GE2025 DC Haniu: Wananchi jitokezeni kupiga kura Oktoba 29, msikubali wasio na nia njema na Nchi

GE2025 DC Haniu: Wananchi jitokezeni kupiga kura Oktoba 29, msikubali wasio na nia njema na Nchi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
161
Reaction score
200
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Jaffar Haniu ametoa wito kwa Wakazi wa Halmashauri ya Rungwe na Busekelo kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika siku ya tarehe 29, Oktoba, 2025.

Uchaguzi Mkuu utahusisha Wananchi Kumchagua Rais, Wabunge pamoja na Madiwani.
WhatsApp Image 2025-10-16 at 13.23.31_9b1ef008.jpg

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo tarehe 16 Oktoba 2025, Haniu amewasihi Wananchi wasikubali kurubuniwa na watu wasio na nia njema kama kuombwa watoe kadi ya kupigia kura, kushiriki maandamano au vurugu zozote kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Haniu ambaye pia ni Mwenyekiti wa ulinzi na usalama wilaya ya Rugwe ameapa kulinda na kusimamia amani na utulivu huku akiwasihi wananchi kutochezea Amani iliyopo kwani kufanya hivyo itadhorotesha shughuli za maendeleo na hata kushindwa kushiriki katika sehemu za ibada.

"Rungwe ni Salama, Itakua salama wakati wa uchaguzi na baada ya Uchaguzi," ameongeza Haniu.
WhatsApp Image 2025-10-16 at 13.23.33_0a0335c6.jpg

Aidha, amewaomba wasimamizi wa uchaguzi kutoa kipao mbele kwa akina mama wajawazito, Wazee, wanaonyonyesha pamoja na walemavu siku ya upigaji wa kura.

Pia, amewasihi wananchi kutovaa sare ya chama chochote cha siasa siku ya uchaguzi na pindi watakapomaliza kupiga kura warejee katika makazi yao au shughuli zao za uzalishaji mali na kusubiri matokeo kwa amani na utulivu.
 
Ccm ndio waliokuwa hawana nia njema na wananchi. Ni lini ccm na serikali yake waliokemea utekaji na uuaji nchini.
 
Sijaamini km Odinga is dead aise maisha ni mafupi mno
 
Back
Top Bottom