Death au DECI? - Masha, Mwema na Othman

Ninavyoelewa serikali haijafungia Deci, waziri mkuu alisema uchunguzi unaendelea.
Ila kwa sababu watu wengi wamepata mashaka na pesa zao na kuamua kwenda kuzitoa Deci, Deci inajikuta haiwezi kuwalipa watu wote pesa zao, ndo maana wamefunga ofisi.

Ponzi scheme!!!!
 
Sijiuzulu NG'O! hata mseme nini.... kwani maneno hata kwenye ukuta utayakuta
nshasema na nimesema.
waliojiunga na DECI walifanya kwa hiari yao na hawakutaka kupoteza muda kuifahamu kiundani hivyo ni budi wamejifunza next time wasijitie hamnazo kukurupukia mambo.
 
Sijiuzulu NG'O! hata mseme nini.... kwani maneno hata kwenye ukuta utayakuta
nshasema na nimesema.
waliojiunga na DECI walifanya kwa hiari yao na hawakutaka kupoteza muda kuifahamu kiundani hivyo ni budi wamejifunza next time wasijitie hamnazo kukurupukia mambo.

Msanii.... we ni nani tena? Maana nashangaa umekataa kujiuzulu... gavana?
 
Msanii.... we ni nani tena? Maana nashangaa umekataa kujiuzulu... gavana?

Mimi ni:-
  • TIS boss
  • IGP polisi
  • Masha
  • Mkullo
  • Ndullu
  • Kitillya
  • Hosea
  • FIS boss
  • n.k
  • Bishop. Mwansota
  • Maaskofu PCT

imetoka hiyo na fedha hairudi kwani imeandikwa aliyenacho atazidishiwa na asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho na kupewa mwingine. Twende na wakati waheshimiwa
 
Naunga Mkono kufungwa kwa DECI, lakini siungu mkono njia zinazotumiwa at the same timu nawahurumia watakaoliwa DECI, sio kwa ujinga wao, bali kwa umasikini wa Tanzania, unaofanya wawe destitute kwa ahadi yoyote ya fedha kujikwamua na umasikini kama Waisraeli walivyopokea mana toka mbinguni.

Viongozi wa DECI mpaka leo asubuhi, wanahubiri kuhusu secret formular ya kuzalisha 100 % profit in 90 days! na watu waliopoteza matumaini wanaamini bila kujiuliza kwa sababu wako desparate for money, na fedha zinaonekana, wanaopata wamepata, na sasa ndio imefikia zamu ya wanaolia watalia.

E-mail iliyotumwa kwa Mzee Mwanakijiji ni hasira za leo tuu, kufikia uchaguzi mkuu mwakani, hasira hizi zitakuwa zimeshapoa na jinsi Watanzania tulivyo wepesi kusahau, 'nambari wani' itaendelea kutesa na kupeta kwa raha zake huku tukisubiria miaka mitano mingine.

Hebu just imagine wale wana wa Israel walipokwama jangwani na kumlilia Musa aliyefikisha kilio chao kwa Mungu, na mikate ya mana ikashuka toka mbinguni, jee kulikuwa na haja ya Waisraeli hao kujiuliza hiyo mana imetengenezwa kwa unga gani, imeokwaje na kushukaje toka mbinguni ili hali mkate uko mkononi kwenye njaa ya kifo?, hakuna maswali ni kuula tuu huo mkate ulio mkononi. ikija tokea kumbe ule mkate unasumu na waiokula wote watakufa, wakulaumiwa ni nani?. ni Musa aliwasilisha kilio kwa Mungu, ama ni Mungu aliyeshusha mikate, ama labda shetani aliyeimwagia sumu in mid-air?.
Ndivyo hali ilivyo kwa waDESI, walipanda pesa na Mungu akaizalisha mara dufu, wamevunas pesa, wamezishika mkononi, wao watakuwa na maswali tena?. sana sana ni kuongeza mtaji ili kuongeza mavuno ya pesa. Wa kulaumiwa ni wale wote wanaojua ukweli wa mambo, na wakaacha mpaka hali ikafikia hapa tulipo.

Na kwa viongozi ninaowajua mimi, hakuna wa kuwajibika sana sana ni kukamata makuwadi wa DESI, kutia ndani na kuwapa msukosuko lakini the bottom line, watu wameliwa, ila pia ulikuwa ni mchezo wa sadakalawe, mwenye kupata apate na mwenyekukosa akose.
Wale wote waliopata, ndio watapaliza sauti zao juu kwa kilio cha ukombozi wa DESI kwa vile wao walipota na hawaamini kuwa ingefika siku ya kukosa, wakati kwa wenye kukosa, ni kilio cha kusaga meno.
A very story with sad end!. Desi bado ni utata utata mtupu.
 
Mimi ni:-
  • TIS boss
  • IGP polisi
  • Masha
  • Mkullo
  • Ndullu
  • Kitillya
  • Hosea
  • FIS boss
  • n.k
  • Bishop. Mwansota
  • Maaskofu PCT

imetoka hiyo na fedha hairudi kwani imeandikwa aliyenacho atazidishiwa na asiye nacho atanyang'anywa hata kile kidogo alichonacho na kupewa mwingine. Twende na wakati waheshimiwa

Sasa mshahara unachukua wa nini kama ndo hivo? Basi tufute BOT, Polisi na makorokoro yote mengine.
 
Sasa mshahara unachukua wa nini kama ndo hivo? Basi tufute BOT, Polisi na makorokoro yote mengine.

Thubutuuu!
Mshahara utaingia kama kawa na kilio chenu ni kama wimbo uburudishao baada ya shibe ya mchana kutwa
Hakifungwi kitu hapa sana sana zitafungwa njia za ninyi kupata majisenti ili msije kulingana na sisi tulio tabaka la jhuu!
 
Kwa mara nyingine uhalifu wa kifedha unafanyika mbele ya vyombo vyetu vya usalama na mkuu wa kijiji huyo anapeperuka kwenda kuomba tena!

Mwanakijiji watajitetea hawa kuwa tuliwaambia kwenye vyombo vya habari kuwa DECI ni upatu. (Wakati wamessema baada ya kuona watu wengi weshajiunga). Siku zote mimi huwa najiuliza the parternal role ya serikali kwa wananchi wake iko wapi?.
 
Nalijua hilo, sikuwa nawatetea.

Ni kweli tunaweza kuwalaumu kuwa wamejiingiza wenyewe lakini tujiulize hao waliopanda DECI ni wangapi wanaofahamu kitu hiki kinachoitwa Ponzi scheme?

Kama ni kweli wamekuja kutaadharishwa baada ya wao kujiunga na DECI kukomaa nani alaumiwe?. Kama mtu ashavuna (kama wanavyosema) mara moja mbili akaiona faida yake na mtu huyo hana elimu ya kujua habari za ponzi sscheme nani alaumiwe?
 
Ni kweli tunaweza kuwalaumu kuwa wamejiingiza wenyewe lakini tujiulize hao waliopanda DECI ni wangapi wanaofahamu kitu hiki kinachoitwa Ponzi scheme?

Kama ni kweli wamekuja kutaadharishwa baada ya wao kujiunga na DECI kukomaa nani alaumiwe?. Kama mtu ashavuna (kama wanavyosema) mara moja mbili akaiona faida yake na mtu huyo hana elimu ya kujua habari za ponzi sscheme nani alaumiwe?
Masha, Mwema, Othman, Dr. Ndulu ndio walaumiwe, kama wenyewe ni watu makini haya mambo yoote yasingetokea. Maana kama walijua ni kitu cha utapeli ni kwa nini waliacha kiendelee? Ni nani aliyetoa vibali? Na Waziri Mkuu anakuja na kutoa kauli bila ya kumuwajibisha mtu yeyote!? Kuna mtu kafanya uzembe somewhere. Lakini kama kawaida yetu hakuna anayechukua lawama.
 
Ni kweli tunaweza kuwalaumu kuwa wamejiingiza wenyewe lakini tujiulize hao waliopanda DECI ni wangapi wanaofahamu kitu hiki kinachoitwa Ponzi scheme?

Kama ni kweli wamekuja kutaadharishwa baada ya wao kujiunga na DECI kukomaa nani alaumiwe?. Kama mtu ashavuna (kama wanavyosema) mara moja mbili akaiona faida yake na mtu huyo hana elimu ya kujua habari za ponzi sscheme nani alaumiwe?

Ndhani tunakubaliana, ni uzembe mkubwa sana kwa upande wa serikali. Wangeufunga siku za mwanzo wangeumia labda watu mia kadhaa, wameacha hadi sasa wataumia malaki kama takwimu za Deci ni za kweli.
 
kwa suala la deci inaonyesha jinsi gani serikali yetu isivyokua makini, suala dogo kama hili usalama wa taifa wameshindwa fahamu au tuseme wamezembea mpaka limekua kubwa namna hii, kweli alisema mkuu wakati akiwachagua mawaziri, uongozi hausomewi ila utajifunza hukohuko ulipopangiwa(bila kufahamu management inasomewa)..tz yetu kwa mwendo huu wa kila kitu ni siasa iko siku itakua ni nchi ya kusadikika kisha tutaendelea kufanya mambo ya kusadikika

Aliposema maneno hayo tu, nikaanza kuhisi ni uongozi gani wa kutegemea kutokana na serikali yake. Tunayoyaona sasa ni matokeo tu ya imani yake kuhusu uongozi.

Haiwezekani na haijawahi kuwezekana kuwa na kiongozi asie na elimu, ujuzi na utaalam wa uongozi kuongoza serikali au hata kujifunzia uongozi kwenye uongozi. Ni lazima awe kwanza na ujuzi, elimu na utashi kabla hajawa kiongozi ili aweze kutathmini, kuelekeza, kupanga na kutawala inavyotakiwa. Uongozi wa umma si lelemama. Ukifanywa lelemama, tutaishia kupoteza maisha, mali na ustaarabu wowote tulionao. Ni sawa na kusema mtu aende tu kuwa Daktari kwa kuwa atajifunzia huko huko. Itakuwa ni kuzalisha balaa na balaa limezaliwa.
 
Mimi nawashangaa hawa wanaojiita wachungaji/ maaskofu ambao wanawadanganya waumini wao kuwa kuna utukufu bila msalaba. Nyie waumini fungukeni masikio. Imeeandikwa kwa jasho utakula

Ni kweli tupu mkuu wangu. Hakuna Pasaka isiyo na Ijumaa Kuu. Hao ni wale wachunaji na maaskofu wanaochambua maandiko nunu nusu. Anatetea na kufafanua kwa nguvu zote nusu sentensi ya Biblia inayomvutia mpaka mate yanamtoka, na ile nusu inayomkera anaitia kapuni, anaikana.
 
Nadhani wengi mnachambua DECI leo, mwanzoni nilitanabaisha ya kwamba huu mchezo ulikuwepo kwa muda sasa. Mara ya kwanza nilipojua nilikuwa nasaka pesa za kujidhami degree ya pili, niliwasiliana na mzazi wangu hapo home nikamwambia naitaji kukopa pahala Million 7 na mimi nichanganye zangu 7 niende graduate school. Mzazi wangu akaniambia kuna pahala mabibo unaweza kuweka 7 ukavuna 7. Nikamuuliza wanawakeza wapi mpaka wakupe hiyo ROI kubwa, akasema BoT. Nikiwa kama mtaalamu wa usimamiza wa fedha nilimwambia kwamba huo ni upatu.

Juzi niliposikia habari, nilichukua kadi nikampigia, na yeye ni victim wa mamilion ya shilling mpaka sasa tunapo ongea.

Siwezi kuwalaumu watanzania wa kawaida sababu Tanzania hakuna enough resource inapokuja swala zima la uwekezaji. USA unaposikia serikali inasema every investor is liable for his/her investments the reason behind ni kwamba muwekezaji ana access ya nyezo zote muhimu. Tofauti na Tanzania, mzazi wangu mimi hajui chochote kuhusu ROI, hajawai kusikia Ponzi Scheme, hana ufahamu wa T-bills or Muni bonds. She just depend kwa serikali kuprovides usalama wake na mali zake.

Nilipoandika wakufunzi kadhaa wa chuo kikuu cha Dar mwanzoni mwa mwaka, nilionyesha concern yangu kuhusu huu mfumo. Nikasema kwamba masikini wengi wataumia mwisho wa siku, kwani mfumo huu umeliza watu wengi sana China.

Ilikuwa imani yangu kwamba usalama wa Taifa watakuwa wameshajua ni njia gani watatumia. Either kufreez asset zote za DECI na kuangalia njia mbadala ya kuzi liquiate ili waweze kuwalipa stakeholders, lakini yalioyotokea ni different. Swala limechukua political face, something which i wasn't expect. BoT walitakiwa kushitaki kwa usalama wa taifa kwamba kuna scheme, then usalama wa Taifa walitakiwa kuingilia kati na kufreeze asset zote. Kisha kuteuwa Czar ambaye ataangalia the investments structure na kudermine walio wekeza watashare vipi loses.

I feel deep sad.... Tanzania a dying angle.
 
.......Ilikuwa imani yangu kwamba usalama wa Taifa watakuwa wameshajua ni njia gani watatumia. Either kufreez asset zote za DECI na kuangalia njia mbadala ya kuzi liquiate ili waweze kuwalipa stakeholders, lakini yalioyotokea ni different. Swala limechukua political face, something which i wasn't expect. BoT walitakiwa kushitaki kwa usalama wa taifa kwamba kuna scheme, then usalama wa Taifa walitakiwa kuingilia kati na kufreeze asset zote. Kisha kuteuwa Czar ambaye ataangalia the investments structure na kudermine walio wekeza watashare vipi loses.

I feel deep sad.... Tanzania a dying angle.

...Baba
Naambiwa kuwa hawa jamaa hata nyumba walizokuwa wanaishi ni za kupanga seuse ofisi zao hakuna hata moja ambayo ni mali zao. Geukia movable properties napo hakuna labda wakafreeze zile kalamu, viti, meza na karatasi wanazotumia.
This is big time scandal.
 
Inapokuja kwenye maswala ya sheria marekani wanashughulikia hivi hizo fraud schemes, sisi taratibu zetu zikoje? Tunazo? Kama hatuna tuzitunge basi!

"PYRAMID SCHEMES"

Law Enforcement Partners

In the U.S., the Federal Trade Commission is just one among many agencies that have the authority to file suit to stop this type of fraud. The Securities and Exchange Commission also pursues these schemes, obtaining injunctions against so-called "financial distribution networks" which in fact sell unregistered "securities."(7) The U.S. Department of Justice, in collaboration with investigative agencies like the FBI and the U.S. Postal Inspection Service, prosecutes pyramid schemes criminally for mail fraud, securities fraud, tax fraud, and money laundering.(8)

State officials independently file cases in state court, often under specific state laws that prohibit pyramids. California defines pyramids as "endless chains" and prohibits them under its laws against illegal lotteries.(9) In a slightly different vein, Illinois classifies pyramid schemes as criminal acts of deception directed against property.(10) Some states like Georgia prohibit pyramid schemes under a statutory framework that regulates business opportunities and multilevel marketing.(11)

At the Commission, we bring cases against pyramid schemes under the FTC Act, which broadly prohibits "unfair or deceptive acts or practices in or affecting commerce."(12) That Act allows the Commission to file suit in federal court and seek a variety of equitable remedies, including injunctive relief, a freeze over the defendants' assets, a receivership over the defendants' business, and redress or restitution for consumers.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom