Decentralization in CHADEMA(Muundo wa Majimbo): A Positive Move

Decentralization in CHADEMA(Muundo wa Majimbo): A Positive Move

Kazi nzuri sana na hata kuwekeza wa watu huko ndio kwenye glassroot kuwa sana katika siasa na watu wamekuwa makini sana leo huko chini kuliko mijini hivyo kuna umuhimu mkubwa sana leo kuona CHADEMA wanafanya mambo yote kwa uhakika na uchambuzi wako umetulia
 
Ninafahamu mfumo wa utawala wa China na jinsi unavyolifaidisha taifa hilo,

Tofauti ya USA na China ni ndogo sana,

Mfano USA majimbo yamepewa mamlaka kamili ya kiuchumi na kisiasa, wakati China imetoa nusu mamlaka tu ya kisiasa, na uchumi ni 70% unashikwa na mamlaka mkuu ya Beijing na Hong Kong!

Sisi sera yetu ina apply Uchina na tutaihushia iendane na jiografia ya nchi yetu!

Naelewa kwamba sera yenu ya majimbo itakuwa na percent ya pesa ambayo itatoka jimboni kwenda makao makuu, ingawa hamjaweka wazi suala hilo. Wewe ndo wa kwanza uliotufahamisha kwamba mtachukua percent za kichina china kuzipaste hapa kwetu Tanzania na kutegemea maajabu kama ya China.

Suala ninalozungumzia mimi kuhusu China ni Central Planned Economy ambapo kwenye sera yenu ya majimbo halipo. Sera yenu inahitaji kila jimbo liwe na mamlaka kamili kupanga mipango yake bila kuingiliwa na serikali kuu au jimbo jingine. Hili ndo mimi nalipinga kwani halitaleta maendeleo nchini mwetu bali litasababisha matatizo ya umasikini zaidi.

Kumbuka vilevile kwamba Wachina walipoanza hiyo decentralisation yao tayari walikuwa wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo chini ya mfumo wa Centralised Economy.
 
Kama kuna wahafidhina waliokubuhu hapa duniani kwa sasa basi ni Wachina kwa kutumia mfumo wao wa central planned economy. Angalia jinsi wanavyowagaragaza mataifa makubwa kama Europe, Japan, USA, n.k kwa maendeleo yao ya kasi ya kiuchumi.

Rudini mkajipange mda bado unaruhusu.

Wachina wapi bwana! nani kakudanganya? vingi walivyonavyo ni mitaji ya kutoka nje na wazungu kwa kujua wao ni wengi kisoko wamewekeza kule ili wapate soko. Alafu pesa ile inarudi kwa wazungu... kwa kutoona tu mnajidanganya hapa. Shauri yako!

Narudia kusema kuigawa mikoa ni jambo lile lile la utawala wa kijimbo.
Kwanza tulipopata uhuru tulikuwa na utawala wa Kijimbo ambayo yalibadilishwa na kuitwa mikoa ambayo waliendela kuikata kata vipande ili kujitengenezea vyeo vya kiutawala.
 
Kwa nini unafikiri wazungu wanapeleka mitaji China na kuwawezesha taifa lao kupanda chati kiuchumi mpaka kufikia wababe wa pili duniani baada ya Marekani na wakati wowote watawapita Wamarekani na kuwa kijogoo wa dunia?
 
Ben
Ntarudi hila umekimbia sababu nyingi sana za msingi kama kwanini marekani kuna states ambazo wao wanavote upande mmoja siku zote bila ya kujali maslahi yao, kwanini kunatofauti kubwa ya kimawazo baina ya states na hii ni nchi inayoongoza kwa demokrasia na ufahamu wa mambo. Halafu kuna enough resources to deal with upheaval and leaders who understand their societies wewe unadhani kwanini John McCain aliposhindwa kitu cha kwanza kukisema 'America has spoken my friends we have lost the battle' na kuendelea na speech yake ambayo ilijaa kutuliza hasira zaidi kuliko normal conceding speeches.

Bado ujagusia majimbo yenye usumbufu huko India au huko Russia mpaka leo hii na wanasumbua serikali zao kwa kuwa bado democracy zao pia ni changa vilevile. Unakimbilia mfano wa uswisi na amerika ambapo huko ni strong liberal democratic societies na mambo yanafanyika tofauti sana. Mfano kuna watu wanaweza wa judge marekani kwa sasa kama wadini kutokana na interest zao za uchumi lakini uliza yule pastor aliechoma quran ndani ya america kama walimuacha au ukienda kwa waingereza uliza jamaa wanaojaribu kuleta ubaguzi wa dini kama maandano yanachukua hata nusu saa na aichukui muda wahusika wakuu kutungiwa kesi.

Point hapo ni kwamba usitoe mifano ya liberal democracies these people know how to control their societies scientifically to maintain peace, na nchi kama Tanzania kujiingiza kichwa kichwa katika vitu ambavyo vipo very complicated and can easily sway people allegiences towards division, leo unaona masheikh na mapadri wanavyo ichachafya serikali na hapa ndio mnasema uwanja wa wasomi na bado watu wanabishana kwa kuwatetea hata pasipo staili. Mtaweza kweli ku-control ukanda.

Bado narudi kwenye effective governance maana huko ndiko kwenye mjadala wenyewe ingawa ujaja na point zaidi ya mifano hewa tu ya kuelezea how governance would be like in your ideal federalism kwenye nchi kama yetu na si America or any other liberal democracy we are far from that sio tu kutokana na wananchi hata siasa zetu zenyewe bado hazija fahamiwa na wengi kuhusu namna gani maendeleo yao yanatakiwa kuja, sasa hivi wamechoka lakini the desperate methods are not encouraged by any developed society of any state formation.

Thank you Eric,thank You!

Kwamba ni kwa nini majmbo yana-vote tofauti na kuwepo kwa tofauti kubwa ya kimawazo ni kwamba kuna number of factors.Mojawapo amabyo ni relevant kwenye Discussion yetu ni kuwa kumekua na historia(historical) na urithi wa kiutamaduni(Cultural Heritage0 ambayo yapo influenced sana na historia ya utumwa,historia ya civil rights movement,Civil war e.t.c. Soma George C.Wallace-D's American Independent Party.
kwa mfano majimbo ya South yamekua aligned sana na Democrats kutokana na sera zao na ilani zao za uchaguzi kuegemea kwenye sentiuments na historia ya watu wa south hivyo kuendelea kuwa-shape katika reasoning in all aspects kwa kuwa politics is toxic and contagious.Majimbo ya kusini yalitegemea wafanyakazi watokanao na biashara ya utumwa kwa kuwa njia zao za kiuchumi zilikua ni Cash Crops.Dini pia imechangia hasa madhehebu ya Catholics na Protestants.

Vyama vya siasa vilipoingia Marekani katika muhula wa Kwanza George Washinton alipata sapoti ya North aliposimamia hoja ya Federalists wakati majimbo ya kusini yalisimama nyuma ya Thomas Jefferson na tafsiri yake ya 10th Amendment.Tofauti iliyokuwepo ya kimsimao katika masuala ya tax,tariffs,civil rights movement na slavery ilipelekea seccesion movement kama niliyoandika katika post zilizotangulia na kusababisha Civil war katika utawala wa Abraham Lincoln.Majimbo ya kusini yalifanya Jaribio hatari la kuunda confederate states of America na mji mkuu kuwa Richmond ingawa majeshi ya union yalishinda dhidi ya confederate Army lakini tunashuhudia walivyojifunza in hard way na mataifa mengine yalijifunza hata nigeria kwenye BIAFRA War.Ku Klax klan na falsafa zake zimeendelea kubaki kuwa learning curve kwenye theories of federation,decentralization and unitary systems.Hata hivyo tofauti ya voting bado imeendelea kuwa shaped kwani Republicans wameweza kuchukua baadhi ya majimbo ya South Kama New England na dems wamechukua Maine na Vermont.DIfferent opinions na deviation inatokana na history.Kwa mfano kuna yale majimbo amabyao ni swing states ambayo hayana uamuzi wa moja kwa moja.Hayo pia yameathiriwa na historia hasa hali ya kisiasa,kiuchumi na demographics.Kuna suala la uhamiaji ambalo huwa linategemea upoepo tofauti na baadhi ya factors ambazo partially ziko fixed kama spanish wanajulikana wako sympathetic na upande mmoja.Majimbo ya kusini yamekua na war veterans(McCain ni war veteran:Refer vietnam War).Katika marais 12 wa kwanza na wakuu wa majeshi Marekani walitokea south.Kwa hiyo kuna factors nyingi ambazo ni traditiona zinaleta influence

Huko india unataka nizungumzie jimbo lipi Eric? unataka nizungumzie jimbo la Jammu na Kashmir?Nagaland?Haya ni masuala ambayo yanaweza kujadiliwa kwenye mjadala mwingine hasa tutakapojadiliana kuhusu Insurgency,terrorism and counter-terrorism.Haya yote yapo kwenye subnationalism movement ambazo ni janga la kimataifa lakini kwa kuwa tunaiga demokrasia ya Magharibi basi hatuna budi kujifunza kutokana na historia ya makosa ya Mababa wa demokrasia tunaowaiga.India baada ya kupata uhuru wanasiasa walijiingiza kwenye mchezo wa power grabbing.uamuzi uliochukuliwa kuhusu Kashmiri na pia wanasiasa kufuata ntend ya lingustic ilikua kupalilia sub-nationalism.Kwa mfano kulikua na ant-hindi kule kwa watu wa Tamil Nadu.Hebu soma historia ya assasination of Indira Gandhi (Pamoja na kwamba kuna mwanasiasa kilaza aliandika hapa juzi kwenye makala na kuupotosha umma kwa maslahi yake) halafu historia ya kifo cha Rajiv Gandhi baada ya kupeleka Jeshi la India kupambana na waasi wa tamil Tigers kule Sri Lanka.Actuaally hapa kuna mambo mengi ambayo tunatakiwa kujifunza kutoka kwa wenzetu kabla hatujasubiria kujifunza kutokana na makosa yetu.Jenerali Ulimwengu juzi aliandika 'kujifunza kutokana na makosa yetu gharama yake ni kubwa mno'.Tusikubali sasa mfumo huu tulio nao utufundishe kulingana na makosa yetu.Suala la Kashmir kuna religious hegemony ambalo ndilo lililosababisha Taifa la Pakistani kuundwa.Haya tunaweza kuyakwepa kwa kujifunza na kuna post yangu hapo juu niliongelea decentarlization na kujadili jinsi tunavyoweza kuwa na harmony kwa pande zote za bara na visiwani in regardless of muslims in Zanzibar and christians in mainland(Ingawa kote kuna dini zote)

Tafiti nyingi zinaonyesha Taifa kubwa kama la India lingeweza kuwa na kiwango kikubwa cha Rushwa bila kufuata mfumo huu.Ingawa bado India haifuati full federalism lakini mfumo huu umelisaidia Taifa hili la pili duniani kwa Idadi ya watu Bilioni 1 nyuma ya China.Kwa mfano ukitaka kuongelea tatizo la India kwenye Mfumo huu utaongelea upungufu wa nilichosema wa Rushwa kwenye Intelligence system ndiyo maana Maoist wanataka kujitenga na kuunda Taifa lao lenye mrengo wa China au Nepali.Wanasiasa wanatumia udhaifu wa mfumo huu kuchochea Movement kwa majimbo kama Jharkhand,Orissa,West bengal,Andhya Pradesh,Mandhya Pradesh,Utter Pradesh East na Bihar.majimbo haya mawili ya mwisho ndiyo maskini zaidi india.Na hata hivyo suala la umaskini wao lingeonekana kuwa mbaya zaidi kama kusingekua na mfumo huu.Pia ni jambo la hatari na linatakiwa kuwa adressed immediately kwa kuwa ni rare case kutokea kwa movement ambayo ina sapoti ya local people kuwa defeated.hili linaumiza vichwa magwiji wa subnationalisms.Hapa tunajifunza,CHADEMA ni chama cha utafiti na kinatumia wataalamu kufanya uamuzi.hayo yote hapo juu yanaeleweka na tumejipanga.Huu ndiyo msingi wa kuhimiza mafunzo na pia ku-encourage vijana,na wanasiasa wetu kuendelea kusoma vitabu kuufahamu mfumo huu ambao ni bora kulinganisha na mfumo tulionao.Tuna mfumo usiokua na kanuni na wala muongozo wa kushughulikia sub-nationalism.Hautoi taswira ya demokrasia zaidi ya taswira ya mabavu na ukoloni usiokua na chembe ya ustaarabu..mfumo tulio nao pamoja na mabavu na vitisho unapanda mbegu za sub-nationalism movement kwa kasi hasa pale ambapo raia wake wanapoelimika.UAMSHO ni mfano mmoja tu.

Switzerland nimetoa mfano kwa kuwa ni taifa lenye makabila,sura ya utaifa tofauti.ndani ya Taifa la Uswis kuna Ujerumani,Ufaransa,Italia,uingereza n.k. Cantonments zimekua na nguvu na kuhudumia raia wake kutokana na ubora wa katiba yao pamoja na kuwa na diversity kubwa.Ingependeza kama vyama vya siasa vingetoa elimu ya uraia kwa karibu kama CHADEMA kinavyofanya ili kutengeneza awareness.Tumeiga demokrasia huko,tutaiga yale mazuri na kujifunza kutokana na makosa.kuna uwezekano Tanzania chini ya CHADEMA ikawa The Giant nation in Africa in regardless kwamba wengine wameshindwa
 
Hata Mwl Nyerere hili suala la utawala wa majimbo alilizungumzia pale alipotamka "The government is putting touches to a wide ranging decentralization process aimed at transfering decision making from Dar to the regions as much as possible". The Standard News Paper on Saturday December 11, 1971.
 
Acha porojo za Nyerere. Tumeanika mezani madhara ya utawala wa majimbo kwa nia njema. Tuyajadili hayo. Mpaka Nyerere anamaliza mda wake ilikuwa ni ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI NA MTUKUFU RAIS. Maneno yake yalikuwa hayaendani na vitendo vyake. Ndo maana leo tupo hapa kama taifa linalotafuta njia ya kutokea baada ya viongozi wote tangu tupate uhuru hadi leo kushindwa ku deliver.
 
Ben

Kwanza asante kwa majibu, pili naona kama vile unajipiga risasi ya mguu mwenyewe na kuanza kuchechemea kabla hata hiyo marathon yenyewe aijaanza na hoja yako. Majibu unayotoa yanatosheleza au yanakubali maswali yangu ya awali ya kwamba hivi vitu vinataka tafiti na kuangaliwa kwa kina athari zake.

Maana decentralization is one thing na mfumo wa majimbo is another. Suala la kuamua kufanya decentralization (kuboresha mfumo wa kuongoza, ambao hata mimi naamini wa sasa aukizi) na kuchanganya na serikali ya majimbo (kitu nisichokubalina nacho) ni kulipeleka taifa katika uncharted territories katika historia ya jamii yetu chini ya utawala wa serikali kuu.

Ajabu hii sera inachukuliwa very easily especially kwa wale walioianzisha. Mfano mtu anakwambia sisi tutaiga ule wa China, unajiuliza does this guy understand how much forces, intimidation and unshakable loyalties have been pledged by party members to maintain the federal states or the historical wars that took place to get to where they are. Does he understand why China is very strict on monopolistic ruling and controlling information na kwanini upinzani autakiwi kwa namna yeyote hata kwa maandishi wewe; ni lupango. Kwa hivyo jitihada zinazofanywa kuendeleza mfumo wa serikali na central powers clearly kwake ni out of site.

Ukipata hiyo picha unaanza kuona wanapopwaya sanasana kwenye uelewa wa science za akili na mahitaji ya binadamu labda ndio sababu una-conclude hata hawezi ona beyond the necessity of power usage huko China na Russia, unaweza na kumwongezea na ufahamu wake wa siasa pia ni wakaida tu kama nilivyosema huko kwenye mafanikio ya mfumo wa majimbo kikubwa ni wao wamefikia liberal democracies na bado wanachallenges zao (hapo sikuwa nakuzungumzia wewe Ben, bali kihere-here mwengine).

Umezungumzia suala la watu kuwa aligned based on their historical past ambazo zipo influential even today. Wenzako wanaona nikimaanisha wenzako ni anthropologists, philosophers na psychologist; kama vile ni akili ambayo imekuwa shaped by the social environment (based on science evidence) na kumweka mtu awe reasonable in that mannerism. Inataka binadamu awe ameelimika na mwenye wider perspectives hili kuona nje ya hapo. Sasa linganisha elimu ya marekani na wasomi waliojaa kwenye jamii zao na bado unaona kuna watu still are committed to their socialization process course, na hiwapo influence kubwa huko ni dini (to be specif religious morals clashing with liberal thinking with their new laws) na right ya mzungu against others (tukitoa economical factors where swing states applies).

Tutaweza sisi wenye high ignorant society tena kuna influence za udini wa chuki, rangi na makabila chungu mtele (look at this interms of ideologies na si kwa namna nyingine yeyote). Unajuaje athari za mbele huko kwenye jimbo sijui la kanda la ziwa watu wa shinyanga hawato washiana moto na watu wa mwanza kuona almasi inatoka shinyanga why mwanza wafaidike na almasi maana ndio madai ya sasa na hiwapo labda kiongozi ni msukuma.

The point I trying to make bado amna enough tafiti ya hivi vitu vitakavyofanya kazi kwenye jamii ya Tanzania kutokana na watu waishio hapo na mindset zao na sio mifano ya amerika na china; god hata sijaanza decentralization yenyewe kwenye misingi ya federalism ilivyo jitosheleza kuchochea hisia maana huko ndio nilikuwa najipanga like i said unaanza na kujipiga risasi ya mguu we mwenyewe na evidence zako unazoleta.
 
Ni mawazo murua kaka Ben!

Ila kuwa kujenga uelewa wa wananchi kuhusu suala hili la majimbo ni vizuri pia chama kiweze kutoa elimu sahihi katika operashen zake ili CCM wasitumie kupotosha uhalisia wake.
 
Acha porojo za Nyerere. Tumeanika mezani madhara ya utawala wa majimbo kwa nia njema. Tuyajadili hayo. Mpaka Nyerere anamaliza mda wake ilikuwa ni ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI NA MTUKUFU RAIS. Maneno yake yalikuwa hayaendani na vitendo vyake. Ndo maana leo tupo hapa kama taifa linalotafuta njia ya kutokea baada ya viongozi wote tangu tupate uhuru hadi leo kushindwa ku deliver.

duh, unahitaji tiba ya ubongo mkuu!
 
Ben

Kwanza asante kwa majibu, pili naona kama vile unajipiga risasi ya mguu mwenyewe na kuanza kuchechemea kabla hata hiyo marathon yenyewe aijaanza na hoja yako. Majibu unayotoa yanatosheleza au yanakubali maswali yangu ya awali ya kwamba hivi vitu vinataka tafiti na kuangaliwa kwa kina athari zake.

Maana decentralization is one thing na mfumo wa majimbo is another. Suala la kuamua kufanya decentralization (kuboresha mfumo wa kuongoza, ambao hata mimi naamini wa sasa aukizi) na kuchanganya na serikali ya majimbo (kitu nisichokubalina nacho) ni kulipeleka taifa katika uncharted territories katika historia ya jamii yetu chini ya utawala wa serikali kuu.

Ajabu hii sera inachukuliwa very easily especially kwa wale walioianzisha. Mfano mtu anakwambia sisi tutaiga ule wa China, unajiuliza does this guy understand how much forces, intimidation and unshakable loyalties have been pledged by party members to maintain the federal states or the historical wars that took place to get to where they are. Does he understand why China is very strict on monopolistic ruling and controlling information na kwanini upinzani autakiwi kwa namna yeyote hata kwa maandishi wewe; ni lupango. Kwa hivyo jitihada zinazofanywa kuendeleza mfumo wa serikali na central powers clearly kwake ni out of site.

Ukipata hiyo picha unaanza kuona wanapopwaya sanasana kwenye uelewa wa science za akili na mahitaji ya binadamu labda ndio sababu una-conclude hata hawezi ona beyond the necessity of power usage huko China na Russia, unaweza na kumwongezea na ufahamu wake wa siasa pia ni wakaida tu kama nilivyosema huko kwenye mafanikio ya mfumo wa majimbo kikubwa ni wao wamefikia liberal democracies na bado wanachallenges zao (hapo sikuwa nakuzungumzia wewe Ben, bali kihere-here mwengine).

Umezungumzia suala la watu kuwa aligned based on their historical past ambazo zipo influential even today. Wenzako wanaona nikimaanisha wenzako ni anthropologists, philosophers na psychologist; kama vile ni akili ambayo imekuwa shaped by the social environment (based on science evidence) na kumweka mtu awe reasonable in that mannerism. Inataka binadamu awe ameelimika na mwenye wider perspectives hili kuona nje ya hapo. Sasa linganisha elimu ya marekani na wasomi waliojaa kwenye jamii zao na bado unaona kuna watu still are committed to their socialization process course, na hiwapo influence kubwa huko ni dini (to be specif religious morals clashing with liberal thinking with their new laws) na right ya mzungu against others (tukitoa economical factors where swing states applies).

Tutaweza sisi wenye high ignorant society tena kuna influence za udini wa chuki, rangi na makabila chungu mtele (look at this interms of ideologies na si kwa namna nyingine yeyote). Unajuaje athari za mbele huko kwenye jimbo sijui la kanda la ziwa watu wa shinyanga hawato washiana moto na watu wa mwanza kuona almasi inatoka shinyanga why mwanza wafaidike na almasi maana ndio madai ya sasa na hiwapo labda kiongozi ni msukuma.

The point I trying to make bado amna enough tafiti ya hivi vitu vitakavyofanya kazi kwenye jamii ya Tanzania kutokana na watu waishio hapo na mindset zao na sio mifano ya amerika na china; god hata sijaanza decentralization yenyewe kwenye misingi ya federalism ilivyo jitosheleza kuchochea hisia maana huko ndio nilikuwa najipanga like i said unaanza na kujipiga risasi ya mguu we mwenyewe na evidence zako unazoleta.

Shukrani Eric,

Sijipigi Risasi kwa kuwa mojawapo ya misingi ya kuunda muundo mpya ni kuwa honest kwamba why muundo uliopita haufai na ni kwa nini mwingine unafaa pamoja na mapungufu na changamoto zake.Kinacholigharimu Taifa letu ni uongo uongo,wizi wizi na ujanja ujanja wa wanasiasa,wanaharakati na wasomi wetu.Hatutaki kusema ukweli kunapokua na threat kwenye ideas na maslahi yetu.hayo ndiyo yaliyokwamisha na kusababisha matatizo hata kwa mataifa niliyotaja kama India (refer: who is responsible for partition?Kwenye case ya India kati ya Mahatma Gandhi na Mwenzake)

Kuhusu uhusiano uliopo kati ya Decentralization na federalism soma my previous post.it's very clear.

Umeongelea kuhusu Tafiti.Ndiyo maana kwenye Post yangu nilisizitiza juu ya kuendelea kufanya tafiti na ni vizuri kufanya research zaidi kwenye changamoto zinazoyakabili mataifa mengine if trully we are aspiring to be the giant of Africa.Ofcourse nimesizitiza juu ya kuyaweka mambo haya kulingana na mazingira yetu ili tusije tuka-fail miserably kama mipango na sera nyingi za serikali tangu tupate uhuru zilivyoshindwa

Kuhusu ideology hilo ni tatizo kubwa in regardless of the system.tangu tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi hatujawahi kuwa serious kwenye suala la ideology.Serikali ya CCM kipindi hicho haikufanya maandalizi ya kutosha kuhusu mfumo wa vyama vingi na darasa la kiitikadi kwa wananchi wake angalao kwenye general concepts.hapa ndipo CHADEMA inapo-score credits kwa kuanzisha movement ya kutoa elimu ya uraia

Tungekua na darasa zuri la itikadi,wanasiasa wasinge-cross carpet dakika za mwisho za uchaguzi kama wanavyofanya wabunge ambao wanakua kinyume na misimamo ya vyama vyao .Kenya wameweza kudhibiti hili kwenye katiba mpya iliyoidhinisha sera za majimbo na kwamba nominations za vyama vyote zinafanywa siku moja though kwenye agenda ya Ideology bado ni tatizo.Sasa tuna a pertnent question Kuhusu western Democracy:Is it universally benefficial?

Kuhusu huyo aliyetoa hoja ya china:Kumbuka Deng xiping alipoingia madarakani mwaka 1978 baadhi ya structure alizotumia zilifuata geo-political map za mwaka 1238 kwa baadhi ya majimbo.huu ni mjadala mpana sana.

Hapo kwenye influence ya culture na religion kwa hayo mataifa niliyotoa mfano ndipo tunakojifunza na kufanya uamuzi sahihi.

Goodevening Eric!
 
Kwani ni uwepo wa majimbo tu ndio decentralization inaweza ikawa effective?[/QUOTE]

Hii ni mojawapo ya njia za ugatuzi wa madaraka. Ni njia nzuri lakini kwa vinchi vyetu hivi ambavyo ni vichanga bado changamoto ni nyingi zaidi. Unaweza kujikuta unakaribisha migogoro mingi na ukabila ukajipenyeza kwa ari na nguvu mpya.
 
Kumbuka sipingani na decentralization process hili watu waweze kuwa karibu na siasa au maamuzi yanayochukuliwa kwa niaba yao bila ya wao kushirikiswa na kuachwa na umaskini nachopinga ni sera za majimbo na athari zake kwa taifa la Tanzania ya sasa.

By the way ideologies sikuwa specific kwenye maandishi yangu lakini kikubwa hapo hilikuwa ppl perspectives and identification of themselves hapo ndio kwenye utata wa hii sera huko baadae maana watu wameshaanza uchokozi wa utaifa wao sasa hivi kwa njia nyingine sera ya majimbo ni moja ya catalyst itakayowapa encouragement ya kuendeleza uchokozi na kutetemesha stability ya taifa, kitu ambacho kitawapa waporaji mwanya wakutogombanisha kiurahisi zaidi iwape kuna haja ya wao kufanya hivyo.

Enjoy ya weekend.
 
Ndipo hapo binafsi nisipo ona eye to eye with this thinking kwakuwa kuna njia nyingine za kuwaweka watu karibu na siasa zao.
 
Kumbuka sipingani na decentralization process hili watu waweze kuwa karibu na siasa au maamuzi yanayochukuliwa kwa niaba yao bila ya wao kushirikiswa na kuachwa na umaskini nachopinga ni sera za majimbo na athari zake kwa taifa la Tanzania ya sasa.

By the way ideologies sikuwa specific kwenye maandishi yangu lakini kikubwa hapo hilikuwa ppl perspectives and identification of themselves hapo ndio kwenye utata wa hii sera huko baadae maana watu wameshaanza uchokozi wa utaifa wao sasa hivi kwa njia nyingine sera ya majimbo ni moja ya catalyst itakayowapa encouragement ya kuendeleza uchokozi na kutetemesha stability ya taifa, kitu ambacho kitawapa waporaji mwanya wakutogombanisha kiurahisi zaidi iwape kuna haja ya wao kufanya hivyo.

Enjoy ya weekend.

Tuna case study nzuri ya vita ya BIAFRA,American Civil war,Kashmir saga,Partition of Pakistan etc.hizi zote zinatuweka kwenye position nzuri ya kutoa mamlaka na kufanya uamuzi juu ya states na muundo wake.by,the way ni lazima iingie kwenye katiba.Sri Lanka bado inasimama kama mfano mzuri wakati huo huo tunafuatilia kwa karibu provision za katiba mpya ya kenya.Hii ni fate ya taifa itakayochukua miaka mingi na vizazi vijavyo.ni lazima tukae na kuangalia mbali na kujifunza kutoka karne 5 au zsaidi zilizotangulia katika evolution ya mfumo huu kulinganisha na huu mwingine

Enjoy Your weekend too!
 
Mkuu Ben Saanane hapo kwenye wekundu labda unifafanulie zaidi kuhusu hizo case studies na mahusiano yake na siasa za majimbo hasa katika nchi kama Tanzania. Sijui kuna uhusiano gani lakini mimi najua hapo kwenye wekundu kulikuwa na misukumo ya kidini zaidi. Biafra ni wakristo dhidi ya waislamu; Kashmir ni Wahindu dhidi ya Waislamu na nadhani pia sehemu hiyo ya bara hindi kuna mivutano kati ya hizo imani mbili ambazo zinasababisha migogoro hadi nchi kujimega kwa mfano Bangladesh.

Kwa upande wa Kenya nadhani ni mfano ambao pia si sahihi kwa jinsi Tanzania tulivyo; Kenya walishajipambanua kwa Ukabila na wamekuwa katika majimbo ambayo ni ya Kikabila pia. Wanachofanya katika hili suala la ugatuzi wa madaraka (Evolution by devolution) ni kujikita zaidi katika lindi la ukabila.

Suala la majimbo siyo baya lakini inabidi liendewe kwa weledi mkubwa vinginevyo kwa nchi kama yetu hii tutapata shida hasa ya ukabila utakaojikita kwenye kanda.
 
CDM ndiyotu inaweza sana tu. Centralization ni usanii na wizi wa CCM. Let people owm, develop, and take care of what they have for the good of their state. That way they should be able to pay tax to the federal govenment. Make the states accountable for their goods and that is common sense to me. We are failing because of the selfishness of our leaders who want it all for themselves. CDM should lead this country now.
 
Ben, naona unaziruka hizi hoja zangu kuzitolea majibu unajibu hoja za watu wengine zilizokuja baada ya hizi hoja zangu.
Hata hivyo bado nasubiri majibu kutoka kwako wewe mwenyewe mleta hoja na sio mtu mwingine.

By Kisindika Mikoa ni tofauti na majimbo kwa sababu kwenye mfumo wa mikoa bado mipango mikuu inabaki kwenye Serikali kuu. Kushindwa kwa elimu Tanzania kwenye mfumo huu wa mikoa sio kwa sababu ya mfumo bali ni usanii wa viongozi wetu kuanzia awamu ya kwanza mpaka sasa hivi. Ni rahisi zaidi kuharakisha maendeleo ya elimu katika nchi inayoihitaji sana kama Tanzania katika mfumo wa Centralisation of power kama tuliokuwa nao sasa hivi kuliko chini ya mfumo wa majimbo.

Tunaendelea kuhusu faida za decentralization

.

Kwanza kabisa Ben mimi nimegusia suala moja tu la elimu na nikaainisha kwa nini elimu yetu kama taifa haitafanikiwa tukifuata mfumo huu wa majimbo. Badala ya kuanza ku copy na ku paste sera zenu za majimbo kwa ujumla wake kama jibu la hoja yangu ulitakiwa uiadress hoja hiyo in line with sera yenu ya majimbo. Sasa kutuo majibu ya ujumla kwenye suala ambalo ni specific ni dalili ya kushindwa kuliaddress suala lililopo mezani kwako.

Sasa turudi kwenye hoja zako moja baada ya nyingine na majibu yangu yako kwenye Italic:

Sita ,Katika jamii yenye makabila na dini mbali mbali kama ilivyo hapa Tanzania,njia hii huondoa misuguano ya makundi mbali mbali yanayokinzana kimaslahi kama haya tuliyoshuhudia hivi karibuni na badala yake mfumo utaleta hamasa na kudumisha misingi ya undugu,maelewano na kuunda jamii yenye muafaka na hivyo kuchochea maendeleo kwa kasi na kudumisha amani kwani njia ya maridhiano na kutafuta ufumbuzi wa matatizo itafikiwa kwa haraka kabla migogoro haijavuka kiwango cha usuluhishi

Tuchukulie mfano wa jimbo la Kanda ya Kaskazini. Kuna Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Tanga. Embu tueleze hapa kinagaubaga jinsi gani kuunda jimbo hilo la Kaskazini kutaondoa ukabila na udini sio tu Tanzania bali katika kanda yenyewe? Yaani jinsi gani jimbo la Kaskazini litasaidia kuondoa udini na ukabila katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Tanga?

Kumbuka kwamba sasa hivi mnaweza kujiona watu wa Kaskazini ni wamoja kwa sababu ya common interest za kisiasa lakini mgawanyiko utatokea kabla hata jimbo halijaundwa wakati wa kugombea ukuu wa jimbo. Ndipo mtakapogundua hata ndani ya mikoa yenyewe nyinyi si wamoja achilia mbali kati ya mkoa na mkoa ndani ya Kanda hiyo ya mashariki.

Ni wazi kwamba mtaanzisha ukabila na udini ndani ya jimbo na kuigawa nchi vipande vipande badala ya kuunganisha nguvu za Watanzania katika kujiletea maendeleo

Saba,CHADEMA kinatambua ubunifu na kutumia vipaji kama njia ya kujiletea maendeleo.Muundo huu unafungua milango mipana katika kutambua na kutumia vipaji tulivyo navyo na kutumia ubunifu huo katika kukabiliana na changamoto katika mazingira husika na hivyo kuchangia maendeleo ya Taifa letu kwa kushirikisha raslimali watu ambayo isingeweza kutumika au ambayo ilikua imeenguliwa katika mchakato wa kushirikishwa kwenye kutatua matatizo au changamoto zinazotukabili kama Taifa

Kwanza mnatakiwa kuelewa kwamba rasilimali watu hapa Tanzania haipo. Watanzania wengi ni wajinga hivyo hawawezi kuwa rasilimali watu mpaka watayarishwe. Hawawezi kukabiliana na changamoto katika mazingira yao mpaka wapatiwe elimu ya kutosha. Kudhani kwamba CDM ikiingia madarakani basi itakuta rasilimali watu ipo tayari ni kushindwa kujua tatizo la msingi la taifa letu. Hapa ndo suala la kipaumbele gani tunakitaka watanzania kama nchi kinapokuwa issue.

Nane,njia hii huongeza mkusanyo wa raslimali katika ngazi za chini na kuongeza thamani na kiwango cha huduma zinazopatikiana.Pia katika muktadha huu wananchi wanapata fursa ya kutambua aina ya raslimali zilizopo ndani ya jimbo na kuamua kushirikiana katika matumizi kupitia uongozi ulioratibiwa vyema.Wananchi wanapata fursa ya kujitolea zaidi kwa kuwa wana uhusiano wa moja kwa moja na aina ya maendeleo yanyopatikana kupita michango na raslimali walizo nazo

Majimbo yanaongezaje rasilimali? Rasilimali ya msingi (Elimu) ambayo ndio chanzo cha kukuza rasilimali zingine zote haipo in the first place. Kuanzishia majimbo hakutaongeza mkusanyo wa rasilimali katika ngazi yeyote ile achilia mbali ya chini kama unavyoainisha hiyo sera yenu hapo juu.

Vilevile majimbo hayawezi kuwa chanzo cha wananchi kutambua rasilimali walizonazo. Nenda sehemu yeyote ile wananchi watakuambia tuna rasilimali gani hapa hivyo hawaitaji majimbo kujua rasilimali zao. Tatizo ni uongozi mbovu na wa kifisadi uliosimikwa na Serikali ya TANU baadaye CCM ambao ndio unaoitafuna hii nchi. Hakuna guarantee yoyote ile kwamba majimbo yakianzishwa basi utawala hautakuwa wa kimagumashi na kifisadi. Sanasana majimbo yataongeza watu wenye mamlaka ndani ya nchi na hivyo kuongeza uwezekano wa ufisadi kupanuka zaidi kwa kuongeza walaji wenye mamlaka katika majimbo yao.

Tisa,Taifa linakabiliwa na ombwe la uadilifu ambalo pamoja na mambo mengine tatizo la Uadilifu linasababishwa na mfumo wa utawala unaochochea matumizi mabaya ya madaraka,mali za umma na kuminya haki na uhuru wa kweli.Matatizo haya yataondoka pale tutakapofanya mageuzi katika mfumo uliopo na kufuata mfumo hu shirikishi utakaochochea mazingira ya ukweli,uwazi na uwajibikaji ambao utapunguza na kumaliza kabisa tatizo la ukosefu wa maadili katika uongozi ,Miiko ya uongozi itakua wazi na kila mwananchi atakua na uwezo wa kufuatilia kwa karibu kile wafanyacho watawala katika majukumu yao.

Suala la uadilifu nimeshalielezea hapo juu kwamba kuanzisha majimbo hakuna uhusiano na kusimika uadilifu. Sanasana majimbo yanaweza kuongeza mafisadi kwani kwani chanzo kikuu cha ufisadi ni kuwa na mamlaka hivyo viongozi wote wenye mamlaka kwenye majimbo yao wanaweza kuyatumia hayo kutafuta nafasi za kuibia wananchi.

Suala la miiko ni la kinadharia tu lakini utekelezaji wake ni mgumu. Mara nyingi matashi ya kisiasa yanafunika ufuatiliaji wa miiko tuliyojiwekea hasa kwenye nchi masikini kama Tanzania. Kwa mfano wakati wa Nyerere kulikuwa na miiko lakini ilikuwepo kwenye maandishi tu na ilitumika kuwabana mahasidi wake kisiasa. Mashirika mengi yalifilisika wakati wake kutokana na ukumbatiaje wake wa matakwa ya kisiasa zaidi kuliko kufuata miiko. Utendaji wa kiuchumi ulikabidhiwa kwa wanasiasa ambao ndio waliyoyafilisi mashirika yale na wanasiasa hawa watiifu wakawa wanahamishwa kutoka kwenye shirika alilolifilisi kuhamishiwa kwenye shirika lingine ili akafilisi zaidi ili mradi maslahi ya kisiasa ya Nyerere yanafuatwa bila kupingwa.

Tayari kuna kelele kwenye jamii kuhusu maadili ya viongozi wa juu wa CDM hasa kwenye suala la mahusiano ya kimapenzi. Je hii si dalili kwamba maadili hayatafuatwa?

Kumi,Kwa mfumo uliopo Asasi za kiraia zinafanya kazi katika mazingira magumu.Kupitia mfumo huu wa majimbo asasi hizi zitafanya kazi katika mazingira bora na kushiriki kikamilifu katika ngazi ya chini ambako kwa kawaida asasi nyingi zinapata tabu sana kufika huko.Wananchi katika mamlaka ya majimbo wataweza kuwatuma wanaharakati kuwa mlinzi wa maslahi yao na kufuatilia kikamilifu katika Nyanja zote bila kukumbana na vikwazo vya kimfumo

Mazingira ya asasi za kiraia yatakuwa magumu zaidi chini ya mfumo wa majimbo kwani kila jimbo litakuwa na mamlaka ya kuanzisha asasi zake. Asasi hizi zitakuwa na nguvu zaidi katika mfumo wa sasa wa centralisation kwani zina uwezo wa kuajiri watu waliobobea kwenye ngazi ya taifa na zinakuwa na mtandao mkubwa zaidi na hivyo kuwa attract wafadhili wa ndani na nje kuzisaidia katika kufikia majukumu yao. Hivyo majimbo hayawezi kuwa suluhisho la matatizo ya utendaji wa asasi zetu bali yataongeza deficiency kwenye utekelezaji wao.
 
By Kisindika Acha porojo za Nyerere. Tumeanika mezani madhara ya utawala wa majimbo kwa nia njema. Tuyajadili hayo. Mpaka Nyerere anamaliza mda wake ilikuwa ni ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI NA MTUKUFU RAIS. Maneno yake yalikuwa hayaendani na vitendo vyake. Ndo maana leo tupo hapa kama taifa linalotafuta njia ya kutokea baada ya viongozi wote tangu tupate uhuru hadi leo kushindwa ku deliver.

duh, unahitaji tiba ya ubongo mkuu!

Jibu hoja kwa hoja. Huu usanii wa kushindwa kujibu hoja na kukimbilia kutukana ndio uliolifanya taifa letu kufika hapa lilipo. Taifa masikini wa kutupwa. Taifa ombaomba. Taifa la wajinga kama wewe.
 
Back
Top Bottom