Death au DECI? - Masha, Mwema na Othman | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Death au DECI? - Masha, Mwema na Othman

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 15, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 15, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Niliandika juu ya DECI kwa kirefu tarehe 14 January mara baada ya kupata taarifa ya uwepo wa shirika hilo na nikaonesha kwa kirefu jinsi gani litaporomoka. Nikatoa mapendekezo ya kutosha ya hatua gani zichukuliwe nikiamini kabisa kwa kuingilia kati mara moja jambo hilo lingeweza kuepusha hatari iliyo mbele yetu.

  Jambo hili lilipoibuliwa tena na vyombo vya habari wiki hizi chache zilizopita sisi "Cheche" tuliandika kwa kirefu juu ya DECI na kuelezea ni kwanini mchezo huu ni hatari. Tulionesha (kama walivyofanya wengine vile vile) kuwa DECI kimsingi ni mchezo wa ulaghai wa fedha (financial fraud). Licha ya ukweli wa DECI kujulikana kwa muda mrefu (haiwezekani isijulikane hadi watu karibu nusu milioni wanajiunga!) serikali imekuwa legelege na inayofanya mambo kama haina akili nzuri.

  Ilipotoka makala yetu ya wiki iliyopita pamoja na makala zilizotoka kwenye Tanzania Daima na MwanaHalisi ambazo tumejitahidi kuzipush ili kuliamsha taifa bado jambo hili linaonekana bado linaleta ukungu mbele yetu. Ninavyoandika leo moyo wangu ni mzito kwa sababu leo asubuhi nimepata email moja ambayo naiweka hapa jinsi ilivyo ya mmoja watu ambao watakuwa wameathirika na uamuzi wa kuifungia DECI.

  Sakata hili la DECI linaendelea kuthibitisha mambo ambayo nimeyavalia njuga kwa muda:

  a. Usalama wa Taifa (namaanisha uongozi wake) una matatizo makubwa mno kiasi cha kuruhusu wizi huu kutokea mbele ya macho yao. Taasisi yao ya Intelligensia pamojana taasisi ya Inteligensia ya mambo ya fedha (FIS) wanaendelea kuthibitisha kuwa hawana uwezo wa kusimamia fedha zetu. Baada ya yaliyotokea Benki Kuu nilitarajia labda wataamka lakini bado wamelala kama pono!

  b. Jeshi la Polisi bado halina uwezo (kiuongozi na kimkakati) kuzuia uhalifu kama huu wa kifedha. Inapofikia Jeshi la Polisi linatoa ulinzi wakati mwizi anaiba basi jeshi hilo linapoteza sifa ya kuwa msimamizi wa usalama wa "raia na mali zao". Inachekesha (kwa kuudhi) kuwa Jeshi la Polisi limekuwa washirika wa wizi huu halafu wao wenyewe ndiyo wanatakiwa kusimamia kuchunguza. Hii inanikumbusha tukio la vifo vya watoto Tabora ambapo Jeshi hilo likijua ubovu wa jengo lile na matukio ambayo yalitokea pale kabla likaitwa kushiriki uchunguzi wa jambo ambalo wao wenyewe walitakiwa wachunguzwe! Kila kitu tunafanya kinyume nyume.

  c. Endapo vurugu zitatokea nchini (kama email hii inavyoashiria) kama ilivyotokea kule Albania 1996 basi kuna viongozi ambao barua zao za kujiuzulul zinatakiwa kuwa mezani mara moja kwani ni ushahidi wa kushindwa kwao kuongoza. Viongozi hao kwa haraka ni Waziri wa Mambo ya Ndani (ambaye sielewi kwanini bado ni Waziri!), Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa Usalama wa Taifa ambaye kwa kila kipimo ameshindwa kulinda usalama wa Taifa au kukusanya taarifa za kijasusi ambazo zingeweza kuzuia upuuzi huu unaoendelea nchini.

  d. Waziri Mkuu ambaye ana matatizo ya kufuata utawala wa sheria ajiandae yeye mwenyewe kuwajibika endapo damu itamwagika nchini kutokana uzembe na usimamizi mbaya wa serikali. Kauli yake kuhusu DECI inaendelea kuthibitisha ni jinsi gani bado Tanzania hatuelewi kitu kinachoitwa "the tyranny of the law" au wakati mwingine kinajulikana kama "the dictatorship of the law". Bado tunafanya mambo kana kwamba sheria is optional!

  Well email yenyewe:
  Ninachosema ni kuwa, mapendekezo yetu yaliyoko kwenye "Cheche" toleo la wiki hii ndiyo njia pekee ya kunusuru machafuko nchini. Vinginevyo, kutokana na uzembe wa watu wachache, tujiandae kulipa gharama kubwa, gharama ambayo CCM isiithubutishe.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Mbona GAVANA wa benki kuu (BOT) bwana BEN NDULLU umemsahau?

  bila kumsahau KITILYA wa TRA ambayo walikuwa wanakusanya kodi huko DECI
   
 3. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Inawezekana walikuwa hawajui, maana michezo hiyo ipo ya kumwaga! Waambie uso kwa uso wengine vichwa vizito kuelewa
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,773
  Likes Received: 83,114
  Trophy Points: 280
  Naam, na hawa BoT na TRA inasemekana waliwasaidia DECI kufungua upatu wao nchini.
   
 5. Kaduguda

  Kaduguda JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2009
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 670
  Likes Received: 281
  Trophy Points: 80
  Leo nimewasiliana na ndugu mmoja ambaye alikuwa DECi kufuatilia mavuno yake. Kwa kusikia kuwa DECI imezuiliwa kuendelea na shughuli zake na mustakabali wa fedha zake alizowekeza haueleweki yule mama alizirai hapo hapo na kuhitaji huduma ya kwanza.

  Ndugu zangu kuvunjwa kwa DECI kumeleta kilio kikubwa sana haswa kwa walalahoi wenzetu Tanzania. Kuna watu waliweka mitaji yao huko sasa hii kasheshe wengine Blood pressure zimekwenda juu na nyumbani hakueleweki. Please serikali kama kuna cha kufanyika ili kuweza kuepusha jambo lolote baya linaloweza kutokea kifanyike. Vinginevyo kama mwandishi wa email ya Mwanakijiji asemavyo watu wanaitupia lawama zote serikali ya CCM na wameapa pamoja na mambo mengine kuisulubisha kwenye uchaguzi wa mwakani. Maana kama wasemavyo kwamba sasa wanajua namna ya kuchagua kati ya pumba na mchele!! Mwenye masikio na asikie, na pia asomaye na afahamu!!
   
 6. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Napata shida kuelewa huu ufungaji wa deci deci! Watu wamahesabu wakowapi ili kuestablish the value of Deci Deci! Unafunga tu maana yake nini? Serikali ilitakiwa kuweka existing strategy ya Deci Deci kupunguza makali ya upoteaji pesa wa wananchi!

  Tafadhali toa taarifa zaidi ya kufugwa kwa Deci Deci kuelewa conditions ambazo serikali imeweka katika kufunga deci kuhakikisha maslahi ya wananchi hayapotei kwa kiasi kikubwa.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu, Pengine mimi niko nyuma sana ya swala hili lakini naomba msaada wenu kuna maswala ambayo siyaelewi vema..
  Mimi nachojiuliza sasa hivi kama Deci imefungiwa, Je serikali amefuatilia na kuzuia fedha za wale ambao bado wamewekesha fedha zao Deci wasije zikwa?
  Je, serikali imeshika nyaraka zozote zinazohusiana na uwekeshaji wa Deci kiasi kwamba wamekuta kuna ubadhirifu na mashtaka yanafuata?.. laa sivyo siwezi kuamini hatua kama hii kuchukuliwa na serikali wakati hawafahamu kinachoendelea ndani ya upatu huu..
  Siku zote serikali ndio hutuambia tuwe na ushahidi!.. Ni ushahidi gani serikali uliokuwa nao kiasi kwamba wamefikia kuwafungia Deci hata kama kuna UTAPELI!..
  Uchunguzi gani ulifanyika na report gani imepatikana kuhusiana na Deci..
  Naomba kuelimishwa!
   
 8. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,122
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Ninavyoelewa serikali haijafungia Deci, waziri mkuu alisema uchunguzi unaendelea.
  Ila kwa sababu watu wengi wamepata mashaka na pesa zao na kuamua kwenda kuzitoa Deci, Deci inajikuta haiwezi kuwalipa watu wote pesa zao, ndo maana wamefunga ofisi.
   
 9. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  watu wakalime... haya mawazo ya 'easy money' ndio yanawafanya wawe victims of fraud!
   
 10. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watu wanalima, wemepinda mgongo kweli! Walanguzi kibao! Dola letu miguu juu! Alisema bibi yangu "aha kulima nilime mimi, jua linipege mimi, aha! mwenzangu umekaa kariako miguu juu, kilo shilingi 700, mie nabakia na mia"

  Lakini mwanamke washoka hakuchoka amepiga jemba kusomesha watoto wake, waliotusomesha sisi, na wale wajukuu maisha yaliyogoma anasomesha pia! Lakini ukimwangalia usoni unajiuliza hii nchi mmemsaidia nini bibi yangu!

  Watu wanayaona hayo kaka, wanagundua jembe halina dili! wanakimbilia mjini! kumbe mjini ndio balaa kabisa!
   
 11. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  "Deci imejikuta haiwezi kuwalipa watu wote pesa zao, ndo maana wamefunga ofisi". Deci imekufa RASMI kama tulivyosema hapa.

  Mi ninahisi haya makampuni ya kitapeli huwa wanaonga na maofisa wetu wa usalama, TRA na BOT.

  FP
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  wewe waongeze tu... si kila kitu mimi nifanye.. unaweza kumuongeza na Mkullo pia.
   
 13. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #13
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwa mara nyingine uhalifu wa kifedha unafanyika mbele ya vyombo vyetu vya usalama na mkuu wa kijiji huyo anapeperuka kwenda kuomba tena!
   
 14. M

  Makfuhi Senior Member

  #14
  Apr 16, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nawashangaa hawa wanaojiita wachungaji/ maaskofu ambao wanawadanganya waumini wao kuwa kuna utukufu bila msalaba. Nyie waumini fungukeni masikio. Imeeandikwa kwa jasho utakula
   
 15. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #15
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ngoja nitawapaka hawa wachungaji wanaochunga matumbo yao!
   
 16. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Na kwanini tusione kuwa hao hao ndio wanashirikiana na matapeli kuandaa uhalifu huo. Fikira zangu zinaniambia Mkuu wa Kijiji anayajua yote haya.
  NDIO MAANA ANASHINDWA KUTOLEA KAULI MAMBO MAZITO KADHAA YANAYOIKABILI NCHI ANAKIMBILIA KUMPONGEZA HASHEEM KUCHEZA LIGI YA NBA.
   
 17. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Mungu antumia njia nyingi sana kufikisha ujumbe wake kwa wanadamu...wanaojua alama za nyakati wanazo kumbukumbu, mambo madogo sana huwa yanasababisha mageuzi ya kihistoria..but am not pretty sure if Tanzanians are ready..
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  DECI ni TISHIO KWA USALAMA WA TAIFA.......

  Sio hulka yangu kukimbilia kuwataka wanasiasa ama watendaji wetu kujiuzulu lakini kwa hili ni wazi kuna uzembe wa hali ya juu katika vyombo vetu vya dola na hivyo wahusika wanapaswa kuwa waungwana na kujiuzulu mara moja........

  Athari za DECI ni zaidi ya zile za kuchumi. DECI ina athari kubwa sana KISIASA na KIJAMII. Mabadiliko tunayataka lakini sio haya ya kuja kuletwa na makundi ya kijami kama yanayohusika na DECI. Ni makosa makubwa kuacha nguvu ya KIROHO na KIUCHUMI kuhodhiwa na mtu ama kikundi chochote haswa katika jamii mchanganyiko kama yetu. Kama kuna wanasiasa ambao wamekuwa wakisadia na kulinda DECI (nafutilia taarifa zao) kwa mtazamo wa POLICAL CAPITAL ni wazi wanapaswa kuanikwa hadharani na wananchi wakawajua. Tuna mengi yanayoendelea kutishia mustkabali wa nchi yetu, tumechoka kuona wazembe na walafi wachache wakiendelea kuchezea mustakabali wetu kwa manufaa yao binafsi.

  omarilyas
   
 19. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #19
  Apr 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...asikusikie Rev. Kishoka
   
 20. KIFARU

  KIFARU Senior Member

  #20
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 172
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa suala la deci inaonyesha jinsi gani serikali yetu isivyokua makini, suala dogo kama hili usalama wa taifa wameshindwa fahamu au tuseme wamezembea mpaka limekua kubwa namna hii, kweli alisema mkuu wakati akiwachagua mawaziri, uongozi hausomewi ila utajifunza hukohuko ulipopangiwa(bila kufahamu management inasomewa)..tz yetu kwa mwendo huu wa kila kitu ni siasa iko siku itakua ni nchi ya kusadikika kisha tutaendelea kufanya mambo ya kusadikika
   
Loading...