DC Mrisho Gambo wa Arusha amhujumu mkuu wa mkoa

DC Mrisho Gambo wa Arusha amhujumu mkuu wa mkoa

Duh kumbe jamaa alishaanza figisufigisu kitambo ili ateuliwe
 
Subutu nani kakudanganya? Kwa taarifa yako gambo ni mtoto wa chuga so chuga anaijua vizuri sana.
 
Ccm kufanya kazi ili uonekane mpaka ugombane Na wapinzani siyo utendaji huyu mzee alikuwa anafanya kazi sana ngoja uone sasa yatakayotokea sasa kila kitu itakuwa ugomvi tu siyo utendaji
Ni shida sana, tuna mfumo wa ajabu ajabu
 
Huyo dogo alikuwa wilaya ya korogwe,,alikuwa msumbufu mno,na alishawah kumtukana mwanasheria wa halmashaur waziwaz,, akapigwa chini,,baadae wakamtupa CHUMVINI kelele zikaisha,naona amerudi mjini anaanza tena
 
Katika hali ambayo haikutarajiwa mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo ameanza kumhujumu mkuu wa mkoa Bwana Ntibenda. Hali hiyo imetokea leo eneo la nane nane Arusha,leo ndio siku ya uzinduzi rasmi wa siku ya nane nane ambako ilitegemewa watumishi wa halimashauri kuhudhuria sherehe hizo ambazo mgeni Rasmi ni Mkuu wa mkoa

Katika banda la halimashauri ya jiji la Arusha hakukuwa na mtendaji hata mmoja baada ya kuitwa kwenye kikao kingine na mkuu w wilaya ya Arusha bwana Gambo katika ukumbi wa chuo cha ufundi Arusha. Haikuweza kufahamika mara moja sababu ya mkuu wa wilaya kumtoroka bosi wake na kuitisha kikao kisicho na tija wakati akijua kuwa sherehe za nane nane ni za muhimu zaidi.

Baadhi ya watumishi walioenda kwenye kikao cha DC wamekerwa na tabia ya DC kujisifu kuwa yeye ndie mteule sahihi wa Rais na kuwa siku si nyingi atapandishwa cheo kuwa RC hivyo watumishi wote wamsikilize yeye vinginevyo atawahamishia Tandahimba au Chato.

Kitendo cha leo ni mwendelezo wa mgogoro wa chini kwa chini unaondelea kati ya mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa unaosababishwa na tabia ya DC kumuhujumu waziwazi RC na wakati mwingine kuongea maneno ya kashfa dhidi ya RC
Kwa maana hiyo huyu alikuwa ameshaongea na Prezidaa kuhusiana na uteuzi wake.
 
Back
Top Bottom