Death au DECI? - Masha, Mwema na Othman

Ngoja nitawapaka hawa wachungaji wanaochunga matumbo yao!

Ukiwapaka utakuwa huwatendei haki, bali waelimishe kwa umakini kama kawaida yako. Kama wamekosea waoneshe ni wapi lilipo kosa lao, maana haiyumkini mpaka sasa hawajajielewa kama tunavyodhani sie.
 
...Baba
Naambiwa kuwa hawa jamaa hata nyumba walizokuwa wanaishi ni za kupanga seuse ofisi zao hakuna hata moja ambayo ni mali zao. Geukia movable properties napo hakuna labda wakafreeze zile kalamu, viti, meza na karatasi wanazotumia.
This is big time scandal.

Asset walizonazo ni pamoja na paper money. Believe me or not kama wangeweza kushika baadhi ya million walizonazo, then kuwa filisi hao viongozi. At the end of the day watu wange writteoff hata 80% ya Investments zao, lather than now ambapo ni 100% loss sababu serikali haiwezi kurecover even sumni out of that.

Unapoingilia hizi scheme most of time zina collapse mara mmoja tuu so ni jukumu la serikali kuchukua hatua muafaka.... Mimi nina jamaa zangu waalio wai kufanya kazi na kampuni moja inayoitwa Stanford Financial, hawa jamaa walikwenda huko visiwani wakawa wanacheza nao upatu. Lakini mwaka jana SEC walipogundua kwamba kampuni inacheza upatu wali ingilia kati waka freeze assets zote, na kuwaambia wawekezaji wasubiri wakati leagal system inaendelea. Lakini mwisho wa siku wapo watakao recover pesa kiasi.
 
Kinyambiss kwani uko Bongo? Kama uko Bongo basi tafuta muda utembelee vijijini uone namna ambavyo wakulima wamekata tamaa. Bei ya pembejeo kama mbolea iko juu then mlanguzi anatoka mjini na mzani wake unaommwibia mkulima na kununua mazao kwa bei anayoitaka yeye, at the end kulima ni sifuri kwa mkulima.

Mimi sielewi kwa kweli ila serikali yetu ni moja ya serikali zilizoshindwa zaidi duniani, masikini hana chake. Infact wana bahati sana kwamba ni TZ otherwise wangekuwa jamaa zetu wa visiwani kule zamaaaaani tuna rais Disco Joker (DJ) au hata utingo ikibidi.
 
Mbona GAVANA wa benki kuu (BOT) bwana BEN NDULLU umemsahau?

bila kumsahau KITILYA wa TRA ambayo walikuwa wanakusanya kodi huko DECI

Kwakweli watanzania tumekuwa kama walevi fulani wasojua haki zao, lakini bado tupo zaidi ya walevi maana walevi hujua haki zao ndo maana ukimwaga pombe yao hata kama yu hoi utakiona.
Nadhani haya ndo maisha bora. Lakini ni bora tukampa mtu madaraka kulingana na utendaji wake na uwajibikaji wake.
Sisi wapiga kura ndo mafisadi kwa kuwarudisha hawa tunaowafahamu kabisa kuwa sasa ni (Chukua chako mapema) wakiongeza walala hoi hawataamushwa kwa maana ukiamusha tu! unalala wewe.
tuelimishane watanzania hali ni ngumu, na michanga ya macho ya hawa akina BOT,Masha,na wengine imeshajaa machoni.
Tukumbuke" wapiga kura wengi hatujui haki zetu, lipi jema kwetu na kwanini viongozi"
 
hawa watu ni wajanja kuliko hata nyani! wamekula maliasili na hata kudiriki kubomoa majumba na kunyang'anya mashamba yetu eti kuna wafadhili/wawekezaji wanataka kujenga au kuwekeza kitu fulani. lakini unajiukiza mbona mashamba, majumba hata viwanda viliuzwa kwa bei che, eti kwa wawekezaji ambao nyuma yake kuna haohao vigogo. nasi hatujui ni halali yetu au la. Masikini watanzania wasioojulikana katika mifumo ya serikali nasema hatutakuja kufika kokote! labda ufanye jambo fulani (nunua pikipiki kwaa jili ya polisi nawe ufanye biashara yako kwa namna yoyote ile.
Kwa suala la deci tena watu wamevuna serikali ikiwa ya kwanza kujua maana ndo wakitoa leseni. ivi wanataka kusema wako mbali kiasi gani na hao wananchi waliopanda hata wakasubiri ifikie hapo. wao si wanaishi nasi na kama wanajua ni kitu halali si wangesema mapema. NADHANI HUU NI USANII MKUBWA.
 
hawa watu ni wajanja kuliko hata nyani! wamekula maliasili na hata kudiriki kubomoa majumba na kunyang'anya mashamba yetu eti kuna wafadhili/wawekezaji wanataka kujenga au kuwekeza kitu fulani. lakini unajiukiza mbona mashamba, majumba hata viwanda viliuzwa kwa bei che, eti kwa wawekezaji ambao nyuma yake kuna haohao vigogo. nasi hatujui ni halali yetu au la. Masikini watanzania wasioojulikana katika mifumo ya serikali nasema hatutakuja kufika kokote! labda ufanye jambo fulani (nunua pikipiki kwaa jili ya polisi nawe ufanye biashara yako kwa namna yoyote ile.
Kwa suala la deci tena watu wamevuna serikali ikiwa ya kwanza kujua maana ndo wakitoa leseni. ivi wanataka kusema wako mbali kiasi gani na hao wananchi waliopanda hata wakasubiri ifikie hapo. wao si wanaishi nasi na kama wanajua ni kitu halali si wangesema mapema. NADHANI HUU NI USANII MKUBWA. ok tutafika tu.
 
Asset walizonazo ni pamoja na paper money. Believe me or not kama wangeweza kushika baadhi ya million walizonazo, then kuwa filisi hao viongozi. At the end of the day watu wange writteoff hata 80% ya Investments zao, lather than now ambapo ni 100% loss sababu serikali haiwezi kurecover even sumni out of that.

Unapoingilia hizi scheme most of time zina collapse mara mmoja tuu so ni jukumu la serikali kuchukua hatua muafaka.... Mimi nina jamaa zangu waalio wai kufanya kazi na kampuni moja inayoitwa Stanford Financial, hawa jamaa walikwenda huko visiwani wakawa wanacheza nao upatu. Lakini mwaka jana SEC walipogundua kwamba kampuni inacheza upatu wali ingilia kati waka freeze assets zote, na kuwaambia wawekezaji wasubiri wakati leagal system inaendelea. Lakini mwisho wa siku wapo watakao recover pesa kiasi.
The idea sounds good but kwa serikali yetu ninavyoijua, uiachie ndo iwarudishie watu pesa/madai yao itakuwa historia. Kwanza watapata wachache tu ambao watatoa rushwa, pili kuna tatizo la kuwa kuna hata wengine wanaweza kuforge vyeti na kudai kuwa nao wanadai lakini sivyo, so matatizo bado yatakuwepo tu. Nashauri first of all ingewastopisha DECI kuchukua michango mipya, pili watoe order kwamba warudishe pesa za watu ndani ya miezi mitatu. Nadhani hiyo inaweza kupunguza makali ya tatizo.

Thanks
 
Ni kweli tunaweza kuwalaumu kuwa wamejiingiza wenyewe lakini tujiulize hao waliopanda DECI ni wangapi wanaofahamu kitu hiki kinachoitwa Ponzi scheme?

Kama ni kweli wamekuja kutaadharishwa baada ya wao kujiunga na DECI kukomaa nani alaumiwe?. Kama mtu ashavuna (kama wanavyosema) mara moja mbili akaiona faida yake na mtu huyo hana elimu ya kujua habari za ponzi sscheme nani alaumiwe?

Lawama kitu gani? Awajibike mtu. Wallai asipowajibika mtu huu ujinga utaendelea milele.
 
"Mwanakijiji, mimi sikufahamu, lakini nimelazimika kukuandikia ujumbe huu mfupi, maelezo uliyoyaeleza kwenye barua kwenye gazeti la mwana halisi, ulichoeleza ni muhimu watu wajue kuwa ukoloni mambo leo umepitwa na wakati, vitisho vimepitwa na wakati, wakoloni walichokiacha ndicho kinachoendelea mpaka leo.

Maana yake mtanzania hatakuwa huru mpaka pale atakapofunguliwa macho aone, wakati huyu mheshimiwa aitwae kipenzi cha watanzania, kikwete, alisema maisha bora kwa kila mtanzania, lakini hatufichi hakuna kilichofanyika, watanzania wana hali mbaya kuliko kawaida, wamenyanga'nywa mali zao nyumba zao, baada ya kukopeshwa na taasisi za fedha, pride, finca, na zingine za aina hiyo.

Ikainuka Deci, iliyotusaidia sana walala hoi, na sasa unasikia ilivyoendelea kuambiwa ni upatu, sasa mwisho wa mambo haya hatujajua nini kitatokea, ila waambie wazi c.c.m. Mwisho wake ndio huo, imetudanganya inatosha, sasa wananchi wanasema liwalo na liwe, hatuwezi kukubali
kupoteza fedha zetu kijinga, wakati serkali yetu ilitoa leseni, sawa hawakufanya ilivyotakiwa, walikuwa wapi?

Tukisema kuwa serkali ya c.c.m. Imetuibia ni sawa. Nalosema mwakani haiwezi kurudi madarakani. Tumeamua, wanachana lak 7. Na wale walionyuma yetu jumla ni m.3. Kama c.c.m. Inataka mioyo yetu irejee watupe hela zetu, kinyume chake. C.c.m. Kwa heri, haitarudi madarakani tena.

Jambo jipya laja. Waambie, waandikie, wameshindwa kuwabana mafisadi walioiba mabilioni, leo wananyang'anya walala hoi vimtaji vyao walivyowekeza Deci. Ok. Inzi kufia kwenye kidonda ni halali yake, jambo laja, hatutanyamaza, nasema jambo laja. Laja. Laja. Asante, sipendi jina langu litajwe, ila mambo ndio hayo. Damu yamwagika nchini. Oh."

Nyie wajinga hamumtishi mtu.

Ndomaana ujinga wa kupindukia hauishi nchi hii. Mijitu kwa tamaa ya pesa na uvivu inajiingiza kwenye upatu afu ikiliwa inaanza kulia na serikali.

Nasema hapana. Wacha wajinga waliwe ili wajifunze. Na mkawasimulie watoto na wajukuu wenu ili wasirudie huu ujinga nao wakaliwa.

The government cannot protect you from your own recklessness.

Na lolote liwe. Do your worst.

There is no such thing as a free lunch. Habari ndo hiyo. Ebo!
 
Mkuu Kikojozi,
Ningekubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa AFTER serikali ilitangaza tahadhari yake. Lakini kabla ya hapo kulikuwa na tahadhari gani au elimu gani iliyotolewa kwa wananchi wa kawaida kuhusu pyramid schemes.
But your arguments are valid, kwani we have to stop thinking in terms ofa NANNY state. Ndo maana tunasema oh, serikali ifanye hivi, serikali ifanye vile..... but let me respond to what I think of the blame game. I think that Masha, Mwema and Othman have nothing to do with this. Not in realistic terms
The primary responsibility of a democratic government is to be a regulator in business and not to manage the economy (ule ulikuwa ni ujamaa) and in this case the arm of the Tanzanian government that regulates financial schemes is CMSA (Capital Market Security Authority) it's like FEderal Securities Exchange Commission (SEC). Hivyo nadhani ni lazima hatua ya kwanza iwe kuwatimua wooote kazi. Kuanzia ngazi ya chini mpaka juu. From this aspect, Gavana wa BoT tunamlaumu bure kwa sababu hivi sasa CMSA is an independent REGULATORY AUTHORITY, yenye bajeti kubwa tu.
After CMSA, ifuate Financial Investigation Unit. Usalama wa Taifa hawana expertise katika masuala haya kwa hiyo tunawalumu bure, in this specialist unit there are investigators who are financial specialists and are capable of doing this job. Kwa hiyo unit nzima itimuliwe. Both CMSA and FIU iko chini ya Wizara ya Fedha, kwa hiyo waziri ajiuzulu.
I think that realistically this is where the blame game stops officially. However on another level, the responsibility goes all the way up to the president, but that is another story.
 
Huu upatu wa Deci ulikuwa umeshafikia mwisho wake. Serikali ilikuwa inasubiri tu upasuke wenyewe ila nadhani wameona unazidi kukaribia uchaguzi. Ukija kupasuka wakati wa uchaguzi ingekuwa balaa.

Shida ya upatu wowote hupasuka pale umaarufu unapofikia kilele kwani investors huwa wengi mno. Waliotangulia hurudisha faida walizovuna kwa kiwango kikubwa. Ila sasa wanakuwa wengi mno na hapo cash outflow za kuwalipa wavunaji inakatika.

Sasa hivi serikali imewasaidia hao vibaka kwani kwa wanachama wao watawaambia tumefungiwa na serikali ndo maana tumeshindwa kuwalipa. Ukweli hawajafungiwa, ila sasa hivi wanaokuja ni wavunaji tu na wanaong'oa mbegu zao. Kundi kubwa zaidi ni la waliopanda katika kipindi kama cha wiki nane kabla ya onyo la Benki kuu.

Humo kuna wengi ambao walikuwa wamekunja mikono wakisubiri muda wao wa mavuno, wakati wale walio watangulia wakivuna pesa zao.

Serikali kuingilia kati sasa kumewapa relief waendeshaji ambao sasa lawama zao ni kwa serikali. Lakini ingechelewa zaidi, balaa lingekuwa kwenye miezi ya October au early 2010. Hii ingeleta undesired effects kwenye uchaguzi.

Ila kuna uzembe why this upatu has gone on for all this long without action. Tulijua huo ni upatu. Tulifnya nini? (wale tulio madarakani).
 
Kipimapembe mkuu, nadhani uko katika cheo fulani na ni kiongozi, naomba kwanza nipongeze analysis yako nzuri, lakini pia nitoe ushauri kwamba inabidi serikali ifanye jitihada nzuri zaidi ya kuwasiliana na wananchi, kwani kutoa tu matangazo katika magazeti na waziri mkuu kufoka haisaidii, kama Mwanakijiji alivyoainisha kwa kiina.
 
Siwezi kuwalaumu watanzania wa kawaida sababu Tanzania hakuna enough resource inapokuja swala zima la uwekezaji.

Ni kweli Mkuu. Kwenye masuala ya uchumi watanzania ni kama kuku wa kienyeji, wameachwa wajichunge wenyewe na matokeo yake mwewe wajanja wanawakamata kama vifaranga. na hili la Deci ni moja tu, kuna mambo mengine kadhaa yanaendelea ambamo Watanzania wanaliwa kutokana na desperation yao kiuchumi
 
.................Maana yake mtanzania hatakuwa huru mpaka pale atakapofunguliwa macho aone, wakati huyu mheshimiwa aitwae kipenzi cha watanzania, kikwete, alisema maisha bora kwa kila mtanzania, lakini hatufichi hakuna kilichofanyika, watanzania wana hali mbaya kuliko kawaida, wamenyanga'nywa mali zao nyumba zao, baada ya kukopeshwa na taasisi za fedha, pride, finca, na zingine za aina hiyo...................

Kutoka kwenye quote hapo juu nimesikia kuna tetesi vile vile msukumo wa serikali kufuatilia zaidi DECI ulitokana pia na baadhi ya taasisi zilitajwa hapo juu baada ya ile target group yao kuwa hawaendi tena kukopa kwao na kukimbilia kupanda DECI.....sijui kuna ukweli kuhusu hili.

Hii ina maanisha serikali yetu na vyombo vyake huwa ni kazi sana ku-initiate mambo mpaka wapate msukumo kutoka nje...!

Pride, Finca etc ...zinaonysha ni jinsi gani bado havijakidhi jinsi gani ya kuhudumia hii segment ya microfinance vizuri.....!
 
Last edited:
Hii deci na iishe sasa tufunge mjadala manakle mafisadi wanachekelea na kuundeleza kiaina ili kuthoofisha mapambano dhidi yao na focus . Tuendelee na hoja ze4tu za UFISADI
 
Mkuu Kikojozi,
Ningekubaliana na wewe kwa kiasi kikubwa AFTER serikali ilitangaza tahadhari yake. Lakini kabla ya hapo kulikuwa na tahadhari gani au elimu gani iliyotolewa kwa wananchi wa kawaida kuhusu pyramid schemes.

Mkuu Susuviri
Pyramid schemes sio kitu kipya nchini kwetu. Huko nyuma zimekuja na kwenda nyingi. Labda hii ya DECI iliingia kwa staili mpya kwa "kuhalalishwa" na Kanisa Pentecoste, BRELA, TRA na BOT. Lakini vitu vingine ni "no brainer". How does mtu mzima, anayefanya kazi, believe unaweza kupata pesa za bure bure?

But your arguments are valid, kwani we have to stop thinking in terms ofa NANNY state. Ndo maana tunasema oh, serikali ifanye hivi, serikali ifanye vile..... but let me respond to what I think of the blame game. I think that Masha, Mwema and Othman have nothing to do with this. Not in realistic terms

Ewaaaaa...

The primary responsibility of a democratic government is to be a regulator in business and not to manage the economy (ule ulikuwa ni ujamaa) and in this case the arm of the Tanzanian government that regulates financial schemes is CMSA (Capital Market Security Authority) it's like FEderal Securities Exchange Commission (SEC). Hivyo nadhani ni lazima hatua ya kwanza iwe kuwatimua wooote kazi. Kuanzia ngazi ya chini mpaka juu. From this aspect, Gavana wa BoT tunamlaumu bure kwa sababu hivi sasa CMSA is an independent REGULATORY AUTHORITY, yenye bajeti kubwa tu.
After CMSA, ifuate Financial Investigation Unit. Usalama wa Taifa hawana expertise katika masuala haya kwa hiyo tunawalumu bure, in this specialist unit there are investigators who are financial specialists and are capable of doing this job. Kwa hiyo unit nzima itimuliwe. Both CMSA and FIU iko chini ya Wizara ya Fedha, kwa hiyo waziri ajiuzulu.
I think that realistically this is where the blame game stops officially. However on another level, the responsibility goes all the way up to the president, but that is another story.

Hii DECI ime-expose some serious weakness kwenye financial regulatory system yetu. The fact kwamba DECI is a legally registered entity inacomplicate sana mambo. Its very tempting to think kwamba wakubwa nao walikua wanakula humohumo.
 
Hii deci na iishe sasa tufunge mjadala manakle mafisadi wanachekelea na kuundeleza kiaina ili kuthoofisha mapambano dhidi yao na focus . Tuendelee na hoja ze4tu za UFISADI

DECI nayo inakaharufu ka ufisadi
 
Hii DECI ime-expose some serious weakness kwenye financial regulatory system yetu. The fact kwamba DECI is a legally registered entity inacomplicate sana mambo. Its very tempting to think kwamba wakubwa nao walikua wanakula humohumo.

Seriously, I think that we sometimes allot too much intelligence to our civil servants, but if you have dealt with them utajua ya kuwa the reason DECI ilisajiliwa na haikufuatiliwa ni kutokana na IGNORANCE na UZEMBE wa watumishi hawa waliopewa dhamana ya usimamizi. Is this an excuse? No! Lakini kuanza kujenga conspiracy theory eti President or usalama wa taifa wali-tunga DECI or something in that breed is ludicrous. What is probable ni kwamba wapo viongozi ambao just like wananchi walidanganywa na kuwekeza but they are victims like others au kama walivuna yaani kuwaibia wenzao basi they are guilty kama yule mlemavu aliyedai kuwa aliwekeza 20,000 na ameshavuna laki 8!
 
DECI imekufa and nothing new.
Tumeambiwa uchunguzi unaendelea hivyo tuwape muda
Sijui kama matatizo yanayowakabili wabongo yanatoa muda mtu kujipanga....
 
Back
Top Bottom