DC Jerry Muro na mbio za mwenge Arumeru

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,387
3,454
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amewabana wafanyabiashara na watumishi wa umma wilayani huko kuchangia mbio za mwenge zitakazofanyika katika wilaya hiyo juni mwaka huu.

Unaletewa barua ofisini kwako yenye muhuri na saini ya mkuu wa wilaya ili uchangie, ambapo ni kama ombi lakini kwa namna nyingine ni lazima.

Mama Samia ukiwa kama Rais wetu, wakati umefika wa kutafakari na kupiga marufuku mchezo huu, maana najua hata wilaya nyingine watakuwa wanashurutishwa hivihivi. Je hii mpaka lini? Mama tunaomba utoe neno
c2998dec-ff21-480d-9458-79acf2f6bd4d.jpg
 
Huduma ya kupiga simu tigo kwenda mitandao yote kwa miaka 3 bado ipo Bei 40000/.
Malipo ni baada ya kazi njoo inbox
 
Barua kama hizi hazifai na si za kuamini. Mtu yeyote anaweza kutoa nakala na kuitumia kuwatapeli watu. Wanashindwaje kuwa na data base ya wafanya biashara wote katika wilaya yao ili kila mmoja atumiwe barua kwa jina? Aidha, wanashindwa nini kupanga watu wa kufuatilia ili barua iwataje kwa majina? Hii itaongeza uwajibikaji na kuwapa uwezo wanaoombwa kuchangia wa kuthibitisha uhalali wa maombi hayo. Ni dalili ya uvivu wa kufikiri.

Amandla...
 
Mkuu, hayo yote hayana maana! Mwenye huu ni wa nani? Serikali au ni CCM? Kama ni wa serikali basi ukimbiwe kwa kodi, kama ni wa CCM ukimbizwe kwa ruzuku, michango ya wana CCM na vyanzo vyao vingine. Pesa zinazochangishwa mikononi hata mapato na matumizi yake hayadhibitiwi.

Ifike mahali wananchi tuhoji gari la halmashauri kutumika na CCM kufanya kampeni, misafara ya CCM. Kodi za wananchi zifanye mambo yenye manufaa kwa umma - sio kikundi cha siasa katika umma!!
 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amewabana wafanyabiashara na watumishi wa umma wilayani huko kuchangia mbio za mwenge zitakazofanyika katika wilaya hiyo juni mwaka huu.

Unaletewa barua ofisini kwako yenye muhuri na saini ya mkuu wa wilaya ili uchangie, ambapo ni kama ombi lakini kwa namna nyingine ni lazima.

Mama Samia ukiwa kama Rais wetu, wakati umefika wa kutafakari na kupiga marufuku mchezo huu, maana najua hata wilaya nyingine watakuwa wanashurutishwa hivihivi. Je hii mpaka lini? Mama tunaomba utoe nenoView attachment 1796599
Wewe changia mwenge ukiishapita utauliza hilo swali lako
 
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, amewabana wafanyabiashara na watumishi wa umma wilayani huko kuchangia mbio za mwenge zitakazofanyika katika wilaya hiyo juni mwaka huu.

Unaletewa barua ofisini kwako yenye muhuri na saini ya mkuu wa wilaya ili uchangie, ambapo ni kama ombi lakini kwa namna nyingine ni lazima.

Mama Samia ukiwa kama Rais wetu, wakati umefika wa kutafakari na kupiga marufuku mchezo huu, maana najua hata wilaya nyingine watakuwa wanashurutishwa hivihivi. Je hii mpaka lini? Mama tunaomba utoe nenoView attachment 1796599

2784752_WhatsApp_Image_2021-05-23_at_3.27.44_PM.jpeg
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom