DC Ole Sabaya: Jabali amelala Hayati Dkt. Magufuli

Mwanaume gani wa kimasai Analialia na kutoa machozi mbele ya wanawake Kama ndito?
Huyu nadhani hajatahiriwa au Ni mkwavi huyu? Haiwesekani huyu akawa moran
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
FB_IMG_1620938613111.jpg
 
UPUUZI MTUPU!
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa na vizazi tutakavyoviacha.Vilio vya wanyonge na wasio na sauti vimefika kwenye kiti cha Enzi. Rest in power John, Tutakutana Baadae.Bado ni salama Rohoni mwangu.

View attachment 1735677View attachment 1735678
 
Huyu atumbuliwe ili arudi uraiani avune alichopanda, aone maisha yanavyokwenda kwa kasi bila cheo. Raia wanavyo msubiri kwa hamu mtaani hata kabla Magufuli hajazikwa, wanaona Mama Samia anawachelewesha sana.
Watu wenye level hii ya ubashiri hebu bashiri kama huyu Rais atalegeza kwenye ajira
 
Viongozi wetu sijui hua wanawaza nini wakipewa nyazifa
Siyo 'viongozi wetu' hao ni raia kama wewe, wamepewa wadhifa ambao ni dhamana ya muda tu.

Kiongozi ni yule aliyepewa karama toka kwa mungu na watu hao katika jamii wapo.

Labda hapo ungesema hivii?...'raia wa Tz sijui wanawaza nini wakipewa nyadhifa'...

Raia wa Tz ni wakarimu na wacheshi sana mabarabarani, misikitini, makanisani, kwenye dhifa mbali mbali lakini mostly ni katili na hovyo sana kuanzia majumbani mwao kwa watu wanaoishi nao kwa kutegemewa na pia mahala pa kazi.

Mtu akipata madaraka, anabadili hadi mwendo na kuanza kupandisha mabega juu na kuwaona watu aliowazidi cheo kuwa ni taka taka.

Sasa mtu kama huyo akifukuzwa, mamaaweee! Hadi aibu!
 
Baada ya Kushuhudia Mwili wa Dr John P.Magufuli ukiwa Akiwa Amelala Sasa Nimeamini Jabali Lenye Moyo wa Simba Na Akili ya Duma Amelala Usingizi wa Mauti.

Usiku ule wa Tarehe 17 March ni usiku Mgumu kuwahi kutokea katika Maisha Yangu, Nilimfikiria Baba, Mwalimu,mtu mwenye Huruma,ambaye kabla ya "kukuhukumu" atataka akusikilize na wewe, Na siku zote akisema USIOGOPE,Mtu asiyejua UNAFIKI wa kupikwa ila aliyezingatia zaidi matokeo ya kazi Aliyokupa, na aliyeamini sana katika nafasi ya pili,Anayesikiliza sana tena kwa Upendo.

Kuondoka kwake kwa wakati huu kuliniingiza Ganzi Nisiyowahi kuiona Maishani, Ninajua Mama Janeth amempoteza Mume, Taifa Limempoteza Baba na Rais, Africa Imempoteza Mwana mapinduzi Jasiri,Lakini Mbingu Imempokea shujaa Wa Imani, Aliyevipiga vita bila Kujali maumivu ya Moyo aliyoyapitia, akailinda imani kwa Kulitambulisha Jina la MUNGU aponyaye kwa mataifa, Na sasa amemaliza mwendo na Amepumzika Miguuni kwa bwana Wa vita. MATENDO uliyoyatenda kwa Gharama ya maisha yako, yamekutangulia.

Nenda Baba Nenda, matendo yako, kazi zako,na kujitoa kwako kumeandikwa kwa wino wa dhahabu kwenye moyo wangu na katika mioyo ya watanzania wa kweli umeandika Dibaji mpya. Hadithi za kazi ulizowatendea wana wa Taifa hili zitasimuliwa na vizazi, kwangu umenipa sababu ya kuamka tena, kutenda kwa Ujasiri bila woga wala Hofu,Nikiona Fahari sana Kwamba nimejifunza na Kuwa Mwanafunzi wako na uwe na Uhakika kwamba sasa Nitatenda kwa ujasiri zaidi bila kutokuonea wala kupendelea na niikijua ipo siku MUNGU mwenyewe, katika ukamilifu wake, atatuita kutoa hesabu ya matendo yetu na Sio Maneno yetu.

Tukutane baadae Nyumbani kwa baba, kusiko na Kuomboleza, kilio wala maumivu,Tutakapohesabiwa haki na Bwana Mwenyewe.

Imenyamaza sauti dhabiti ya wanyonge, imenyamaza kimya kiranja mkuu na mkufunzi wapigania usawa kwa vitendo, Amelala Mjamaa Asiyetishika,Ardhi imemeza shujaa na kaka wa Taifa,Bwana Ataitia Nguvu Mioyo iliyosinyaa, wala Hataacha Taifa Lililolitetea Jina Lake liaibike kamwe.

Umetufunza ushupavu na misimamo imara,Nyayo na Kumbukumbu zako vitatupa hasira za kufanya kwa ajili ya Taifa na vizazi tutakavyoviacha.Vilio vya wanyonge na wasio na sauti vimefika kwenye kiti cha Enzi. Rest in power John, Tutakutana Baadae.Bado ni salama Rohoni mwangu.

View attachment 1735677View attachment 1735678
Unapomtegemea mwanadamu kama vile alijiumba mwenyewe, haya ndio yatakayokupata!
 
Siyo 'viongozi wetu' hao ni raia kama wewe, wamepewa wadhifa ambao ni dhamana ya muda tu.

Kiongozi ni yule aliyepewa karama toka kwa mungu na watu hao katika jamii wapo.

Labda hapo ungesema hivii?...'raia wa Tz sijui wanawaza nini wakipewa nyadhifa'...

Raia wa Tz ni wakarimu na wacheshi sana mabarabarani, misikitini, makanisani, kwenye dhifa mbali mbali lakini mostly ni katili na hovyo sana kuanzia majumbani mwao kwa watu wanaoishi nao kwa kutegemewa na pia mahala pa kazi.

Mtu akipata madaraka, anabadili hadi mwendo na kuanza kupandisha mabega juu na kuwaona watu aliowazidi cheo kuwa ni taka taka.

Sasa mtu kama huyo akifukuzwa, mamaaweee! Hadi aibu!
Dah noma sana
 
Ole Sabaya, Paul Makonda, Ally Hapi, Byakanwa, Chalamila, Mnyeti walikuwa wanafanya uovu kama vile Magufuli ataishi mikele

Wengine ni Biswalo Mganga, Lazaro Mambosasa, Wilson Mahera, iko siku hata Kama siyo utawala wa Mama Samia watakuja wajibika kwa matendo maovu waliyotenda wakidhani Magufuli ni mungu.
Namba inasoma, Sabaya tayari
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom