Umaskini unavyowaingiza watoto kwenye biashara ya ngono

Song of Solomon

JF-Expert Member
Aug 5, 2021
2,733
5,490
BIASHARA ya ukahaba, licha ya kushamiri katika maeneo makubwa ikiwemo Dar es Salaam, madhila wanayokutana nayo makahaba ni makubwa ikiwemo kushiriki ngono na kutolipwa, kubakwa, kupigwa na pia ni kazi ambayo inahatarisha maisha yao na pengine kupoteza maisha.

Uchunguzi uliofanywa na Habarileo Online katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, umebaini kuwepo kwa madanguro ambapo wanawake na wasichana walio na umri kati ya miaka 15 - 40 hujihusisha na biashara hiyo.
Biashara hiyo kongwe katika historia ya maisha ya binadamu, imekithiri zaidi katika majiji makubwa duniani ambapo wanawake huuza miili yao ili kujipatia fedha za kuendesha maisha.

Maeneo maarufu ambayo biashara hiyo ya dada poa ufanyika ni Sinza, Magomeni, Friends Corner, Kinondoni Masaki, Oysterbay, Ubungo, Urafiki, Riverside, External, Manzese, Maeneo mengine ni Kimboka (Buguruni), Tabata Magengeni, Segerea, Kinyerezi, Temeke Mwisho, Sudan, maarufu kwa Wahaya, Mbagala Kizuiani, Zakhem na maeneo yanayotazamana na Mlimani City Barabara ya Sam Nujoma.

Mtandao huu pia imebaini baadhi ya wanandoa wanashiriki katika vitendo ama kwa wanaume kununua au wanawake kuwa sehemu ya dadapoa wanaosaka wateja kwa makubaliano ya malipo ya fedha.

Aidha mtandao huu pia umebaini kuwa wengi wanajitumbukiza kwenye biashara hiyo ya ukahaba ili waweze kujikimu kimaisha, lakini je yapo matumaini?

Hatari wanayopitia:
Sarahabiba binti anyejihusisha na ukaaba maeneo ya Manzese anasema “Tunaonekana ni watu tusio na maadili kwenye jamii, tunaepukwa na wengi kwenye jamii inayotuzunguka, wanatunyanyapaa.

“Tunapitia hatari nyingi, tunajiweka rehani maisha yetu ili tu tuhakikishe familia zetu zinapata kula,” anasema Rahel, binti mwingine anayefanya biashara ya ukhaba eneo la Ubungo External jijini Dar es Salaam.
Kuna wakati tunapitia misukosuko mingi, kukamatwa na askari, kupigwa na wateja wetu, wakati mwingine kuuliwa.

“Mtu anakuchukua mnaelewana vizuri, akishapata huduma hataki kutoa hela ukihoji wakati mwingine unaishi kushambuliwa kwa kipigo, wapo waliopoteza maisha kutokana na kazi hii.

“Kuna mwenzetu alichukuliwa vizuri lakini hakuonekana na baada ya siku mbili tukapata taarifa za mwili wake kuonekana ukiwa umetelekezwa kwenye majani maeneo ya ustawi wa jamii.”anasema Rachel
Amina, mwenye miaka 22 sasa , mkazi wa Kinondoni, anasema alianza biashara ya ngono akiwa na umri wa miaka 15 alipopata mimba ya mtoto wake Subira, mpenzi wake alimuacha,

“Napitia haya yote kwa ajili ya binti yangu, nimepitia uchungu mwingi sana eneo hili, nataka mwanangu aje kuwa wakili ili anipiganie mimi na wengine wanaodhulumiwa
Binti mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Rose mkazi wa Sinza, akielezea alivyojitumbukiza kwenye biashara ya ngono anasema “Wazazi wangu baba na mama walifariki nikiwa mdogo (kilio).”Ninaambiwa walifariki kwa ajali, nililelewa na bibi, lakini nikiwa na miaka 10 bibi yangu alifariki, pale ndipo nilianza kuishi maisha ya uchungu, sitaki kuyaongelea haya (kilio).

Mikasa kwenye maisha ya Rose iliendelea baada ya kulazimika kukatisha masomo na kuingia mitaani kufanya kazi za ndani ambako alijikuta akiishia kubakwa na baba mwenye nyumba.
“Kutokana na maisha niliyoyapitia, nikajikuta naingia kwenye biashara ya ngono, yale niliyoyapitia sitaki wapitie wengine, ndio maana nimekuwa nikisimama imara napigania maisha yangu kwa nguvu hadi tone la mwisho la damu yangu.

Happy mkazi wa Magomeni, akielezea madhila ambayo amewahi kukumbana nayo katika kazi yake hiyo ya biashara ya ngono anasema “Nilikutana na jamaa klabu, akanichania nguo, akachukua na hela yangu sh 60,000 kutoka kwenye sidiria yangu, nilikuwa nang’ang’ana kutoka ila alinipiga kwa nyuma ya shingo, angeniua maana alinishtukiza ila mabaunsa wa klabu walinisaidia na alichukuliwa na Polisi.

Kuna wakati pia tunakamatwa na Polisi kwa uzururaji unalazwa lokapu hujui nyumbani watoto inakuaje?
Umaskini:
Chonge mkazi wa Mwananyamala, anayefanya biashara ya ngono maeneo ya pembezoni mwa Leaders Club anasema “wengi tunalea watoto wenyewe bila ya usaidizi wa baba, maisha ni magumu, pesa inavyoadimika ndio na hatari zaidi kwetu inavyoongezeka, maana ili tujikimu inabidi tuendelee tu kufanya biashara hii.

Tumekuwa tukikutana na madhila mengi, ni biashara ngumu wengine wamekuwa wakiishi wengi kwenye chumba kimoja maarufu ya ghetto, lakini wengine wamepangisha vyumba na kuishi maisha mazuri.
Corona yachagiza ugumu wa maisha:

Ugonjwa wa Corona umefanya maisha yao kuwa magumu zaidi, kuanzia mwaka jana mwezi wa tatu serikali ilipotangaza kuwa na mlipuko wa ugonjwa wa Corona nchini, biashara imekuwa ngumu zaidi kwa madada poa.
“Kidogo sasa hivi hali inaanza kuwa nzuri, lakini kipindi Corona imeshamiri biashara ilikuwa ngumu, ilifika kipindi unapigwa na baridi hupati mteja hata wa buku yaani,” anasema dada Poa aliyefahamika kwa jina la Pili mkazi wa Magomeni Usalama na kuongeza “Lakini kwa sasa hesabu ya wateja angalau inaanza kuongezeka.

Kabla ya Corona mtu unauhakika wa kupata kuanzia sh 50,000 hadi 100,000 kwa usiku mmoja, na wakati mwingine siku inakuwa nzuri zaidi unaweza pata zaidi ya kiasi hicho.

Lakini tangu kuingia kwa ugonjwa huu, mambo ni magumu, ukipata sh 30,000 unashukuru, wateja walipungua sana
Wanenavyo wanaume:
James Lweno (sio jina halisi) anasema, huwa tunawafuata mitaani kwa kuwa kuna kahaba zaidi ya 1,000 mjini Dar es Salaam wanaohangaika kusaka maisha.
Gerald mkazi wa Kigamboni anasema “Kwangu mimi naona biashara hii ya ukahaba imeota mizizi nchini kwa kuwa wanaume wengi wana msongo wa mawazo, hakuna sheria kali, umaskini na malezi, ushawishi toka kwa makundi rika.

Akifafanua anasema “Wanaume wanakuwa na msongo wa mawazo hawana mahusiano mazuri na wenza wao hivyo wanaona chaguo sahihi ni kwenda kununua ngono. Pia hakuna sheria kali inayozuia biashara ya ukahaba nchini, kungekuwa na sheria kali ya biashara hiyo, ukimkamata kahaba, mkamate na anayemnunua, biashara hii ingepungua nchini.

Aidha amesema “Watoto wamezaliwa katika familia duni wanajikuta wanaingia mitaani kujitafutia kipato na kujikuta wanakuwa katika malezi yasiyo sahihi, hivyo wanajitumbukiza kwenye ukahaba ili wapate mkate wa kila siku.

Pia Makundi rika mabinti wanashindwa kujizuia tamaa za mwili, kwa kuona wenzake wana maisha mazuri hivyo nae anafuata mkumbo.

Takwimu za Corona:
Kwa mujibu wa takwimu za Tanzania zilizorekodiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) hadi Novemba 9, 2021 zinaonyesha watu 26, 196 wameambukizwa Corona huku kati yao watu 725 wakipoteza maisha.

POLISI
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, anasema elimu itolewe kwa wanaume kwani ndio chanzo cha madada poa, wakiacha kuwanunua wataacha kujiuza.

“Wanaume wakiacha kuwafuata huko mtaani, mara moja watakosa soko na wataachana na vitendo hivyo. Mimi kwa sasa sitatoa SMG kwenda mitaani kukamata dadapoa, ninapambana na majambazi na wahalifu," anasema.
WANASHERIA
Wakili wa Kujitegemea, Daniel Kalasha anasema hakuna sheria inayowabana wanawake wanaojiuza (dadapoa), bali iliyopo inawabana wamiliki wa madanguro na baa zinazotumika kufanya biashara hiyo.

"Mmiliki wa danguro anashtakiwa kwa kosa la kuendesha danguro na akipatikana na hatia anahukumiwa kwa mujibu wa sheria," anasema.
Wakili Kalasha anasema dadapoa akikamatwa, hushtakiwa kwa makosa ya uzururaji katika Mahakama ya Jiji na wakipatikana na hatia wanalipa faini ambayo ni kuanzia Sh. 50,000 hadi 200,000.
Anasema wanaoshindwa kulipa faini, wanakwenda jela miezi sita lakini uzoefu wake unaonyesha kesi hizo mara nyingi haziendelei mpaka mwisho.

Naye Mwanasheria Reuben Semwaza ‘Kinara’ anasema kuthibitisha makosa ya kujiuza ni vigumu kutokana na uhitaji wa uthibitisho kwamba aliposimama au eneo ulipomkuta alikuwa akijiuza.

Semwanza, anasema wamiliki wa madanguro hushtakiwa hata kwa makosa ya kufanya biashara haramu ya binadamu ambayo adhabu yake iko kisheria.
"Ukimiliki danguro kisheria unashtakiwa kwa kuzuia uhuru wa mtu, ukikamatwa una watu umewahifadhi, ukashindwa kujieleza wako kwa ajili ya nini, hakuna taarifa za uwapo wa watu hao, hawana kazi yoyote, unaweza kushtakiwa kwa makosa mawili.

"Kwanza; unashtakiwa kwa kuwa na nia ovu, kumiliki danguro na kosa la pili unaweza kushtakiwa kwa kufanya biashara haramu ya binadamu," anafafanua.
Wakili huyo anarejea kifungu cha namba 4(5) cha Sheria ya Biashara Haramu ya Binadamu inatoa adhabu ya kulipa faini Sh. milioni tano na isiyozidi Sh. milioni 10 au kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka miwili hadi 10.

"Kifungu namba 4(1a) cha Sheria ya Biashara Haramu ya Binadamu kinazungumzia madanguro, uzinzi, umalaya na makosa yote hayo adhabu yake ni faini Sh. milioni tano na isiyozidi Sh. milioni 10 ama jela miaka miwili na isiyozidi miaka 10," amefafanua

Habari leo Nov 18,2021
 
Hali inatisha
IMG-20211120-WA0073.jpg
 
Biashara kongwe duniani ni vigumu Sana kuizuia Bora watengeneze mazingira rafiki ya dada zetu kuifanya kwa usalama na pia serikali inufaike .....Kuna ambao mtahukumu ila Amna jinsi hao wanaosimama ni tip of a iceberg mtandaoni wamejaa Sana
 
we vip, maisha magumu af unataka tena serikali ipeleke tozo kwa madada poa, vifurushi vikipanda bei?
 
Wengi ni kama wamekata tamaa ,haiwezekani unapata 50 kwa siku bado ung'ang'anie biashara hiyo
Sio kujikatia tamaa , hawa pia wana tamaa sana anaona hata akiacha hiyo biashara anawaza atafanya biashara ipi ili apate pesa hiyo kwa siku , biashara za kuingiza faida elfu 15 au 20 , anaona hapana bora nirudi kule kule kwenye uhakika wa 50 mpaka laki ,
Pia tamaa inawaponza
 
Sio kujikatia tamaa , hawa pia wana tamaa sana anaona hata akiacha hiyo biashara anawaza atafanya biashara ipi ili apate pesa hiyo kwa siku , biashara za kuingiza faida elfu 15 au 20 , anaona hapana bora nirudi kule kule kwenye uhakika wa 50 mpaka laki ,
Pia tamaa inawaponza
Exactly uko Sahihi mkuu
 
Kuna wakati nilijiuliza ni kwa nini kumekuwa na matamko ya kila mara ya kupambana na Ukahaba lakini hazifanyiki juhudi kumaliza tatizo la Watoto wa mitaani?.

Hivi Jamii tunajua kuwa wakati wale wa kiume wanaishia kwenye Ujambazi, Uteja n.k wale wa kike huishia wapi?.

Leo hii hata tukiwasweka ndani Makahaba wote (maana ndio akili rahisi ya kutatua mambo kwa Mswahili) vipi hao wanaokuja wakitokea Mtaani?.

Katika utafiti wangu usio rasmi nimegundua ya kuwa hawa Wanawake wamegawanyika kwenye makundi makuu kama matatu hivi:-

1)Wapo waliokata tamaa ya maisha na wanajihisi hawana tena cha kupoteza hapa Duniani.

2)Wapo wanaofanya kwa kukosa njia mbadala ya kupata kipato, hawa unaweza kusema wanajiendekeza.

3)Wapo wanaofanya kama starehe, hapa wengi utakuta ni Wanywaji, Wavutaji na wapenda starehe kupindukia...na wanapenda ngono hivyo hutumia hilo kama pia chanzo cha mapato.

*Nikianza na hilo kundi la kwanza...hawa ni kundi hatari sana na kama huna uwezo wa kuwang'amua haraka utakuwa wa kulizwa mara kwa mara. Hawa wapo tayari hata kufanya dili na kukutoa uhai kwao si jambo kubwa, na sidhani kama hawa kamwe huangukia kwenye kundi la wanaodhulumika au kuonewa na Wateja wao, hawaogopi na wapo tayari kwa lolote kujitetea.

*Kundi la pili hapa unaweza kukutana na Mwanamke mwenye sifa zote za kuwa Mke (wife material). Huku utawapata Wanawake wenye tabia za kawaida kabisa, wana aibu, waoga, wanaokata tamaa haraka, ni rahisi kusikilizana, unaweza kuanzisha nao mjadala na wanaweza kukupa madini ambayo hujawahi kuyapata na unaweza usiamini kwa nini yupo hapo, na mara nyingi wanakuwa kama wanajutia wanachokifanya na huwa wanategemea sana wasikie unawashauri nini kama nawe ni Mtu wa kushauri, Wengi wana Watoto na hata Wenza, na kama wamekuona umekaa kiheshima na busara wanafunguka kirahisi sana stori za maisha yao.

*Kundi la tatu ni wale ambao hawajafuata sana pesa na unaweza hata kuwapata kwa kumnunulia pombe tu. Hawa kama muda umeenda anaweza kukubana umnunulie hata chupa moja ya bia muende.

Na hata pale Mamlaka zitakapoendesha mapambano ni rahisi kuwatikisa hawa makundi mawili lakini sio hao kundi la kwanza...hao ni kama tu Majambazi.
 
Kuna wakati nilijiuliza ni kwa nini kumekuwa na matamko ya kila mara ya kupambana na Ukahaba lakini hazifanyiki juhudi kumaliza tatizo la Watoto wa mitaani?.

Hivi Jamii tunajua kuwa wakati wale wa kiume wanaishia kwenye Ujambazi, Uteja n.k wale wa kike huishia wapi?.

Leo hii hata tukiwasweka ndani Makahaba wote (maana ndio akili rahisi ya kutatua mambo kwa Mswahili) vipi hao wanaokuja wakitokea Mtaani?.

Katika utafiti wangu usio rasmi nimegundua ya kuwa hawa Wanawake wamegawanyika kwenye makundi makuu kama matatu hivi:-

1)Wapo waliokata tamaa ya maisha na wanajihisi hawana tena cha kupoteza hapa Duniani.

2)Wapo waofanya kwa kukosa njia mbadala ya kupata kipato, hawa unaweza kusema wanajiendekeza.

3)Wapo wanafanya kama starehe, hapa wengi utakuta ni Wanywaji, Wavutaji na wapena starehe kupindukia...na wanapenda ngono hivyo hutumia hilo kama pia chanzo cha mapato.

*Nikianza na hilo kundi la kwanza...hawa ni kundi hatari sana na kama huna uwezo wa kuwang'amua haraka utakuwa wa kulizwa mara kwa mara. Hawa wapo tayari hata kufanya dili na kukutoa uhai kwao si jambo kubwa kwao, na sidhani kama hawa kamwe huangukia kwenye kundi la wanaodhulumika.

*Kundi la pili hapa unaweza kukutana na Mwanamke mwenye sifa zote za kuwa Mke na akatulia, huku utawapata Wanawake wenye tabia za kawaida kabisa, wana aibu, waoga, wanaokata tamaa haraka, ni rahisi kusikilizana, unaweza kuanzisha nao mjadala wanaweza kukupa madini ambayo hujawahi kuyapata na unaweza usiamini, na mara nyingi ni wnakuwa kama wanajutia wanachokifanya na huwa wanategema sana wasikie unawashauri nini kama nawe ni Mtu wa kushauri, Wengi wana Watoto na kama wamekuona umekaa kiheshima wanafunguka kirahisi sana maisha yao.

*Kundi la tatu ni wale ambao hawajafuata sana pesa na unaweza hata kuwapata kwa kumnunulia pombe tu. Hawa kama muda umeenda anaweza kukubana umnunulie hata chupa moja muende.

Na hata pale Mamlaka zitakapoendesha mapambano ni rahisi kuwatikisa hawa makundi mawili lakini sio hao kundi la kwanza...hao ni kama tu Majambazi.
Nzuri hii. Unajua Hili andiko lako unaweza kulifanyia utafiti zaidi kuliandikia kitabu.
 
Back
Top Bottom