Naunga Mkono kufungwa kwa DECI, lakini siungu mkono njia zinazotumiwa at the same timu nawahurumia watakaoliwa DECI, sio kwa ujinga wao, bali kwa umasikini wa Tanzania, unaofanya wawe destitute kwa ahadi yoyote ya fedha kujikwamua na umasikini kama Waisraeli walivyopokea mana toka mbinguni.
Viongozi wa DECI mpaka leo asubuhi, wanahubiri kuhusu secret formular ya kuzalisha 100 % profit in 90 days! na watu waliopoteza matumaini wanaamini bila kujiuliza kwa sababu wako desparate for money, na fedha zinaonekana, wanaopata wamepata, na sasa ndio imefikia zamu ya wanaolia watalia.
E-mail iliyotumwa kwa Mzee Mwanakijiji ni hasira za leo tuu, kufikia uchaguzi mkuu mwakani, hasira hizi zitakuwa zimeshapoa na jinsi Watanzania tulivyo wepesi kusahau, 'nambari wani' itaendelea kutesa na kupeta kwa raha zake huku tukisubiria miaka mitano mingine.
Hebu just imagine wale wana wa Israel walipokwama jangwani na kumlilia Musa aliyefikisha kilio chao kwa Mungu, na mikate ya mana ikashuka toka mbinguni, jee kulikuwa na haja ya Waisraeli hao kujiuliza hiyo mana imetengenezwa kwa unga gani, imeokwaje na kushukaje toka mbinguni ili hali mkate uko mkononi kwenye njaa ya kifo?, hakuna maswali ni kuula tuu huo mkate ulio mkononi. ikija tokea kumbe ule mkate unasumu na waiokula wote watakufa, wakulaumiwa ni nani?. ni Musa aliwasilisha kilio kwa Mungu, ama ni Mungu aliyeshusha mikate, ama labda shetani aliyeimwagia sumu in mid-air?.
Ndivyo hali ilivyo kwa waDESI, walipanda pesa na Mungu akaizalisha mara dufu, wamevunas pesa, wamezishika mkononi, wao watakuwa na maswali tena?. sana sana ni kuongeza mtaji ili kuongeza mavuno ya pesa. Wa kulaumiwa ni wale wote wanaojua ukweli wa mambo, na wakaacha mpaka hali ikafikia hapa tulipo.
Na kwa viongozi ninaowajua mimi, hakuna wa kuwajibika sana sana ni kukamata makuwadi wa DESI, kutia ndani na kuwapa msukosuko lakini the bottom line, watu wameliwa, ila pia ulikuwa ni mchezo wa sadakalawe, mwenye kupata apate na mwenyekukosa akose.
Wale wote waliopata, ndio watapaliza sauti zao juu kwa kilio cha ukombozi wa DESI kwa vile wao walipota na hawaamini kuwa ingefika siku ya kukosa, wakati kwa wenye kukosa, ni kilio cha kusaga meno.
A very story with sad end!. Desi bado ni utata utata mtupu.