evangelical
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 5,989
- 9,946
Aomboleze tu maana mwisho wake umefika
Haaaaa jamaa ulitabiri,
Jambazi ole sabaya limefungwa
Aomboleze tu maana mwisho wake umefika
kumbe wewe nabii?? unafahamika kwa jina la nabii nani mkuu??Ndugu yangu ukweli umeondokewa na kupungukiwa ulikanyaga Sheria upendavyo hakuna wa kukukemea ulidhalilisha watu ukaonekana shujaa,ulidhulumu watu na kufanya ujambazi wa mchana Ila waliotakiwa kukuwajibisha wakakulinda na kusema ni mtakatifu yote ujue hatujasaha km ubongo wako ulivyomsahaulifu Ila ss siku zako zinahesabibika suntashangaa siku nikija kukuona gereza la karanga hapo
Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
[emoji40]Huyu atumbuliwe ili arudi uraiani avune alichopanda, aone maisha yanavyokwenda kwa kasi bila cheo. Raia wanavyo msubiri kwa hamu mtaani hata kabla Magufuli hajazikwa, wanaona Mama Samia anawachelewesha sana.
ANAANDIKA DC SABAYA LENGAI
_
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.
Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.
Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.
Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.
Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana's Mwenyewe.
Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.
Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa .
Pumbavu sana hili toto la kimasai. Yaani lilidhani Magufuli ataishi millee?
Naona kama mwonekano wake hapo 2051 hivi!
Ohh basi sawa.Thanks kwa maneno haya DC wetu mzalendo
OhoooSabaya sasa uwe makini yule mtu aliyekuwa anakukingia kifua unavamia biashara za watu, unakamata watu hovyo na kuwafunga jela ameondoka.
AiseeeeHuyu ni miongoni wachache walioshusha heshima ya cheo cha DC ni imani yangu atavuna mapema alicho panda.Mama Samia tunaimani nawe Mola akutangulie katika yote.
SwadaktaSabaya mvamiaji wa makazi ya watu na silaha za moto hata ujisafishe vipi watu wamekuweka kwenye radar
Njoo usome ugoro wakoHata Makonda mlisema mnamsubiri uraiani lakini huyo hapo hamumfanyi chochote
Sauti kidogo huku nyuma hatujasikiaThanks kwa maneno haya DC wetu mzalendo
Kweli mkuu level za huyu mwamba ni kufungwa gereza kubwa Tanzania avenue rekodi kisongo n gereza ndogo sanaSabaya ni moja ya viongozi ninaowatabiria makubwa kwa nchi hii.
Kweli mkuuWatoto wadogo hawawezi kuliona hilo.
Hujakosea hata kidogoSabaya ni hazina ya uongozi nchi hii.