DC Ole Sabaya: Jabali amelala Hayati Dkt. Magufuli

Penye wanafiki hofu hutanda wala wasijuwe wafanye nini, maana kisasi ni cha Mungu aliye hai siku zote hata milele

Bali walio haki hawana hofu siku zote.
Uzi ufungiwe hapa....mengine ni matango pori....

Heshima kwako chief,
 
Sabaya na genge lako mmechanganyikiwa kwa hii counter attack mliyopigwa na Mungu. Huo uhakika wa kwamba Magufuli kwa sasa yuko miguuni kwa Mungu umeutoa wapi?
Wewe una uhakika gani kuwa yupo pahala kwingine nje ya miguuni pa MUNGU?!
 
ANAANDIKA DC SABAYA LENGAI
_
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana's Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajilya Taifa .
Sabaya bado kijana, na ilikua mda wa kuonyesha kipaji zahidi, but sifa, ujuaji, umimi nk, utamfanya kutokua kiongozi mzuri,yahani utembee na silaha usiku wa name na gari UN feki, ujeruhi watu, kisa kujipendekeza,mbona watu wenye akili Kama mh MTAKA wametulia kipindi hichi Cha utawala japo ilikua ngum jutoboa,by mh Jerry muro, fanya kazi KWA utaratibu,heshim watu I wish ningekua Arusha nimchape makofi nifungwe Kama kamanda mmoja wa Iringa alivyo fanya KWA mkuu wa mkoa enzi mh Nyerere, ni utovu wa nidham,kwa baadhi ya wa kuu wa wilaya na mikoa
 
Mungu wa kweli ametimiza maandiko kwake lazima tutarejea tuishi kwa usawa na sio mambo ya kishamba ya kutekana na kuuwana hakika kila mja atavuna alicho panda!
 
Huyu tuachieni akija pale Riverbills kuchukua changudoa na kuimba Kareoke tutamfundisha

Achia kashfa zake za kupora pora ‘wachumba na wake za watu’

Afu kuna hawa wa dada wa mjini na kuna mmoja aliwahi nisimulia story yake (hasa akiwa Dar) huyu kwamba ni mtu anaependa kulala na mwanamke zaidi ya mmoja (naona ni fantasy yake ) na ni mambo binafsi kweli na ukizingatia huyu ni kijana lkn kwa wadhifa wake na kutumikia ofisi za umma/serikali kuna mambo mtu unatakiwa kujidhibiti
 
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa na vizazi tutakavyoviacha.Vilio vya wanyonge na wasio na sauti vimefika kwenye kiti cha Enzi. Rest in power John, Tutakutana Baadae.Bado ni salama Rohoni mwangu.

View attachment 1735677View attachment 1735678
Yawezekana bwana DC hukumjua beana magufuli. Huyu ni mtu hatari kuwahi kutokea katika dounia hii. Mtu aliyeamini kwamba akiamincho ndiyo alfa na omega.... mungu anwapenda watanzania angetawala co kuongea kwa maika 10 hiyi watanzania tungepigana baada ya kiongozi wake.ALIKUWA FEDHULI
 
Acha kuuza madawa mkuu utafungwa!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom