DC Ole Sabaya: Jabali amelala Hayati Dkt. Magufuli

Huyu Sabaya ni Monster.
Ametesa sana Binadamu wenzake hapa Hai.
Binafsi nasubiri Kwa hamu kuliona anguko lake.
 
ANAANDIKA DC SABAYA LENGAI
_
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana's Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa .
Bora Maro alijisemea atarudi Yanga kuliko kutapatapa huku
 
Sabaya sasa uwe makini yule mtu aliyekuwa anakukingia kifua unavamia biashara za watu, unakamata watu hovyo na kuwafunga jela ameondoka.
Kati ya Viongozi wanafiki, waongo, wazandiki, limbering wa madaraka katika A5 ya JPM huyu Mmasai Ole Sabaya alikuwa mmoja wao.
Ma- RC nz Ma-DC wapuuzi kabisa akiwemo Makonda aliyetupwa nje, Ally Happiness wa Iringa, Chalamila wa Mbeya aliyewadanganya Watz kuwa aliongea na JPM akiwa marehemu....!!!!
Ole Sabaya ajue huu ni msimu mpya, Its another new season! Ole, Ole na Ole wake kama hatabadilika....!!!!Aliyekuwa ana mkingia kifua is no more!!!
 
ANAANDIKA DC SABAYA LENGAI
_
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana's Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa .
hili ZIMWI halieleweki.
 
Naumia sana mtu akifa hasa ambaye niliyekuwa namfahamu hata kwa mbali tu. Marehemu JPM amefariki kiutu lazima mtu usikitike sana. Lakini kuna sifa zingine hazifai tumpe Baba yetu. Kumuita Mwanamapinduzi wa Afrika sio kweli. Mimi ningependekeza aitwe mkombozi wa Watanzania kutoka katika makucha ya wezi wa mali ya Umma. CCM
 
Kinatumia ndio basi tena wewe Pimbi , malipo ni hapahapa duniani subiria malipo yako muda ndio huu umewadia ndugu .
 
Naumia sana mtu akifa hasa ambaye niliyekuwa namfahamu hata kwa mbali tu. Marehemu JPM amefariki kiutu lazima mtu usikitike sana. Lakini kuna sifa zingine hazifai tumpe Baba yetu. Kumuita Mwanamapinduzi wa Afrika sio kweli. Mimi ningependekeza aitwe mkombozi wa Watanzania kutoka katika makucha ya wezi wa mali ya Umma. CCM
Mkombozi gani anachukua hela kwa mafidadi anapeleka nyumbani kwake underground house huo ndio ukombozi ?
 
Sabaya sasa uwe makini yule mtu aliyekuwa anakukingia kifua unavamia biashara za watu, unakamata watu hovyo na kuwafunga jela ameondoka.
Akiendeleza ubashite style yatamkuta ya mwandindi maana ma mangi wametumwa pesa mjini.
 
Ataandika sana yeye na vibaraka wenzake , angefanya kazi kwa kufuata sheria na katiba asingekuwa na Cha kupoteza , sasa kutegemea mtu matokeo yake ndio haya Sasa kibarua ndio basi tena yeye na wajinga wenzie .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom