ya kisheria mko tayari kuyaweka pending tena huku maisha yenu yakiendelea kuwa magumu?
Kama kuna wahanga wakubwa wa utawala huu ni watumishi wa umma. Maslahi yenu yamekuwa si kipaumbele cha utawala huu. Wengi walicheleweshewa kupandishwa madaraja, hawakupewa nyongeza zao zilizoko kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira. Vitendo hivi si tu kwamba vinaathiri kipato cha siku kwa siku cha mfanyakazi, bali vinaathiri hata pensheni zenu za uzeeni, kwa dababu accumulation ya hizi nyongeza ndo zinatunisha hata pensheni. Kwa muktadha huu, kuna lipi linaeeza kumfanya mfanyakazi afikirie tena kuupigia kura utawala huu.

4. Wananchi wa Kagera, mliokutwa na tetemeko, mkaambiwa serikali haitoi chakula kwa kuwa haina shamba
Mimi sijui, lakini kwa wale wananchi wa Kagera waliokutwa na zahama ya kutisha kabisa ya tetemeko kisha mkaambiwa kuwa kwa nini majanga mengi kwenu, ukimwi kwenu, mto ngono uko kwenu, sijajua mnafikiri vipi lakini je, mmesahau kadhia hiyo?

Pale mlipoambiwa Serikali haina Shamba na wala siyo chama cha mapinduzi au serikali vilivyoleta tetemeko, mmesahau haya ndani ya miska hii mitatu minne? Binafsi sijasahau na ndiyo maana naona uchaguzi huu ni uchaguzi wa kufa na kupona, ni uchaguzi baina ya kuweka serikali inayojali majanga na madhila ya wananchi au serikali inayoona majanga ya wananchi ni mambo ya wananchi wao wenyewe "watajiju"

5. Wakulima wa Korosho machozi ya kilio chenu bado mabichi sana, makovu yenu bado yana vuja
Watanzania hawawezi kusahamu miliyopitia, Jasho lenu lingali bado halijakauka, sidhani kama mnaweza kupumbazwa na propaganda za ujenzi wa flyover, Stieglers au reli wakati kile ambacho mmekitolea jasho nyie wenyewe kikichukuliwa kwa nguvu huku malipo yenu yakiwa hayajulikani hatma yake.

Korosho ndiyo uhai wenu, ndiyo elimu ya watoto wenu, dawa zenu, ndiyo suruali, kanga, kitenge n. k. Sasa uamuzi ni wenu kwenye uchaguzi mkuu wa October, mchague serikali ileile iliyowafanyia yale, Au mfanye mabadiriko mlete serikali itakayojali jasho lenu, Serikali itakayowasaidia kilimo chenu kukua na kuwaongezea kipato zaidi, kuliko ile inayoona vyaelea basi yenyewe yataka ichukue tu bila kuinvest vya kutosha!

5. Vijana mliomaliza vyuo, shule za sekondari mustakbali wa ajira zenu ukoje?
Sasa hivi hali ya serikali kuajiri imekuwa ni kwa manati, tangu 2015 rekodi ya serikali hii kuajiri imekuwa butu mno, hata hivyo watendaji wa serikali hii hii wanaoishi kwa kodi zetu, wamesikika wakisema kuwa mdingoje kuajiriwa, bali mjiajiri. Je wewe kihana umewahi kuwauliza wao, kwa nini walikimbilia siasa badala ya kujiajiri? Je, utajiajiri vipi, katika kilimo kipi, viwanda vipi, collateral gani utakayoweka benki ili upate mkopo wakati hata sima yako ilikuwa ni. kwa bumu ambalo sasa unadaiwa anyway? Pengine ulikuwa mdogo mika mitano hadi kumi iliyopita. Wakati ule magazeti yalijaa nafasi za ajira, kila ulikuwa ukifunua gazeti unakutana na page kadhaa zenye matangazo ya ajira za serikali na zisizo za serikali, vipi leo hali ikoje?

Sasa uchaguzi wa October ni uamuzi wako, uendelee na serikali hii hii iliyoshindwa kutoa ajira rasmi kwenu, au kupitia sanduku la kura ufanye mabadiriko ya msingi yatakayochochea neema ya ajira katika nchi kwa faida yako na ndugu zako

6. Kwa wale wenye hofu ya deni la Taifa kupaa na kuathiri hatma ya watoto wenu na wajukuu zenu
Ndani ya miaka mitano ya serikaki hii, tumekopa utadhani kesho haipo, deni la nchi hii linazidi kupaa kwa kasi, riba ya mikopo hii si rafiki. wanatueleza kuwa deni ni himilivu na tunaweza kuendelea kukopa. Lakini sasa ewe mwananchi mwenzangu, athari moja ya kukopa ni kuwa lazima ulipe, Tunatumia mipesa mingi kila mwezi kulipa madeni tena na riba juu, na baadhi ya mikopo tunafanyia miradi ambayo sehemu kubwa pesa inarudi nje kupitia kandarasi za kigeni na malighafi kutoka nje bdala ya kupatikana humuhumu ndani. Matokeo yake miradi hiyo tunanufaika kupata ajira za makuli, mama ntilie, mafundi uashi lakini madola mengi yanarudi nje kupitia kampuni hizo.

Cha msingi ni kujiuliza, je baadi ya miradi inachochea uchumi au ni miradi ya show? Je, uwanja wa ndege Chato kwa mfano bila kujali ni pesa za mkopo au la ni mradi wenye kipaumbele. Je, tukiendelea kukopa namna hii, kisha tukawarithisha mzigo watoto wetu nao wakashindwa kulipa halafu rasilimali zetu zikawekwa rehani kulipia deni hilo tutakuwa tumetenda haki gani juu ya kizazi kijacho. Ndiyo masna ipo haja ya kubadiri serikali kupitia uchaguzi mkuu unaokuja, Ndugu zangu tusifanye makosa, this is a time for change, bahati haiji mara mbili.

7. Je, wewe Mtanzania, unaridhika jinsi bunge la utawala wa awamu hii lilivyofanya kazi, unaridhika na katiba hii?
Ewe Mtanzania mwenzangu, sote tuliona jinsi utawala wa awamu hii ulivyokuwa ukiingilia bunge, na bunge likawa kama limeachia mamlaka yake ipokwe na mhimili wa serikali, serikali iliyobypass bunge kufanya manunuzi mbalimbali ya ndege, serikali ambayo imejenga mazingira manunuzi hayo yasikaguliwe na CAG, serikali iliyotufungia bunge live lakini ikatuwekea Rais Live. Katika mazingira haya ewe Mtanzania mwenzangu, uko tayari kuendelea na serikali inayogeuza bunge kama rubber stamp, au unadhani lazima serikali hii ibwagwe kwenye uchaguzi tuweke nyingine itakayoheshimu mihimili mingine?

Sasa hivi, badala ya bunge kuidimamia serikali, serikali imekuwa yenyewe ndo msimamizi wa bunge, katika hali kama hii ndugu zangu tunahitaji mabadiriko makubwa. Lakini kikubwa ni kuwa serikali hii imekataa katakata kutupa katiba mpya, katiba ambayo haiepukiki katika mazingira ya sasa ya vyama vingi, katiba ambayo ni hitajiyo lililomo katika ilani ya chama chake.

Je, ndugu zangu tuendelee na serikali ya aina hii au tuibadirishe?, Binafsi natamani uchaguzi uwe kesho ili nikapige kura yangu ya hasira kali kabisa kuwakataa hawa jamaa.

8. JF tumewahi kufungiwa miezi miwili, magazeti yamefungiwa kila kukicha, Vijana wa mitandaoni wamekula sulubu, Vyombo vya habari sasa hivi ni propaganda tu
Ndugu yangu Mtanzania, katika utawala huu, wengi wakiosema wamekumbwa na zahama, uhuru wa maoni tatizo, vyombo vya habari vilivyokuwa vikiikosoa serikali leo ukienda kwenye mabanda ya wauza magazeti kuangalia gazeti la leo ni kusifiasifia tu, yake yaliyojaribu kuandika tofauti hatima yake mnaijua. Sasa ndugu zangu, katika hali kama hii mnafikiria nini kufanya mabadiriko kwenye uchaguzi unaokuja.

Je, mnataka kuendelea na hali kama hii ya kuleta giza nchini, au mnataka mabadiriko yenye kuleta mwanga. Tukumbuke siyo mbali ni. miaka mitano tu iliyopita, ulikuwa ukienda kununua magazeti kwenye vyombo vya habari unapata magazeti ya aina yoyote unayotaka, yale ya kukosoa, yale ya hoja fikirishi, yale ya udaku, yale ya kusifu. Lakini leo muelekeo ni mmoja zaidi ni. kusifu na kuimba mapambio. Je tunataka miaka mingine mitano ya aina hii?

Ndugu zangu mambo ni mengi sana, nimeorodhesha machache tu hata hivyo tunalo tumaini, Tunaye ndugu Bernad Membe, Mtu ambaye amesimamia hoja zetu zote hizi akiwa ndani ya CCM.

Hskutishika wala kuogopa, na kwa ujasiri mkubwa aliamua potelea mbali, Taifa langu kwanza mengine baadae. Membe kazungumzia utawala wa haki, utawala wa sheria, Demokrasia, haki za binadamu, Ajira kwa vijana wetu, Diplomasia makini, na katiba mpya iliyo bora.
Lakini pamoja na hayo, Membe ana huruma, ana moyo wa utu.

Kwa kweli ukinipa uchaguzi baina ya serikali hizi mbili, ile ambayo Membe anajenga picha kichwani mwake kuijenga na hii ya awamu ya tano, ni dhahiri kuwa Membe ana vision kubwa, vision ya maendeleo ya Taifa na ya mtu mmoja mmoja.

Kwa hiyo ndugu zangu, hii ni nafasi adhimu sana ya kujinasua kutoka katika zahama hii ya utawala wa awamu ya tano.

Ndugu zangu, Membe amekuja na leso ya kutufuta machozi yetu, machozi yaliyosababishwa na utawala huu wa awamu ya tano, ni zawadi kubwa iliyoje

Ndugu zangu
Twende na Membe
Membe is a real deal

Hapa Chini, Mheshimiwa Membe anasisitiza umoja wa Wapinzani kwenye kuuondoa utawala uliofeli wa CCM Madarakani.

Ipo haja ya kumpongeza sana na kumshukuru mheshimiwa Membe kwa kusimama kijasiri, na kujitolea kushiriki kikamilifu kwenye kuinusuru nchi yetu na watu wake wasiangamie!
Niyawekee mkazo haya maneno uliyoandika hapa:
"...kumshukuru mheshimiwa Membe kwa kusimama kijasiri, na kujitolea kushiriki kikamilifu kwenye kuinusuru nchi yetu na watu wake wasiangamie"
Ni maneno mazito, ila hukuyapa maelezo na mkazo ni jinsi gani 'atajitolea', na atakavyosimama kijasiri.

Kutokana na aliyoyasema wakati anakaribishwa, sikuona na kusikia maneno yaliyoashiria wewe kufikia hitimisho ulilofikia.

Naomba nisieleweke kuwa napinga ujio wa Membe kwenye upinzani. Ninachosema hapa ni kuwa nadhani hapajawa na msisimko wa kufikia huko ulikofikia wewe haraka haraka kiasi hiki.

Tumpe muda, na tuone atakavyoshirikiana na wenzie kuleta mabadiliko tunayoyataka sote.

Niseme tu wazi, nami nina mategemeo kwamba ataleta mchango wa kutosha katika kuwatikisa waliojifanya wana hati miliki ya uongozi ndani ya nchi hii.

Nimeisoma orodha ya 1 hadi 8.

Ni ajenda nzuri ya kuwakumbushia wananchi wakati huu, ila nadhani inakosa ile "punch" ya kumtikisa mhusika, na kuwafanya wananchi wajione walivyowekwa mateka.

Kuna umhimu wa kuwaambia wananchi, bila vifichoficho, kwa lugha rahisi wanayoielewa na kwa mifano hai wanayoitambua, mambo yasiyofaa yaliyofanyika, na kutoa tahadhari ya hali hiyo mbaya kwenda mbele.

Ngoja nikupe mfano: Chaguzi za viongozi wao. Wananchi wanaponyimwa haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka wawaongoze kwa mizengwe mbalimbali, rejea serikali za mitaa hawa wananchi watashindwa vipi kuona utawala wa hira unaowanyima haki?

Watawala hawataki pawe na tume huru ya uchaguzi, kwa nini wananchi wasione moja kwa moja tatizo kwenye hizi chaguzi.

Kwa hiyo, orodha yako ni nzuri ya kuanzia, hasa kwa wapinzani kuitengeneza iwe rahisi kuipeleka kwa wananchi, lakini orodha hii imechukua mambo mepesi mepesi mno. Yapo mazito zaidi ya hayo ambayo yanalazimu wananchi wayakumbuke wakati wanapoingia kwenye chumba cha kupigia kura.

N.B. Nirudi kule juu kwa ndugu Membe
Alizungumzia baadhi ya mambo ambayo bila shaka ndio mwelekeo wa wenyeji wake. Baadhi ya mambo hayo yana matatizo. Nina hakika patakuwepo na nafasi ya kuyazungumzia zaidi huko mbeleni, na huko ndiko tutakaposhiriki mjadala huo.
 
Mbona Umetusahau wengine kamanda?

1. Wauza ngada jinsi tulivyobanwa kiasi kwamba siku hizi biashara imekuwa ngumu, mateja yamepungua saaana mitaani.
Twende na Membe tufufue biashara zetu.

2. Wenye vyeti feki - twende na Membe tuendelee kuitafuna nchi.

3. Wafanyakazi hewa tuna kila sababu ya kumuunga mkono Mh Membe tuendeleze madili. Twende na Membe turudi kwenye yale maisha ya "Unanijua mimi? "
 
Niyawekee mkazo haya maneno uliyoandika hapa:
"...kumshukuru mheshimiwa Membe kwa kusimama kijasiri, na kujitolea kushiriki kikamilifu kwenye kuinusuru nchi yetu na watu wake wasiangamie"
Ni maneno mazito, ila hukuyapa maelezo na mkazo ni jinsi gani 'atajitolea', na atakavyosimama kijasiri...

Hiyo ya kushukuru nimeiona kwa sababu kiukweli kabisa kabisa mtu yeyote yule hata kama ni wewe humu ndani ya JF au kwenye public anayeweza kujivika ujasiri na kuikemea serikali hii iache kuvunja haki za kimsingi za kikatiba za wananchi, kwa mfano haki ya kutoa maoni ambayo watawala hawayapendi, mtu akatetea freedom of speech, mtu anayetetea demokrasia nchini, akakemea matendo ya watu wasiojulikana kwa kweli huyu ni mtu jasiri sana na yapasa kumpongeza na kumshukuru.

Siyo Membe pekee aliyefanya hilo, wapo watu wengi sana waliofanya hayo na kwa kweli katika utawala huu wamehatarisha maisha yao, uhuru wao, biashara zao, kazi zao na future zao kwa ajili ya kusimamia hayo. Si vibaya watu hao kuwashukuru kwa kazi yao njema. isiyo na ubinafsi

Nikimzungumzia Bernad Membe, kwa kweli alisimama kidete ndani ya CCM bila woga, alisema wazi, alitamka kuwa hayo mambo si sawa, na to his credit nasema alikuwa sahihi sana. Kilichomtofautisha Membe na wezie wakati alipokuwa CCM, yeye alisema, wao waliufyata.

Umezungumzia kuhusu jambo ambalo sikulitaja kwenye uzi wangu la jinsi utawala huu ulivyovuruga uchaguzi wa serikali za mitaa, asante sana kwa kulileta katika mada hii, kiukweli Serikali ya awamu hii, imevuruga mengi, nisingeweza kukumbuka au kuorodhesha yote hapa maana ni mengi mengi sana ambayo serikali hii imevurunda.

Hata hivyo namna ulivyolileta inathibitisha kabisakabisa lengo la hii mada kuwa, Serikali ya awamu ya tano imepoka haki nyingi za wananchi ikiwemo haki ya kuchagua viongozi wawatakao, mfano mzuri ni huo ulioleta wa kupoka viongozi wa serikali za mitaa, kwa kuwapandikizia viongozi aa serikali za mitaa wanaowataka wao. Hiyo ni dharau kubwa sana kwa wananchi.

Kuhusu mengine niliyoyaorodhesha kama maslahi ya wafanyakazi, maslahi ya wakulima wa korosho, ajira za vijana, kuvuruga bunge, sidhani kama ni mambo mepesi maana wananchi wanahitaji hiyo demokrasia lakini pia wanahitaji ugali mezani. Lazima uangalie jinsi utawala wa awamu hii ulivyovuruga uchumi wa mtu mmoja mmoja na kupelekea hali yao ngumu sana kiuchumi.

Kwa hiyo mabadiriko ya kuuondoa utawala wa awamu ya tano haukwepeki
 
Membe hawezi kuwa mwarobaini. Huyu ni mwizi tu na hana lolote.

Wapinzani aliowakuta wanatosha. Unampaje nafasi ya kugombea jioni mtu aliyehamia asubuhi? Ni dharau kwa “wapinzani” na ni dalili kwamba hawapo tayari kushika dola. Msiwachukulie poa wapiga kura
 
Membe hawezi kuwa mwarobaini. Wapinzani aliowakuta wanatosha. Unampaje nafasi ya kugombea jioni mtu aliyehamia asubuhi? Ni dharau kwa “wapinzani” na ni dalili kwamba hawapo tayari kushika dola. Msiwachukulie poa wapiga kura

Ni suala la nyakati tu ndugu yangu. Uraisi inapaswa kumpa mtu mwenye uwezo, vigezo, aliyejiandaa kisaikolojia kwa muda mrefu kushika nafasi ile na pia mwenye misimamo sahihi juu uchumi, haki za msingi za watu wetu na utawala wa sheria

Kwenye utawala huu, ni kweli Membe hakuwa mpinzani wa kuvaa gwanda au Zambarau, lakini alikuwa ni mpinzani wa ndani kwa ndani, hiyo ni credit kubwa sana. Wengi ndani ya chama chake waliufyata.

Na ujue sababu za Membe kufukuzwa kwenye chama chake cha zamani, ni kwa sababu alisimamia haki yake ya kikatiba ambayo kimsingi alikuwa pia anatetea haki yako ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa na pia alifukuzwa kwa sababu ya misimamo yake isiyoyumba ya kuutaka utawala huu uheshimu fundamental rights za wananchi. Japo alikuwa CCM, lakini kazi hii ya upinzani wa kweli aliifanya vizuri sana humohumo ndani ya CCM.

Sikatai, kama akiwepo mpinzani mwenye vigezo bora kumzidi Membe na yuko tayari kugombea basi tumpe mpinzani huyo, lakini tusisimamishe mgombea kwa sababu tu ya upinzani wake bila kuwa na vigezo vya ziada.
 
Kwa jinsi wananchi tunavyojitambua kwa sasa, hatuhadaiki na hili pandikizi lenu lililokuja kuuwa upinzani.Huu ni mchezo mwingine wa kutukatisha tamaa wapiga kura ili CCM itawale milele.maana tunajua atarudi CCM baada ya uchaguzi.
 
Safi sana Mkuu. Huyo ni Lowassa Part 2
 
Kwa kweli kama kuna siku nimefarijika ni jana tarehe 16 July 2020. Hii ni siku ya historia kubwa kwetu sisi wazalendo wa nchi yetu ya Tanzania.

Nimefurahi kuona kuwa katika usiku wa giza totoro la ukosefu wa matumaini ya watu wetu, na shimo refu la kuzikia haki za watu wetu kumbe bado Taifa lina watu wapambanaji, watu ambao wako tayari kusacrifice 'comfort zone' zao kwa ajili ya kulinusuru Taifa na watu wake wasiendelee kupotea katika giza hilo au kuangamia katika Shimo hilo.

Ipo haja ya kumpongeza sana na kumshukuru mheshimiwa Membe kwa kusimama kijasiri, na kujitolea kushiriki kikamilifu kwenye kuinusuru nchi yetu na watu wake wasiangamie!

1. Watanzania tusisahau kilio cha vyuma kukaza

Toka mwaka November 2015 utawala huu wa awamu ya tano ulipoingia madarakani, hali za kiuchumi za wananchi zimekuwa ni ngumu sana, Badala ya watawala kusaidia kuondoa hali hii wao waliona njia muafaka ni kupiga marufuku kutumia maneno vyuma kukaza, kwao maneno hayo yaliwakera zaidi kuliko hali halisi ya wananchi mifukoni mwao.

Pamoja na tambo za nchi kuingia kwenye uchumi wa kati, hebu jiulize wewe binafsi, jiangalie wewe binafsi je kipato mfukoni mwako kimeongezeka au haya ni maneno maneno tu? Jiulize, je hali yako mfukoni ni njema kabisakabisa sasa kuliko mwaka 2015? Kama wewe una kumbukumbu nzuri na unajitambua hali yako ilivyo, basi uamuzi ni wako, ama ukubali miaka mingine mitano ya maumivu, au utumie fursa hii tuliyopewa na katiba kufanya mabadiliko ya uongozi nchini.

2. Je, umesahau vilio vya waliobomolewa nyumba zao bila huruma, na wenye huzuni walivyoangaliwa kwa macho makavu?

Je, unakumbuka vunjavunja ya nyumba za watanzania wenzako huko Kimara - Mbezi? Unakumbuka zile picha na video za akina mama, wazee kwa watoto wakiwa pembeni ya mabaki ya mawe, matofali na kokoto vilivyovunjwavunjwa huku wanawake, wazee na watoto wakiwa pembeni ya nyumba zao zilizosagwasagwa na matingatinga, unakumbuka vilio, sononi na nyuso za kukata tamaa.

Wakati hayo yalipofanyika wananchi walikwenda mahakamani kutafuta zuio la mahakama na mahakama ikazuia zoezi hilo lakini bado tu wenye mamlaka ya dola wakaamua hilo zoezi liendelee bila kujali zuio la mahakama, Je wewe mwananchi umesahau haya? Je utawalipa waliofanya haya miaka mitano mingine au utawabadirisha ili watakaoingia waende wakafanye utu kwa wahanga wote waliotendewa yale? Je, una uhakika gani kuwa kama hawa walioko madarakani sasa kama wakipewa miaka mitano mingine hawatorudia tena kufanya kama waliyowatendea wananchi wale kwa wananchi wengine?

3. Wafanyakazi wa umma, je maslahi yenu ya kisheria mko tayari kuyaweka pending tena huku maisha yenu yakiendelea kuwa magumu?

Kama kuna wahanga wakubwa wa utawala huu ni watumishi wa umma. Maslahi yenu yamekuwa si kipaumbele cha utawala huu. Wengi walicheleweshewa kupandishwa madaraja, hawakupewa nyongeza zao zilizoko kwa mujibu wa mikataba yao ya ajira. Vitendo hivi si tu kwamba vinaathiri kipato cha siku kwa siku cha mfanyakazi, bali vinaathiri hata pensheni zenu za uzeeni, kwa dababu accumulation ya hizi nyongeza ndo zinatunisha hata pensheni. Kwa muktadha huu, kuna lipi linaeeza kumfanya mfanyakazi afikirie tena kuupigia kura utawala huu.

4. Wananchi wa Kagera, mliokutwa na tetemeko, mkaambiwa serikali haitoi chakula kwa kuwa haina shamba

Mimi sijui, lakini kwa wale wananchi wa Kagera waliokutwa na zahama ya kutisha kabisa ya tetemeko kisha mkaambiwa kuwa kwa nini majanga mengi kwenu, ukimwi kwenu, mto ngono uko kwenu, sijajua mnafikiri vipi lakini je, mmesahau kadhia hiyo?

Pale mlipoambiwa Serikali haina Shamba na wala siyo chama cha mapinduzi au serikali vilivyoleta tetemeko, mmesahau haya ndani ya miska hii mitatu minne? Binafsi sijasahau na ndiyo maana naona uchaguzi huu ni uchaguzi wa kufa na kupona, ni uchaguzi baina ya kuweka serikali inayojali majanga na madhila ya wananchi au serikali inayoona majanga ya wananchi ni mambo ya wananchi wao wenyewe "watajiju"

5. Wakulima wa Korosho machozi ya kilio chenu bado mabichi sana, makovu yenu bado yana vuja

Watanzania hawawezi kusahamu miliyopitia, Jasho lenu lingali bado halijakauka, sidhani kama mnaweza kupumbazwa na propaganda za ujenzi wa flyover, Stieglers au reli wakati kile ambacho mmekitolea jasho nyie wenyewe kikichukuliwa kwa nguvu huku malipo yenu yakiwa hayajulikani hatma yake.

Korosho ndiyo uhai wenu, ndiyo elimu ya watoto wenu, dawa zenu, ndiyo suruali, kanga, kitenge n. k. Sasa uamuzi ni wenu kwenye uchaguzi mkuu wa October, mchague serikali ileile iliyowafanyia yale, Au mfanye mabadiriko mlete serikali itakayojali jasho lenu, Serikali itakayowasaidia kilimo chenu kukua na kuwaongezea kipato zaidi, kuliko ile inayoona vyaelea basi yenyewe yataka ichukue tu bila kuinvest vya kutosha!

5. Vijana mliomaliza vyuo, shule za sekondari mustakbali wa ajira zenu ukoje?

Sasa hivi hali ya serikali kuajiri imekuwa ni kwa manati, tangu 2015 rekodi ya serikali hii kuajiri imekuwa butu mno, hata hivyo watendaji wa serikali hii hii wanaoishi kwa kodi zetu, wamesikika wakisema kuwa mdingoje kuajiriwa, bali mjiajiri. Je wewe kihana umewahi kuwauliza wao, kwa nini walikimbilia siasa badala ya kujiajiri? Je, utajiajiri vipi, katika kilimo kipi, viwanda vipi, collateral gani utakayoweka benki ili upate mkopo wakati hata sima yako ilikuwa ni. kwa bumu ambalo sasa unadaiwa anyway? Pengine ulikuwa mdogo mika mitano hadi kumi iliyopita. Wakati ule magazeti yalijaa nafasi za ajira, kila ulikuwa ukifunua gazeti unakutana na page kadhaa zenye matangazo ya ajira za serikali na zisizo za serikali, vipi leo hali ikoje?

Sasa uchaguzi wa October ni uamuzi wako, uendelee na serikali hii hii iliyoshindwa kutoa ajira rasmi kwenu, au kupitia sanduku la kura ufanye mabadiriko ya msingi yatakayochochea neema ya ajira katika nchi kwa faida yako na ndugu zako

6. Kwa wale wenye hofu ya deni la Taifa kupaa na kuathiri hatma ya watoto wenu na wajukuu zenu

Ndani ya miaka mitano ya serikaki hii, tumekopa utadhani kesho haipo, deni la nchi hii linazidi kupaa kwa kasi, riba ya mikopo hii si rafiki. wanatueleza kuwa deni ni himilivu na tunaweza kuendelea kukopa. Lakini sasa ewe mwananchi mwenzangu, athari moja ya kukopa ni kuwa lazima ulipe, Tunatumia mipesa mingi kila mwezi kulipa madeni tena na riba juu, na baadhi ya mikopo tunafanyia miradi ambayo sehemu kubwa pesa inarudi nje kupitia kandarasi za kigeni na malighafi kutoka nje bdala ya kupatikana humuhumu ndani. Matokeo yake miradi hiyo tunanufaika kupata ajira za makuli, mama ntilie, mafundi uashi lakini madola mengi yanarudi nje kupitia kampuni hizo.

Cha msingi ni kujiuliza, je baadi ya miradi inachochea uchumi au ni miradi ya show? Je, uwanja wa ndege Chato kwa mfano bila kujali ni pesa za mkopo au la ni mradi wenye kipaumbele. Je, tukiendelea kukopa namna hii, kisha tukawarithisha mzigo watoto wetu nao wakashindwa kulipa halafu rasilimali zetu zikawekwa rehani kulipia deni hilo tutakuwa tumetenda haki gani juu ya kizazi kijacho. Ndiyo masna ipo haja ya kubadiri serikali kupitia uchaguzi mkuu unaokuja, Ndugu zangu tusifanye makosa, this is a time for change, bahati haiji mara mbili.

7. Je, wewe Mtanzania, unaridhika jinsi bunge la utawala wa awamu hii lilivyofanya kazi, unaridhika na katiba hii?

Ewe Mtanzania mwenzangu, sote tuliona jinsi utawala wa awamu hii ulivyokuwa ukiingilia bunge, na bunge likawa kama limeachia mamlaka yake ipokwe na mhimili wa serikali, serikali iliyobypass bunge kufanya manunuzi mbalimbali ya ndege, serikali ambayo imejenga mazingira manunuzi hayo yasikaguliwe na CAG, serikali iliyotufungia bunge live lakini ikatuwekea Rais Live. Katika mazingira haya ewe Mtanzania mwenzangu, uko tayari kuendelea na serikali inayogeuza bunge kama rubber stamp, au unadhani lazima serikali hii ibwagwe kwenye uchaguzi tuweke nyingine itakayoheshimu mihimili mingine? Sasa hivi, badala ya bunge kuidimamia serikali, serikali imekuwa yenyewe ndo msimamizi wa bunge, katika hali kama hii ndugu zangu tunahitaji mabadiriko makubwa. Lakini kikubwa ni kuwa serikali hii imekataa katakata kutupa katiba mpya, katiba ambayo haiepukiki katika mazingira ya sasa ya vyama vingi, katiba ambayo ni hitajiyo lililomo katika ilani ya chama chake.

Je, ndugu zangu tuendelee na serikali ya aina hii au tuibadirishe?, Binafsi natamani uchaguzi uwe kesho ili nikapige kura yangu ya hasira kali kabisa kuwakataa hawa jamaa.

8. JF tumewahi kufungiwa miezi miwili, magazeti yamefungiwa kila kukicha, Vijana wa mitandaoni wamekula sulubu, Vyombo vya habari sasa hivi ni propaganda tu

Ndugu yangu Mtanzania, katika utawala huu, wengi wakiosema wamekumbwa na zahama, uhuru wa maoni tatizo, vyombo vya habari vilivyokuwa vikiikosoa serikali leo ukienda kwenye mabanda ya wauza magazeti kuangalia gazeti la leo ni kusifiasifia tu, yake yaliyojaribu kuandika tofauti hatima yake mnaijua. Sasa ndugu zangu, katika hali kama hii mnafikiria nini kufanya mabadiriko kwenye uchaguzi unaokuja. Je mnataka kuendelea na hali kama hii ya kuleta giza nchini, au mnataka mabadiriko yenye kuleta mwanga. Tukumbuke siyo mbali ni. miaka mitano tu iliyopita, ulikuwa ukienda kununua magazeti kwenye vyombo vya habari unapata magazeti ya aina yoyote unayotaka, yale ya kukosoa, yale ya hoja fikirishi, yale ya udaku, yale ya kusifu. Lakini leo muelekeo ni mmoja zaidi ni. kusifu na kuimba mapambio. Je tunataka miaka mingine mitano ya aina hii?

Ndugu zangu mambo ni mengi sana, nimeorodhesha machache tu hata hivyo tunalo tumaini, Tunaye ndugu Bernad Membe, Mtu ambaye amesimamia hoja zetu zote hizi akiwa ndani ya CCM.
Hskutishika wala kuogopa, na kwa ujasiri mkubwa aliamua potelea mbali, Taifa langu kwanza mengine baadae.
Membe kazungumzia utawala wa haki, utawala wa sheria, Demokrasia, haki za binadamu, Ajira kwa vijana wetu, Diplomasia makini, na katiba mpya iliyo bora.
Lakini pamoja na hayo, Membe ana huruma, ana moyo wa utu.

Kwa kweli ukinipa uchaguzi baina ya serikali hizi mbili, ile ambayo Membe anajenga picha kichwani mwake kuijenga na hii ya awamu ya tano, ni dhahiri kuwa Membe ana vision kubwa, vision ya maendeleo ya Taifa na ya mtu mmoja mmoja.

Kwa hiyo ndugu zangu, hii ni nafasi adhimu sana ya kujinasua kutoka katika zahama hii ya utawala wa awamu ya tano.

Ndugu zangu, Membe amekuja na leso ya kutufuta machozi yetu, machozi yaliyosababishwa na utawala huu wa awamu ya tano, ni zawadi kubwa iliyoje

Ndugu zangu
Twende na Membe
Membe is a real deal

Hapa Chini, Mheshimiwa Membe anasisitiza umoja wa Wapinzani kwenye kuuondoa utawala uliofeli wa CCM Madarakani.

View attachment 1509109
Huna hoja ya msingi.Fanya mjitathimini kwanza na hicho chama chako

Tanzania ni nchi ya kwanza Africa mashariki na ya kumi 10 Africa kuwa na wananchi wenye furaha.kwahiyo bas tumeridhika na utawala wa awamu ya tano na tunaenjoy.
 
Back
Top Bottom