Decentralization in CHADEMA(Muundo wa Majimbo): A Positive Move

Decentralization in CHADEMA(Muundo wa Majimbo): A Positive Move

By Kisindika Acha porojo za Nyerere. Tumeanika mezani madhara ya utawala wa majimbo kwa nia njema. Tuyajadili hayo. Mpaka Nyerere anamaliza mda wake ilikuwa ni ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI NA MTUKUFU RAIS. Maneno yake yalikuwa hayaendani na vitendo vyake. Ndo maana leo tupo hapa kama taifa linalotafuta njia ya kutokea baada ya viongozi wote tangu tupate uhuru hadi leo kushindwa ku deliver.



Jibu hoja kwa hoja. Huu usanii wa kushindwa kujibu hoja na kukimbilia kutukana ndio uliolifanya taifa letu kufika hapa lilipo. Taifa masikini wa kutupwa. Taifa ombaomba. Taifa la wajinga kama wewe.

akili yako inategea sana, ni dhaifu sawa na kiungo cha uzazi pale kinapoguswa. Ili kumkashfu Mwl Nyerere inahitaji kujiondoa welevu wako na kujivisha uwendawazimu. Ni nani asiyejua mchango wa Mwalimu ktk taifa hili na Afrika kwa ujumla?. Hoja unazotaka ni zipi, nikufundishe kuhusu 'decentralization process'.
 
akili yako inategea sana, ni dhaifu sawa na kiungo cha uzazi pale kinapoguswa. Ili kumkashfu Mwl Nyerere inahitaji kujiondoa welevu wako na kujivisha uwendawazimu. Ni nani asiyejua mchango wa Mwalimu ktk taifa hili na Afrika kwa ujumla?. Hoja unazotaka ni zipi, nikufundishe kuhusu 'decentralization process'.

Unaendeleza umbumbumbu wako. Kama hujui hoja gani ya kujibu basi sina mda wa kubishana na vilaza.
 
Mkuu Ben Saanane hapo kwenye wekundu labda unifafanulie zaidi kuhusu hizo case studies na mahusiano yake na siasa za majimbo hasa katika nchi kama Tanzania. Sijui kuna uhusiano gani lakini mimi najua hapo kwenye wekundu kulikuwa na misukumo ya kidini zaidi. Biafra ni wakristo dhidi ya waislamu; Kashmir ni Wahindu dhidi ya Waislamu na nadhani pia sehemu hiyo ya bara hindi kuna mivutano kati ya hizo imani mbili ambazo zinasababisha migogoro hadi nchi kujimega kwa mfano Bangladesh.

Kwa upande wa Kenya nadhani ni mfano ambao pia si sahihi kwa jinsi Tanzania tulivyo; Kenya walishajipambanua kwa Ukabila na wamekuwa katika majimbo ambayo ni ya Kikabila pia. Wanachofanya katika hili suala la ugatuzi wa madaraka (Evolution by devolution) ni kujikita zaidi katika lindi la ukabila.

Suala la majimbo siyo baya lakini inabidi liendewe kwa weledi mkubwa vinginevyo kwa nchi kama yetu hii tutapata shida hasa ya ukabila utakaojikita kwenye kanda.
Kimbunga,

case ya Biafra ni ya kidini na kikabila lakini ilipaliliwa na mfumo wa utawala.Historia ilianza hata kabla ya uhuru wa Nigeria.Kwenye mapambano ya kudai Uhuru tayari mwanasiasa kijana msomi Abafemi Awolowo(kutoka Yoruba) alishaanza kupambana na Nnamdi Azikiwe(Kutoka Igbo).Kikundi cha Action group cha Awolowo kiliitwa 'Fascist Organistaion'.Baada ya uhuru Azikiwe alijaribu kiutengeneza strong unitary government.Igbo's walitapakaa sehemu nyingi Nigeria.Urais wa azikiwe ulikua kama ceremonial tu.Igbo's walikua wakijisikia haki zao zikiminywa na kuwa marginalised sana.Kulikua na subnationalism spirit ambayo viongozi walishindwa ku-adress mapema na mfumo ambao ulikua ni loose confederation ulikuja kuwa structured baada ya vita ya Biafra.Kosa kubwa lililofanyika ni kufanya dini na lugha(linguisti8c) kuwa kigezo kikuu cha kuunda majimbo.Tanzania tuna makabila zaidi ya 120.Hatuwezi kuunda majimbo na kukuta jimbo moja lina watu wa kabila moja tu.Vita ya Biafra ilionekana Wakristu wanashambuliwa na waislamu north ingawa mtawala wa Kijeshi alikua Mkristu General Ayoub na makamu wake alikua mkristu Abafami Awolowo.Jumuiya ya kimataifa,OAU na mataifa mengine yaliunga mkono Nigeria.Kama kuna kitu kinachukuliwa kama mfano ambao si mzuri sana katika Lecture nyingi kwenye International Relations and diplomacy basi ni kitendo cha mwalimu nyerere na serikali ya Tanzania kuunga mkono na kulitambua taifa la Biafra kinyume na Msimamo wa OAU,Zambia chini ya Kennet Kaunda ilitambua Biafra,hali kdhalika Gabon na Cote D'ivoire pamoja na Red cross na World christian Association.Case ya Red cross pengine inatambulika kutokana na utu kwa kuwa Generali Obasanjo kipindi hicho aliingia katika historia akiwa jeshini kwa kuvunja daraja na miundo mbinu ili vyakula vispelekwe Igbo na kuwaua kwa njaa.Zaidi ya watu millioni moja walikufa ndani ya miezi 30.Sasa unaona ni lazima tuwe na sera ambayo inadidimiza subnationalism spirit na tuzingatie equality kwa wananchi na kila jimbo na serikali kuu iwe kama baba ambaye anarekebisha kwenye mgawanyo wa raslimali na haki sawa kwa wote.Case ya Igbo ni sawa na ya mzozo wa jimbo linalotaka kujitenga la Kashmir

Pakistan na Bangladesh hawa walikua wakitengwa sana na serikali yao.Upande wa mashariki ulitengwa kimaendeleo kutokana na power struggle ya wanasiasa.Kulikua na movement ya kichini chini kama ya Zanzibar na ilianza kichini chini kama movement ya kusini kwa watu ambao wanaona wako marginalised kwenye maendeleo ya nchi hii.historia inaonyesha kwamba ni lazima kuwe na mfumo ambao unatoa mwongozo wa matumizi ya raslimali,haki ya kuongoza na kuwa na sauti.Pamoja na kuwa maeneo mengi ambayo ni marginalised yametoa viongozi wakuu serikalini lakini tatizo linaonekana watu hao hawawezi kuleta changes kutokana na kukosekana na system imara.So suala la Bangladesh lilikolezwa zaidi na external factors.Ukiacha nyufa hizi ni rahisi kwa force kutoka nje kuwaumiza.Soma theories za power of nations and balance of power.India ilikua kwenye rivalry na Pakistan.Vita iliyoongozwa na waziri mkuu wa Mwanamama indira Gandhi dhidi ya Pakistan iliyokua inapewa msaada na China (adui wa India) pamoja na Marekani(Adui mwingine wa India) ilisababisha eneo la mashariki la Pakistani kujitenga na India likawa Taifa la Kwanza kuitambua Bangladesh.Hakuna kovu litakalosahaulika kwa pakistan kama hili.Sera ya utawala ya Pakistani haikuangalia mgawanyo sawa wa Raslimali.Sera za PPP zilikua nzuri lakini zilishindwa kurekebisha muundo9 wa utawala na kufanya kuwe na mgawanyo sawa wa haki kwa maeneo yote bila kujali makabila,itikadi za kidini na Kisiasa

Katiba ya Kenya tunaendelea kuisoma kama itaendelea kuleta ufanisi kwa taifa lililokubuhu kwa ukabila.Kwa mfano katika county zote umeona magavana ndiyo watendaji wakuu.Maseneta wanabeba ajenda za County na kuzijadili kwenye National Level.Mabunge mawili yataleta balance of power.Kwa mfano ukambani umeshuhudia akian Alfred Mutua(msemaji wa serikali ya kenya) akigombea uwakilishi,Charity Ngilu naye akipambana .Kitui,Makueni,Machakosi zinatoa wawakilishi wengi na wenye weledi ambao huko ukambani hawakuwahi kupata uwakilishi kwa namna muundo huo ulivyokua zaidi ya siasa za akina Kalonzo Musyoka na charity ngilu au Mutinda mutiso (Balozi wa kenya hapa nchini).So Makabila yaliyokuwa yanajiskia kuwa marginalised yataweza kuwa na sauti na kujisemea yenyewe kupitia wawakilishi wao ambao wapo karibu na wananchi kulingana na mfumo wa utawala ulivyo.Yale mapungufu machache tutayakwepa kama ncha za sumaku zinazofanana

Kama nilivyosema tunajifunza kutokana na makosa.kule Nigeria bado kuna kazi inafanyika kutokana na aina ya federation iliyopo.Ni lazima kuwe na true federation na si federation ya kimzaha mzaha.Bado vuguvugu la muslim north na south linaendelea.agenda ya zoning inaendelea kwenye suala la urais 2015 kama ilivyo hapa kwetu na Zanzibar.Bado kuna coverty movement inaitwa Movement for the Actualisation of a Sovereign State of Biafra (MASSOB).Ingawa shujaa wa waigbo Jenerali Ojukwu hayupo lakini bado wana ari hadi watakaporidhika.Kwa hiyo solution hapo ni True Federation na sio Loose.Solution hapo siyo kuwagawa wajitenge kama alivyoshauri shujaa wangu Ghaddafi au kama Mwl.nyerere alivyounga mkiono vita ya Biafra.Hawa wote Nyerere na Ghaddafi walikua Pro-PAN AFRICANISM ila sasa waliishangaza dunia kwa kuunga mkono partition
 
Roll the ball first and you will see how hard to keep it in grip.
Watanzania tumezoea kuiga vitu kutoka kwa wengine bila kuangalia mazingira yetu halisi.
Hili suala la majimbo litarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu badala ya kuliendeleza. Nchi zote zinazotolewa mifano ya implementation ya Federalism ni nchi ambazo zilishaendelea wakati zina introduce mifumo hiyo. Zilishaondoa tofauti za kiujima kwenye jamii zao tofauti na sisi watanzania ambao ni taifa masikini kwa ujumla wetu.
Kwa sasa taifa letu linahitaji kipaumbele kimoja tu cha msingi nacho ni elimu. Ku decentralise eneo hili ni hatari sana kwani taifa halina resources za kutosha kutoka kwenye majimbo kuliwezesha kila jimbo ku emplement sera yake ya elimu. Isitoshe, tunahitaji kuwa na mkakati wa kitaifa kwenye hili suala ili kuwe na unity of efficiency katika kusambaza elimu nchi nzima badala ya kuliwacha hili suala kwenye ngazi ya jimbo.

Kisindika,

Asante na sorry kwa kutangulia kujibu hoja za wengine kabla yako.Pole!

Mfumo wa elimu unaweza kuwa decentralized.System inaonekana kuwa na subsystems.Kwenye serikali ambazo zime-adopt federalism zimeachia states authority ya ku-deal na mambo ambayo ni simple lakini yale mambo ambayo ni complex yameachwa kwenye central government.In federal systems, education usually is the legal responsibility of the state governments rather than the national government. Still, even in federal systems, national interests in such matters as equality of opportunity and educational adequacy and excellence inevitably cause the national governments to play a role in education.

Uingereza imetoa mamlaka kwa elected school boards kufanya mamauzi chini ya local governments wakati maamuzi makuu ya kisera yakifanyika london.Marekani nayo ime-adopt mfumo wa kutoa maamuzi katika Elimu kwenye board za shule ,local governments lakini maamuzi makuu ya common curriculum yanafanyika kwenye serikali kuu isipokua sasa kuna debate juu ya testing,Examination and curriculum.So ili kulinda vision na maslahi ya Taifa kwenye elimu kwa kuzingatia ubora,excellence na mengineyo ni bora yanaachwa kwenye level ya juu.Australia walifuata highly centralized education sysytem hadi miaka 1980's lakini wakafanya Reform wakaachia mmalaka kiasi fulani kwenye states
 
Kisindika,

Asante na sorry kwa kutangulia kujibu hoja za wengine kabla yako.Pole!

Mfumo wa elimu unaweza kuwa decentralized.System inaonekana kuwa na subsystems.Kwenye serikali ambazo zime-adopt federalism zimeachia states authority ya ku-deal na mambo ambayo ni simple lakini yale mambo ambayo ni complex yameachwa kwenye central government.In federal systems, education usually is the legal responsibility of the state governments rather than the national government. Still, even in federal systems, national interests in such matters as equality of opportunity and educational adequacy and excellence inevitably cause the national governments to play a role in education.

Uingereza imetoa mamlaka kwa elected school boards kufanya mamauzi chini ya local governments wakati maamuzi makuu ya kisera yakifanyika london.Marekani nayo ime-adopt mfumo wa kutoa maamuzi katika Elimu kwenye board za shule ,local governments lakini maamuzi makuu ya common curriculum yanafanyika kwenye serikali kuu isipokua sasa kuna debate juu ya testing,Examination and curriculum.So ili kulinda vision na maslahi ya Taifa kwenye elimu kwa kuzingatia ubora,excellence na mengineyo ni bora yanaachwa kwenye level ya juu.Australia walifuata highly centralized education sysytem hadi miaka 1980's lakini wakafanya Reform wakaachia mmalaka kiasi fulani kwenye states

Well said kwamba ni bora yakaachwa kwenye level ya juu na sio kwenye majimbo. Kwenye post iliyotangulia iliyoonyeshwa kuwa posted na Mnyika, ilitolea mfano wa hili suala na kusema kwamba elimu haitafanyiwa maamuzi yote Dar es Salaam wakati anahalalisha suala la majimbo in the context of Mtwara case. Ndipo nilipoitilia shaka hii sera ya CDM ya majimbo kwa sababu katika hali hii tuliyonayo ambayo ni sawa na kutokuwa na mfumo wa elimu kabisa, huwezi kukasimu responsibility ya elimu kwenye level ya jimbo.

Lakini kuna issues nimezi raise kwenye kila point ya sera yenu ya majimbo kama nilivyoainisha hapo juu. Nazo zinatia mashaka kama mfumo wa majimbo utatutoa hapa tulipo na kutupeleka kwenye neema.

Nasubiri majibu kwenye hizo points zingine ili tuweze kuona kama sera ya majimbo itatufaa au la.
 
Ben tuanze na kuingalia hii point ya sita ya sera ya majimbo na madukuduku yangu kuhusu hatma ya sera hii kama nilivyopost hapo juu: Madukuduku yako kwenye italic.

Sita ,Katika jamii yenye makabila na dini mbali mbali kama ilivyo hapa Tanzania,njia hii huondoa misuguano ya makundi mbali mbali yanayokinzana kimaslahi kama haya tuliyoshuhudia hivi karibuni na badala yake mfumo utaleta hamasa na kudumisha misingi ya undugu,maelewano na kuunda jamii yenye muafaka na hivyo kuchochea maendeleo kwa kasi na kudumisha amani kwani njia ya maridhiano na kutafuta ufumbuzi wa matatizo itafikiwa kwa haraka kabla migogoro haijavuka kiwango cha usuluhishi

Tuchukulie mfano wa jimbo la Kanda ya Kaskazini. Kuna Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Tanga. Embu tueleze hapa kinagaubaga jinsi gani kuunda jimbo hilo la Kaskazini kutaondoa ukabila na udini sio tu Tanzania bali katika kanda yenyewe? Yaani jinsi gani jimbo la Kaskazini litasaidia kuondoa udini na ukabila katika mikoa ya Kilimanjaro, Manyara, Arusha na Tanga?

Kumbuka kwamba sasa hivi mnaweza kujiona watu wa Kaskazini ni wamoja kwa sababu ya common interest za kisiasa lakini mgawanyiko utatokea kabla hata jimbo halijaundwa wakati wa kugombea ukuu wa jimbo. Ndipo mtakapogundua hata ndani ya mikoa yenyewe nyinyi si wamoja achilia mbali kati ya mkoa na mkoa ndani ya Kanda hiyo ya mashariki.

Ni wazi kwamba mtaanzisha ukabila na udini ndani ya jimbo na kuigawa nchi vipande vipande badala ya kuunganisha nguvu za Watanzania katika kujiletea maendeleo
 
[h=3]kanda 10 za kiutendaji za chadema[/h]


1. Kanda ya ziwa magharibi
mwanza
geita
kagera


2. Kanda ya ziwa mashariki
mara
simiyu
shinyanga


3. Kanda ya ziwa tanganyika
kigoma
tabora
katavi
rukwa


4. Kanda ya kati
singida
dodoma
morogoro


5. Nyanda za juu kusini
mbeya
ruvuma
iringa
njombe


6. Kanda ya kusini
lindi
mtwara


7. Kanda ya mashariki
pwani
dar es salaam


8. Kanda ya kaskazini
kilimanjaro
manyara
arusha
tanga


9. Kanda ya pemba (mikoa yote ya pemba)


10. Kanda ya unguja (mikoa yote ya unguja)
huo ndio muarobaini wa matatizo yetu
 
Back
Top Bottom