Decentralization in CHADEMA(Muundo wa Majimbo): A Positive Move

Decentralization in CHADEMA(Muundo wa Majimbo): A Positive Move

Ben Saanane

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2007
Posts
14,580
Reaction score
18,227
Nimefarijika sana na taarifa za chama changu CHADEMA kufuata muundo wenye sura ya majimbo. Kumbe ndani ya chama changu kulikuwa na watu wenye mawazo kama haya.

Hii ilikuwa kiu yangu ya muda mrefu na hoja hii iliwakuna vijana wengi wakati nagombea uenyekiti wa BAVICHA.

Wachambuzi na wasomi wengi wanakubaliana na hoja hii hata hapa JF tumeona baadhi ya wanachama na wapenzi wa CHADEMA wakihimiza na kushauri sana kuhusu muundo huu. Nimefarijika sana kwakuwa hii ilikuwa mojawapo wa ajenda zangu na niliipa kipaumbele namba 8 kama nilivyotangaza Tarehe 28/04/2011 pale Travertine Hotel nilipotangaza nia yangu ya kugombea nafasi ya kuongoza BAVICHA na nilidhamiria kuunda Baraza lenye muundo huu chini ya kauli Mbiu yangu katika uchaguzi ule ya MOVEMENT FOR RADICAL CHANGE.

Katika ajenda yangu namba 8 niliandika:-
''8. Nitaliongoza baraza kuhakikisha chama kinafika katika kila kona ya nchi yetu kwa kuunda mtandao wenye sura ya mfumo wa majimbo ili kurahisisha ugawanyaji wa raslimali za kuliendesha baraza katika ngazi zote na kulisogeza karibu zaidi na wananchi (Decentralization).

Hili ni vuguvugu la nguvu (Aggressive Movement) lenye lengo la kukabiliana na chama dhalimu (Brutal party) kama CCM chenye fursa za ziada (Added advantages) za kumiliki raslimali za taifa kwa maslahi yake tangu enzi ya mfumo wa chama kimoja, katika kipindi ambacho Chama na Serikali vilikuwa haviwezi kutenganishwa.

Hii ni ajenda nyingine, inahitaji mjadala lakini nitaifanyia kazi.''

Nimefurahi kuona jinsi chama changu kilivyo flexible na kufanya utafiti wa kina. Inawezekana kipindi kile ningeonekana nimekurupuka lakini CHADEMA siku zote wanatanguliza tafiti na kufanya siasa za kisayansi. Hii ni faraja kwangu kwamba hata sisi vijana tunaweza kuwa na mitizamo ambayo ikifanyiwa kazi kwa umakini inaweza kuleta mabadiliko ya kisiasa, kijamii na kiuchumi. Ndiyo maana CHADEMA kimeendelea kuwa kinara kwa kupendwa na vijana wa kada zote.

Naendelea kuamini kuwa hakuna chama kinachoweza kwenda na kasi ya vijana katika mabadiliko tuyatakayo zaidi ya CHADEMA ambako mawazo huru na yenye muelekeo chanya yanafanyiwa Tafiti kwanza na kisha kuwekwa katika matendo.

Muundo huu utakisaidia sana chama chetu.

Robert Oberst aliandika kuhusu muundo huu wa majimbo changamoto na faida zake katika kitabu chake kiitwacho Administrative conflict and decentarlization : The case of Sri Lanka.

Pia Dr. Ugo Mattei aliandika kuhusu hili alipokua akijadili kwa undani utungaji katiba Afrika katika andiko lake
‘Patterns of African Constitution in the Making''.

Sasa kwa kuwa lengo la CHADEMA ni kuishi kulingana na tunayohubiri na kutoa taswira ya serikali yetu ya baadae naendelea kuhimiza wanasiasa vijana ndani ya chama changu kuendelea kusoma vitabu mbalimbali na kuuelewa mfumo huu kwa haraka wakati mafunzo yanaendelea kutolewa na kitengo husika.
Diana Conyers wa Chuo kikuu cha Sussex anaendelea kufanya uchambuzi katika kitabu chake kwa kujiuliza '' Decentralization: The Latest Fashion in Development Administration?

CHADEMA, tuendelee kuweka katika matendo yale tunayohubiri ili kujitofautisha na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachohubiri kuwa ‘Chama cha Mapinduzi' lakini kinoogopa Mabadiliko makubwa ya kimfumo (Radical Reform) na wakati huo huo wakisindikizwa na unafiki wa kueneza itikadi ya Ujamaa huku Rushwa ikishamiri ndani ya chama chao kutokana na kutoka kaktika mfumo wa wa maadili yenye kiwango (deviation from moral standards). CHADEMA tunaendelea kujikita kwenye misingi yetu huku CCM wakiendelea kuondoka katika misingi waliyojiwekea. Ni dalili ya chama kinachoingia kaburini. Miaka miwili kabla ya Uchaguzi UNIP walionyesha dalili hizi kule Zambia, KANU walionyesha Dalili hizi miaka 4 kabla ya Uchaguzi kule Kenya baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 1997, Chama cha Congress nchini India kilionyesha Dalili hizi kuanzia mwaka 1998 kabla ya kuwekwa Kando chama cha Bharhat Janarta Party (BJP) na hivyo kuwapa fursa ya kurudi kwenye misingi yao ndipo kikaweza kurudi madarakani.

Nampongeza Mhe. John Mnyika kwa kubeba ajenda ya Baraza Huru la Vijana na kutumia fursa yake ya kuwa mbunge kupeleka hoja binafsi bungeni. Huu ni mfano wa kuweka mahubiri katika matendo kwani alipokua akiongoza kurugenzi za vijana alipambana sana kuhusu BARAZA huru la vijana. Nilimuunga mkono katika mapambano hayo na ajenda hii niliendelea kuibeba katika kinyang'anyiro cha uchaguzi BAVICHA. Ilikuwa ajenda namba 5.

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-wagombea-hawa-wa-bavicha-chadema-taifa.html

Siku za usoni nitaandika kwa kina kuhusu umuhimu wa muundo huu kulingana na itikadi na falsafa ya CHADEMA ya "Nguvu ya Umma" na pia nitalinganisha na vyama vya siasa na serikali zilizofanikiwa kwa kufuata Muundo huu.
 
Safi sana kamanda, naunga mkono hoja, ni mkweli vijana inabidi kuusoma ili kuelimisha umma, maana maCCM hayakawii kuogopesha Umma, nadhani hii iwe ni kama agenda kuu katika kila mkutano uwe wa ndani ama majukwaani, ili sisi wenyewe vijana tuuelewe.

Mkuu hii kama ilikuwa ni moja ya agenda yako, ni muda wa kutoa ushirikiano kwa uzoefu wako namna ya kuuborresha kisha tusonge mbele.

Una maono, na CDM kwenda na tafiti(sayansi) utasaidia sana,
Binafs nimefarijika pia...hakuna kulala..
 
Kwani ni uwepo wa majimbo tu ndio decentralization inaweza ikawa effective?
Mkuu neno "jimbo" ni jina tu, nadhani admistrative ili iwe effective, inabidi kuwafikia watu wote... Ndio kinachomaanishwa hapa, centrisation kwa bongo imeprove failure, kila kitu kwa sasa mpaka rais o PM, wakuu wa mikoa wamepaki majina tu,

Kwa muundo huu wa majimbo hata rusha na ufisadi utakuwa ni ndoto...
 
Mkuu neno "jimbo" ni jina tu, nadhani admistrative ili iwe effective, inabidi kuwafikia watu wote... Ndio kinachomaanishwa hapa, centrisation kwa bongo imeprove failure.
Kila pahala duniani centralization is a problem hata kwenye big-organisation is a problem. Kunakuwa na matatizo ya communications and diluted interpretation to name a few.

Kwa maana hiyo kwenye taifa kuna umuhimu wa kugawa madaraka na maamuzi na hii aichagui either ni 'federal states' or a 'unitary state' miundo yote ya serikali inazidi kuzipa nguvu local authorities to prepare policies of their own and have a say on government policies.

Swali nililiouliza mimi ni kwanini mpaka kuwe na sera ya majimbo ndio kuwe na effective power distributions. maana kama ni kuzipa nguvu local authorities na kubadilisha mfumo wa uongozi wa mikoa si lazima sera ya majimbo.

Ndio maana nauliza kwanini ni sera ya majimbo iambatanishwe na ugawiwaji wa maamuzi kwenye mikoa? kumbuka sera ya majimbo sio tu kwa sababu ya kupunguza maamuzi ya central government but also has other divisive implications ndio sababu ya kuuliza swali langu.
 
Eric,

Katika Demokrasia ,vyama vya upinzani na hata chama Tawala vina wajibu na dhamana ya kuwaelimisha wananchi kuhusu misingi ya Demokrasia.Kwa bahati mbaya suala hili limekua tofauti nchini mwetu

Ni Chama cha demokrasia na Maendeleo pekee kilichoamua kuvunja utamaduni huu na kuamua kuanzisha mkakati wa kutoa elimu ya Uraia kwa wananchi wake kuanzia OPERESHENI SANGARA hadi sasa tuna vuguvugu la mabadiliko M4C(Movement for Change) nakuanzisha utamaduni mpya(usher in a new culture) unaojenga uwezo na kuongeza ari kwa wananchi katika kushiriki,kushinikiza na kuiwajibisha serikali yao

CHADEMA kinaamini kwamba wananchi wanapoielewa vyema misingi ya demokrasia inakua Rahisi kwao katika kushiriki katika Nyanja zote za utawala.

Katika Dira,Falsafa na Mtazamo wa CHADEMA unalenga kuweka nguvu ya umma au wananchi mbele katika shughuli zote zinazohusu utawala na maamuzi kupitia falsafa yake ya nguvu ya umma ambayo ndiyo msingi wa maamuzi na kichocheo cha mfumo au muundo wa utawala wa majimbo badala ya kulundika mamlaka yote kwa watawala kama ilivyo sasa na hasa sehemu moja bila kuwa na mawasiliano ya karibu ya wananchi.Ni kukasimisha madaraka kutoka makao makuu na kuyapeleka kwenye utawala wa kikanda kupitia mgawanyo huu(decentralization through zoning).Kulundika mamlaka sehemu moja kama ilivyo sasa ni kujiweka mbali na hisia za wananchi na hili limekua tatizo kubwa katika uendeshaji wa nchi na hata katika Mashirika makubwa.

Muundo huu wa majimbo unaoendana na uwezo wetu kiuchumi unatoa Taswira Chanya ya serikali ya Baadae ya itakayoundwa na CHADEMA na sasa CHADEMA kimeamua kwa muda huu ulioaki kiunde mfumo wa aina hii katika kipindi hiki cha mpito kabla ya kuchukua Dola mwaka 2015 ili wananchi wapate kuona ubora wa mfumo huu utakaoleta matumaini mapya,Uhuru na fursa katika kufanya maamauzi bna kushiriki moja kwa moja katika kuendesha Taifa lao kwa ufanisi zaidi
 
Kuna mambo mengi tu mpaka sasa yanafanyika kikanda kwa hiyo hii sera ya majimbo ni muafaka kabisa kwa mfano swala la Afya tuna hospitali za kanda Bugando kanda ya ziwa KCMC kanda ya kaskazini Mbeya kanda ya nyanda za juu kusini ,Muhimbili kanda ya pwani na kati
Kisheria mahakama za rufaa nazo ziko kikanda
Kilimo tunesema the big four nayo ni kanda za nyanda za juu kusini
Viwanda kanda ya pwani ya mashariki
utalii kanda ya kaskazini
Elimu tunaendeleza kanda ya kati
kwa hiyo tunapaswa kuiboresha tuu na kuweka kwenye katiba yetu mpya nchi ni kubwa hii hatuwezi kucentralise maamuzi ya maendeleo hata isipobidi,kuwe na mambo ya serikali kuu na mambo ya serikali za majimbo
 
Nimefarijika sana na taarifa za chama changu CHADEMA kufuata muundo wenye sura ya majimbo. Kumbe ndani ya chama changu kulikuwa na watu wenye mawazo kama haya.

hapo kwenye red - that was uncalled for

Mimi nimeanza kusikia sera ya majimbo muda mrefu zaidi, sasa sijui kama ulikua husikilizi wakuu au vipi

Ilishawahi kurushwa na baadhi ya "wenye nchi" wakasema itawagawa waTZ

to me, hii ni sera ya muda mrefu sema utekelezaji umechelewa
 
Ben Saanane mi nilipoona tu comment yako moja ambayo uli-quote kitabu cha " The 48 Laws of Power" nilifarijika sana. Siku zote naamini kuwa Leaders must be readers. Iwe changamoto pia kwa vijana wengine wanaopenda kuwa viongozi katika siasa vinginevyo tutajikuta tuna wanasiasa uchwara.
Keep it up!!
 
hapo kwenye red - that was uncalled for

Mimi nimeanza kusikia sera ya majimbo muda mrefu zaidi, sasa sijui kama ulikua husikilizi wakuu au vipi

Ilishawahi kurushwa na baadhi ya "wenye nchi" wakasema itawagawa waTZ

to me, hii ni sera ya muda mrefu sema utekelezaji umechelewa

Timing,

Sera ya majimbo ni ya muda Mrefu.Nadhani hukunielewa hizuri hapo ulipo -Bold in red.Katika hoja zangu kipindi cha uchaguzi nilionyesha dhamira ya kuweka sera hizi katika matendo hasa kwa kuanzia kufuata muundo huo ndani ya chma kwa kuunda baraza lenye muundo wa majimbo.
 
Kuna mambo mengi tu mpaka sasa yanafanyika kikanda kwa hiyo hii sera ya majimbo ni muafaka kabisa kwa mfano swala la Afya tuna hospitali za kanda Bugando kanda ya ziwa KCMC kanda ya kaskazini Mbeya kanda ya nyanda za juu kusini ,Muhimbili kanda ya pwani na kati
Kisheria mahakama za rufaa nazo ziko kikanda
Kilimo tunesema the big four nayo ni kanda za nyanda za juu kusini
Viwanda kanda ya pwani ya mashariki
utalii kanda ya kaskazini
Elimu tunaendeleza kanda ya kati
kwa hiyo tunapaswa kuiboresha tuu na kuweka kwenye katiba yetu mpya nchi ni kubwa hii hatuwezi kucentralise maamuzi ya maendeleo hata isipobidi,kuwe na mambo ya serikali kuu na mambo ya serikali za majimbo

Katika Demokrasia ,vyama vya upinzani na hata chama Tawala vina wajibu na dhamana ya kuwaelimisha wananchi kuhusu misingi ya Demokrasia.Kwa bahati mbaya suala hili limekua tofauti nchini mwetu

Ni Chama cha demokrasia na Maendeleo pekee kilichoamua kuvunja utamaduni huu na kuamua kuanzisha mkakati wa kutoa elimu ya Uraia kwa wananchi wake kuanzia OPERESHENI SANGARA hadi sasa tuna vuguvugu la mabadiliko M4C(Movement for Change) nakuanzisha utamaduni mpya(usher in a new culture) unaojenga uwezo na kuongeza ari kwa wananchi katika kushiriki,kushinikiza na kuiwajibisha serikali yao

CHADEMA kinaamini kwamba wananchi wanapoielewa vyema misingi ya demokrasia inakua Rahisi kwao katika kushiriki katika Nyanja zote za utawala.
Katika Dira,Falsafa na Mtazamo wa CHADEMA unalenga kuweka nguvu ya umma au wananchi mbele katika shughuli zote zinazohusu utawala na maamuzi kupitia falsafa yake ya nguvu ya umma ambayo ndiyo msingi wa maamuzi na kichocheo cha mfumo au muundo wa utawala wa majimbo badala ya kulundika mamlaka yote kwa watawala kama ilivyo sasa na hasa sehemu moja bila kuwa na mawasiliano ya karibu ya wananchi.Ni kukasimisha madaraka kutoka makao makuu na kuyapeleka kwenye utawala wa kikanda kupitia mgawanyo huu(decentralization through zoning).Kulundika mamlaka sehemu moja kama ilivyo sasa ni kujiweka mbali na hisia za wananchi na hili limekua tatizo kubwa katika uendeshaji wa nchi na hata katika Mashirika makubwa.
Muundo huu wa majimbo unaoendana na uwezo wetu kiuchumi unatoa Taswira Chanya ya serikali ya Baadae ya itakayoundwa na CHADEMA na sasa CHADEMA kimeamua kwa muda huu ulioaki kiunde mfumo wa aina hii katika kipindi hiki cha mpito kabla ya kuchukua Dola mwaka 2015 ili wananchi wapate kuona ubora wa mfumo huu utakaoleta matumaini mapya,Uhuru na fursa katika kufanya maamauzi bna kushiriki moja kwa moja katika kuendesha Taifa lao kwa ufanisi zaidi

Ni muhimu sasa kueleza faida za muundo huu kwa nchi yetu ili wananchi waelewe pamoja na kwamba kuna mapungufu machache katika mfumo huu ukilinganisha na faida zake nyingi

Kuongeza ufanisi katika matumizi ya fedha na kuondoa urasimu katika kupanga mapato na matumizi na kupeleka maamuzi katika ngazi za chini(fiscal decentralization) hivyo kuongeza kasi ya maendeleo.kumbuka kwa mfumo wa sasa kuna tataizo la kupanga mapato na matumizi kwa hiyo njia hii itaondoa tatizo hili la kulundika majukumu yote makao makuu
Kwa sasa serikali inakusanya mapato nje ya Dar Es Salaam hasa mikoa ya pembezoni (from Periphery) kupitia raslimali zilizopo na kulundika mapato hayo Dar Es Salaam.Sasa kwa mfumo wa majimbo ni kwamba mapato yotokanayo na raslimali yatabaki sehemu husika na mengine kuwa chanzo cha mapato kwa serikali kuu ili kupanga vipaumbele vyake katika kuleta uiano.Kwa mfano sehemu ya mapato ya kanda ya kaskazini au kanda ya ziwa magharibi yanaweza kuingia kwenye mfuko wa makao makuu na kupangiwa matumizi kama vile kutoa ruzuku katika kanda nyingine kama Nyanda za juu kusini n.k

Hoja ya Pili,Muundo huu unawakilisha njia murua ya kukabiliana na tatizo la mlundikano wa madaraka kwa serikali kuu kama tuliyo nayo hivi sasa na ambayo ni kikwazo kikubwa kwa utawala bora kupitia misingi ya uwazi,haki na uwajibikaji.kukasimisha mamlaka kwenye ngazi ya chini itakua kikwazo kwa vikundi vichache vya watu,iwe serikalini au vikundi binafsi vyenye maslahi kujipenyeza katika ngazi za kitaifa na itarahisisha kuwapa fursa katika maamuzi watu wenye mawazo tofauti ndani ya mfumo huu

Tatu,njia hii hurahisisha ushiriki wa wa umma kwa kiwango kikubwa katika utawala na pia wananchi wanapata fursa ya kuwa karibu na uongozi hivyo kujenga uhusiano wa karibu kati ya watawala na watawaliwa(kwa hapa itakua kati ya viongozi na wanaoongozwa).Kwa hiyo njia hii inaileta serikali karibu zaidi na watu na kuufanya umma uelewe mfumo mzima wa kiutawala tofauti na hali ilivyo sasa ambako mtawala hana tofauti na mkoloni na kuwafanya wananchi waonekane wanyapara ndani ya nchi yao.

Nne,Hii ni njia mojawapo ya kutambua ubora na ufanisi wa huduma zinazotolewa na serikali.Mfumo huu shirikishi unasaidia kutambua aina,ubora na kiwango cha huduma wanachohitaji wananchi na gharama ambazo wananchi wapo tayari kugharamia inapobidi na hivyo kurahisha mchakato wa kufanya mamauzi yatakayokuwa na tija kwa watu wote.hii ndiyo hasa Falsafa ya nguvu ya Umma.Mfumo tulio nao ni kwamba maamuzi yanachukuliwa bila kushirikisha wananchi kwa kiwango cha kutosha na hata pale inapohitajika Elimu haiwezi kutolewa kwa ufasaha kutokana na mfumo mbaya wa kuratibu kila kitu makao maku.Wananchi wanaona hiyo ni ajenda ya makao makuu na si ajenda yao.Wanajua serikali ni ‘Huko Dar es Salaam' na hawajioni kama wao ni sehemu ya maamuzi

Tano,Mgawanyo bora na sahihi wa kazi katika menejimenti ya umma huletwa kupitia mfumo huu shirikishi.Uundaji wa utawala bora na imara wa majimbo utasaidia kusimamia masuala yaliyo ndani ya mamlaka husika na pia utatoa fursa kwa serikali kuu(makao makuu) kujikita zaidi katika mambo makubwa na yenye uzito zaidi.Hili linaongeza ufanisi na kuleta ulinzi katika matumizi ya mali za umma (Check and balances in public affairs)....nitaendelea
 
Timing,

Sera ya majimbo ni ya muda Mrefu.Nadhani hukunielewa hizuri hapo ulipo -Bold in red.Katika hoja zangu kipindi cha uchaguzi nilionyesha dhamira ya kuweka sera hizi katika matendo hasa kwa kuanzia kufuata muundo huo ndani ya chma kwa kuunda baraza lenye muundo wa majimbo.

Agree with you... NI ile tu kuweka mambo sawa, wengine wanaweza kuichukulia ndivyo sivyo

Pamoja sana
 
mfumo wa majimbo ni suluhisho la matatizo mengi saana, hasa kwa nchi yetu, wapo wanaoupinga, si vibaya ila watoe hoja za msingi na si kejeli
 
Ben Saanane

Hiii sera ndio umeiweka kuwamaliza kabisa. Tutafutane after mwaka mmoja mkianza kuitekeleza mungu akijalia uniambie.

Naomba nieleweke sipingani na sera yenyewe kama yenyewe bali uwezo wa ku-implement CDM hamna.

Jiulize mahitaji ya sera hii ni yepi hilo moja kwa kuwasaidia...,nijuavyomie ili sera yenu iwe effective kitu cha kwanza nilazima muwe na watu firm ambao wanaweza kuisimamia kwa implicitly hasa ngazi ya chini huko mnaposhusha nguvu za maamuzi. Wapo wapi watu hao?je wapo firm na unauhakika??BAVICHA tu imewashinda watu wamebadilishwa muelekeo itakua nchi nzima????na tena wanakua na mahamuzi ebu fikiria mfano ndio mmoja wa mliowatimua yupo mkoa wenye nguvu kama dar na madaraka ya maamuzi anayo patachimbika..nawambieniCCM wanawafata huko huko kuwamaliza..hamna resources na capabilities za kutosha kuendesha mfumo huu..hauwezi kuweka mfumu huu kwa chhama ambacho hata uwezo wa kifedha bado kinachangisha hata kama mfumo ni mzuri ukafanya kazi.

Thax
 
Raslimali tulizo nazo ni akili,ubunifu na uzalendo wa kutosha wa viongozi na wanachama wetu.Kuchangishana ni njia inayotumika kuleta mageuzi ya Kizalendo.Hata TANU waliitumia kumuondoa mkoloni mweupe.

Hao waliofukuzwa wangekua kwenye muundo huu wasingeshughulikiwa huku juu kwani huko ngazi za chini tayari wangekua easly detected!

Kuhusu suala la CCM kuja huku,ni bora waje ili waturahisishie kazi.
 
Kwa kweli Ben haya maamuzi ya chama yamekuja wakati muafaka.

Sikubahatika kujua kama haya yalikuwa ni moja ya mambo yaliyokuwa kwenye ilani yako.

Huku ndiko kupeleka madaraka kwa wananchi wenyewe.Ushauri wangu kwa chama wahakikishe wanapatikana viongozi imara kwa kila kanda.

Ben umefika wakati sasa na wewe kuwemo ndani ya vikao vya maamuzi ili kusukuma zaidi hoja nzuri kama hizi.Ni imani yangu wakati muafaka ukifika utakuwa miongoni mwa vijana watakaogombea nafasi mbalimbali hasa kuongoza mojawapo wa hizi Kanda ama kuomba nafasi za Baraza Kuu na Kamati kuu.

Mawazo yako ni muhimu sana kwa mustakabali wa Chama.Kila la kheri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom